Ninatuma ujumbe huu ili uwafikie wasanii, directors, na producers wa filamu za Tanzania. Ningeomba wawe wana hariri (edit) hizo subtitles wanazoonyesha kwenye filamu zao kwa ajili wasioelewa Kiswahili.

Kwakweli ukifuatilia subtitles katika filamu zetu hizi unaweza kudhani kuwa waandaaji hawako serious na kazi. Yaani tafsiri ni mbovu kupita kiasi, na kunakuwa na makosa ya kisarufi chungu nzima.
Mfano filamu 'the Cold Wind' ya kina Ray na Dokta Cheni. Story-line ni nzuri ila mtu aliyetafsiri amechemsha tokea mwanzo hadi mwisho wa filamu.

Nilikuwa naangalia na rafiki yangu mnaigeria, yeye hakuweza kuielewa filamu kwani makosa katika tafsri yalikuwa yanamchanganya.

Kama basi mnataka kuuza filamu zenu nje, basi tafadhali tafuteni wataalam ili wahariri subtitles, naongelea mtu aliyekuwa fluent kwenye lugha zote mbili. Tumeni kazi basi Taasisi ya Kiswahili hapo UDSM, au mkizidiwa, siku hizi kuna hata google translator ya kiswahili mtandaoni:

http://translate.google.com
mdau J.M


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Mdau J.M umeongea mambo ya msingi kabisa hta mm ni mshabiki mkubwa wa filamu za kiswahili tokea nipo nyumbani, ila maumivu ni kwamba subtitles ni zaidi ya mbovu, jamani tuwe makini maana filamu zinaenda mbali siku hzi, mbona mnatutia aibu!!!!!

    HYD.

    ReplyDelete
  2. Mdau aliyepost hii kitu labda uzungumzie movie zingine, ila kwa hii uliyopost yapo mimi naona subtitle ziko vizuri tu. Usitegemee hata siku moja subtitle zikawa precise na jinsi maneno yanavyotamkwa...lazima kuna baadhi ya maneno yatarukwa, tena hiyo google translate uliyoisema wala sishauri watu waitumie sana kwani hata yenyewe inachapia maneno meengi sana ya kiswahili, hususan katika uumbaji wa sentensi. Hata ukiangalia movie zinazotoka huko Holywood lazima utakuta subtitle hazikidhi, na tatizo linakuja kwa mtu ambaye unajua lugha zote mbili zinazotumiwa, yaani inayoongewa na iliyoandikwa kwenye subtitle. Kwa mtu asiyeelewa kiswahili akisoma hizo subtitle anapata ujumbe wa movie na ndio lengo kuu la subtitles. Nawasilisha.

    Mdau.
    Poriwood.

    ReplyDelete
  3. Wewe mdau JM, acha ushamba wewe, wewe unafikiri wanigeria ni watu wa maana sana...hizo subtitles mbona hazina makosa yoyote, huwezi kuandika subtitle neno kwa neno....usiandike kitu bila kufanya uchunguzi...ukiandika neno kwa neno basi mtu hataangalia movie na badala yake atakuwa anasoma maneno tu..kwa hiyo kutoa brief intro. ni sahihi kabisa..UPO HAPO???

    ReplyDelete
  4. Ankal Michuzi, nimeguswa na mada hii. Napenda kutoa mchango kwa wasanii wetu. Nafahamu kuwa wanafanya kazi sana, na papo hapo wanadhulumiwa sana na jamii yetu, kwa maana ya kutothaminiwa ipasavyo, na kuporwa malipo ya kazi zao.

    Hujuma hizi zinaendelea humo mitaani muda wote, kutoka kwa wafanyabiashara matapeli na jamii ambayo au haielewi au haiheshimu haki za hao wasanii. Tunapoongelea ufisadi, tuwe tunaongelea pia suala hilo.

    Mimi ni mwalimu wa ki-Ingereza, na kwa wakati huu nafundisha somo hilo kwenye chuo kimoja huku Marekani.
    Najitolea kuhakiki tafsiri za kwenye filamu za hao wasanii wetu.

