Nguza Viking a.k.a Babu Seya (kulia) na
wanawe watatu wakiwa kizimbani


Mwanamuziki Nguza Vikingi, ambaye anatumikia kifungo cha maisha baada ya kukutwa na hatia ya kulawiti na kubaka watoto 10, amedai kuwa hukumu kesi hiyo dhidi yake ilikuwa ni kisasi cha mpenzi wake aliyemuapia kulipiza kisasi, baada ya kuachana naye.

Hayo yalijulikana leo katika Mahakama ya Rufaa Tanzania, wakati mahakama hiyo ilipokuwa ikisikiliza rufani ya mwanamuziki huyo na watoto wake, waliopinga kuwa wakipinga hukumu hiyo ya kifungo cha maisha, iliyotolewa na Mahakama ya HAKIMU Mkazi Kisutu.

Mbali na hilo imedaiwa kuwa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Addy Lyamuya alitoa hukumu kwa mwanamziki huyo pamoja na watoto wake kwa kutumia mawazo yake binafsi.

Katika rufani hiyo, Nguza (babu Seya) pamoja na watoto wake - Papi Ngunza, Nguza Mbangu na Francis Nguza - wameiomba mahakama hiyo, kupitia mwenendo mzima wa ushahidi uliopelekea wao kutiwa hatiani na kusababisha kuhukumiwa kifungo hicho.

Wakili Mabere Marando ambaye anawatetea washitakiwa hao, aliwasilisha hoja hizo mbele ya Jopo la Majaji watatu lililokuwa likiongozwa na Nathalia Kimaro pamoja na wenzake ambao ni Jaji Mbarouk Salim Mbarouk na Jaji Salum Massati.

Marando alidai kuwa Babu Seya alikuwa na mpenzi wake aliyemtaja kwa jina la Farida ambaye mara baada ya kuachana alimuambia kuwa atamkomesha ambapo alidai kuwa kunauwezekano kesi hiyo ikawa ni kisasi cha mwanamke huyo ambaye alitoa vitisho hivyo.

Aliendelea kudai kuwa kunauwezekano wa Farida kuwafundisha watoto hao wanaodaiwa kubakwa, kusema uongo Mahakamani ili kuweza kumfunga Babu Sey na wanawe kama kisasi alichodai kumlipia.

Awali Marando alidai Mahakamani hapo kuwa upande wa utetezi unaondoa sababu za kutaka rufani hizo ambazo ni sababu ya 1,2,3,5,6,7,8,11,14 na 15 ambapo alidai kuwa katika rufani hiyo wataanza na sababu namba tisa kutokana na misingi ya kisheria.

Alidai kuwa sababu hiyo inaeleza maelezo ya anayeitwa Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi ambapo alidai kuwa mujibu wa sheria za motto kutoa ushahidi Hakimu ananatakiwa kumuhoji kabla ya kutoa ushahidi wake ili aweze kuona kama motto anauelewa gani juu ya kiapo cha ushahidi.

Marando alidai kuwa katika rufani ya awali katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam, nchini ya Jaji Thomas Mihayo alisema kuwa utaratibu uliokuwa umetumiwa na hakimu aliyekuwa ametoa hukumu hiyo ilikuwa na makosa kutokana na watoto ambao walitoa ushahidi kutohojiwa kabla ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa mahojiano ya awali na mtoto anayetoa ushahidi ni ili kupata maamuzi na kujua kama mtoto anajua maana ya kiapo ambapo mahojiano hayo baina ya hakimu na mtoto yanatakiwa kuhojiwa.

“Kwa kutozingatia mambo hayo ushahidi ambao utakuwa umetolewa na mtoto huyo utakuwa batili na hauna maana yoyote,” alidai Marando.

Aliongeza kuwa muelekeo wa Jaji Mihayo aliyesikiliza rufani hiyo kwa mara ya kwanza haukuwa mzuri kutokana na sheria mbalimbali alizozitumia kugongana ambapo alidai kuwa kutokana na hali hiyo Jaji huyo alifanya kosa kisheria.

Wakili huyo alidai kuwa mashahidi 10 kati ya tisa wa upande wa Jamuhuri ambao walitoa ushahidi wao hawakuapishwa wala kuangalia uwezo wao kama wanaelewa maana ya kiapo.

Pia alidai kuwa katika rufani iliyosikilizwa na Jaji Mihayo alisema kuwa hakimu aliyetoa hukumu hiyo kwakuangalia ushahidi wa pande mbili ambapo alidai kuwa Jaji huyo alikosea kwakua ushahidi wa utetezi haukuangaliwa vyema.

“ Katika nyaraka rejea zilizotumiwa na hakimu aliongeza mawazo yake binafsi kutokana na kupingana na maelezo ya mashahidi, katika ukurasa wa 532 mstari wa saba katika hukumu hii, hakimu anapingana na shahidi aliyejitambulisha kwa jina la Lubaba ambaye mama yake ni Mzaramo na baba yake Mkongo.

