

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya marehemu Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakisindikizwa kuelekea chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar mchana huu.

Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mtoto wa Chifu Abdallah Fundikira, marehemu, Swetu Fundikira, MTM 1900 Sajenti Roda Robert(42) wa kikosi cha JKT-Mbweni na MT 75854 Koplo Ally Ngumbe (37) wa JWTZ-Kunduchi wakiwa katika chumba cha Mahakama leo.

Ndugu wa marehemu, Swetu Fundikira wakiwa nje ya mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi ya mauaji ya ndugu yao ikiwa inaendeklea.
Kushoto ni Nzwala Fundikira na kulia ni Ismail Fundikira.
Washtakiwa wamefikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Geni Vitus Dudu na mashtaka yameendeshwa na wakili wa serikali Monica Mbogo aliyekuwa akisaidiwa na Beatrice Mpangala
Mh. Dudu aliwaeleza washitakiwa hao kwamba kwa mujibu wa kosa linalowakabili hawatakiwi kujibu chochote na kwamba kosa hilo halina dhamana kwa sababu hiyo mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu na kuairisha kesi hiyo Februali 10 mwaka huu, itakapokuja kwaajili ya kutajwa. Akaamuru washitakiwa wote wamepelekwe rumande.
Ndugu wa marehemu Swetu walikuwepo mahakamani na kusikiliza kesi kwa utulivu, huku wakisema wana imani kwamba haki itatendeka.
Swetu Fundikira alifariki dunia Jumapili asubuhi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambakoo alilazwa toja Ijumaa usiku baada ya kupigwa sana na wanajeshi watatu, wawili wakituhumiwa kuwa ni hao pichani na mwingine wa tatu haijulikani alipo na msako unaendelea.
Marehemu Swetu alizikwa jana kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar. Kifo chake kimezua zogo kubwa miongoni mwa wananchi ambao wanadai uongozi wa majeshi yote ya ulinzi na usalama uwe wakali kuhakikisha askari wachache wenye mtindo wa nidhamu hawapewi nafasi ya kuchafua majina mazuri waliyo nayo pamoja na ushirikiano mwema kati yao na jamii.
Hivi jamani jeshini mtu anaachiwa kufika hadi size kama ya huyu mama hapo juu? mwenyewe hajiwezi kwa uzito atawezaje kubeba vifaa vyake vitani? au kwa vile tanzania toka katika amani hatujiandai kwa vita basi jeshi letu linajiachia namna hii?
ReplyDeleteanko nanihii, mie naomba kitu kimoja. Tunamuomba mwanaharakati wetu, yohanna mashaka aandike atiko moja kuhamasisha wananchi ili tulivalie hili swala la nidhamu njuga. Nadhani bulogu ya jamii ina sauti kubwa sana katika jamii na tunapokuwa na wahamasishaji wanaokubalika kama mashaka nadhani kila mtu atajiunga kupinga hizi tabia chafu za kinidhamu katika majeshi yetu ya ulinzi. siyo kwamba natetea uchochezi, la hasha, nataka mtu au kijana anayekubalika kutuongoza katika hili. hii tabia ipo pia kwenye jeshi la polisi ambao nao wananyanyasa raia kupita kiasi kana kwamba hakuna sheria nchini kwetu. muda umefika huu ujinga ukomezwe
ReplyDeleteKaka Michuzi pole na kazi!! Huwezi amini tangu asubuhi nilikuwa nachungulia kila sikunde kwenye blog yetu ya jamii ili nione hii habari kwani huwa uko shapu kutoa habari haraka. Kifo cha huyo kaka kimenisikitisha sana na ninaniomba sheria ichukue mkondo wake kwa kuwaathibu watuhumiwa kwa kosa walilolitenda yaani kupigana pasi kunatoa roho ya mtu. Hivi tunaelekea wapi?? Watu tumekosa ubinadamu ila malipo ni hapa hapa duniani. Ee Mungu mpumzishe kwa amani kaka yetu.
ReplyDeleteINAWEZEKANA KABISA,KUNA HILA KATIAK JAMBO HILI LA KINYAMA.
ReplyDeletePENGINE HAWA WANAJESHI WALITUMWA ITS A CONSPIRACY (issue)REAL,MAANA SABABU YA KUMPIGA MTU NA KUUMUA SIO KITU CHA KAWAIDA.
NI MAONI YANGU TU.
