Wa kwanza kushoto kabisa juu ni Mwenyekiti wa jumuiya ya TSAH Bw ABDILLAH NKYA akiwa na wachezaji wa timu ya tsah (watz) kabla ya kuanza mpira uliondaliwa kwa ajili ya kuadhimisha uhuru wa Tanzania Tisa Desemba
Timu ya Uganda
Wachezaji wa Tanzania wakipata msosi kabla ya gemu lao na Uganda mashabiki wa Tanzania wakifuatilia mchezo
kwenye byke ni mtoa habari wa jumuiya ya tsah Bw Dani msemo
katika maadhimisho haya kulikuwa na mambo mbalimbali kama vile chakula cha pamoja cha wachezaji pamoja na kuandaliwa kwa mechi hii ambapo watz waliibuka kuwa washindi kwa magoli 3-1 dhidi ya waganda





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Aisee haya mazingira yananikumbusha kwetu Iringa, safi sana!

    ReplyDelete
  2. Kwani hawawezi kukaa mezani na kwa utaratibu mzuri wa kula, badala ya kusimama na kila mtu kula kivyake na kwa wengine kusimama, kuongea na hata hakuna mpangilio..hivi ni vitu vidogo vidogo vyenye nafasi katika kujenga nidhamu katika timu.

    ReplyDelete
  3. Anonym wa kwanza kanichekesha sana!.Sasa wahindi wako kama sisi,there's nothing new.Halafu wewe WWW.Tanzaniasports.com,hiyo inaitwa "Buffett" siyo lazima ukae,hata Tanzania kuna mambo haya try to mingle with Tanzanian high society.Nothing personal!

    ReplyDelete
  4. Mbona wote mko kwenye pikipiki? Ina maana hakuna magari huko? Njooni huku tuwapeni magari ya bei chee.

    ReplyDelete
  5. sasa hao nao wanakula ubwabwa na maharage then wakakipige ,wataweza kukimbia kweli au wataishia kutapika tuu

    ReplyDelete
  6. Naona wachezaji wanapati pilau kabla ya gemu.

    Ina maana mumesahau nasaha za Dr. Licky kwamba pilau na soka wapi na wapi na kwamba munatakiwa mupate fibre.

    Dr. Licky wakumbushe vijana.

    Michuzi mbona dokta hatukumsikia siku nyingi? Mlete atupe mawili matatu.


    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. Du inanikumbusha sana maeneo ya watu mchangani udongo mwekundu na vipando vyao lol! India ni noma!

    ReplyDelete
  8. ww ulosema wahindi wako kama ss,kwanza tofautisha katia ngozi nyeusi na nyeupe hivi nivi2 tofauti ss ww unaesema tuko sawa sawa muongooo mkubwaaaaa

    ReplyDelete
  9. Wow!!!!! namiss sana hayo mazingira katika uwanja huo wa manviguda Sainikipuri...Najua ningekuwepo mzee mzima hapo tungewapiga waganda hata bao 5-0...
    Jamani msishangae hivyo ndivyo viwanja vya India...asubuhi choo cha public, mchana ni wakati wa nguruwe kufukua fukua na kusafisha mazingira ,jioni soccer au Cricket inapigwa

    Sikieni tu jamani watu tunatoka mbali.

    Rodrick Mwambene
    Ex Osmania Unversity ,Hyderabad India.

    ReplyDelete
  10. Anon wa 9:50,
    India kuna magari? Ndiyo kuna magari. India wanatengeneza magari (TATA, Nanocar, etc.) pikipiki (bajaj, n.k.) computers, generators,simu, wao wenyewe na hata wagonjwa wengi sana kutoka hapa TZ wanakwenda kutibiwa huko. LESSON? Kama India na China wameweza kuwa totally self-reliant katika teknolojia na uchumi wao unaendele kukua kwa 10%, then na sisi pia tunaweza. Cha kujifunza kutoka kwao ni "we too can do it". Tuone wamefanyaje hivyo, ili na sisi tuige yale bora. La sivyo in 20 years time gap hiyo itakuwa kubwa sana. Mdau Mushi.

    ReplyDelete
  11. www.tanzaniasports.comDecember 11, 2009

    Tanzania kuna mambo haya try to mingle with Tanzanian high society.Nothing personal!. THIS IS VERY PERSONAL."BUT WWW.TANZANIASPORTS.COM DO GO PLACES BIG TIME!!"

    ReplyDelete
  12. jamani huo uwanja upo kijijini ndio maana upo mazingira hayo ukenda town ni tofauti kabisa na ni bomba tu

    ReplyDelete
  13. Tupeni picha nyingi za india. nafanya hapa kazi na hawa wahindi fulani wanajisikia kweli. kwa vile tukisikia habari za india ni taj mahal tu...Kumbe kuko hivyo. Hebu Jumatatu ifike niwaonyeshe sijui watasemaje...wanajiadai africa africa

    ReplyDelete
  14. Jamaa anacount nimewekewa nyama ngapi hapa jamani. Au lilikua pilau ya vegans?

    ReplyDelete
  15. mdau wa dec 12,01:23:00 wahindi wasikutishe kabisa africa tena tz ni kuzuri sana na hao wanaosema hivyo nina uhakikia awajafika india maana wakija huku nao hao wanakuwa wageni tu kama sisi tunaosoma huku pia wahindi ni maskini sana ukitaka picha nakupa email yangu wasiliana nami alafu nitakuytumia picha za huku india nipo hapa walipo vijana wangu wa soka mdau jjozzee@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...