“Lakini katika maelezo ya hakimu anaonyesha kijana huyo ni Mzaramo wakati si kweli, hiyo yote inaonyesha jinsi gani hakimu alivyokuwa akiweka mawazo yake binafsi,” alidai Marando.

Marando alidai kuwa kwa muda wa miaka 30 ambayo amefanya kazi ya uwakili hajawahi kuona hukumu ya namna hiyo ambayo hukumu inatolewa kwa kufuata mawazo ya hakimu badala ya ushahidi wa pande mbili.

Aliendelea kudai kuwa hakuna ushahidi ambao ulionesha mshitakiwa wa pili alibaka au kulawiti kabla au baada ya kufanya safari zake za kimuziki katika mikoa ya Mwanza na Arusha ambapo alisema kuwa hakimu aliweza kuweka mawazo yake binafsi ili kuwezesha mshitakiwa huyo kuwa na hatia ya kumfunga gerezani.

“Mbali na hayo mshitakiw ahuyo wa pili alidai kuwa kati ya Agosti na Septemba alikuwa akirekodi albamu yake na mwanamuziki Lady Jee dee , lakini badala ya hakimu kuandika maelezo hayo na matokeo yake aliandika ‘So what?’,” alidai wakili huyo.


Alidai kuwa hakimu huyo hakuandika maelezo ya mashahidi wa upande wa utetezi na badala yake aliandika idadi ya mashahidi ambao walifika kutoa ushahidi wa upande wa utetezi ambapo wakili huyo alihoji hali hiyo iliyofanywa na hakimu huyo.


Wakili huyo alidai kuwa kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na watoto ambao wanadaiwakufanywa vitendo vya ubakaji na kulawitia walitaja baadhi ya watu ambao hawakuweza kuitwa na upande wa mashitaka kufika Mahakamani kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

Alidai kuwa watoto hao walimtaja Mangi ambaye anauza duka ambalo lipo karibu na nyumbani kwa Babu Seya ambaye anadaiwa kuona watoto hao wakati wakiingia na kuchukuliwa na mshitakiwa huyo wa kwanza na pia anadaiwa kusikia wakati watoto hao wakilia wakati wakifanyiwa vitendo hivyo.

Pia mbali na Mangi pia ilidai kuwa watoto hao walimtaja dada na bibi ambao walikuwa wakikutwa katika nyumba hiyo ambapo Marando alihoji kutokuitwa kwa watu hao kufika kutoa ushahidi ili kuweza kuthibitisha madai hayo.

“Kitu cha kushangaza zaidi ni madai ambayo yalitolewa kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo tarehe 11 Oktoba wakati siku hiyo ilikuwa ni Jumamosi na pia mshitakiwa wa kwanza alikuwa amekamatwa na katika maelezo ya watoto hao inadaiwa kuwa walikuwa wakifanyiwa vitendo hivyo wakati wakitoka shule.

“Je siku hiyo ya jumamosi mbona haikutajwa wakati maelezi yanadai kuwa walifanyiwa siku za katikati ya wiki, Jamuhuri ingeweza kufanya uchunguzi ili kuweza kubaini mtu ambaye aliweza kuwabaka watoto hao na si kama jinsi inavyodaiwa,” alidai.

Alidai kuwa baadhi ya shahidi mtoto alishindwa kumtambua Babu Seya na mwingine alikanusha kubakwa na mshitakiwa wa 3 na 4 ambapo alidai kuwa hakimu aliandika kuwa kutokana na watoto hao kujuana alihisi kuwa ni lazima watoto hao walibakwa licha ya watoto hao kutothibitisha.

Aliongeza kuwa katika kielelezo kilichotolewa na Hospitali ya Mwananyamala kilidai kuwa mtoto mmoja aliambukiza Kisonono ambapo washitakiwa hao kupitia mawakili wao waliomba kwenda kuwapima washitakiwa hao ili kuweza kuona ni mshitakiwa yupi aliyekuwa amemuambukiza ugonjwa huo wa zinaa.

Alidai kuwa licha ya ombi hilo upande wa Jamuhuri ulikataa kuwapeleka washitakiwa hospitali kwa ajili ya kuweza kuwapima ugonjwa huo ambapo alidai kuwa mtoto mwingine katika maelezo yake alidai kuwa alilazimishwa na Babu Seya kumkamua vipele vilivyokuwa katika sehemu zake za siri vilivyokuwa vikitoa usaha na maji.

Hata hivyo wakili huyo alidai kuwa upande wa Jamuhuri haukuwa tayari kuwafikisha watuhumiwa hao katika kituo cha afya ili kuweza kuthibitisha madai hayo yaliyokuwa yamedaiwa.

“Mshitakiwa wa nne ambaye alikuwa ni mwanafunzi naye pia anadaiw akushiriki katika vitendo hivyo lakini upande wa Jamuhuri haukuwahi kumuita Mkuu wa shule ya sekondari ya Mbezi ambayo alikuwa anasoma ili kuweza kuthibitisha kama mwanafunzi wake alikuwa hafiki shule.

“Lakini mambo yote hayo hayakuweza kufanywa wakati kila mmoja anaelewa kuwa muda ambao anatoka mwanafunzi huyo watoto hao wanakuwa tayari hawapo lakini hazikuweza kufanyika jitihada mbalimbali,” alidai.