    Miaka kadhaa iliyopita, niliwahi kuona tovuti fulani inayoelezea habari za nchi yetu. Ni tovuti rasmi. Niliona kuna haja ya kufanya marekebisho ya ki-Ingereza kilichotumika, nikapeleka barua pepe kwa wahusika, nikijitolea kusahihisha. Hawakunijibu, na Taifa liliendelea kudhalilika kutokana na ki-Ingereza kibovu kwenye tovuti ile.

    Naleta ujumbe kwa hao wasanii wetu, kuwa niko tayari kuwanyooshea ki-Ingereza bila malipo. Wanafanya kazi nzuri sana, na mimi nataka tuendeleze libeneke. Anwani yangu ni info@africonexion.com.

    ReplyDelete
  5. translator ya 'google' au hata ya kwenye kompyuta vile vile huharibu dhana, maana. misemo, nahau n.k

    Mimi naamini kuna watu wengi tu wanaoweza kujitolea kuwafanya tafsiri sahihi ya kiswahili kwenda kiingereza bureee, ila mradi tu kina Ray na Cheni wakubali mtu/watu waliofanya tafsiri pia wawe wanatambulishwa kwa majina na title zao kama directors/actors/makeup/wardrobe-dressing etc

    Tuheshimu lugha zote, tusiwe kama magazeti ya kiswahili Tanzania yanayoandika kiswahili cha mtaani kama 'diwani ashikwa pabaya' wakimaanisha ameumbuliwa kwa kula pesa za maemdeleo, hapa hata gazeti la serikali la HabariLeo pia wanatumia kiswahili cha kujiweni ingawa si gazeti la udaku.

    Mie huona hata magazeti ya Udaku kama The Sun la Uingereza pia hutumia kiingereza sanifu cha kiwango cha 'plain english' ambapo hata mtanzania anaweza kujiendeleza ktk lugha ya kiingereza kwa kutumia gazeti la The Sun.

    Kwa Tanzania ni kinyume, maana mgeni hawezi kujifunza kiswahili kwa kutumia magazeti au hata movie za kiswahili kwa kuwa waandaaji wa magazeti na movie za kiswahili wanatumia kiswahili cha 'kijiwe cha mtaani kwao'.

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  6. MALALAMIKO YA MZAZI MAKINI KTK GLOBALPUBLISHERSTZ.COM 29/12/2009pengine ni kukosa umakini wa kila kitu kuanzia uandaaji, uchapishwaji na lugha pia:

    Leo naomba kutumia blog hii kuonya wazazi wenzangu na walimu kuhusu vitabu ambavyo watoto wetu wanatumia ilikujiongezea maarifa. Kitabu hichi ni cha Science kinaitwa "Primary Science Workbook - Fountain of Tests and Examination" by DASIANUS B. CORNEL.



    Below are some of the questions and answers as written on the book and there are the ones which are so obvious that one can tell the answers are wrong. Imagine the ones I do not know or have forgotten, it could even be 20/50 answers were wrong.
    Try yourself out.

    N.B MAJIBU YA MWANDISHI WA KITABU YANABAINISHWA NA HERUFI KUBWA:
    1. Communicable Diseases can be caused by?
    (a) Heredity
    (b) ALLERGIES
    (c) Chemicals
    (d) Organisms

    2. John was suffering from a burning sensation in the stomach. The possible cause is
    (a) Flu
    (b) FATIGUE
    (c) diabetes
    (d) Excess acid.

    3. Killing of disease causing germs either by boiling, burning, or by the use of disinfectant is called
    (a) Vaccination
    (b) ISOLATION
    (c) Sterilazation
    (d) Sanitation

    4. Which of the following drugs may affect your health if often abused in your presence
    (a) Tobacco
    (b) COCAINE
    (C) Khat
    (d) Cobber's glue.

