WAFUNGWA 4,135 WASAMEHEWA
Rais Jakaya Kikwete amesamehe wafungwa 4,135 kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 48 ya Uhuru wa Tanzania Bara.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na kusainiwa na Laurence Masha, imeeleza wafungwa walionufaika na msamaha huo ni ambao wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano na ambao hadi jana walikuwa wametumikia robo ya vifungo vyao.
Masha kupitia taarifa hiyo, alisema msamaha huo, aliotoa rais kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya nchi na kwamba unawahusu pia wafungwa wenye ugonjwa wa ukimwi, Kifua Kikuu na saratani ambao hali zao siyo nzuri kiafya.
"Wafungwa hao, watathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au wilaya," alisema Masha kupitia taarifa hiyo.
Taarifa hiyo, imeelez kuwa msamaha huo, unaotolewa karibu kila mwaka Desemba 9, utawahusu pia wazee wenye umri wa miaka 70 au zaidi, ambao umri wao utathibitishwa na jopo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa mkoa au Wilya, wafungwa wa kike waliofungwa wakiwa wajawazito na walioingia gerezani na watoto wachanga.
Wafungwa wengine waliosamehewa ni wale wenye ulemavu wa mwili na akili, ambao ulemavu wao utathibitishwa na jipo la waganga chini ya uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa ya Wilaya.
Msamaha huo, hauwalengi wafungwa waliohukumiwa kunyongwa na kifungo cha maisha.
"Msamaha huo, pia hauwahusu wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, makosa ya rushwa, unyang'anyi wa kutumia silaha na wafungwa waliopatikana na hatia katika makosa ya kupatikana na risasi na silaha.
"Wafungwa wengine ambao hawamo katika msamaha huo ni waliohukumiwa kwa makosa ya kujamiiana chini ya 'Sexual Offences Special Provisions Act, 1998 ambao walifanya makosa dhidi ya watoto kama vile kubaka, kunajisi na kulawiti," ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Taarifa imefafanua kuwa msamaha huo wa rais hauwahusu wafungwa waliohukumiwa kwa makosa ya wizi wa magari kwa kutumia silaha, waliowapa mimba wanafunzi wa shule za msingi.
Pia msamaha huo, hauwahusu wafungwa waliopatikana na hatia katika makosa yanayohusu uharibifu wa miundombinu, ikiwemo wizi wa nyaya za simu na umeme, njia za reli na transfoma na wafungwa ambao wanatumikia kifungo cha pili au zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo msamaha pia hauwahusu wafungwa waliowahi kupunguziwa kifugo kwa msamaha wa rais na bado wanaendelea kutumikia sehemu ya kifugo kilichobaki, wafungwa waliohukumiwa chini ya sheria ya bodi ya Parole ya mwaka 1994, sheria ya huduma kwa Jamii ya mwaka 2002, na wafungwa waliowahi kutoroka au kujaribu kutoroka chin ya ulinzi.
Pamoja na msamaha huo wa wafungwa rais Kikwete jana alikagua gwaride la vikosi vyote vya ulinzi na usalama katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambako sherehe hizo, zilifanyika.
Mbali na Gwaride hilo, vijana 1000 wa shule za msingi na sekondari kutoka Tanzania na Zanzibar, nao walionyesha umahiri wao kwa kujikusanya na kutengeneza neno la 'Uhuru wa miaka 48'.
Home
Unlabelled
JK ateta na simba wa vita
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Ahsante Michuzi kwa kutuletea habari hizi. Mzee Kawawa anaonekana bado ananguvu kabisa. Lakini ndiyo hasikiki kabisa katika mambo ya siasa siku hizi ameeamua kutumia vizuri pension yake.
ReplyDeleteHi!Michuzi asante,Simba wa Vita bado ngangari kinoma,
ReplyDeleteMazungumzo ya JK na Mzee Kawawa huenda yalienda hivi?
ReplyDeleteJK: Umewasikia kina Butiku, Warioba na Qaresi wanavyonisema vibaya?
Kawawa: Achana nao hao. Siku zote wamekuwa wasumbufu. Wewe weka mkazo kwenye KILIMO KWANZA wananchi wetu wapate chakula cha kutosha na usiwasikilize hao wapu...vu.