Alidai kuwa katika jarada la kesi hiyo, mashitaka mawili yalikuwa yakiingiliana ambapo shitaka moja lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo hivyo Oktoba ambapo shitaka jingine lilidai kuwa watoto hao walifanyiwa vitendo vinvyo kwanzia April hadi Oktoba.

Alidai kuwa katika maelezo ya mashahidi hakuna shahidi aliyedai kuwa alifanyiwa vitendo hivyo kati ya Aprili hadi Julai na kwamba kwa kipindi hicho ambacho kimetajwa mshitakiwa wa 2 na 3 walikuwa wakishinda katika kambi yao ya mazoezi ya FM Academy.

Naye wakili wa upande wa Jamuhuri uliokuwa ukiongozwa na Justuce Mlokozi alikili watoto hao kutorekodiwa na pia kutofanyiwa kiapo ambapo alidai kuwa Mahakama iliegemea ushahidi wa Jamuhuri na kwamba hata kama kulikuwa na makosa madogomadogo yanaweza kutibika chini ya sheria namba 388 ya mwenendo wa mashahidi.

Mlokozi alidai kuwa waliamua kuwaleta watoto katika ushahidi huo kutokana na wao ndio walikuwa walengwa zaidi na wakati wakifanyiwa kitendo hicho hakuna watu wengine waliokuwa wakiona.

Aliendelea kudai kuwa kuhusu kutofautiana kwa miezi katika jarada la kesi hiyo alidai kuwa hakukuw ana tarehe maalum ambayo watoto hao wlaifanyiwa vitendo hivyo na kwamba walikuwa wakifanyiwa kwa nyakati tofauti.

Aliongeza kuwa kuhusu kusafiri kwa mshitakiwa wa 2 alidai kuwa hiyo si hoja kuwa hajatenda kosa ambapo alidai kuwa anaweza kuwafanyia kipindi ambacho anakuwa hapa jijini Dar es Salaam na kudai kuwa kuhusu Farida haiwezekani kuwafundisha watoto wote kusema uongo kama inavyodaiwa na utetezi.

Akihairisha kesi hiyo Jaji Kimaro, alisema kuwa Mahakama itatoa tarehe ya hukumu ya rufani hiyo baada ya kusoma maelezo yote yaliyotolewa na pande hizo mbili ikiwa ni pamoja na nyaraka rejea zilizotolewa.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa umati mkubwa watu ulimiminika Mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza rufani hiyo ambapo watu walijaa katika chumba cha Mahakama na katika naeneo ya Mahakama hiyo.

Mara baada ya kuhairishwa kwa kesi hiyo Marando alionekana kuwa mfalme na mkombozi kutokana na maelezo ambayo aliweza kuyatoa jambo ambalo liliwafanya mashabiki wa wanamziki hao kumita Simba wa Yuda Simba wa Yuda huku wakimpigia makofi.

Licha ya hayo wakati rufani hiyo ikiendelea hali isiyo ya kawaida watu walijikuta wakipiga makofi wakati ndani ya chumba hicho kilichokuwa kikitumiwa wakati wa kusikiliza rufani hiyo.

Babu seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha mwaka 2004, baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa Jamuhuri dhidi ya kesi ya kudhalilisha kijinsia watoto wa kike.

Kesi hiyo iliyovuma kwa wakati huo ambayo ilikuwa ikisikilizwa na kutolewa hukumu na Hakimu Mkazi Addy Lyamuya ambaye amestaafu hivi karibuni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 40 mpaka sasa

  1. washindwi (losers) mara nyingi hufanya kila liwezekanalo kuwaangusha washindi (winners) bila kujali.

    Hata kama akina seya hawana hatiya wanaweza kuozea magereza.

    Nchi isiyojali haki ya sheria ni mbaya mno.

    ReplyDelete
  2. I dont know why but toka hii kesi inaanza moyo wangu unakataa kabisa kuamini kama kweli hawa watu wanahatia, ningekuwa ninauwezo ningeweza kuwasaidia, Lakini Mungu yupo na ndo anaejua ukweli, na Mungu atawasaidia, my prayers are with them.

    ReplyDelete
  3. kila la kheri wikili marando dah hii nchi haina haki kabisa dah inaniuma sana inshaallah m/mungu atawasaidia amin kwako hakuna linaloshindikana

    ReplyDelete
  4. kumbe hukumu ilitolewa kwa kuzingatia maneno ya mdomoni na si kisayansi???

    jamhuri aibu nyingine hii, fukuza mawakili wote hao wa serikali wameshindwa kazi.. wao kila kesi wanakosea kufungua jalada

    ReplyDelete
  5. Hao hawana hatia kabisa wanawaonea mimi roho inaniuma sana na inshaalah aliewasingizia hivyo hata funga jicho bila na yeye kumkuta kwani mungu analipa hapahapa duniani na akhera kunabakia hesabu tuuuuuuuuuuuu kila ile sekunde moja wanayoteseka waja hao jukumu analibebe huyo mtu na kila anaeshirikiana na huyo mwenye roho ya kinyama kwa hilo tupo hapa tutaona kama kweli na yeye limemfika hata kma na cheo gani au ana wadhifa gani serikalini litamfika tu.dua zangu zooooooooooote kwenu babu sea mungu atawanusuru kwa hilo na jingine aminnnnnnnnnnnnnnnnn.

