Habari za kuaminika ambazo Globu ya Jamii imezipata ni kwamba Shirika la ndege Tanzania (AIR TANZANIA) limewaachisha wafanya kazi wake 155 na kubakiza 100 katika mfumo wa awamu mpya ya shirika hilo ambalo limeingia ubia na kampuni moja ya Kichina.
Habari zinasema leo shirika hilo linazindua ndege mpya inayoanza awamu hiyo mpya kwa kishindo, kabla ya ndege zingine kadhaa za masafa marefu na mafupi kuanza kazi katika njia zake zote ambazo zimekuwa hazitumiki kwa ukosefu wa ndege.


Wafanyakazi walioachishwa waliitwa na kupewa barua zao za kuachishwa kazi na kulipwa mafao yao yote Jumatatu.
Habari zaidi pamoja na taswira kufuata baadaye...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Air tanzania wamefulia siku nyingiii hadi aibu vibosile kazi yao ilikuwa ni kulifisadi hilo shirika ebu ona hii aibu kila kitu hadi aje mwekezaji na wanapokuja watu wanapiga kelele wee ooh mali za wazawa sijui upuuzi gani wakati wazawa wenyewe kazi zimewashinda ni kuiba tuu bila huruma na ufisadi mzito hapo angewekwa meneja mzungu lol!! kila kitu kingekuwa shwari huu upuuzi usingekuwepo kamwe sasa vijana wanaosomea u pilot wakimaliza school wakae nyumbani tuu au?? hii ni kukatisha watu tamaa kabisa kweli huu ufisadi unaipeleka nchi pabaya mie ningeshauri kila kampuni nyeti awekwe meneja mzungu tukianza na paleTRA NA BANDARINI uzandaki rushwa na uonevu vingepungua kwa asilimia kubwa na kazi zingefanywa vizuurii sasa watu wakimaliza shule na kung'ang'ania majuuu mnawatupia madongo kutwa kuna mapilot wa 4 walikuwa majuu na walikuwa wanarusha domestic flight ambapo ni poa saana tuu wakajidai kurudi hm na kufanya kazi pale air tz mwaka mmoja tu shirika kwishney nadhani sasa wanajuuuta kwa nini walirudi hm sweet hm makanisani misikitini majamatini tunaiombea nchi kweli kweli na viongozi wake lakini wapi kumbe tunawaombea mafisadi wazidi kuneemeka lol SHIRIKA LIBINAFSIHWE FULL STOP!!

    ReplyDelete
  2. haiwezekani shirika lina ndege mbili halafu wanyakazi 150, wanafanya nini?

    waajili wawe wanatumie maprofile ya enterviewees kuajiri kama hao wa air tz hawafai kuajiriwa na kampuni yoyote lkn cha ajabu hapo ni kama wamehama shirika moja na kwenda shirika lingine, ni bora kuajiri fresh graduates kuliko hao waliokwisha kuonesha mfano

    Chonde jamani kama mnalitakia mema shirikakuajiri waajiriwa wapya kujuana kusiwepo

    next RELI, TTCL,...baraza fulani,wakuu fulani na fulani..
    tunaweza kufika..

    ReplyDelete
  3. kama kungekuwa na Kampuni ambayo watanzania wangejisifia ni Air Tanzania, lakini imekuwa uozo mtupu toka mwanzo. Kila kiongozi anayeingia anakosa maadili na misingi ya kazi Bora. Watu wameishia Kula bila kujua na kutadhmini ni kiasi gani kinaingia na Control yake inakuwa vipi?
    Sio kwamba hawajasoma ila ni work ethics ambazo hawa watu wamekosa toka kichwani mpaka miguuni. Its fine wacha kampuni ife! it was nonsense to the rights Tanzanians who were genuinely coming back from wherever and facing stupidity at the terminal!

    ReplyDelete
  4. kweli bongo shwari.ngoja nikapige box langu mie.

    ReplyDelete
  5. safi sana hata na wizara kama ya madini na wizara ya utali ingefanya hivyo ingekuwa vizuri sasa naona tanzania tutasonga mbele,naipongeza sana hiyo management mpya nadhani na vitengo vingine navyo vitaiga nfano tunataka mae3ndeleo nchi yetu ni tajiri sana ila hao walio juu ndio wanaotuangusha.

    ReplyDelete
  6. Haiwezekani kukawa na wafanya kazi 255 kwa shirika lenye ndege 1 sijui 2 linawafanyakazi wengi hivyo ndio maana haliendelei,
    Pili kuhusu hizo ndege,kusema la ukweli mimi nimekuwa nikitumia ndege ya huyu mchaga kusafiria mara nyingi,but one daya nilikuwa natoka mahali kwenye airport ndogo mikoani nasubiria ndege yangu ya kichaga nipande,mara wafanyakazi wa AirTZ wakanifuata wewe unakwenda Dar,nikasema ndio ndwende na Ndege yetu kuna nafasi,basi nikakubali mie huyo nikaenda,unaambiwa nilikuwa sijawahi kupanda AirTZ ndani kumbe ni nzuri sana kuliko ya huyu mchaga kama hisia zinavyotutuma,lakini kitu kimoja wafanya kazi wao humo ndani wale wanaotangaza ni hawajui kizungu kabisa,inapoboa wakiongea kizungu anauma maneno kujikaza na anasoma kwenye kitabu hadi inaboa kuliko hawa wa wachaga wajua na hawajikanyagi kama hawa wa AirTZ. sasa mtu unashangaa wameajiriwa vipi wakati wanaonekana hawajui kusoma hata kizungu,na matamshi hawawezi kutamka vizuri ya kizungu.

