---------------------------------
Hi Issa!
Hicho kikosi nakikumbuka sana hata siku hiyo ya hiyo game nafikiria nilikuwepo nation stadium,wakati nikiwa mdogo,yule wa pili baada ya mzee Abdulrahman Juma ni mzee mzima Othman Kilambo, halafu anafuatiya mmanyema Rwambo Kapera na mtu mzima late Gibson Sembuli na halafu mwengine pale ni Seleman Saidi.
hicho kilikuwa ni kikosi changu kikubwa sana enzi za akina kaka Sunday Manara na bro Kitwana wakicheza mpira mimi nilikuwa sina shida ni kuwasubiri mlangoni mkuu wa magari na halafu star Sunday alikuwa anatoka kuniingiza ndani ya bus la yanga.
sizisahau enzi hizo,siku ya mechi kubwa hulala kwa grand mother wangu marehemu Bi Mkali ambaye alikuwa ana nyumba hapo hapo karibu na uwanja wa taifa,ticket yangu ilikuwa ni mguu wangu kufika kwa bibi yangu na the rest kaka Sunday alikuwa akiniingiza katika bus la yanga naingia nao uwanjani bure,ilikuwa yanga kweli kweli enzi hizo ,hakuna kama mzee Mangara Tabu kuhusu uongozi wa mpira na yule Shiraz Sharif siku hizi yuko wapi?mara ya mwisho najua alikuwa Pan Africa yeye na mzee Jim Mdo
Karenga
Karenga
---------------------------------------------------
Michuzi,
Picha hiyo imenikumbusha mbali sana.
Ni kweli kabisa alikuwa hatumwi mtu dukani kikosi hicho kikiwa uwanjani.Kikosi hicho kilikusanywa takriban miaka 40 iliyopita na kilikuwa pamoja hadi mwaka 1973 wakati kilipodunguliwa bao moja kwa bila na mahasimu wao Simba kwa bao zuri la kichwa lilofungwa na nahodha wa simba Haidar Abeid na hivyo kuvuliwa ubingwa wa Tanzania.
Kikosi hicho kilifanyiwa mabaliko kiasi pale walipoingia kina Tenga 1974 na hivyo kufanikiwa kuurudisha ubingwa Jangwani mwaka huo.
Kikosi kamili kilikuwa kama ifuatavyo
1) Muhidin Fadhili
2) Athumani Kilambo
3) Suleiman Said
4) Hassan Gobos
5) Omari Kapera
6) Abdulrahman Juma
7) Godfrey Nguruko
8) Sunday Manara
9) Kitwana Manara
10) Gibson Sembuli
11) Maulidi Dilunga
Pichani kutoka kulia kwenda kushoto ni Abdulrahman Juma,Hassan Gobos ,Omari Kapera , Suleiman Said , Godfrey Nguruko , Muhidin Fadhil ,Sunday , Maulidi Dilunga , Kitwana Manara , Athumani Kilambo, Kocha Victor Stanslaus.
1) Muhidin Fadhili
2) Athumani Kilambo
3) Suleiman Said
4) Hassan Gobos
5) Omari Kapera
6) Abdulrahman Juma
7) Godfrey Nguruko
8) Sunday Manara
9) Kitwana Manara
10) Gibson Sembuli
11) Maulidi Dilunga
Pichani kutoka kulia kwenda kushoto ni Abdulrahman Juma,Hassan Gobos ,Omari Kapera , Suleiman Said , Godfrey Nguruko , Muhidin Fadhil ,Sunday , Maulidi Dilunga , Kitwana Manara , Athumani Kilambo, Kocha Victor Stanslaus.
Kikosi hicho kilikuwa chini ya uongozi imara wa Mzee Tabu Mangara na Mfadhili mkuu wa wakati huo Shiraz Sharif
Maalim Mrisho
East Bay CA
--------------------------------------
...not to be beaten, the fourth from right is the late Gibson Sembuli. Zaidi ni swali - ...nini maana ya mtoto kutotumwa dukani?