    ReplyDelete
  6. WAFUKUZWE NA KUTIWA NDANI HAO MAWAKILI.KWA NINI HAWAFUATI HAKI ,LABDA NI VIHIYO NINI?.TUWAFUATILIE ,INAWEZEKANA WANA MAKOSO YA KUFOJI VYETI.HUWEZI KUWAHUKUMU HAO JAMAA KWA NJIA HIYO TU YA MDOMO.VYOMBO VYETU VYA SHERIA VINABIDI VIJIFUNZE KUTOKA NJE.KWA MFANO KUNA JAMAA MMOJA MMAREKANI ALISEMA KUWA ALIMUUA MTOTO MDOGO,AMBAYE ALIPOTEA.FBI WALIMSOMA NA BAADAYE WAKASEMA SIO WEWE WALIMKANA.LAKINI KAMA KESI HIYO INGEKUWA HAPA NYUMBANI UMEFUNGWA ,KWANI ETI UMESEMA MWENYEWE.KUNA WATU NI MATAHIRA HAPA ,LAKINI UKIWAONA WANATEMBEA.HATA MIMI SIKUAMINI KAMA KWELI HII KESI NI KWELI.SASA ILI KUSITOKEE TENA.INATAKIWA HAO WALIOHUSIKA NAO SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE.NA IWE FUNDISHO KWA WALE WANYE TABIA HIYO.

    ReplyDelete
  7. kaza buti marando hii kesi itakutoa kimasomaso watainamana na kuona haya utakaposhinda haiingii akilini kabisa kwa maamuzi yao ya upendeleo but eeeeeeeeh mola tenda miujiza yako wape haki zao waja wako Nguza na wanawe

    ReplyDelete
  8. Nilipata kumuuliza rafiki yangu mwanamuziki mkongwe toka Kongo kuhusu kesi hii. Siku zote nilikuwa nafikiri namfahamu yule mwanamuziki na kwamba ni rafiki yangu. Siku hiyo ndipo nilipojua kwamba simjui lakini ni rafiki yangu.

    Baada ya kumuuliza hilo swali yule jamaa yangu alinyamaza kwa muda ukunjufu wa sura na mwili wake ukabadilika kabisa. Halafu akaniangalia machoni, macho yake yaligeuka kuwa mekundu sana na kuniambia kwa sauti ya chini sana ambayo sijawahi kumsikia nayo hata siku moja "..Hii kesi anayejua ukweli ni wao na Mungu.. ..Lakini hii kesi haiko sawasawa.. ..Mimi namjua Nguza na wewe unamjua Nguza.. ..Sijui kama wewe ulikuwa unajua kama anaweza kuwa na mambo ya kishetani kama haya?.. ..Mimi sijui, wewe unajua?.." Baada ya kuniambia hivyo akanyamaza akawaananiangalia usoni nikashindwa kumjibu kwa kuduwaa.

    Orchestra Marquiz Du Zaire Company Limited (OMACO) ni bendi pekee ambayo iliwahi kuwa kampuni inayojitegemea; Ilikuwa ni bendi ya muziki wa dansi iliyomiliki vyombo vyake yenyewe, wanamuziki walikuwa wanahisa wa kampuni, walimiliki wa ukumbi wa dansi, walikuwa wakulima wamiliki wa mashamba, walimiliki majumba ikiwemo hiyo nyumba aliyokuwa akiishi Mzee Nguza kabla ya kupatwa msukosuko huu, pia walikuwa wamiliki wa magari kadhaa. Na ndiyo bendi iliyopiga muziki wa kuongoza kwaya za shule za msingi za Dar es Salaam siku ya kuzaliwa kwa chama kipya 5.2.77 pale Uwanja wa Taifa. Mimi na marafiki zangu tuliimba ile kwaya na mmoja waongozaji wa kwaya aliyeimba na Marquiz tulikuwa naye darasa moja shuleni.

    Sasa hivi ninavyoandika maoni haya bado nina nia kubwa sana ya kumuomba Mzee Jenerali Ulimwengu tufanye utafiti (TV Documentary research) na wanaMarquiz waliohai ili tuweze kujua nini kilichoifika OMACO hadi ikafa.

    ReplyDelete
  9. Mashoga woote walioko bongo wametokana na tabia za mijitu mizima kuwafanya vitu vibaya watoto wa kiume utotoni.

    Hakuna binti anayemaliza darasa la saba akiwa bikra kutokana na walimu mashuleni kuwafanyia unyama.

