Vodacom Tanzania imetangaza kuanzishwa kwa promosheni ya TUZO M-PESA ambapo itatoa zawadi ya mamilioni ya shilingi kwa wateja wake waliojisajili na huduma yake ya Vodafone M-Pesa zitatolewa.
Meneja Matukio na Promosheni wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa aliwaambia Waandishi wa Habari Jijini kuwa promosheni hiyo ya “Tumia huduma za M-PESA na Ushinde” inaanza kesho tarehe mosi na kumalizika tarehe 31 Desemba mwaka huu.
“Kupitia promosheni hiyo, wateja wetu wataweza kujishindia shilingi milioni arobaini kwa mwezi huu wa Desemba,” amesema.
Alisema wateja 20 wa Vodafone M-PESA watajishindia kila wiki shilingi 500,000/- na hivyo kufanya jumla ya zawadi za fedha taslim kwa wiki kuwa shilingi milioni 10.
Alisema kushiriki ni rahisi kwani kila wakati mteja atakapotumia huduma mojawapo ya Vodafone M-PESA atakuwa ameweza kuingia kwenye droo hiyo na kupata nafasi ya kujishindia Zawadi.
Alizitaja huduma hizo kuwa ni pomoja na kutuma pesa, kununua muda wa maongezi pamoja na kulipia ankara za huduma mbalimbali.
Alibainisha kuwa hivi sasa kupitia Vodafone M-PESA Vodacom Tanzania inawawezesha Watanzania kutuma pesa kwa ndugu na jamaa zao wa karibu pamoja kuhifadhi amana zao.
“Kwa maana nyingine huduma hii inawaingiza Watanzania wengi waliokuwa wako mbali na mfumo rasmi wa kifedha,” Alifafanua
Alibainisha kwamba hivi sasa kupitia Vodafone M-PESA wateja wa Vodacom Tanzania pia wanaweza kulipia Ankara mbalimbali za huduma muhimu za kila siku kama vile maji, nishati ya umeme na huduma nyingine nyingi.
Aliwaomba wateja wa Vodacom kuitumia huduma hii ya Vodafone M-PESA katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu kwa kutuma pesa kwa ndugu na jamaa pamoja na kuitumia kupata huduma mbalimbali katika msimu huu wa sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya
Yeeeiiiii thats my girl Nector Pendaeli Foya... endelea na kazi nzuri sana ya kuwakilisha unachokifanya...Hongera sana Nector..
ReplyDeleteMdau, Kibosho girls-USA
Elihuruma naona mambo yako! Hongera sana,kaza buti!
ReplyDeleteMdau Tom, Dallas TX,US