Timu ya Taifa ya Tanzania Bara maarufu kama Kilimanjaro Stars imeichapa Zanzibar Heroes 1-0 na kufufua matumaini ya kusonga mbele kwenye michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.
Alikuwa ni mshambuliaji Mrisho Ngasa aliyeipa raha Tanzania Bara baada ya kuunganisha pasi ya kiungo anayecheza soka ya kulipwa nchini Norway, Henry Joseph, na kumtungua kwa shuti kali kipa wa Zanzibar, Ally Muhidin, katika dakika ya 18.
Mchezo wote ulitawaliwa na ubabe baina ya wachezaji kiasi hata Kigi Makassi wa Kilimanjaro na kipa wa Zanzibar, Ally Muhidin, walilimwa kadi nyekundu na mwamuzi Thomas Onyango wa Kenya.
Hii ni mara ya pili katika mwaka huu kwa Bara kuishinda Zenji, kufuatia mchezo wao wa michuano hiyo iliyofanyika mwezi Januari nchini Uganda ambapo Bara ilishinda 2-1.
Eritrea na Zimbabwe zilitoka suluhu 0-0 katika mchezo wa Kundi B wa michuano hiyo uliofanyika jijini Nairobi.
Leo Ethiopia itacheza dhidi ya Zambia, wakati wenyeji Kenya watakwana na a Djibouti, huku mabingwa watetezi Uganda wakivaana na vibonde wa Kundi C, Burundi, mjini Mumias.

Ugali wa Mhogo vs mtata za urojo za Adinani wapi na wapi bwana!!!
ReplyDelete(US Blogger)
Yaani hii game ni kama:
ReplyDeleteUS Blogger vs John Mashaka, so hapo si unajua tu kama US Blogger atatandikwa!
Mashaka ni noma kaka!
K'dume
maximo kapumua!pangekuwa hapatoshi maana alishawqahi kuwaita legelege wale wenzetu wa kanchi jirani!
ReplyDeletevipi tena naona mlipochapwa 2 na uganda mlibana kimya tena hata hamkusema znz imeshinda 4 na nyinyi mmechapwa sasa hivi mshakuwa na mdomo hivi una hakika mtakenda mbele nina asilimia mia kwa mia hamuendi pahala popote. Hata kuingia duru la pili sijui kama mtaingia, hivi nyinyi munaingia ktk mashindano ili kumfunga znz tu. Hemu kuweni na akili musichengue watu, bara mpira wapi na wapi, angalia rank ya dunia utajua kama sisi kwa mpira au kula huo ugali na muhogo. Mijitu mengine mijinga kweli.
ReplyDeleteHapa kipofu kaona mwezi, tunaiombea kila la kheri Kilimanjaro Stars.
ReplyDeleteNB: Maximo timu isiporudi na kombe lazima tukutie adabu uwanja wa ndege au kwenye ofisi za TFF. Nadhani hujawahi kuonja BAKORA za Wazalendo wenye uchungu na nchi yao na waliochoka kusindikiza wenzao.
nyie acheni ubaguzi,sasa kama mmeifunga mara ya pili zanzibar ndio nini?UBABE TU NDIO MLOWEKA MBELE,HAMNA MPIRA WOWOTE,LAKINI hapa hakujaharibika kitu kwani ni sawa mechi hii kufanya mazoezi yote ni nchi moja,HAYA BURUNDI ISHAKUA VIBONDE KWA KUWA ZANZIBAR WAMEWAFUNGA,SASA WAKIKUFUNGENI KESHO Mtasema wamebebwa?BWANAEH SOTE SISI NI WAMOJA SIO.TANZANIA IDUMU NA TIMU ZOTE ZIENDE MBELE MSITUBAGUE SIASA ZA MUUNGANO ZIONDOENI KWENYE MIPIRA.IKISHINDA ZANZIBAR AU BARA TUSHANGIRIE PAMOJA
ReplyDeleteKama US Blogger atatandikwa kwa nini Mashaka alikimbia mdahalo?
ReplyDeleteMichuzi hapo umechemsha mie nilijuwa ni Blog ya jamii sasa Juzi tumefungwa na Uganda hatujaweka leo jirani zetu tumewafunga mnaweka basi ungerudisha juzi tumepigwa na tuwape nafasi Jamaa zetu pembeni walishinda 4-0. YEMEN basi nao tulipigwa 2-1 uliweka?. Ndosi. Maximo atolewe bwana.
ReplyDeleteVp nchi moja ina peleka timu mbili za Taifa?
ReplyDeleteHii blogu inaelekea aipendi kufungwa? Starz ikifungwa ham2pi habari, ikishindika kelele kibao mpaka wa2 kulala 2nashindwa. 2pende mpira na 2we Wazalendo 2kifungwa. Kwani umesahau wahenga walivyosema asiekubali kushindwa sio mshindani au wananpopigana wawili basi mmoja ushindwa, kwaiyo 2kifungwaga uwe una2pa mistari ili 2jue timu ye2 imefanyaje. Wengine 2naishi mabonge maporomoko hata mbili saba saba se2 azinasi vizuri, uwe una2pa mistari kaka Michu, kufungwa ni kawaida. Au nyinyi YANGA? Maana Yanga hawapendi kufungwa
ReplyDeleteUNASHANGAA NCHI MOJA INAPELEKA TIMU MBILI ZA TAIFA NENDA UINGEREZA UKASHANGAE KUNA ENGLAND,NORTH IRELAN NA SCOTLAND NA WOTE WANACHEZA KOMBE LA DUNIA
ReplyDelete