Mimi ninafikiria tatizo la umeme nchini linaweza likapatiwa ufumbuzi iwapo tukiamua sasa kuwa nchi inabidi iangalie matumizi ya nishati ya umeme itakavyoongezeka miaka ijayo hivyo tujiandae kuongeza Megawati nyingi kwa ajili ya miaka ijayo na pia kuboresha usambazaji.

Unaweza ukachagua kampuni isiyokuwa sahihi kwenye mchakato mzima iwapo maamuzi yako yanakuwa yale ya haraka na yaliyofanyika kutokana na matatizo yanayowakabili watu wako kwa muda huo. Lakini iwapo ukiwa na muda wa kutosha ninaamini tunaweza tukaamuavizuri kwa ajili ya kusuluhisha matatizo ya umeme yanayotukabili.

Kitu kingine ambacho wataalam mbalimbali walioulizwa (consultancy experts) jinsi ya kulitatua tatizo hilo walikuja na njia moja kuu. Wakasema kuwa ili nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ziweze kujinasua kwenye tatizo hilo inabidi zijenge vituo viwili au vitatu vikubwa vya kuzalishia umeme kwa pamoja, kuliko kila mtu kuanza kutengeneza kituo chake ambacho kitakuwa kidogo na gharama yake ya uzalishaji inaweza ikawa kubwa kuliko ile ya vituo vikubwa.
Kwa mjadala mzima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. ILI AFRIKA IJITATUE KWENYE TATIZO VIJENGWE VITUO VIWILI AU VITATU VIKUBWA VITAKAVYOHUDUMIA NCHI ZOTE BADALA YA KILA NCHI KUJENGA KITUO CHAKE! HUU NAO NI MGOGORO MWINGINE NI KIONGOZI WA NCHI GANI AMBAYE HATATKA KIJENGWE NCHINI MWAKE! NANI HATAKI KARICHIMONDI AKAPATE YEYE HAPO NDIPO VIONGOZI WETU WATAKAPOANZA KURUSHIANA MANENO YA KILA AINA NA GIZA LITAENDELEA KUWAKABILI WANACHI. USHAURI HUU HAUNA MAANA KWA VIONGOZI WANAOSHINDWA KUZIENDELEZA NCHI ZAO MIAKA KADHAA BAADA YA UHURU. BAADA YA UHURU TU TULIANZA KUUONA MWANGA UPANDE WAPILI WA HANDAKI LAKINI KILA MIAKA ILIVYOKUWA IKIENDA MWANGA ULE ULIKUWA UKIFIFIA BADALA YA KUONGEZEKA, LEO HII TANZANIA HAINA VIWANDA, KIUBISHIUBISHI INAVYO VIWANDA HEWA; KILA MTU ANAJUA SIASA NCHINI NA KILA MTU NI MSEMAJI WA NCHI NA KILA MTU NI MLALAMIKAJI WA NCHI. GIZA LITAEENDELEA KUDUMU ZAIDI TANZANIA NA VYIVYO HIVYO WATANZANIA TUTAENDELEA KUCHAPA USINGIZI.

    ReplyDelete
  2. Mbona watu usemaga kwamba mashaka hajui Kiswahili? Jana nilimsikia akihojiwa BBC na kuongea vizuri tu? Naona wameanza kushirokiana kwa ajili ya 2015? Mie nataka ukuu wa TRA

    ReplyDelete
  3. MOHAMED DEWJI KUUNGANA NA JOHN MASHAKA, DR. SHAYO NA JANUARY BASI TANZANIA ITAKUJA JUU 2015. WAKUU MPIGANE, NADHANI HATA JK ANAWAOGOPA SASA HIVI ILI AWAZIME NI LAZIME AWAPE KAZI ZA KUPIGA RANGI PARE KA IKURU IRI MSIMUANDAME, KWA MAANA WATU MAKINI KA NYIE NI WA KUOGOPWA SANA

    ReplyDelete
  4. hawa jamaa wanazungumzia mambo mengi mazuri sana, ila je serikali yetu ipo tayari kuyasikia maoni yetu? tuseme mna nia njema, lakini wasomaji wenu ni watu ambao mara nyingi hawana upeo na wataanza kumwaga uchafu kwamba
    hawa ni watu ambao wanajipanga 2010 kuwa wapinzani ndani ya CCM. moo, unajiunga na nabii john mashaka,