ReplyDeleteHapo namuona, Abdulrahman Juma, Gibson Sembuli, Omari kapera, Sunday Manara, Kitwana Manara, Maulidi Dilunga, Kilambo; Boi Wiked na wengine nimepoteza memory kidogo.
ReplyDeletetoka kushoto.abrahman juma(captain)athumani kilambo(baba watoto)omar kapera,gibson sembuli(rip)ally yusuf,leonard chitete(rip)muhidin fadhil,sunday manara(computer)maulid dilunga(mexico)na kitwana manara(bapo).mdau challa boy,.amstd
ReplyDeletewajameni hivi macho yangu au...kaka muhidin wachezaji wetu siku hizi mbona hawana miili........au tunatoa nanihii hazina nguvu ..au wanakula pamba...
ReplyDeletemaana wachezaji wenye miili waliichia miaka ya 90 baada ya hapo digidigi...
angalia hata makipa wa siku hizi wafupi kweli..tofauti na kina mwameja.....
nadhani kuna haja ya kuwapeleka vijana waliogunduliwa copa coka cola kwenye kambi maalum ya KULA,MAZOEZI, KUCHEZA...kwa sababu bado wanakua labda watapata maumbo....
hawa taifa stars wa sasa wamechakomaa hata ukiwalisha nundu hawatakaa wapate body...na kuku zote walizopewa na jk ......bado tu ...viombo
halafu wachezaji wa mpira siku zile walikuwa wana kimo kidogo. Ni kwanini hawa wa siku hizi ni wadogowadogo tu? Au ni matatizo ya lishe haya..
ReplyDeleteina maana watanzania wanazidi kuwa wafupi kadri muda unavyosogea?
ReplyDeletesababu ya kusema hivyo ni kwamba wachezaji wengi wa sasa wanaonekana wafupi kuliko hawa. any scientific explanation?
Kweli siwajui....ila nataka uliza mbona wachezaji zamani walikuwa wanajifunga mabendeji mengi? au ndio ilikuwa style ya wachezaji?
ReplyDeletekutoka kushoto Abrahman juma ,Kilambo,kapera,nanihii,chitete,muhidini issa michuzi, nanihii, halafu nanihii,kitwana , halafu nanihii hao wengine kesho
ReplyDeleteKwa kumsaidia mdau Chala boy wa amstd mtu aliyemucha ni mmoja , wa kwanza kushoto baada ya Victor ni Gilbert Mahinya . mdau Mzee Kasri Leicester UK.
ReplyDeleteTatizo la wachezaji wa sasa kukosa miili
ReplyDeleteHawana nidhamu ya michezo,fuatilia ratiba yao utakuta kama hii
anatoka mazoezi jioni anaenda kuoga na kula kidogo chakula alichopikia na mkewe labda ugali na tikiti maji maana hajacha hela,anatoka kwenda magomeni mapipa kukutana na wenyenazo ili anywe na kula na mainly msosi ni chips mayai au kiti moto na atakunywa mpaka late atapewa posho kidogo wenye nazo watakapo ondoka,naye atatoka kwenda kwa macheni kuchukua vimeo au ataenda kwa mariam kwenye ahadi. Hiyo mpaka tisa kurudi nyumbani atalala mpaka asubuhi na ataamka amwone wife ndio aende kwenye mazoezi. Na kama siku ya mechi atapewa ofa ya lunch ataenda kula biriani. sasa watanzania wenzangu mwili mkubwa utaupata wapi? wenu Mtzed
Ni vyema kuanza kutupatia majina labda kuanzia kushoto kwenda kulia au kuanzia kulia kwenda kushoto.
ReplyDeleteUkitaja majina tu haitotusaidia sisi ambao hatuwafahamu na enzi hizo kulikuwa hakuna runinga na gazeti pia ilikuwa shida
Kutoka kushoto aliposima Mrumania Professor Victor Stanculeseisni Mchezaji Hassan Gobos, Kitwana Manara, Maulid Dilunga, Sunday Manara, Kipa Mudin Fadhil,Leonard Chitete, ALIEFUATA NIMEMSAHAU, halafu Gibson Sembuli, Omar Kapera, Ramadhan Kilambo na Abdulrahman Juma.