    Ona wake zetu makazini wanavyofanyiwa na mabosi.
    Ona ma-housegirls wanavyolambwa na baba mwenye nyumba.
    Ona watoto wadogo kama hao walivyofanyia.
    Zingatieni pia athari za kisaikolojia wanazopata waathirika

    Ngonjera za kisheria na mawakili wazuri wapo ila kama wamefanya uchafu kama huo iwe fundisho kwa wengine

    ReplyDelete
  10. I will cry and stand for every soul which has been victimized by those gruesome and evil people.
    Abused kids (Boys & girls), our wives victimised by their ugly bosses, students by their prudent teachers and all that

    Teach them a reason if they did it

    ReplyDelete
  11. KWA KWELI HII KESI IMEGUSA WATU WENGI SANA HAKIKA HUYO WAKILI ANAEWATETEA NI MUNGU AMEMTUMA NI MALAIKA WAO MKOMBOZI LKN MSIJALI KWANI PAULO NA SILA WALIOMBA MILANGO YA GEREZA IKAFUNGUKA NAMI NAAMINI MUNGU ATAWAFUNGULIA HAKIKA NASALI KILA SIKU MIUJIZA ITOKEE MUWE HURU KWANI HII KESI NI CHUKI BINAFISI HAINA UKWELI. MFANO KUNA KIPENGELE NIMESOMA ATI ALIMWOMBA MTOTO AMTUMBUE KIUPELE MIE NI MWANAMKE LKN NAJUA MAUMIVU YA ZINAA YANAVYOUMA JE ANGEFANYAJE HICHO KITENDO KWA NINI TUSIMWOGOPE MUNGU HAKIKA HIZI NI SIKU ZA MWISHO. PIA NDUGU ZANGUNI NAAMINI NI WENGI WAKO KTK MAOMBI NA MUNGU ATASIKIA SALA ZETU NA MTAKUWA HURU TU HAKUNA JAMBO LILO GUM KWA MUUMBA WETU.MUNGU AWE NANYI DAIMA

    ReplyDelete
  12. Mungu ni wa haki na kweli. Haki yenu kama kweli ipo mtaipata tu..

    ReplyDelete
  13. KAMA WAPO WATOTO WALIOFANYIWA HAYO BASI NAO PIA WAENDE MAHAKAMANI KUFUNGUA KESI BINAFSI YA MADAI DHIDI YA AKINA NGUZA ILI KUTHIBITISHA YALIYOTOKEA.

    ReplyDelete
  14. Ndugu zangu wabongo, tuache longolongo na ushabiki na kutoa hitimisho kwamba huyu kaonewa au haki haikutendeka, ili hali kesi bado iko mahakamani. Kama kuna mtu anadhani kuna aliyeonewa na hakutendewa haki na anajua kwa undani maelezo ya kesi hii, basi aende mahakamani sasa, akatoe maelezo yake ili yawasaidie hao wanaodaiwa kuonewa. Lakini si sahihi kushabikia na kulalama mtandaoni wakati ukweli hamuufahamu bali anayejua ukweli wa yote haya ni hao watuhumiwa, waathirika na Mungu wao. Anachofanya Marando ni kutimiza wajibu wake kama wakili kama sehemu ya mchakato wa kesi nzima. Kesi ya Zombe iliwaacha midomo wazi watu wengi kwasababu ya ushabiki na longolongo nyingi za vijiweni mitaani kama hizi badala ya kuwaachia wenyewe wafanye kazi yao. Acheni longo kama hamna cha kusema nyamazeni ili sheria ichukue mkondo wake

    ReplyDelete
  15. UZURI NI KWAMBA WATU WOOOTE WALIO COOK HII SCANDAL WANAFAHAMIKA...... TIME WILL TELL....KESI YA KUSINGIZIWA KIFUNGA CHA MAISHA UFISADI................

    ReplyDelete
  16. Nakubaliana na Annony wa Fri Dec 04, 12:12:00 PM. Watanzania ni watu wa ajabu sana, yani mtu anabisha kitu sichokijua kabisa, ili mradi awe upande wa wengi.
    wadau mnaowatetewa kina Babu Seya mshawahi kwenda pale shuleni kufuatilia kujua kama issue hii ni kweli au uongo, maana am sure kitendo cha kulawiti watoto kumi hakiwezi kuwa siri, hao watoto wanajulikana kwa majina na sura.
    Mi nasubiri hao watoto wafikishe 18, niwape ukweli wa wazi wazi!
    Wanaosuggest fidia...ndio walewale wanaoshabikia vitu wasivyovijua, hukumu ina fidia ya fedha kwa watoto!

    ReplyDelete
  17. @ Mdau aliyepata kuuliza mwanamziki mkongwe wa kikongo kuhusu kesi hiyo....ushawahi kuuliza hao watoto waathirika kuhusu kesi hiyo? kumbuka mahakama imesikiliza pande zote...yani we umesikiliza upande mmoja tu na kuhukumu! Hufai kabisa!

    ReplyDelete
  18. sina la kusema zaidi ya hisia zangu zinaanza kuonesha ukweli niliokuwa nawaza, hawa wafungwa wameonewa sana,

    ReplyDelete
  19. Jiang Fri Dec 4, 12:50:00 PM

    Naomba utuonyesha ni wapi ambapo mdau aliyeeongea na mwanamuziki mkongwe wa Kikongo amehukumu?

