Siku kombe la dunia lilipotua Dar, Mpiga Picha Mkuu wa Globu ya Jamii Francis Dande alinasa picha hizi za mazungumzo kati ya JK na Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga uwanja mpya wa neshno.
Je mdau unadhani Tenga alikuwa anasema nini ukizingatia kwamba muda mfupi baadaye JK aliwatolea uvivu viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kusema wasipobadilika kwa kuendekeza ushabiki na kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mapato ya mechi badala ya kuwekeza kwenye maendeleo ya soka, Tanzania itabaki nyuma mpaka mwisho wa dunia!
kusoma habari kamili













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Naona Tenga aliamua kumtolea uvivu kwa kumweleza kile kinachokwamisha soka la Tanzania, mpaka JK akalowa!!

    ReplyDelete
  2. Rais Anaonekana akisema SIDANGANYIKIIII

    mdau Dee

    ReplyDelete
  3. Tenga anajaribu kumpa live mheshimiwa rais kuwa hawa wata-tz bwana washamchoka huyu maskio(sorry, ni maximo. So cha kufanya hapa mkuu ni kumtoa nduki tu!

    Then rais, anamuuliza, wewe binafsi unasemaje? tumchunie au tumkurupushe!

    Tenga: Aah, mi mwenyewe nimeshamchoka achape lapa tu!

    Rais: lakini si unakumbuka tulivyopanda chap chap kwenye viwango vya FIFA?

    Tenga: Sawa lakini pia ci unaona tulivyoshuka fasta fasta huko huko FIFA?

    Jamani ndugu zangu, naomba nisaidiwe, kama huyu ndugu (maximo) hatumtaki na analipwa mshahara kwa kodi yako na yangu, hakuna jinsi ya kufanya ili tum-stopishe?

    Then nahisi leo, hata wazenji (mdebwedo stars) watatufunga. Sorry sio mdebwedo stars, ni mapinduzi stars!

    k'dume

    ReplyDelete
  4. anony hapo juu, wala hujakosea, hawa jamaa wanaitwa Mdebwedo Stars (lakini ukiwatoa Abdul Kassim na Canavarro tu) kwa sababu wanatokea yanga.

    Mdau
    Maputo, msumbiji.

    ReplyDelete
  5. Hapo wanam-discuss maximo tu!, hakuna kingine.

    Na kama hamjui ndugu zangu, equation ipo hivi:

    Kikwete + Tenga - Watz wengine = Maximo + timu kuvurunda.

    ReplyDelete
  6. Ni cheche za SUMU tuu!!

    ReplyDelete
  7. Wadau ni mimi pekee ndio ninae ona tatizo la hiyo picha ya mwanzo?

    JK amevaa skuna (viatu vya ofisini) huku akiwa na treki la mazoezi!

    ReplyDelete
  8. Mazungumzo yalikuwa ifuatavyo (mazungumzo yamepangwa kwa mtiririko wa picha toka juu kwenda chini)

    LT: Kama nilivyokwambia mheshimiwa, tunaweza hapahapa kuandaa fainali za kombe la dunia.
    JK: Acha utani wewe Leodgar.

    LT: Sasa sikiliza mimi nikupe mikakati ya kuandaa na hata kulichukua kombe....
    JK: Enhe....

    LT: Umeelewa sasa, mheshimiwa?
    JK: Mmh! Sijui!

    LT: Muhimu zaidi vitu hivi vitatu: Nia, sababu na uwezo.
    JK: Hivyo viwili ndio, lakini uwezo kweli...sijui...

    LT: Kwani unafikiri uwezo ni nini mheshimiwa, uwezi pochi tu.
    JK: Si ndo hayo sasa...

    LT: We nenda kafikirie halafu nijulishe...
    JK:Mh, haya...

    LT: Au bado una mashaka...
    JK: Kwa kweli si madogo. Hebu tuangalie kidogo nchi ambazo zimewahi kuandaa kombe la dunia...

    LT: Ah, sasa usianze tena. Si tushamaliza?
    JK: Kusema kweli, lakini haya kwa heri...

