anko zawadi ya picha yao alipoja vekesheni bongo
Habari Mkuu, na pole kwa majukumu.
Napenda kuchukua nafasi kumjibu mdau aliyetuma hoja kuhusu mimi. Kwanza kabisa nimefurahi sana hili, kuwa kuna watu bado wananipenda na kunikumbuka, sikutegemea kabisa.
Napenda kuchukua nafasi kumjibu mdau aliyetuma hoja kuhusu mimi. Kwanza kabisa nimefurahi sana hili, kuwa kuna watu bado wananipenda na kunikumbuka, sikutegemea kabisa.
Pili ninawahakikishia kuwa sikufukuzwa kabisa, ila majukumu ni mengi sana wakati huu, yaani nimetingwa sana na ubebaji box kama wasemavyo wadau, na kama kawaida ya maisha. Nipatapo tu chanzi nzuri nitarudi kwa kishindo kama kawaida, pia nipo daima na ninafuatilia sana kwa karibu sana na kila siku hii blog yetu ya jamii.
Asante sana mdau uliye nikumbuka, na ninakusalimu sana na kufurahi sana kwa kunikumbuka kwako.
Pia salamu sana kwako Mkuu Michuzi na wadau wote hapa, nasema tupo pamoja daima na tuzidi kupendana siku zote.
Asanteni
Baraka wa Chibiriti
Cesena, Italy
sasa jamani weye chibiriti mie nataka nikutunuku zawadi ya laptop ya aple mbona email address yako hutoi jamani ni zawadi tuu na sio utani
ReplyDeletemdau canada
Chibiriti safi karibu sana.
ReplyDeleteMichu kweli hawa watu wanaleta changamoto katika blogu yako tungefurahi pia kuwatambua na wengineo kwa majina yao halisi si kwa nia mbaya bali kuwapongeza katika mwaka 2009 maana kweli wametoa michango mbalimbali ya maana au ya kuchekesha kama vile akina kidume, mkata issue, mtoto wa Coast, Al- musoma, Nalitoleala, US- Bloger,Lidya,La mbegu, makusalo,Nyakatakule,Kibajaji,
kwani huyu jamaa, chibiriti ni mmakonde???
ReplyDeleteAnko Michu, mbona wafanana hivyo na Uncle Chibi! Si bure hapo kuna namna inawezekana nyie hamjui tu!!!
ReplyDeletemichuzi unatucheleweshea habari za babu seya na wanawe wadau tuko makini kuona kama haki itatendeka
ReplyDeletePOA MDAU WA CANADA, NILIKUWA SIJAKUPATA. NITUMIE SMS KUPITIA NAMBA HII +39 380 3115382. Nitakupatia E-mail. Asante.
ReplyDeleteNI MIMI:
CHIBIRITI MWENYEWE KABISA SI UTANI.
Du Chibiriti kaibuka?? poa karibu sana..mzee
ReplyDelete