    ReplyDelete
  20. we unayejiita jiang ndo kihiyo kabisa, me nimepata kuhudhuria mwenendo wa kesi hii katika mahakama ya rufani, na mimi ni wakili najua jinsi kesi ya kupika ilivyo, kesi hii imepikwa kabisa, hauwezi kusema mtoto kabakwa alafu ushahidi wa doctor uoneshe bikira imetoka wapi?

    haiwezekani mtoto wa miaka saba abakwe na kulawitiwa, alafu aulizwe kuhusiana na maumivi hasame hakusikia chochote kile,

    Sizani kama mtoto wa miaka 8 hanaweza kubakwa au kulawitiwa na kupoteza kumbukumbu za sura ya wabakaji wake.

    Msibishe vitu vilivyo wazi bwana!!soma vizuri stori hiyo alafu jaribu kutafuta waliofuatilia mwenendo kwa maelezo zaidi.

    ReplyDelete
  21. Tatizo malawyer mnajifanyaga mmesoma kuliko watu wengine...eti mi ni wakili, so what? mi mwandishi wa habari...I know everthing in town, sio vya mahakamani tu...najua nnachosema!
    Mdau anaonyesha kuwa upande wa Babu Seya...as ameonyesha mwanamuziki wa kikongo alivyosikitika na kuonyesha huzuni kubwa...hapo anatafuta public sympathy ili watu waamini anachosema huyo mwanamuziki wa kikongo...maana yake yeye ashakubali anachosema!

    ReplyDelete
  22. we mwandishi wa mtandao na blog au gazeti?ulishawahi kuhudhuria mahakamani hata siku moja?je vyuoni waandishi mnafundishwa sheria?hacha ubishi et tu kwa sababu unatetea hoja yako, kubali husikubali babu seya hana hatia bili ni miapngo tu, we inaingia akilini mtoto wa mika 5 abakwe zaidi ya mara tatu na watu tofauti tena kwa mara moja,na wazazi washindwe kugundua kwa haraka?

    ReplyDelete
  23. Jiang Fri Dec 04, 04:24:00 PM

    Umesema

    "I know everthing in town, sio vya mahakamani tu...najua nnachosema!"

    Kwa kusema hili ulilosema hapo umewakata midomo wote wanaokujibu. Wakirudi tena kukujibu watakuwa watu wajinga sana.

    Big up mkuu.

    ReplyDelete
  24. Anon aliyesema Fri dec 4, 12:11:00 AM Umeongea Point.

    Hili suhala watu wengi wanalirukia tu tuone wenyewe watasema nini? Hao kina Babu Seya. Watanzania tunarukia tu kwamba kigogo mara vile na hivi tusubiri Tuone ndio tutajuwa.


    Aliyesema Documentary pia ni vizuri ukifanya kwa manufaa yako watu watamuelewa vizuri ila sio ndio ufunuzi wake babu Seya.

    Mie Maoni yangu namuona kama hana kosa ila ndio hatuwezi kujuwa.

    Watanzania tusubirini ukweli kwenye mdomo wao wanasema nini sasa hivi ndio Kesi itafunguka kotekote pande mbili au tatu.

    Kama kaonewa mwenyezimungu atamsaidia na kama hajaonewa aendelee ndani mwenyezi pia ndio muhukumu wa mwisho. Pazi.

    ReplyDelete
  25. eeh baba mungu uliye juu wewe ni muweza wa yote. wewe unaujua ukweli wa jambo hili. na kesi ina miujiza pia, wabakwaji bado wako virgin, ugonjwa walioambukizwa waambukizaji waliomba wakapimwe mahakama ikakataa. mambo mengi yamejificha nyusoni mwetu lakini hayajajificha kwako. basi ukatende miujiza yako na watanzania waujue ukweli. kama wameonewa hawa watu basi baba ukawasaidie waweze kuondokana na mateso haya. ninaomba haya katika jina la yesu kristo mwanao. kila goti kwako litapigwa na wafitini watakuwa na mengi ya kujibu siku ya mwisho, mbele yako uliye muweza wa yote. WASAIDIE BABA WATOKE, NA SI HAWA TU HATA WALE WOTE WANAOTESEKA MAGEREZANI KWA KESI ZA KUBANDIKIZIWA UKAWASAIDIE NAO WATOKE.
    METHEW,NAMFUA.

    ReplyDelete
  26. Sidhani kama watu wanaweza kupika kesi na hukumu ya jinsi hii ikajitokeza, anaweza akajitokeza wakili wa kutetea wahusika, hata kama ana uchu kiasi gani na fedha. Binafsi sidhani kama huyo wakili ana 'reputation' yeyote ya kutetea wanyonge. Inasikitisha kuona kwamba watu hawajali kabisa maslahi ya watoto halafu mnamuomba Mungu kuwanusuru waliopatikana na hatia ya kunajisi watoto. Nani atatetea watoto?