    ReplyDelete
  5. Wanaume wa Shoka kazini,,,, kazi kwe kwe

    ReplyDelete
  6. PETER NALITOLELADecember 01, 2009

    HUU NI MFANO WA KUIGWA SANA. MHESHIMIWA ROSTAMA AZIZI, KARAMAGI NA EDUARDO LOWASANA PIA WACHANGIE HII MADA YA UMEME YA WATU MAKINI TOKA MUZUMBE CHUO KIKUU CHA UNIVESITI CHA KULE MOLOGOLO YA WAKINA NABII MTUME YOHANNA MASHAKA NA MHESHIMIWA MOHADEDI DEWIJI WA KULE CHUO CHA HAVADI YA MALEKANI YA WATU MAKINI PIA. SASA HII MBONA IMEMUACHA SWAHIBA WA MASHAKA WA KULE LONDON DAKITARI HILDEBANDI SHAYO??? MBONA HAMTENDI HAKI WAJAMENI. DAKITALI WALA USIWE NA SHAKA KULA UTAPATA TU NA IKULU UTAINGIA KWANI JINA LAKO LIKO KWENYE BALOTI BOXI. HII TU NDIO DAWA YA KUIONDOA TANZANIA GIZANI AMEN!

    ReplyDelete
  7. Mo hii safi sana kuona kizazi kipya kikiongozwa na mashaka wakifanya vya maana Kama kawaida tunawaunga mkono Kama taifa

    ReplyDelete
  8. Matajiri wote watoto na wajitangaze

    ReplyDelete
  9. Hongera Bw. Mo. Nimependa unavyofikiria kwani mawazo yako yanafanana na ya kwangu - ila kwa sababu mimi ni mtu mdogo katika nii nchi, nikiyasema hayatasikika.

    Tanzania inaweza ikajikwamua vizuri sana na kuzalisha umeme wa kuuza nje kama ikiweza ku-exploit Steigler's Gorge. 4GW Minimum. Huu ni umeme msafi na usiohitaji mali ghafi ya mafuta.

    Challenge hapa ni kwamba zinahitajika pesa nyingi sana, na wawekezaji nadhani hawana hamu tena na Tanzania baada ya kuona jinsi mradi wa IPTL ulivyofanyiwa fujo na wa-TZ.

    Sidhani kama serikali yetu ina uwezo wa kipesa kuujenga huu mradi - labda ipewe msaada tena, lakini sidhani kama kuna nchi itayotoa msaada mkubwa kiasi hicho.

    ReplyDelete
  10. Lyidia Halphani (Dubai)December 01, 2009

    NDugu wasomaji, mimi nafikiri sasa somo limeanza kueleweka. Waswahili wanasema kimya kingi kina kishindo.
    Vijana wetu akina John Mashaka, Dr Shayo, na wengineo ndiyo waliojitoa mhanga kuanza kutoa muamko wa haya mambo. Si kwamba hayakuwepo, ila upeo wao ulikuwa ni chachu mpya.
    Si lazima wawe viongozi 2015, ila kutoa ushauri kunatosha, na nafikiri, kuona wanasiasa wanajitokeza hadharani kuzungumzia yale waliokwisha yaona ni dalili nzuri kuwa ujumbe umewafikia walengwa.
    Ila Mshaka kutuambia unachukua likizo ya kuandika ndani ya blog hii siyo fresh, tupe angalau mchango wako.

    Dr Shayo kwa siku nyingi sijakusikia, sijui kulikoni kimya hivyo?.

    ReplyDelete
  11. John Mashaka ndio yatakuwa yaleyale yakulalamikia waliopita kwani hata wasasahivi si wanalalamikia waliopita? zote pumba tupu. mwaka 94 gazeti la Uhuru liliandika 2007 kutakuwa na umeme haukatiki tena. huu mwaka sasa ni 2009.