    ReplyDelete
  7. Oh my God, at last the ATC imebinafsishwa! mungu wangu. So what about wale vigogo wakina D.M na wenzake? wanaendelea?

    Vipi pia ile bodi iliyokuwa inaongozwa na Mh. Nyang'anyi? itaendelea?

    Anyway, sasa hutu tuchina tusije tukawa kama wale wahindi wa TRL.

    Mdau

    Nyokoinyo.

    ReplyDelete
  8. Asante kaka Michuzi kwa kutuhabarisha hilo. Nipeni miaka michache tu nimalizie ka-elimu kangu huku ughaibuni halafu nirudi kuliendeleza libeneke la Air Tz. Bado ninaamini tunaweza kufanya kitu kwa ajili ya hilo shirika.
    Mdau Ughaibuni.

    ReplyDelete
  9. I HOPE WEZI WOTE WA PALE AIRPORT WAMEPEWA BARUA YA KUACHIA NGAZI SAFI SANA. WEKENI WACHINA HUKUNA KUIBIA WATU HOPA, WATAWACHAPA BAKORA MAANAKA JAMAA KWA BUSINESS HAWANA MCHEZO. AM HAPPY, I WISH WANGEBINAFSISHA EVERYTHING IN TZ.

    ReplyDelete
  10. Tatizo si watanzania.Wapo watz wenye uwezo lakini hapewi nafasi.Serikali ndio inafanya makosa kuteua watendaji ambao ni wabovu,hiyo haitoshi nayo inachota fedha bila kuangalia km shirika linapata faida.
    Kila kitu tunawapa wachina.wageni;ok.Je hiyo kampuni imefanyiwa evaluation ya kutosha.Mimi nadhani kuna something fish.kampuni hiyo ya kichina haijawi kufanya biashara yoyote ya mambo ya airline.Inahusika sana na uchimbaji wa mafuta,gesi,na miradi ya ujenzi, angalia websiti yao http://www.chinasonangol.com/eng/index.asp
    Naomba waTZ tukatae uwekezaji usiokuwa na tija.
    Yasije kuwa ya TRL,ATCL na SAA,Tanesco na Net group.

    ReplyDelete
  11. Kwa hiyo ndege zinafanya kazi au hazipo? kama hakuna basi precision wataongeza nauli sasa hivi hasa ktk kuelekea Xmas!!!

    ReplyDelete
  12. hakuna haja ya kuwato kama shirika litakuwa na wana invest......wachina watakuja kureplace hizo nafasi wacht out!

    wajinga ndio waliwao, long way to go mother land , i love africa , ilove tanzania

    pk

    ReplyDelete
  13. Jamani, wafanyakazi 255 na ndege moja au mbili, tija iko wapi?? na wala hai-make sense.

    Sasa kwa muda wote huu management tena wazalendo walikuwa wanafanya nini mpaka wamsubiri muwekazaji atoe shinikizo la kupunguza. Wamelala and they still call themselves managers!!!!

    Watu unakuta wana elimu zao nzuri tu lakini inapokuja kwenye utanzania ile professionalism and work ethics vyote vinawekwa kando, why?? tutafika??

    ReplyDelete
  14. NAOMBA KUULIZA JE WALIOACHISHWA KAZI NI KINA NANI KWA MAJINA? MASKINI, SASA ITAKUAJE, I HOPE WAMELIPWA FIDIA YA KUTOSHA.
    NAKUBALIANA NA MDAU MMOJA HAPO JUU ALIYESEMA. AIRTANZANIA INGEBINAFSISHWA TUU FULL STOP.

    ReplyDelete
  15. Anko,
    Unajua tatizo la hii inji yetu ni kichwa mbovu ya watu wasiopenda kulipeleka taifa pazuri. ATCL ilitakiwa ichukue hatua hizi long time. Kupeana kazi kishkaji bila sifa kumeliua shirika hili na kuwapa walipakodi mzigo mkubwa. Sasa wachina wako onboard bado nina wasiwasi wale wazee wa serikalini na jamii zao wataendelea kuliandama kwa complementary tickets na maamuzi ya kisiasa badala ya kiufundi.
    Mimi ni msafiri wa ndge wa muda mrefu katika masafa mengi na naiombea ATCL maisha mapya turudi ulee wakati wa ATC original in DAR-Frankfurt-London-Muscat, Dubai,Johanesburg NK NK NK

    ReplyDelete
  16. Kristo tuepushe na hili balaa la utapeli na ufisadi AIRTz,,,jamani?yani mmeingia ubia na wachina???tena?

    hope things will move,ila kuna kero jamani pale airport utafikili tunapanda ndege bure ilhali ni migharama ya kufa mtu just local flight!!ivi iki ni nn lakini?

    yani inauma sana unalipa laki 3.5 karibu na laki 4 na huduma za kishenzi/ovyo kabisa

    ngoja siku ipo

    hahahaaa eti ndege ya kichaga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...