    5. If a person is suffering from Anemia, he should eat more
    (a) Green leafy Vegetables
    (b) MEAT AND FISH
    (c) Maize and Beans
    (d) milk and Uji

    6. Drinking too much alcohol causes a disease of the liver called
    (a) Cataract
    (b) Malaria
    (c) Cholera
    (d) Cirrhosis

    7. Which of these diseases is caused by the mosquito
    (a) tuberculosis
    (b) influenza
    (c) CHOLERA
    (d) Malaria

    8. A child took a meal of Ugali, Biscuits and soda. This meal has far too much
    (a) Carbohydrates
    (b) PROTEINS
    (c) Vitamins
    (d) Fats

    9. Cancer cells are distroyed by
    (a) Chemotherapy
    (b) Pathogens
    (c) VACCINES
    (d) Viruses

    ReplyDelete
  7. Hata mimi nimshabiki wa movies za kiswahili. na toka nimeanza kuziangalia hizi za kiswahili za kinigeria naona kama uchafu vile. Kwa kujitahidi watanzania wamejitahidi sana kuonyesha kama ni office ipo inayoeleweka, hospitali kachumba kanaeleweka etc etc...compare to Nigerian movies…..(I nees some witness here) …Ila ombi langu ni kwa wahariri wa hizi movies Scenes Editors..(I guess that is what they are called.) Mimi ningewaomba wajaribu kuondoa scenes nyingine ambazo hazina umuhimu ili kupunguza muda wa Movie. Mfano 1) Kama mtu akiwa anatoka nyumbani kwenda kazini basi onyesha anavyoingia kwenye gari then kidogo onyesha anavyofika
    2) Kama watu wanakula basi onyesha kidogo tu mwanzo wa dinner lao la mchana na mwisho. 3) kama ni romatic scene unataka kuonyesha watu wako beach basi onyehsa in brief….imi kitenda cha kutumia 15 minutes kuonyesha mtu yupo kwenye gari tokea sijui sinza au mlimani mpaka mjini , 20 minutes kuonyesha watu wanakula pilau that is insane. Sio kwa vile movies za kinigeria zinakua refu basi na za kwetu tufanye hivyo hivyo. Movie ikiwa nzuri na fupi kesho nitapenda kununua movie nyingine kutoka kwao lakini movie inakua na party mbili mpaka tatu just to stretch unnecessary things is not nice. Kama mnataka market ya movie zenu nje ya nchi one party is enough…kama unaweka sequel basi maliza movie halafu uanze na nyingine. Movie masaa matatu huo muda uko wapi wa kukaa chini hivyo?

    Halafu ukianza na hadithi hii maliza na hiyo hiyo mambo ya too much twists and turns too much wala hayapendezi…

    ReplyDelete
  8. mdau londonumefafanua safi sana sana duh kaka michuzi umetukutanisha safi sana mjadala unaendelea safi na tunarekebishana tabia kanumba unakipaji safi sana mzee song limetulia sana san yaani tena ulivyomshirikisha mtanga pamependeza sana sana kaka wewe msanii tena wadamu sio wakuchovya kula bata kwakwenda mbele mzee Mdau sweden

    ReplyDelete
  9. Wadau mnaomponda JM naona mnachemka, jamaa wanahribu zaidi ya sana haswa filamu za RAY na KANUMBA. Yaani unaona haya kussema hzi filamu zinatoka Tanzania kwa kua mgeni akiiona atajua tu kwamba kuna makosa ya makusudi . Mfano filamu za Three divorce na Too late kna makosa mengi ya kimaandishi. Jamani msiongee kiubishi.

    HYD

    ReplyDelete
  10. YAANI WEWE JM NI BONGE LA MSHAMBA SANA SASA MNIGERIA WEWE NDO UMEMUONA NI MTU WA MANA SANA? PLEASE CHAGUA CHA KUSEMA SIYO HUO UJINGA WAKO. TUWAPE SIFA ZAO WANAJITAHIDI WACHA KUKASHIFU ILI UMFURAHISHE HUYO MPOPO WAKO.

    ReplyDelete
  11. Ok ni kweli kabisa translation ni ya ki layman! Yaani imetafasiriwa na mtu layman ambaye anajua jua kiingereza. Direct translation ambayo haikubaliki, hapo ndio linakuja sauala la profession akina Kanumba ni kati ya vijana wa kitanzania wanathubutu! std 7 with such a profound daring spirit! Its simply amazing! Wangapi wana shahada za sanaa and yet hatujawaona katika movie industry!
    Ushauri wangu kwa wasanii wa Kibongo hasa hasa armatures jaribu kutafuta ushauri kwa wataalamu tengeneza kitu kinachokubalika na tabaka zote wapo watu wanaojua kutafasiri vizuri watumieni