Mh hapo mzigo wa kesi utamuangukia huyo aliotoroka ninavyozijuwa hukumu na mahakama zetu,si tunakumbuka ya ZOMBE? na kamwe hatopatikana.TANZANIA ZAIDI YA UIJUAYO!
ReplyDeletehawa jamaa wameua bila kukusudia.ni kwa aajili ya hasira tu.Unaweza kuta fundikira nae alikuwa na magonjwa mengine.wasamehewe tu kama wanavyosamehewa mafisadi wengine kama ditopile mzuzuri.Hawa wanajeshi watapata shida sana.nawaonea huruma sana kwani hawajulikani.ila angekuwa kigogo!!!!!!!!!!!!!!pole yaooooooo
ReplyDeleteyaoneni kwanza hilo lingine linaangalia pembeni tusione sura wauaji nyinyi mbona hapo mko kimya wapigeni na hao walio wa arest si mna hasira sana nyinyi? yani naomba mungu mfungwe miaka mia na kenda kama maddoff tapeli wa majuu jela ndo dawa yenu shwain sana handsome wa watu mmemnyofoa roho hivi hivi kwa nini mnamsaidia Mungu kazi yake ??mfungweeeee hata mkinyongwa ni poa sana tuu mnadhani vile zombe aliachiwa na nyinyi mtaachiwa?? hii imekula kwenu mlikutwa kwenye tukio mkiwa mnafanya ufirauni wenu lazima mfungwe tuuu na huyu mwanamke kazaa kweli?? kachangia na yeye kifo cha marehemu aibu sanna mfungwe mfungwe mfunweeee EE MUNGU WA MBINGUNI HATA KAMA UKO LIKIZO RUDI TU UJE USIMAMIE HII KESI HAWA WAUAJI MANDULI KATILI WAFUNGWE AMEN!!
ReplyDeleteroda pole sana najua you are innocent, you are such a kind girl.i am so sad to hear this, hang on there we are praying for you and your family.edith
ReplyDeleteWewe Edith unampa pole Roda unasema unajua kuwa yeye hana makosa,kwanini haukuenda mahakamani kuprove?au na wewe ndio hao wenye tabia zakina roda?
DeleteUle usemi unaosema "USIMPE KICHAA RUNGU" ndo maana yake hiyooooo....wengine hawa hawakutakiwa kuwa wanajeshi...walitakiwa wapimwe akili zao kwanza...!!
ReplyDeleteHivi kweli huyo dada ni mwanajeshi? kwa size hiyo hivi huwa kweli anafanya mazoezi ya kijeshi huyo?
ReplyDeleteMWANZO MZURI LATIKA KUDAI HAKI. MATUMAINI YANGU MWUISHO WAAO NI JELA. HIZII JEURI ZA WANAJESHI ZINASIKITISHA, HATA KWA AKINA MAMA? KWELI HII NI BALAA.
ReplyDeleteKWA KAWAIDA KWENYE UGOMVI WAKIWEPO WANAWAKE, SULUHU HUWA INAKUWEPO. LAKINI HAPA NADHANI HUYU MAMA NAYE ALIKUWA KINARA KWENYE HUO UKAATILI.
KUMBUKA, MSHAHARA WA DHAMBI NI MAU............
duh ama kweli tanzania ni tambarare, idadi ya washitakiwa ishapunguwa mara ile na kuwa wawili mmoja akiwa kibonge asoweza hata kufukuza paka wa miguu mitatu.
ReplyDeleteWANAJESHI WENYE VIBURI KAZI KWAO KWANI KUSEMA KWELI HAKUNA MTU BORA KUZIDI MWEZAKE!! MACHONI PA MWENYEZI MUNGU SISI WOTE TUKO SAWA KWA MTU MWENYE MAADILI MWENYEKULELEWA NA AKAELIMIKA NA MALEZI UNAPASWA KUWA NA UBINADAMU KILA MMOJA WETU
ReplyDeleteTIZAMA SASA WALIVYOUBULIWA NA MWENYEWE MUUBA HIVI KWELI UNASIMAMISHWA KTK KESI YA KUTOA UHAI WA BINADAMU MWEZAKO HATA KAMA HUTOFUGWA JE UNAJISIKIAJE NA NAFSI YAKO KUWAFANYA WATOTO WA MWEZAKO YATIMA KWA NGUVU ZAKO??????
