Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wapya wa Tanzania katika nchi za nje mara tu baada ya kuwaapisha rasmi ikulu, kutoka kushoto ni Balozi Dr.James Nzagi anayekwenda Burundi,Rais Kikwete, Balozi Bibi Salome Sijaona anayekwenda Japan na Balozi Prof.Abillah Omar anayekwenda Saud Arabia.


Habari ni kwamba Mama Salome Sijaona ameteuliwa kuwa Balozi wetu huko Tokyo, Japan, baada ya Balozi Elly Mtango kustaafu. Kabla ya uteuzi hii Mh. Sijaona alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi




Dr James Nzagi anakwenda kuwa balozi Bunjumbura, Burundi, kuchukua nafasi ya Brigedia Jenerali Mstaafu Francis Mndolwa ambaye amestaafu. KAbla ya hapo Dr. Nzagi alikuwa Mkurugenzi katika ofisi ya Rais.




Pia Profesa Abdillahi Omari anakuwa Balozi wetu Riyadh, Saudia. Kabla ya uteuzi huu Dr Omari alikuwa mkurugenzi wa Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa jijini Dar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hongera wote mlioteuliwa...tuna imani utatuwakilisha vema katika nchi husika.

    ReplyDelete
  2. Na Mashaka anakwenda wapi?

    ReplyDelete
  3. mdau hapo juu mashaka anarudi bongo

    ReplyDelete
  4. Maisha bora kwa kila Mtanzania aliyekuwa nacho anaongezewa ....Maisha ya sasa aliyekuwa nacho anacho na asiyekuwa nacho hana maisha yamekuwa magumu afadhali ya jana ...Mjomba nikipata nauli nitakuja mjomba

    ReplyDelete
  5. Anko Issa tunashukuru kutuhabarisha libeneke la uteuzi. Na tunawatakia heri kuwakilisha Tanzania. Sasa huyo ni Professa au Dr Omari? Kwa uelewa wangu mdogo hizo ni ngazi mbili tofauti kwenye taaluma.

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Mama Salome... unastahili kwa kweli umefanyakazi kwa moyo na malipo yake ni kupumzika kwa raha. WaTZ ukifanya mema utalipwa tuuu.. na mabaya subutu... JK, kwa sasa unagawa kazi uzuri kwa anaye stahili
    Bite

    ReplyDelete
  7. ivi uarabuni lazima achaguliwe balozi muislamu tuu???imani zingine au wasio na imani inakuweje?

    mdau apo juu,ni utendaji kazi mzuri na kujulikana na wakubwa

    curiosity!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...