    ReplyDelete
  12. Scripts za google translate ni kwamba zimewekwa kila neno na maana yake ya kila lugha kwa hiyo ukibadili lugha inabadili neno moja moja si sentensi nzima wala tense,hapo zipo mchanganyo wa lugha unapo anza

    ReplyDelete
  13. sioni kosa lolote katika tafsiri hizo, wanaijeria hawamudu kiingereza zaidi ya watanzania

    ReplyDelete
  14. MSIZUNGUKE SANA TATIZO HAPA NI KANUMBA HAJUI KIINGLISHI

    ReplyDelete
  15. Aisee KILO hebu chunga lugha yako. Please stop using superlatives ambazo zinadhalilisha wenzako. Alaa!! I agree with JM kuwa subtitles zinazotumiwa kwenye movies hizo zinashusha hadhi ya hizo films. Kwa kweli na filamu zenye stories husika hazina ubunifu kwa sehemu kubwa. Mengi wanaiga from Nigerians. Angalia filamu za Ghana na Kenya na hata Senegal zimetungwa na watu wenye elimu. Nchi yangu naihurumia ya Tanzania si wanamuziki si wainjilisti si wanasiasa sote tumeshupalia kuiga. We have nothing indigenous to offer. Just compare matangazo juu ya Tanzania ndani ya CNN na ya nchi nyingine kama Kenya, Malaysia, Croatia. La kwetu wala it is not eye catching. Jamani siyo naponda ila nakosoa tu.

    ReplyDelete
  16. Jamani ukweli lazima tuseme, binafsi hata kabla sijasoma maoni ya wadau niligundua makosa ya wazi kabisa kwenye hizo tafsiri, na nadhani zinaweza kutumika kama mfano wa tafsiri zilizo chini ya kiwango kwenye darasa la tafsiri. Tatizo watayarishaji wa filamu huko nyumbani wanataka wafanye kazi zote wao, suala la mgawanyiko wa majukumu ni kama halipo. Unakuta kinara wa filamu ndiye aliyeandika ‘script’, huyo huyo ndiye mwongozaji, ndiye mchagua maeneo, sasa katika hali kama hiyo nani atagundua makosa? Tugawane ulaji huo jamani ili kuongeza ubora wa kazi zetu.
    Asante; mdau wa Lugha za Kigeni na Isimu!

    ReplyDelete
  17. Wadau,
    Naomba nitoe mfano huu, subtitle inasomeka 'Three Divorce; je Mmarekani/Muafrika ya Kusini/Mhindi/Mjapani au Muarjentina,n.k, ambae hana ufahamu wowote kuhusiana na jamii ya Kiswahili ataelewa nini kuhusu 'movie' ambayo ina subtitle hiyo ili ainunue anapoikuta dukani au Maktaba ili aiazime?
    Kutohoa Kiingereza kwenda Kiswahili sio tatizo kwa sababu mtumiaji wa mwisho ni Mswahili ambaye. Tatizo linakuja pale ambapo tunataka kutohoa Kiswahili kwenda Kiingereza,HIYO HAIWEZEKANI KWA SABABU MTUMIAJI WA MWISHO SI MSWAHILI.
    Hii ni kama vile Bw Kanumba alivyosema kuwa 'anaclose'akimaanisha anafunga kwa ajili ya Swaumu.
    Mtanzania,
    tmajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
  18. Try writing a perfect English sentence on the Google language tools, translate it to other swahili then you will see after that do the vice versa.

    ReplyDelete
  19. Nakubaliana na wadau wanaosema kwamba subtitles za kiingereza kwenye filamu za kiswahili zina makosa makubwa. Na hizo ni kwa filam nyingi za bongo.

    Hapa wanalofahamishwa watengeneza filamu ni kujaribu kupata wataalamu waandike vitu vilivo kwenye standard inayoeleweka, na sio mtu mmoja kujaribu kufanya kila kitu kwenye filam.

    Na kinachochefua zaidi ni vile watanzania wanavoiga tamaduni za kinigeria wakati sisi ni tofauti na wao. Angalia vivazi na hivi karibuni hata kujipata yale marangi usoni!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...