JE LEO HII HULALI KWAKO WATOTO ZENU WANAJISIKIAJE MAMA YAO MUUWAJI AU BABA YAO MUUWAJI NA HATA MASHULENI WATAONGEA NINI NA WENZAO NA WALIMU WAO WANA WATIZAMA VIPI???
This case is SUBJUDICE and as such its beyond the scope of public debate.If there is substantial public anger/outcry against the defendants it can be claimed by the defence that those two can never get a fair trial.So tahadhari na maoni ya wadau kwenye blog ya jamaa.Wenye ujuzi wa sheria tuelezeni
ReplyDeleteWakatabahu
Mbona mkao wao hauna nidhamu? Ukiwa mahakamani mbele ya hakimu utajiachiaje hivyo kama umekaa baa? Hasa huyo mwanaume aliyening'iniza mikono!!
ReplyDeleteAibu
wewe Edith wa Jan 27 02.46pm. Hebu vaa viatu vya baba wa marehemu, wadogo zake na wanae.
ReplyDeleteNijuavyo mimi, mwanajeshi hata awe mpole vipi nyumbani kwake au mbele ya ndugu zake. Akiwa kazini ni mtu mwingine kabisa,tena akiwa mbele yamtanzania wa kawaida atataka kila mtu amuone yeye ni zaidi bila ya kujali yeye amekosea au la. Huwa nashindwa kuelewa hawa watu huwa wanafundishwa nini huko kwenye training zao. Kazi yao ni kuthreat raia na kuwanyanyasa kivyovyote vile eti kwa ticket ya uanajeshi wao. Wamenyanyasa sana watu na hizo kombat, na zipo incidence nyingi sana za hawa watu kunyanyasa raia. Sasa hakuna mtu anaejua kuwa huyo roda wako ni innocent, au kwa sababu ni rafiki au nduguyo? Na wenye ndugu yao alokufa? Tunajua kisheria hao wanajeshi watatoka cuz itakua ni kuua bila kukusudia but GOD MUST ACT, Damu ya mtu haiendi hivihivi. Edith keepon prayin for ya sister but remember Mungu nae anaangalia. Simjui marehemu wala huyo roda na wala sina undugu nao ila imeniuma saana sababu ni matukio mengi yanafanywa na wanajeshi ya unyanyasaji wa raia na mengi hayaripotiwi, watu wanaumizwa kila siku wengine wanabakwa but no action is taken. Then mtu analia eti we knw u r innocent n we r prayin for u. kha!
Hapa Kaka Mithupu ni kujiuliza Enzi zile za Nyerere vilikuwepo hivi?Jibu ni BIG NO hii imeanza miaka ya 20.. ni kutokana na mfumo mbaya wa Serikali ya TZ wao wanajinunulia Mashamba ,Majumba ,NHC wakijenga huko Boko wanajiuzia wao Wakurugenzi,Ma Profesa,Mawaziri etc etc ,Nyumba ya Gavana billion 1.27 jamni wakati Hawa JWTZ,,Walimu wako Stressed na life hawaona mbele wanakoenda hasira zao wanamalizia huku hakuna mtu wakusikia kilio cho kaka ,Na ndo maana Enzi za Mwalimu kulikuwa na Barracks wanaishi huko vizuri tuu hiv sasa mtu napanga na nyumba Dar zilivyo ghali hao wakubwa wanapangisha manyumba ya bila laki 250 hupati hiv jamn hii nchi inakoelekea wapi?NHC zilikuwa ni nyumba za wanyonge sasa Wahindi ndo za kwao hiv Nyerere hakuwa mjinga kupangisha wazawa alijua wananchi wachini hali zao, ukitaka maisha ya loko ukaishi Uswahilini ,Kiwanja bila 1.5m hujanunua ,Hiv wanadhani Mlalahoi,Mfanyakazi wakima cha chini,Wanajeshi,Walimu,Mfanyakazi wa chini wa serikali atajenga kweli ?Hasira zao zinaishia kwetu ila hawa wanaojiita Viongozi ipo siku kutakuwa badogo hapa TZ maana watu maisha ni magumu afadhali ya jana sidhani km wanaliona hili?Ujambazi kila kona ,Police,Traffic wanapata ulaji wakati mwingine akitoka kwake na 500 jua atarudi na 500 hawa JWTZ hawana hata pakupata sh 2000 apewe rushwa na dereva dalaladala,taxi etc etc bora traffic police na Police wanapata hata kijisenti.Ila kaka Michuzi huu Uchaguzi tuweni Macho hilo walijue kuwa wananchi wamechoka ,Majambazi ni hao hao wastaafu wa JWTZ na wengineo wako kazini unadhani raia wakawaida anaweza tumia mabomu au bastola jueni na wao wamechoka ,Hii kesi isikilizwe tuu lakini mwisho wa yote hakuna la maana ,Watanzania tumeumia kwani sio kesi ya kwanza hii ,Wafiwa poleni hii nchi aliye nacho anacho asiye nacho basi!!!!
