Mdau Dominic Mosha na mai waifu wake Deborah Sumari baada ya kumeremeta katika Kanisa la St. Mary's Catholic Church Modeco mjini Morogoro na kabla ya kwenda kwenye mnuso wao ulioandaliwa Magadu Officers' Club.

Dominic na Deborah wanameremeta
maharusi na wazazi
maharusi na wapambe wao, ikiwa ni pamoja na Men in Black

Dominic akimwimbia Deborah wimbo wa Elvis Presley 'I cant help falling in love with you'

I-ringi moja la nguvu lilipigwa wakati wa mnuso huo....






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Ee bwana ee, hilo limduara hapo ni mambo ya ... motere, tereterete, moteree ... Aisee kama ningekuwepo vile.

    Maharusi mmependeza mashallah.

    ReplyDelete
  2. Daaah Kaka Michuzi maharusi wamependeza. Nawapongeza sana.Naipongeza pia hii glob kwa kutupa habari hasa wadau tulio mbali na nyumbani. Hawa ni wadau wangu wa long time. Nilikata nao skuli hapo Mlimani na nawatakia kila la heri.Huyu jamaa tulikuwa tunamwita Engineer "Domi Bonge" sasa sijui baada ya kurasimisha hili tukio lake tuendelee kumwita Domi Bonge au tufanyaje.
    Nawapongeza sana kwa kweli wametulia.
    Mdau wa Karibu

    ReplyDelete
  3. maharusi mmependeza sana. hii nilazima harusi ya kichaga.

    ReplyDelete
  4. DUH WAMPENDEZA KWELI MZEE DOMI ANAENDA KULA TUNDA CHANGA KWANI HATA ZIWA HALIJAANGUKA, BIBI HARUSI WALA HAITAJI JEKI (SIDIRIA) KULIINUA ZIWA LAKE, HONGERA SANA MDAU DOMI KILA LA KHERI KATIKA NDOA YAKO.

    ReplyDelete
  5. Bro Mithupu, kwanza nakupa pongezi kwa kutupa habari za home... Pili kwa huyo Mhandisi alofunga pingu Domi, wapi Patoo au yeye ashajitwisha kimya kimya? Aisee hongera sana....

    ReplyDelete
  6. haya sasa nyie mliekuwa mnatusumbua na snow snow zenu, mnaona kitu kilivyomwagika kwa mbali kule kwenye hii milima ya ulugulu?? tazama vizuri utaona jinsi barafu zilivyomwagika milimani kule, global warming dunia nzima sio huko tu. snow lilimwagika la nguvu sana hapa moro juzi kati hapa.

    ReplyDelete
  7. Hongera sana Kaka.. Maisha mema marefu yatawale nyumba yenu.

    Mdau Japan.

    ReplyDelete
  8. BI- MTEMBEZIDecember 30, 2009

    JAMANI MBONA WENGINE WANAJISHAUA SANA, YULE CHIZI-MLUPO WA DUBAI MWENYE BULOGU NA MZUNGU KOKO ANAJIDAI HETI ARUSHI YAKE ILIKUWA NZURI KULIKO ZOTE TANZANIA, WAPI HII HARUSI NI KALI KULIKO YAKE ABISHE

    ReplyDelete
  9. Oyaah Dominic hongera sana kijana. Mzee nakumbuka Kiunga tulikuwa tunakuita ""Energizer Never Say Die"". Hongera sana kaka harusi yako imependeza sana. halafu hicho kifaa kaka itabidi ununue bunduki kama huna maana!! Powa Bro nakutakia maisha mema kaka. Mdau mwenzio toka enzi za Kiunga..

    ReplyDelete
  10. kaka Domy...,Ebwana hongera sana..,kwanza mmependeza Mno..,karibu Tanga mjiachie Tanga Beach Resort www.tangabeachresort.com ,ninawatakia maisha Mema na heri ya Mwaka Mpya

    ReplyDelete
  11. Hongereni sana
    Domi & Deborah mmependeza sana tena sana.
    Nawatakia kila la kheri katika ndoa yenu.

    -silmal

    ReplyDelete
  12. maharusi mmependezaaaa,wishin u a happy maried lyf!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Teheheheheh!
    Domi sikujua kuwa hata katika fani ya kuimba umo, lakini mi naamini ni Deborah syndrome wewe mwenye kuimba ngumu sanaa, Big up mpoli poli! I missed it anyway!!!! and may God bless u all!
    From The Netherlands!!

    ReplyDelete
  14. Hongera kaka Domi, Mungu awajaalie katika ndoa yenu mzae matunda mema.
    nimimi Mchamahago

    ReplyDelete
  15. Kaka Domi, Hongera sana kudadeki, karibu kwenye chama cha wanaume. mwambie Gwakisa Mwakyusa nae aoe.
    by Mwakalebela

    ReplyDelete
  16. Hongereni sana maharusi.hiyo ngoma ni ya kichaga maana wao ndio lazima washikane mikono wakati wanacheza kwa kuwa wanaogopa kupigana sachi mifukoni,siunajua wachaga kwa pesa.safi sana.


    mdau scand...

    ReplyDelete
  17. Hongera Mhandisi Mosha.Mmependeza sana.

    ReplyDelete
  18. mdau hapo juu umenichekesha mm pia mchaga bwana inaonekana ww mtani,si kweli kuwa ni sababu ya kushikana mikono thou ni kweli wachaga wanapenda hela na wanajua kuitafuta pia!ni utamaduni tuu kama zilivyo kabila nyingine!Jamani maharusi mmependezaaaa hadi nimetamani na mm wedding!kila la heri!

    ReplyDelete
  19. Mumependeza na nawapa hongera.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  20. Hongera Dom!!!!!!!!!!!!!!!!!

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  21. Kaka Michuzi, Huyu Mhandisi ataleta mageuzi. Unajua wahandisi wengi waliokata shule hapo UDSM walikuwa wanaogopa hata kuongea na mademu. Huyu ni miongoni mwa wahandisi wajanja. Nampa FIVE...ametulia kwa kuvuta hii ""Chei Chei" ambayo nayo imetulia. Nadhani jamaa zake nao wataanza kuwa serious na kuweka vitu ndani ya nyumba kama huyu mdau...
    Big Five and best of LucK

    ReplyDelete
  22. HONGERENI ILA MIMI NIMEPAKUBALI SANA HAPO MAGADU OFFICERS CLUB,INANIBIDI AFTER NEW YEAR NITAKAPOKUWA LIKIZO NIJIVINJARI MAHALA HAPO.KAMA DESEMBA PAKO GREENISH HIVYO,JUNE C NDO ITAKUWA BALAA!!!

    ReplyDelete
  23. big up mhandisi domi unawakilisha chama Foe mpo wapi bonus,pongwe,mchachuzi,tmann (mzee wa ishu mbuyu),baba guna,raph,isaac,sapu proof,nyoka na masela wote wa foe.
    FoE 2004.

    ReplyDelete
  24. picha nzuri sana.

    ReplyDelete
  25. Wamependeza sana, Mungu awe nanyi katika maisha yenu mapya mliyoyaanza.

    ReplyDelete
  26. Kaka Domi aka Maprosoo umependeza babake,Domi ni moja ya kizazi pekee cha Tanga tech ambacho hakitasahaulika,nakumbuka enzi zile nipo O'Level domi yupo A'Level jamaa alihama vyumba vya A'Level na kuja kujichanganya na O'Level ili kuondoa gape lililokuwepo,Kimsingi Domi ni mujanja na ndio mana kapata Kifaa,Big up kijana,Tupo pamoja.
    加油!

    Nyoni

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...