Mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi (kulia) akimtoka beki waMtibwa Sugar Shaban Aboma katika mchezo wa Kombe la Tusker uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar. Simba ilishinda 2-1

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Naomba tukutane na Yanga kwenye nusu fainali ili wapumzike mapema,kwani wana ngebe sana,jana walikuwa wanawashangilia mtibwa lakini baadae baada ya samba kali wakatuunga mkono- safari ni safari tu lazima muondoke tu,poleni mtibwa nyie bado kwetu
    shabiki wa kweli wa Simba.

    ReplyDelete
  2. Mimi ni Yanga ila naona kila dalili za kombe kwenda kwa mnyama-Simba.

    ReplyDelete
  3. Michu..thanks for a wonderful picture,..namuona Haruna Moshi ' Boban' Professional Player akichanja mbuga,tuweke unazi pembeni huyu ndo mchezaji bora wa Tanzania kwa sasa

    ReplyDelete
  4. hata mzuge kwa kuweka picha za simba na vimaoni vyenu vya kuisifia ukweli upo palepale... ferg kafuliaaaa kamuiga wenger kupanga vitoto mechi kubwa wajanja wamemla mchonyo... he!he!heeeeeee!
    after mark hughes, benitez is a dead living body... mchonyo wake usha komaa

    ReplyDelete
  5. Mkuu wa wilaya Tageta kwanza nasikia utapewa mkoa wa Kigamboni Kikwete akishinda uchaguzi mara ya pili maana kaamua kuwapa madaraka vijana. Turudi kwenye mpira wachezaji wetu ni wadogowadogo mno siku hizi ni nadra kuona mwenye umbo kubwa kama zamani sijui kama tutaweza kufanikiwa kuingia kombe la dunia siku moja.

    Wako wapi wachezaji wenye siha kubwa kama Nteze John, Kitwana Suleiman, Innocent Haule, David Mwakalebela, Bakari Malima, Pita Tino, Juma Mgunda,Yasin Abuu Napili, Said Mwamba Kizota, Salum Kabunda, Pita Muhina, Mustapha Hoza, Fikiri Magoso, Issa Athuman, Makumbi Juma, Hussein Masha, Gebo Peter,Mohamed Mwameja, Rifat Said, Gasper Lupindo, David Mihambo, Mbuyi Yondan, Atanas Michael, Edward Chumila, Dua Said, Rashid Mandanje,Jimmy Mored, Rajab Rashid "Msingida" na wengine? Inakuwa vyema kuwa na wachezaji mwenye mwili mkubwa ili wachanganyikane na wale wa kawaida na wenye umbo dogo kwenye timu ya Taifa.

    Utakuta hata wale wenye umbo la kati enzi za Mwalimu na Ruksa wanaonekana wakubwa kwa wachezaji wetu wa siku hizi wachezeji kama Ramadhani Renny, Method Mogella, Fumo Felician, Rashid Abdallah, muhidn Sisso, Michael Paul, Kassongo Athuman, Abeid Mziba, Danny Muhoja, Agustin Haule, Rajabu Risasi, Seif Bausi, Abdul Malaika, Mchunga Bakari, Abdallah Waswa, Abdallah Msamba, Shaaban Anania, Suleiman Mkati,Abuu Juma, Kaungulila Maufi, Suleima Pembe, Maarufu Yassin na wengine ukiwaweka leo na timu yenu wataonekana mapandikizi ya watu.

    Na wale wenye umbo dogo wakati wa Mwalimu na Ruksa wataonekana kawida siku hizi wachezaji kama, Zamoyoni Mogella, Abubakar Salum, Erick Sagala, Roster Ndunguru, Thomas Kipese, Beya Simba,Ayub Mzee na wengine ndio wachezaji wetu wenye siha ya kawaida siku hizi. Chakula kimepungua siku hizi Tanzania au ni nini?

    ReplyDelete
  6. WE ANONY UNAYESEMA NI MCHEZAJI BORA WA TANZANIA NI KWA VIGEZO GANI? AME-ACHIEVE NINI KWA SASA ZAIDI YA KUPATA TEAM?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...