Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam, imetupilia mbali ombi la Serikali la kuitaka mahakama hiyo iipe kibali cha kugawa bure samaki aina ya jodari, ambao wanadaiwa kuvuliwa bila kibali katika bahari ya Hindi upande wa Tanzania.
Akitoa amri hiyo Jaji wa Mahakama hiyo Radhia Sheikh, alisema kuwa maamuzi hayo yalifikiwa baada ya kugundulika kuwapo kwa dosarikatika hati ya kiapo iliyoambatanishwa na maombi hayo.
Jaji Radhia alisema kuwa hapo awali Mahakama hiyo ilipokea ombi la Serikali lilokuwa likiomba kibali cha kugawa bure samaki aina ya Jodari, waliovuliwa na wavavu haramu katika ukanda wa bahari ya Hindi eneo la Tanzania.
Sheikh alisema kuwa hati hiyo ya kiapo ambayo iliwasilishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka katika kesi namba 46/09, ilikuwa na dosari mbali mbali zikiwamo za kutokuweka wazi aliyefanya tathimini ya thamani halisi wa samaki hao.
Kufuatia hilo, Jaji Sheikh alisema kuwa kiapo hicho kilikuwa hakijakamilika, ikiwa ni pamoja na kuwa na makosa makubwa ya kisheria.
Kutokana na hilo, matumaini ya baadhi ya watu ambao walikuwa wakisubiria mgao huo wa samaki, yamezimika kutokana na amari hiyo ya mahakama
Awali Waziri wa Mifugo na Uvuvi Dk. John pombe Magufuli, alitangaza kuwagawa samaki hao bure, kwa madai kuwa Serikali haifanyi biashara.
Uamuzi huo wa Waziri Dk. Magufuli, ulikuwa ukienda kinyume na amri ya mahakama iliyotolewa hapo awali, ambayo ilitaka samaki hao wauzwe kwa wananchi ikiwa ni pamoja na fedha kuwekwa katika akaunti na kuhifadhiwa kwa stakabadhi za mauzo hayo.
Hata hivyo uamuzi wa ugawaji wa samaki hao, uliingia dosari baada ya kukosekana kwa mizani ambayo ingetumika kupimia samaki hao, wakati wa ugawaji.
Katika kesi ya msingi, Serikali inawashikilia raia 37 wa kigeni ambao wanadaiwa kuwa kwa pamoja walivua samaki hao bila kibali, katika bahari ya Hindi katika ukanda wa Tanzania.
Raia hao ambao ni wa kutoka nchi za Uchina, Uphilipino, Vetnamu na Kenya wanadaiwa kuvua tani 296.32 za samaki aina ya Jodari, ambao wana thamani ya zaidi ya Sh Bilioni 2, katika mwambao wa bahari ya Indi sehemu ya Tanzania kwa kutumia Meri ya Tawariq 1.

Kupata stori ya siku ya kutoa tamko
la kugawa samaki hao bure
hivi mwezi ule tuliambiwa gharama za kuwahifadhi zilifikia 7 bil na thamani halisi ya samaki ni 2 bil. Sasa hivi uhifadhi siutakuwa umefikia bil 10?
ReplyDeleteau kuna kamradi kamtu ka kutunza fish?
That's your government at work. No rush no hurry even if it involve perishable goods. There is something wrong with African governments. Very corrupt, inefficient,arrogant, etc etc. We cling on titles while can't really deliver, very very sad.
ReplyDeleteKwenye issue kama hiz kungetengenezwa kautaratibu kakisheria ka papo kwa hapo,Mtu umekamatwa umefanya uvuvi sehemu isiyoruhusiwa meli pamoja na samaki wanataifisha wahusika wanapigwa fain na kutimuliwa kwisha biashara.Kwa mfano mtu anapokamatwa amevunja sheria za barabaran anapigwa fain hapohapo biashara inaisha manake hakuna maana kuendelea kutumia kodi za walala hoi kuhifadhi samak pamoja na gharama za mahakama.
ReplyDeletesiamini...dah ama kweli ishi uone
ReplyDeletepale check n balance za serikali zinapokua hazina maana, hapa mahakama inaenda taratibu, kama kawaida yake, na kusimamia misingi isiyo na maana kwenye kesi kama hii.
ReplyDelete