ReplyDeleteMDAU wa Blogu
www.uksokainbongo.blogspot.com
Storming
Wadau,
ReplyDeleteNiliposti mapema na nikataja Timu nzima ila kuna Mchezaji nilisema nimemsahau sasa nimemkumbuka ni Gilbert Mahinya na alikuwa ni Kiungo Bora sana enzi hizo, Hafu Beki Siksi!!!
Shukran,
MDAU wa Blogu www.uksokainbongo.blogsport.com
Storming
Siku hizi Bwana wachezaji wetu tatizo lao Bongo Lishe Mbaya, Pombe na Madawa ya kulevya, hasa Bangi; Wengi nguvu za Unyoya tu.
ReplyDeleteI love Bongo, zamani kila kitu kilikuwa kizuri. Sasa mmhhmm, el balah wal balah
ReplyDeletenashukuru wadau kwa kugundua hilo .mpira wa bongo hupo pale pale tunachoshindwa nikuwa na afya duni
ReplyDeleteWa 4 kutoka kulia ni Gibson Sembuli. Katika historia ya Soka Tz Sembulia ndie aliekuwa wa kwanza kuchana nyavu kabla Gaga Lino. Nyavu zilikuwa azijalowa wala kunyeshewa na mvua. Unaambiwa Sembuli alikuwa na msuri wa ajabu. Jamaa atosahaulikwa. Wa pili kuchana nyavu alikuwa Hamisi Thobiasi Gaga a.k.a. GagaLino Simba ilipocheza na Maji maji. Yanga wakadai nyavu zilikuwa zimeloa, ooooohh zimenyeshewa na mvua mara azikufungwa vizuri. Yanga walitoa sababu kibao kwaajili msimu uliopita Gaga alihama Yanga na kuja Simba. Alifunga gori hilo kwa njia ya penati lilikuwa shuti kali hata Pita shimaiko awezi kudaka. Je mnajua nani alishawai kuchana nyavu Ulaya? Ushauri kwa Watanzania 2pende soka le2
ReplyDeleteHata mie pia nataka kujuwa Kuhusu Tunaendea Ufupi au? Sababu Hawa wachezaji mie nilivyowaona nikataka kusema picha au? Siku hizi Hata ukikuta Mrefu basi mwili hana Vyakula vya Kopo na chips Kuku hizi.
ReplyDeleteTATIZO WALE KUKU TAIRA WALE WA KIZUNGU SI WAZURI TUWACHENI KULA WALE.
hizi totoz zimenyooka simchezo hadi raha!
ReplyDeleteKudadadeki kwa kikosi hichi cha mwaka 47 hata DROGBA angepata tabu sio siku hizi eti namba 3 Juma Jabu 6 Nurdin Bakari, 10 ngassa, 9 mgosi, 2 nsajigwa 8 Banka 4 Kanoni yaani kikosi cha sasa ni kama vikosi vya UMISETA miaka ile.
ReplyDeletehivi siku kama Tz tukicheza na Ivory kosti nani atamkapa Kalou, Drogba, Yaya Toure? Ngassa atampita Kalatoure?
Maximo aende kigoma kuna waha wanakipiga si mchezo sio mambo ya simba na yanga tu.
Anko, hebu waweke sawa wadau wenzangu: GODFREY NGULUKO alichezea Coastal Union ya Tanga na Taifa Stars na sio Yanga.