    ReplyDelete
  12. @LYDIA WA DUBAI. kazi nzuri, nadhani moto uliowashwa na Dr. Shayo pamoja na john mashaka nadhani kweli umeeleweka, hawa vijana wawili historia ya tanzania itawatambua kama waasisi wa muamsho katika kizazi chetu, sijui kwa nini wakimbie kutoa mada. yule shayo alikimbiaga zamani, mashaka tena anakimbia matokeo yake wanaacha wanasiaasa kama kawaida. mie natamani wawe viongozi wa kesho, kura tutawapa tu

    ReplyDelete
  13. nadhani viongozi wa leo, wameanza kuyaona machungu ya vijana wetu mahiri. huu tu ni mwanzo na walijificha nao wajitokeze wasiogope serikali

    ReplyDelete
  14. muunganeni pia kushambulia ufisadi pamoja na spika sixxi. il kusema kweli nimependezwa mno na hii jitihada, mashaka na wenzake mmekuwa mfano kweli kwetu sisi, nadhani hata us blogger atafurahiswha na hii ushirikiano

    ReplyDelete
  15. Mbiu ya mgambo ikilia basi kuna jambo. Wanasiasa wanaungana na raia wa kawaida mashaka na moo kufanya kazi pamoja kunaashiria nchi kuchoka na ufisadi ambao umetanda kula sehemu hasa kwenye wizaravya jishati ya mzee ngeleja yeye sijui anasemaje mwenyewe

    ReplyDelete
  16. michuzi kwenye mada nzuri Kama hizi kwanini unaweka jina la John mashaka kwa sababu kuna watu ambao wanakuja siyo kuchangiana hoja Bali kuponda ilimradi wameliona jina la John mashaka. Watanzania hii mambo ya kujaribu kuwaangusha wengine siyo freshi lazima tujitahidi kuwaunga mkono wenzetu ambao wanadiriki kufanyia taifa mema

    ReplyDelete
  17. Hizi ideas na plans zipo toka siku nyingi,nadhani mheshimiwa angefanya jambo la busara kutuambia kwanini hamna utekelezaji kwamaana yupo karibu na wahusika na sio ku offer new ideas kwanza.

    ReplyDelete
  18. Mo=US Blogger?

    ReplyDelete
  19. hoja akitoa mo ni poa sana ,hoja akitoa mashaka anashambuliwa utasema mpira wa kona.watanzania ni vituko sana.


    mo wewe ni mbunge hoja hizo peleka bungeni ndio zitaweza kusikilizwa kufanyiwa kazi hili zitusaidie wananchi.

    ReplyDelete
  20. Watu wenye akili Kama mashaka mara nyingi hawawezi kuwa marais. Wao uwa nyuma ya pazia wakitoa ushauri tu. Kwa hiyo washabiki wa mashaka itabidi watafakari mara mbili ili kujipanga

    ReplyDelete
  21. US. Blogger)

    Mr. Dewji, I have respect for you because you can write better than the Saint Prophet of doom Mr. John Mashaka who is deceiving the whole world

    Yesterday, I did hear how Mashaka is lying through the whole world in BBC. I am glad he is out of the game, and thank you to me because I am the only person who can kick him out of the blog ya jamii

    Dewji had very good points only intelligent people had. Mr. Prophet called me corrupt because he was charged a dollar in Bagamoyo, and I am employing more than 4000 people in Tanzania, investing more than 70million dollars and masaka does invest nothing but blame on the government

    Right now, my 2.4million penthouse in Dubai has been devalued to $500,000 but I dont go to the whole world telling the people. Mashaka goes to BBC and tells the whole world that he is broke, and lost all his savings, all I did was lough

    Nabii akikosa kazi, basi nitamsaidia apate angalau kazi ya kuchoma nyama pale kwenye hoteli yangu ya Dar... Mashaka nadhani ujumbe umeupata. MO ana upeo mkubwa kukuliko wewe

    US-Blogger

    ReplyDelete
  22. US-BLOGGER -shame on you!none sense! you deliberately use blog ya jamii to write your short-minded ideas,always when i see comments,i get annoyed,the way act will have impact to your family (kids),they inherit your iodiotic ideas,

    Michuzi-Have you been bribed by US-BLOGGER?why acceptig Us-blogger comments? Modulation is all about Quality in terms of blog ethics,value,culture etc ,my advise don't accept Us-bloger comments as he is polluting our blog ya jammii

    ReplyDelete
  23. Nasikitishwa sana na Balozi Michuzi. Wadau wengi wanataka kutoa maoni lakini yanabanwa. Inabidi na sisi tujitahidi kuwa na blogu yetu ila maoni wasiopenda wana CCM kusoma yaweze kusomwa.

    Tutafika tu, hata kama baada ya miaka 100. Uhuru wa wananchi utaheshimika kama sio leo basi kesho.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...