Wajumbe wote wa UVCCM nchini Urusi mnatangaziwa kuwa , kutakua na Kikao cha kwanza cha mkutano wa pili wa baraza la vijana wa chama cha mapinduzi tawi la CCM –MOSCOW , (UVCCM-URUSI) Kwa mwaka 2009.
Mkutano huo Utafanyika tarehe 06/12/2009 siku ya jumapili, ukumbi wa mikutano wa block 6 –mikluho maklaya(moscow) , kuanzia saa 8:30-11:30 jion.
Mkutano huo utaongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM –URUSI Ndg. Bakunda Chrispin .
Ajenda za mkutano ni nne na zimeanishwa katika barua za mwaliko kwa wajumbe husika kwa email zao. Wajumbe mnakumbushwa kuangalia email zenu na kupitia ajenda ili kujenga hoja yakinifu na zenye maslahi kwa tawi.

FIKA BILA KUKUOSA!

Katibu-UVCCM-URUSI.
contact! 119526 Moscow,
Russia ,
146 Leninsky prospec
Fax : +74954386744
Tel: +79150901289
Email : ccmmoscow @gmail.com
website: www.ccmmoscow.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. ebu toeni upuuzi wenu hapa ati uvccm urusi ebo! kuleni nondo huko acheni kutafuta sifa mkitaka siasa rudini bongo huko hakieleweki ni misifa tuuu ili tujuwe na nyie mmo

    ReplyDelete
  2. Kila siku mnalialia hapa kwa Mithupu kuwa hampewi posho za tuition za vyuo, afu leo bado mko CCM. Wabongo bwana sijui nani aliumba hii jamii ya watu wasioelewa???

    ReplyDelete
  3. Yaani Kikwete alivyoahidi tu kuwapa uwaziri vijana akichaguliwa tena basi ndio mnajikusanya vikundivikundi ughaibuni. Poleni, wenzenu wala vumbi hawadanganyiki na ahadi za kihivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...