JK: Ndio mzee hicho ndo kinanipeleka sehemu nyingi duniani kukamilisha mipango hii ya KILIMO KWANZA. Wao wazungumze tu lakini mimi nakuhakikishia najitahidi kuleta maisha bora kwa kila mtanzania.
Kawawa: Hata mimi naona unajitahidi sana. Watasemaa lakini watachoka. Wewe weka mipango ya maendeleo sana.
JK: Asante mzee. Basi kabla hujaondoka nitakuona.
Kawawa: Asante mheshimiwa karibu kwetu KIJIJINI, japo siku hizi hakuna maji na umeme sio wa uhakika sana.
Mambo vipi kaka Michuzi,
ReplyDeleteNahisi hii picha iko chini ya viwango na ni ya pili kuiona week hii, nyengine ni ile ya JK aliopiga na Jenerali Mwamunyange. Huyo aliekupatia ni wazi bado hajui kutumia manual settings za kwenye camera yake vizuri, au kama imekuwa edited basi contrast imekuwa nyingi mno. Siku hizi digital cameras zina computer mahiri sana zinaweza kupiga picha nzuri sana bila utalamu. Washauri wadau ambao hawajabobewa kwenye upigaji picha wakiona picha zao zinatoka vibaya basi waweke auto mode ili camera iamue yenyewe settings nzuri.
Nawasilisha.
Mimi nahisi mambo yalikwenda kama inavyoonekana katika picha:
ReplyDeleteJK - Mzee Simba wa Nyika Shikamoo
Simba wa Nyika: Marahaba
JK: Mzee kichwa kinaniuma kwa mambo mengi mno, hasa hili la "mafisadi" - ambalo nimelikalia kimya. Sasa wengi waliopo katika kundi la washtakiwa eidha nimekuwa nao au ni marafiki zangu wa karibu. Nitafanyaje?
Simba wa Nyika: Wewe umeifikisha nchi pabaya. Baba wa Taifa akiamka kweli atajiuliza ilikuwaje uwe madarakani wakati alikuwa na wasiwasi na wewe wakati uleeeee!! Ninapenda kukuonya kwamba, hakuna cha kilimo kwanza wala umeme kwanza, fanya juu chini uwashughulikie hao watu kabla 2010 kwani ifikapo mwakani hujafanya chochote, kweli unaweza usirudi.
JK: Mzee Simba wa Nyika nimeyasikia na nitayafanyia kazi. Lakini nitawaahidi watu kwamba nitakuja na Nguvu Mpya Zaidi, Ari Mpya Zaidi na Watu watapata Imani Mpya ya Kunirudisha, au unaonaje? Na zaidi nina mpango kamambe wa kupangua kikosi changu cha anga (sio mwavuli), na hivyo niwe na sura za ujana kwenye safu yangu. Si unajua miaka hii ni vijana wengi zaidi wanaenda kwenye "booth" kurudisha viongozi?
Mzee wa Simba: JK nakutakia kila la heri ya sikukuu, lakini nchi imefikia pabaya kijana wangu. Sisi wakongwe tulipopigania uhuru hatukujua kwamba tunakuja kufikia hapa. Lakini tuombe Mungu kunakucha kunakutwa - na amani bado tunayo Tanzania yetu njema
nimefurahi sana kuona maongezi ya JK (Jakaya Kiwete) na RK (Rashid Kawawa) au Simba wa Nyika. Kwa kweli inasikitisha kuona kwamba hayati mwalimu JK (Julius Nyerere) na wengine waliokuwa wakisema vijana ndio viongozi wa kesho - tunawaona wanavyoKULA Nchi yetu!! Ubinafsi utaimaliza Tanzania Yetu Njema. Wananchi wakiamka tu, sijui hali itakuwaje. Viongozi wetu wasichezee baloon, inaweza kupasuka!!! Na kwa hili ninawaomba waangalie kwamba wananchi wakifikia mahali "watapasuka" na nchi haitakuwa mahala pazuri.!!!
ReplyDeleteNilikua sijui kwamba kuna Tanzania na zanzibar
ReplyDelete