Hey Joe
Mashabiki wa Jimi Hendrix,mpiga gitaa maarufu (electric guitar) ambaye anasemekana kuwa ndiye bora kuliko yeyote yule aliyewahi kutokea,watapata nafasi ya kusikia vitu vipya kutoka kwa mkali huyo hivi karibuni.
Familia yake kwa kushirikiana na Sony Commercial Music Group wanatarajiwa kutoa album “mpya” tarehe 8 mwezi Machi. Album hiyo imepewa jina la Valleys of Neptune imesheheni rekodi za Hendrix za kutokea mwaka 1969. Nyimbo zilizomo katika album hiyo ni zile ambazo hazijawahi kupatikana kibiashara sehemu yeyote ile duniani.
Jimi Hendrix alizaliwa tarehe 27 mwaka 1942 huko Seattle,Washington na kufariki jijini London nchini Uingereza akiwa mwaka 1967 akiwa na umri wa miaka 27 tu.Ukitaka kujua zaidi kuhusu maisha ya Jimi Hendrix ambayo yalikuwa na mikasa ya kila aina,bonyeza hapa.{ http://en.wikipedia.org/wiki/Jimi_Hendrix}
Written for Blog ya Jamii by
Written for Blog ya Jamii by
www. bongocelebrity.com
Alifariki 1970 na sio 1967
ReplyDeletehilo ndo falme la gitaa toka enzi hizo mpaka leo hakuna kama yeye
ReplyDelete