    ReplyDelete
  9. Alikuwa anaambiwa aache longolongo na siasa zake chafu...watu wanakufa njaa vijijini huko wao wamefumba macho.Iko siku watakiona wale wote wanaokula kupitia mgongo wa wavuja jasho,naomba michuzi uiweke hii kama ilivyo hata kama ni swahiba wako kwani rafiki ni yule anayekuambia ukweli na kukutoa kasoro na sio kukusifia na kupamba ujinga.

    ReplyDelete
  10. This shows our President Hon. JK is a good listener and takes time to interact with people.He seems to be interested insports too. Mr Tenga is grabbing the opportunity to influence the President. They seems to be old colleagues. After all they all studied at Kibaha Secondary School. So do I. Try rember KSS and snake emblem/logo on our white shirts.Or life in Scandia, Kibo, Nyanza and Pangani Houses and the Malambugi football ground. Keep it up leaders for the good future of .

    ReplyDelete
  11. Hapo Tenga ni siasa tu, hakuna lolote la maana analoongea. TFF mipango mibovu soccer letu halikui. zogo kibao kazi kuiba pesa tu za viingilio. Ukiuliza account ya TFF inabei gani huta amini...Hii tutafika wapi, badala ya ku base na kuibua vipaji vya watoto ili baadae tuje nufaika nao wao wanang'ang'ana tu na maghalasa, ni nini hii.... Hata ndugu zetu wa Zenji wametupita kwa soccer, unabisha utaona results za game ya leo pale Kenya....

    Nia hayo tu maoni yangu.

    Pzl.

    ReplyDelete
  12. Hapa Kikwete nadhani alikuwa amemuuliza swali Tenga

    JK: Sasa Tanzania itaendelea kuwa mtazamaji tu wa Kombe la Dunia mpaka lini?

    Tenga: Ahaa usijali sana Mheshimiwa kombe lijalo lazima tushiri.(Ndio maana JK anaonekana kutokumweleo vizuri)

    JK:Je TFF ina mikakati gani kuhakikisha Tanzania inapiga maendeleo ya soka?

    Tenga: Mheshimiwa mkakati ipo tena madhubuti kabisa, Kwanza lazima tuhakikishe tunakusanya mapato vizuri. Mechi kubwa siku hizi kwenye uwanja huu ni milioni mia kadhaa zinapatakana.

    JK: Ehee, kukusanya mapato kuna uhusiono gani na kwenda kombe la dunia?

    Tenga: Mheshimiwa, mchezo wa mpira siku hizi ni biashara lazima tujali mapato zaidi, bila hela hatufiki mbali mheshimiwa. Jambo lingine si unaona mwenyewe timu zetu Simba na Yanga, zote sina makocha wa kigeni, lazima tuhakikishe zinacheza na kushinda ligi ya Vodacom. Yanga na Simba ndio uhai wetu sisi TFF kwani zinaingiza mapato mengi kwetu. Kwanza si unajua mimi nilicheza Yanga enzi zangu. Mimi Yanga damu damu.

    JK: Bwana Tenga naona nyie mnatilia mkazo vitu ambavyo havitatufikisha mbali, yaha mambo ya mapato na Simba na Yanga hayatatupeleka popote. Lazima kuwa na mikakati muhimu ya kukuza vipaji na kuviendeleza.

    Tenga: Haya mheshimiwa, Lakini mpira biashara mhemshiwa rais

    JK: Fanyani mipango kabambe ya kukuza mpri bwana Tenga. Achana na mambo ya kujali zaidi mapato na ushabiki wa Simba na Yanga

    ReplyDelete
  13. duuu hapo alikuwa anamwambia kuwa bwana maximo siyo kocha kabisa mimi nilikuwabia yule ni kocha wa kufundisha kucheza ngoma za samba lakini siyo mpira wa miguu
    sasa ni bora tumfukuze .....

