Mdau mkuu wa Cesena, Italy, Baraka wa Chibiriti
akiwa kampuzika nyumbani kwake
Habari na heshima yako mkuu wa nanihii. Nafurahi sana na kufarijika kila siku niingiapo katika blog yetu ya Jamii, ni kitu kizuri sana tena sana.

Ombi langu ni kuhusu Chibiriti a.k.a Chibatari mbona siku hizi kimya sana hapa? Vipi umemfukuza nini? Maana alikuwa akitokeza tu wadau wengi wanafurahi sana, maana mambo yake lazima watu wafe kwa vicheko, mi nashauri hapa ndani ya blog ya jamii ungempa hata kitengo flani hata cha uchekeshaji.

Ndo hili mkuu nawakilisha.

Mdau Mkuu wa hapa ndani ya nyumba.
---------------------------------
Mdau umenifurahisha mno kwa ujumbe wako.
Ila nakuhakikishia Chibiriti hajafukuzwa na hafukuziki kwenye Globu ya Jamii kwani ni mmoja wa wadau wanaoleta chachu kubwa sana humu. Na nina uhakika akishapata ujumbe huu ataibuka na kujibu mapigo. Tulia uone. kwa wasiomfahamu Chibiriti na kichango ambayo amewahi kutoa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. aaah hivi kweli ijamani chibiriti wetu kaishia wapi?? we miss yuuuu katka libeneke uko kimya saana kulikoni?by the way andika email address yako nataka nikutumie zawadi nzuri ya xmas lap top ya aple niko serious zawadi ni zawadi hope utafurahi au michuzi mtumie email yangu
    mdau canada

    ReplyDelete
  2. Hahahah wewe Chibiriti hizo fanicha na computer bado unazo tu?umefulia wewe!!

    ReplyDelete
  3. LOve them or hate them but Chibiriti, Dr. US Blogger na US Blogger hawawezi kufukuzwa hapa.

    Blogu ya jamii kweli ni blogi ya jamii, Michuzi hana chama cha siasa, hana dini, hana rangi, hana jinsia (hahaha).

    Anachojua yeye ni kuendeleza libeneke kama kawa.


    (US Blogger)

    ReplyDelete
  4. Kweli Chibiriti umefulia, hiyo computer mbona kama ya mwaka 47? Mdau uliejitoa kumtumia laptop naomba ufanye haraka maana ndugu yetu Chibiriti anaaibika.
    Amy

    ReplyDelete
  5. We US Blogger wacha misifa, kwani we umetajwa?? Hovyo!


    Nyokoinyo

    ReplyDelete
  6. wadau msijali nipo busy sana maana mimi ndo msaidizi wa MORINYO pale Inta, namsaidia kuwasiliana na Etoo maana yeye haelewi kiswahili cha Etoo

    ReplyDelete
  7. Kaka Chibiliti mimi kwa moyo mweupe najitolea kukununulia fenicha, computer na raba nzuri za kisasa.. hebu nitumie email then tuwasiliane jinsi gani nitakavyokutumia hela

    ReplyDelete
  8. John Mashaka, Peter Nalitolela, Dr. Shayo, Baraka wa Chibiriti, US-blogger hawafukuziki hata ulete usalama wataifa kumtishia mashaka maisha. jamii globu hoyeeeee

    ReplyDelete
  9. nshimimana aka dumisaneDecember 02, 2009

    Taratibu hapo, nani kawaambia nimeondoka!?

    ReplyDelete
  10. umeoa??

    jibu plizz

    ReplyDelete
  11. chibiriti jamani nasubiri email address yako kuhusu laptop ya aple niko serious si utume tu sometimes watu tuko serious wengine mnadhani utani niko serious kwa hili ni zawadi tu ya xmas
    mdau canada

    ReplyDelete
  12. Nyokoiko umenichekesha sana,what u wrote na jina lako pia.
    Jamani kweli Chibiriti mbona kimya sana hp upo ok huko,mi nakutakia kila la kheri ila don be a stranger kwenye kijiwe chetu!!!!
    Miss u loads!
    Michuzi kazi nzuri kp it up mtu wetu.

    ReplyDelete
  13. *************
    Wewe Us-blogger, unamatatizo gani?
    akili zako ziko sawa kweli? mie ninawasiwasi kwa mambo unayoyaandika humu ndani.
    hii sio Ze utamu, unaingia huku na kuanza kutapika tapika maneno yako yasiyokuwa na msingi.
    kwa akili zako, unafikiri tumeamini hayo yote uliyosema? usifikiri unapoandika humu ndani watu wote tumepungukiwa na akili. alaaa
    huna lolote, move, move get out of the way. unatuwekea usiku.
    tembea, tembea mbele huko usituletee ukulima wako

    ***************
    DEBE TUPU HILO LAVUMA. WADAU JIHADHARINI
    ******************

    Holaaaaa

    peace

    mdau
    Canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...