ReplyDeleteweweeeeeee..nimefurahi..mie kufikishwa hapo mahakamani nimefurahi kwani kila mtanzania amewaona wakatili hawa....haijalishi kuna mwanamke sijui wataonewa huruma wala nini lazima haki itendeke sawa...huyo Roda km ni mwanamke wakuonewa huruma kwanini hakuwaambia hao wenzie waacha kumsulubu kaka Swetu km kweli naye ana utu.....wewe Edith hapo juu unasema Roda is innocent and kind girl or woman?? unatakiwa umshangae kumbe linaweza kushiriki kuua ht wewe na ndugu zako mtakutwa na haya kupitia huyo huyo innocent Roda.....shauri yako.....naombea huyo mwingine akamatwe shwaini kabisa....kila muhusika aadhibiwe vilivyo bila kujali gender na nani aliyeanzisha kurusha ngumi....kutoa maisha ya mtu jamani kwa ugomvi wa kijinga jinga...........tena Jeshi liwe linawaadhibu zaidi watu hawa wanaochafua majina ya jeshi...kwani mimi mwenyewe hapa never in my life nitafeel safe nikionana na mwanajeshi hasa nisiye mfahamu siku zote nitarun for my life.....bastard's wanajeshi wote wenye roho za kuua raia na kujichukulia sheria mikononi kwani polisi kazi yao nini....si mkiona wahalifu muwapeleke huko polisi wadili nao...nyie kazi yenu kulinda nchi na maharamia wa nje zaidi.......
ReplyDeleteHere we go again its a privilege for a lot of people to post our comment on a Michuzi blog otherwise tunge chora kuta za majumba ile mbaya thanks to MICHUZI BLOG SPOT to keep us connected indeed we came a long way but it look like we all gat the same goal and that goal my honorable fellow TANZANIAN is peace and justice to have same equal rights it is sad not before tragedy happen we bound together let us be as one our daily whining of every aspect. my comment: Wed Jan 27 10:21 AM ordain SWETU RAMADHAN peace be upon him AMEN as our ADVOCATE OF PEACE and JUSTICE let us not bad mouth the system or our man and woman in uniform and let not forget that there other Government organization officials can drive some one insane we stop right here Wajeshi and Police we had bad mouth them not all are bad people as one our struggle with capacity to organize and courage to defend our rights of ruthless power on all areas and not forget Land Office how my people good TANZANIAN are being treated, why now all these came up because of our brother Swetu people are tired the saw a case similar to this our brothers walk away with blood on their hands, we cry for SWETU and stop crying and start P U S H (Pray Until Something Happen) may again peace be upon him the ADVOCATE OF PEACE and JUSTICE my condolence to all RAMADHAN MLAWILA
ReplyDelete..........Pale askari wa JW wenye hasira kali wanpoamua kujichukulia sheria mikononi........
ReplyDeletekama wanajeshi wenyewe huko bongo wanaosifiwa kwa ubabe ndiyo wako hivi, basu jamii yenu imejaa watu ambao ni choka mbofu sana. Hao wawili hapo juu hata wangekuwa wanane hawawezi kunipiga mimi mpaka nikafa. Mtu mmoja tuu ambaye siyo mgonjwa hawezi kuangushwa na huyu roda na mwenzake ali bila ya kutumia silaha ya moto.
