Habari ni kwamba Mama Salome Sijaona ameteuliwa kuwa Balozi wetu huko Tokyo, Japan, baada ya Balozi Elly Mtango kustaafu. Kabla ya uteuzi hii Mh. Sijaona alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi
Dr James Nzagi anakwenda kuwa balozi Bunjumbura, Burundi, kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Francis Mndolwa ambaye amestaafu. KAbla ya hapo Dr. Nzagi alikuwa Mkurugenzi katika ofisi ya Rais.
Pia Profesa Abdillahi Omari anakuwa Balozi wetu Riyadh, Saudia. Kabla ya uteuzi huu Dr Omari alikuwa mkurugenzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa jijini Dar.
Hongera wote mlioteuliwa...tuna imani utatuwakilisha vema katika nchi husika.
ReplyDeleteNa Mashaka anakwenda wapi?
ReplyDeletemdau hapo juu mashaka anarudi bongo
ReplyDeleteMaisha bora kwa kila Mtanzania aliyekuwa nacho anaongezewa ....Maisha ya sasa aliyekuwa nacho anacho na asiyekuwa nacho hana maisha yamekuwa magumu afadhali ya jana ...Mjomba nikipata nauli nitakuja mjomba
ReplyDeleteAnko Issa tunashukuru kutuhabarisha libeneke la uteuzi. Na tunawatakia heri kuwakilisha Tanzania. Sasa huyo ni Professa au Dr Omari? Kwa uelewa wangu mdogo hizo ni ngazi mbili tofauti kwenye taaluma.
ReplyDeleteHongera sana Mama Salome... unastahili kwa kweli umefanyakazi kwa moyo na malipo yake ni kupumzika kwa raha. WaTZ ukifanya mema utalipwa tuuu.. na mabaya subutu... JK, kwa sasa unagawa kazi uzuri kwa anaye stahili
ReplyDeleteBite
ivi uarabuni lazima achaguliwe balozi muislamu tuu???imani zingine au wasio na imani inakuweje?
ReplyDeletemdau apo juu,ni utendaji kazi mzuri na kujulikana na wakubwa
curiosity!!!