    ReplyDelete
  27. wewe anon una uhakika gani kama kweli hao walifanya hicho kitendo? anaejua kama ni kweli au si kweli ni m/mungu na wahusika na si mwingine kwahiyo nyamaza usihukumu watu bila kujua, ila kwann kama kweli walifanya mahakama ilikataa kwenda kuwapima ili wajue nani mwenyewe kisonono? na kwann wasifanye uchunguzi wa haja any away tunataka kujua ukweli sio ubabaishaji ili kuonea wanyonge nyie mafisadi kwa ufisadi wenu mnaofanya mnauwa watanzania wangapi?

    ReplyDelete
  28. @ Annony aliyeuliza maswali haya: we mwandishi wa mtandao na blog au gazeti?ulishawahi kuhudhuria mahakamani hata siku moja?je vyuoni waandishi mnafundishwa sheria?

    Mimi ni mwandishi wa habari kamili, mtandao (http://dailynews.co.tz/) blog click jina langu utaona na gazeti (Daily News), sha hudhuria mahakamani si mara moja wala mara mbili, na kwa taarifa yako waandishi wanafundishwa vitu vingi kuliko unavyofikiria, including hiyo sheria yako!

    ila hizo zote ni nje ya hoja (na wewe ndio ulitake kwenda nje ya hoja, mi nakujibu tu!ukiwa wakili u have to stick to the issue in question, ndio mnaoshindwa kesi kila siku nyie!!!)

    tukirudi kwenye hoja ya msingi niliyosimamia tangu mwanzo, nani kati yenu alishawahi kwenda pale shuleni kutafuta ukweli?
    nani aklishawahi kuwatafuta hao watoto akawahoji akjiridhisha kuwa wanadanganya? au tunahukumu kwa kusikia story za mtaani ambazo hata hatujui zimeanzia wapi?
    muda muafaka ukifika mimi nitatafuta side ya wale watoto, hata kama ni miaka 5 toka leo, na ntawadhibitishia nani anasema ukweli kati yao.
    wazazi wangapi watoto wao anafanywa mashoga hawajui, wanakuja kugutuka mtoto keshaharibika, unashangaa hili la hawa?
    na hata kama mtu ana nia mbaya na Babu Seya, haihaji watoto 10, maana hapo jumlisha wazazi 20, hiyo siri utaicontain vipi?
    ukipata kijana mmoja wa miaka 17 tu anatosha kupanga nae mpango na ukamfunga huyo babu seya, y take the risk ya watoto wadogo na wazazi wao kibao?-does that make sense to you?

    ReplyDelete
  29. Hawa akina babu seya na wanawe watu wasiwaonee huruma kwami vip[imo vya madaktari vilishathibitisha ukweli wa kile kilichotokea ila Marando anajaribu kuudanganya umma kwamba Nguza alioonewa.

    Mimi mtoto wa dada yangu ni miongoni mwa watoto waliolawitiwa, kimsingi inasikitisha sana na zaidi ya yote nguza anasema kuwa ameonewa? naomba aseme ukweli kwani yeye ndiyo anaujua.

    Akumbuke jinsi alivyowalisha watoto wetu kinyesi walichokuwa wanakitoa wakati wanalawitiwa, ni mambo magumu sana ambayoi naamini hayafai kueleza ila mimi nimeumia sana na kutesena sana.

    Nguza huyu huyo ndiye alikuwa anawalambisha mbengu zake za kiume watoto wetu, hawa.

    Mama yake nguza anaujua ukweli na yeye alikuwa akiwashawishi watoto kuingia chumbani kwa bwabu seya ili kutengeza dawa ya mafanikio katika muiziki, huo ndiyo ukweli na wamehukumiwa kwa makosa waliyofanya na inatakiwa kuyajutia na kutambua kuwa ukifanya baya utalipwa baya na kwamba ukiua kwa upanga na wewe utakufa kwa upanga tu.


    watu wanasema haiwezekani mtu na watoto wake kubaka, hilo ni jambo linalowezekana bila shida kwa mana kama mtu anaweza kufanya mapenzi na mama yake au binti yake atashindwaje kufanya hivyo na wanawe.


    Tafadhali sana naomba watu wasiseme jambo wasilolijua kwa maana wanajipalia laana.


    Mimi nahakikisha kuwa siku akitoka nitamuondoa tuniani kwa njia yoyote ile kwani alichomfanyia mpwa wangu ni jambo baya na la kudhalilisha sana.

    ReplyDelete
  30. Sasa baada ya maoni ya Anony wa 10.04 watu endeleeni kuchonga. Mbona wote kimya? Mimi pia ni baba wa mtoto mmojawapo aliyefanyiwa hivyo na hamjui shida niipatayo mpaka leo kumlea mwanangu kisaikolojia ili awe confident tena na kuacha kuwachukia wanaume. Kwa kweli akitoka nitaifanya kazi ya justice mwenyewe kwa mikono yangu ili mwanangu awe huru!! Hongera mwandishi wa habari, unajua ukisemacho.