    ReplyDelete
  14. Alichokuwa akielezwa JK, na Mheshimiwa Tenga....
    TENGA....Eti Mheshimiwa, hawa watanzania wanasema MAXIMO hafai, si mwenyewe, unakumbuka ulitubembeleza weeeee, tukuletee jina na gharama za kocha wa kigeni, SI tulifanya hivyo??????

    JK...NDIO NAKUMBUKA,
    TENGA: SI UNAKUMBUKA ZILE JUHUDI ZA MWANZO ZA FUNIKA KOMBE MWANAHARAMU APITE, TIMU IKIFANYA VIZURI NA SIKU NYINGINE KUBORONGA???
    JK.....NDIO TENGA
    TENGA: SI UNAJUA KUSAPOTI KWAKO TAIFA STARS, KUMEKUFANYA UWE JUU, NA KUJIHAKIKISHIA TTENA USHINDI WWA KISHINDO MWAKANI??????
    JK:..... HIVYO... HIVI UNAFIKIRI....... WATANIELEWA KWELI??

    TENGA; SASA TUSILAZE DAMU, WE ALIKA TU TIMU IKULU NA KUWAPONGEZA, KUUNGA MKONO JUHUDI ZAKO A'FU WAPIGA KURA TUTAJUA LA KUFANYA.......
    JK: SASA USIONGEE KWA SAUTI.... DNO MAANA NABADILI POZI KILA POINTI TUNAYOZUNGUMZA HAPA......TEHE TEHE TEHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEETEEEEEE

    ReplyDelete
  15. Mimi naona hapo,anamsuta Kikwete kwa kumzalilisha,maana JK Wakati anawaponda jamaa alikuwa anacheka kichina hivi chini huku akimuangalia.
    sasa jamaa kashuka chini anamsuta ,
    LT: Kwa nini umetuzalilisha vile mbele za watu,wewe mshikaji wangu kabisa jamani unanitoa nishai,
    Bora ungeniambia mwanzo kama utanipaka kiaina ili uvutie mashabiki waliokuja kutazama Kombe,mimi ningejificha sasa wewe utoa mabomu LIVE
    tehe tehe tehe

    ReplyDelete
  16. Hapo anamwambia hiviii, "SI UNAONA MATUNDA YA UONGOZI SHUPAVU WA TFF MKUU? LEO TUMEINGIA KWENYE HISTORIA KWA KUWA TIMU PEKEE DUNIANI KUCHUKUA WEDI KAP YA KOMBE LA DUNIA MARA MBILI, BILA KUCHEZA HATA GEM MOJA!!!..., SIYE NI NOMA"

    chiggs,deslam

    ReplyDelete
  17. ELIBARIKI MASUKEDecember 01, 2009

    HAPO INAONEKANA RAIS ANAAMBIWA MUHESHIMIA HILO TUMBO NI SHY INABIDI UANZE MAZOEZI MEPESI HAPA HAPA UWANJANI....!

    ReplyDelete
  18. Mazungumzo hayo yalikuwa kama ifuatavyo:

    JK: Habu nieleze kuhusu mgawanyo wa mapato kati ya Simba na Yanga?

    LY: Ni kwamba TFF inachkua (1/2) nusu ya mapato yote

    JK: kwa nini kiwango kikubwa hivyo?

    LT:Sasa mheshimiwa unategemea tutapata wapi kula yetu.

    JK:Na vijana wanoumia uwanjani kwa kujituma kikamilifu nao wanapata nini?

    LT:hawa wanapata 5% ya mapato yote

    JK:Are you serious? ndio maana timu zetu hazifanyi vizuri kwa sababu nyie ndio mnaopata zaidi kuliko hao vijana.Sasa nakuagiza kuanzia sasa vijana wapate 3/4 ya mapato yote halafu tuone kama soka la nchi hii halijakua.

    ReplyDelete
  19. hahahaaa wadau 'kidume na mrfroasty'

    JK huvaa sana mokasini na treki sijui kwanini???

    to hell with ur chandimu/football

    ReplyDelete
  20. Na kutembea kote,mokasini haiji kabisa, ni sawa na kuvaa bukta na koti la suti. Fashion Police wakija itakuwa sokomoko!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...