ReplyDeleteHAPO KWELI KUILIKUWA NA MPIRA SIO SASA - WATU WANAPENDA PESA NA WAKATI STANDARD YA MPIRA HAMNA TENA. NA PIA GODFREY NGULIKO HAKUCHEZEA YANGA WADAU - ALIKUWA WINGER WA COASTAL UNION YA TANGA. IKIWA TUNATAKA MPIRA UENDELEE TANZANIA BASI TUSIZISHUGHULIKIE TIMU MBILI TU YAANI YANGA NA SIMBA - TIMU ZIKIWA NYINGI ZINA STNADARD YA KIMPIRA BASI HATA MPIRA UNAKUWA KIWANGO CHAKE KINAPANDA - TIMU NYINGI ZIPO NAZO ZISAIDIWA - KAMA PAN AFRICA, COSMO, COASTAL UNION, AFRICAN SPORTS, MSETO, PAMBA, NYOTA YA AFRIKA,LEO ZIPO WAPI TIMU HIZI? kwa sababu tunashughulikia Simba na Yanga tu. Kila mchezaji au mshamba akitoka mikoani anataka achezee timu hizi. Vipi serikali iingilie mambo haya- kwani wafadhili wazitizame timu zote sio Simab na Yanga tu.
ReplyDeleteSIKUMBUKI GODFREY NGURUKO KUCHEZEA YANGA, ILA YULE NI MAREHEMU LEONARD CHITETE NA BEKI NAMBA MBILI NI ALI YUSUFU, SELEMAN SAIDI SANGA HAYUPO KWENYE HIYO PICHA
ReplyDeleteHAWA WACHEZAJI SIO WAREFU SANA KAMA WENGI WANAVYOSEMA, ILA TATIZO BUKTA ZAO NI FUPI, NDIO MAANA WANAONEKANA WAREFU.
ReplyDeleteKITU CHA PILI, WATU WENGI WANASEMA LISHE MBAYA WAKATI HAWA WACHEZAJI WETU WASHAKUA WATU WAZIMA, LISHE BORA INATAKIWA WAKATI WAKIWA WADOGO
check this out wa kwanza abdulrahman juma,athman kilambo,omar kapera,gibson sembuli,ally yussuf,leornard chitete,muhidin fadhil,sunday manara,maulidi dilunga,kitwana manara na hassan gobbos, kocha professor victor stan----
ReplyDeleteNAPENDA KUJUA WAKATI NIKIWA MDOGO KAMA SIKOSEI KUNA MCHEZAJI MMOJA WA YANGA ALICHUPA KWANYE BASI BAADAE ALIFARIKI NI NANI HUYO NA ALIKUWA AKICHEZEA TIMU GANI NA HIYO AJALI ILIKUWAJE MWENYE DATA NAOMBA NA WENGINE WATAFAIDIKA.
ReplyDelete-ahsanteni nyote kwa majina..tafakuri jadidi ya picha hii: 1. kama sikosei kikosi kilipangwa: m. fadhili, h. gobbos, a. yusuf, o. kapera, a. kilambo, a. juma, l. chitete, s. manara, g. sembuli, k. manara & m. dilunga. Ukiangalia maumbo,unaweza kuona kuwa ukiondoa a. yusuf (ambaye alisifika kwa kasi na kupandisha mbele) walobaki wamejengeka. Vivyo hivyo washambuliaji (ukiondoa s. manara na dilunga - ambao nao walisifika kwa kasi na ujanja wa kimchezo) walobaki wana maumbo ya ki-uana-riadha..B: kwa kutazama jezi hizo na wanazovaa yanga kwa sasa - hivi ni zipi rangi rasmi za klabu hii?..naona wachache wamevaa kinga-ugoko (shin-guards), sijui zilikuwa bei mbaya ama wakati huo 'wanaume wa shoka' walikuwa 'hawamaindi'..Angalia team-spirit, hii ni timu ya wanaojiamini mno na marafiki miongoni mwao, kwa hiyo matokeo yao ya wakati huo si ajabu..Hawa ni wachapakazi na waadilifu, sioni urembo, mitindo ya nywele (kwa sasa rasta, viereni n.k.) wala ubishololo kwa saana hapo (kasoro hizo bendeji, chitete kabenjua bukta na sunday kavuruga nywele na kushuuusha soksi, na daluga kazibandua three-stripes za
ReplyDeleteadidas)..Mtu you wish hawa ndo wangekuwa kwenye hii ligi ya Vodacom - UzenG!