    ReplyDelete
  31. siku zote huwa nasimamia ukweli...sio kile watu wanachotaka niamiani...annony mwenye mpwa ameprove my point...haya mnaomuonea huruma babu seya semani sasa!au mnataka hadi watoto wenu wangefanyiwa hivyo ndio muamini ni ukweli????

    ReplyDelete
  32. Mlioathirika pole na naamini maneno yenu kwamba ndugu zenu walinyanyaswa.

    Tunataka utawala wa sheria na hatuamini majungu. Hivyo kama walifanya na ushahidi unaonesha walifanya wape mvua

    Mawakili wasitafute umaarufu wa bure kwakuwa kinachotokea ni huruma tu ya vigogo wenye mapenzi mema na kupindisha sheria bongo ili watolewe ni kama CCM kushinda uchaguzi-kafala kibao.

    Kuna wazazi nimewasikia walilia sana wakati wa kesi hiyo walipogundua waliyofanyiwa watoto zao

    Acheni unzabe-Nasali watoto zenu yawafike pia muone hw it pains

    ReplyDelete
  33. si kwamba wa2 wamenyamaza ni hivi wewe mwenye mtoto hapo na huyo mwenye mtoto wa dada yako;tutawaamini vipi kama mnasema ukweli kwani tunawaona nyie?what if mmeamua kudanganya..wanataka watu haki itendeke tu basi;kama wamebaka tutajua na kama wamesingiziwa tutajua pia;what i biliv ni kwamba siku zote ukweli utabaki pale pale hata kama baada ya miaka20.

    ReplyDelete
  34. anon 10:51 umeongea ukweli umtupu hapo hatutaki ubabaishaji sie tunataka haki itendeke ili watu tujue ukweli.

    ReplyDelete
  35. nchi hii haina haki hata kidogo.rais yuko wap?kwa mtazamo wangu wananchi tumeshaanza choka kwa uonevu wa kila siku.tutakapo anza tumia uamuzi tunaojua wenyewe nchi itkua haikaliki hii.mm naona kuna viongoz wasiopenda amani.ona uonevu huu.tumechoka.sooooooon kazi itaanza kama kbinda.

    ReplyDelete
  36. kuna watu wanataka tuamini kuwa kina babu seya kuachiwa ndo haki!! Kunaweza kukawa na matatizo kwenye mahakama zet lakini haimaanishi kila kinachoamuliwa sio haki. I believe hao wanaplalamika hawana watoto au wanafikiri hiyo haiwezi kuwapata watoto wao. Binafsi nawaonea huruma kina babu Seya lakini sitaki kuamini kuwa mahakimu na majaji wote waliofanya uamuzi wooote wamekosea. Hii kesi ina ushaidi wa kutosha hawa jamaa walifanya hicho kitendo. Na hicho kilichotokea ndo haki. sio kuwa haki ni kuachiwa

    ReplyDelete
  37. hiyo ndo haki. walifanya wameadhibiwa sio kuachiwa ndo haki tu

    ReplyDelete
  38. JAMANI MBONA HILI SUALA LA BABU SEYA NA WANAWE LINA SURA KADHAA ZA HABARI!! KUNA UVUMI ETI KIKWETE RAIS WA SASA WA TANZANIA WAKATI HUO ALIKUWA ANAGOMBEA MWANAMKE NA BABU SEYA. UVUMI MWINGINE ETI KIKWETE HUYO HUYO ANA DADA AMBAYE ALIACHIKA KWA MUMEWE KWA VILE ALIKUWA ANTEMBEA NA BABU SEYA. NA NAFIKIRI NDO SYMPATHY YOTE INAKOTOKA. MIMI NASEMA KAMA MAHAKAMA IMETENDA HAKI INAYOTAKIWA NA MUNGU HAWA WANGEONGEZEWA MIAKA MARADUFU. NA KAMA WANGEACHIWA KAMA MIMI NI MZAZI NINGEWACHARAZA NA MAPANGA HADI WAFE NA MIE NIFILIE MBALI MENDE HAWA WAHARIBU WATOTO. WAWAACHE WATOTO WAFIKIE MIAKA 18 AMBAPO WANAWEZA KUWA NA MAAMUZI YA MAISHA YAO. WASHENZI HAWA WAFILIE MBALI KAMA KWA HAKI YA MUNGU WALIWAFANYIA WATOTO VITENDO HIVYO VYA KIFIRAUNI. UMAARUFU WAO WA MUZIKI USIWE NDO KINGA.

    ReplyDelete
  39. Naona nchi yetu ingekuwa na sheri a za kama Indonesia kwamba ukishindwa Rufaa basi unaongezewa adhabu yako. kama ulishahukumiwa maisha ukashindwa kwenye rufaa adhabu yako itakuwa kunyongwa mapaka kufa nadhani baada ya kufuatilia hii kesi Babu Seya anapaswa kunyongwa...sishabikii mijitu mizima kuharibu maskini watoto watu!!

    ReplyDelete
  40. Hili taifa halijulikani wapi linaelekea,yani mzazi anakamatishwa hela ili alie mahakamani na kujifanya mwanae kadhalilishwa,haiingi akilini baba na mtoto kushirikiana kubaka,haki itapatikana tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...