ReplyDeleteMimi ninadhani mamlaka ya hawa wanajeshii ambao wamejiweke kwamba waooo ndioo kila kitu kwa wananchiii inabidiii jeshii liweke sheria kwakoo ili ilindee jamiii ambayooo inakatwaa kodii ili iwapee waooo mishahara ya kuishii duniani.Kwa kweli inasikitisha kwa jamii nzima yote ya usalama kujichukulia sheria mkononi,ambayoo ni kasumba ambayooo wamejiwekea wanausalama wengiii kuwadhibu raia kutokana na magwanda yaoo..kuwapola kila kitu bila mpangilio wowote kwa matumaa yaoo tuu.kuadhibiwa kwa hawa kwa kifungo cha maisha kutawashaa taa kwa wanausalama wengine kujua kwamba kuchukua sheria mkononi ni kitu mbaya sana katika jamii hii.Tatizoo laooo ni kwamba jeshii kiujumla kutoa mafunzoo ya mara kwa mara kuwafundisha na kuwakumbusha usalama wa raia na jinsi ya kutatua matatizoo ya raia ni ngumu zaidii .Kazi rushwaaa tuuu na kuandika proposal za kupata fedha bila kufanya kitu chochote.
ReplyDeletenyie wapiga box mbona mna bwabwaja tu kama si vile wasomi au kazi za box haziitaji usomi.kwanza kabisa hii story haijatimia hatujui kisa ni nini pili awa watoto wa wakubwa nao wana jeuri sana maybe marehemu ndiye alijifanya mbabe watu wakamuonyesha undava.
ReplyDeletehawa wanajeshi wenyewe choka mbovu hinakuwaje waliweza mpiga mtu adi kufa au marehemu alikuwa tungi.Mimi nazani huu ugovi ulitokea bar. Je adi upige hivyo wananchi walikuwa wapi. kutokana na hali halisi ya uchumu ali himekuwa ngumu sana adi wanadamu wanageuka kuwa animals .
hali ni ngumu sana bongo sasa mtu anaweza kukutoa roho kisa shilingi mia tu !! mimi ningependa jua chanza cha jamaa kupigwa .
Asante mdau Afghanistan
huyu dada anaonekana kabisa kaonewa.
ReplyDeletejamani ebu tazameni picha ya marehemu na huyu dada then linganisha.hata mimi na kamwili changu huyu dada hata kama ni mwanajeshi am 100% awezi kuzichapa am sure nita mpiga OK .
ebu tumieni common sense huyu jamaa kwanini walimchapa ? Lazima alileta ubishi au alikuwa anadaiwa .From no where akuna mtu mwenye akili zake timamu anze kumpiga tu mtu bila sababu.
ReplyDeletepili wanajeshi wetu jamani wanaishi kwenye hali ya shida sana kuliko hata wangekuwa wana pelekwa vitani. so wanamachungu sana bale unapo wakosea heshima . nimaoni tu jamani
From mpiga box odari sana
jijini Landon
tusiwahukumu wakati bado hawajahukumiwa. wengi wenu mnaogopa kupigwa mpaka kufa ndiyo maana mnatoa maoni mengi. lakini hao hao mna-suport au mmeshiriki kuwapiga/kuwachoma moto watu kwa kusadikika kuwa ni kibaka au mwizi hatakama mtu huyo ni mtiifu tunatabia ya kujichukulia madaraka wenyewe.
ReplyDeleteDuu mdau hapo juu NOT SUBJUDICE but ni PREJUDICED, and you are right if the public outcry is sooo bad they can use that defence kwamba kesi ikisikilizwa Dar or Tanzania kwa ujumla mahakama imekuwa influenced na public opinion so they will not get a fair trial ...remember INNOCENT UNTIL PROVEN GUILTY ,by COURT OF LAW that is. So please jamani punguzeni jazba mahakama ifanye kazi yake ,ndio ajali imeumbwa na kufa kwa ridhaa ya Mwenyezi Mungu kupo na ziraili wa binadamu ni sometimes binadamu but also some wanajeshi thinks they are above the HAND of LAW and WE WANT JUSTICE for uncle Swetu wetu !
ReplyDeleteMdau .
hao watuhumiwa na askari police wanaowalinda hapo mahakamani wamechoka.ukimpiga kikumbo lazima afe. hivi tuna jeshi kweli?
ReplyDeletehivi unamsindikiza mtu mwenye kesi ya mauaji kama bibi harusi? vibaya zaidi ni askari ambao wamefundishwa kuua na wanajua kutumia silaha. hawajapigwa hata pingu? watuhumiwa wamekaa mahakamani kama wanaangalia movie. ni kichekesho!!!!!
We Edith wacha ujinga...eti "we are praying for you"...Ngoja usikize kwanza mashahidi na ushahidi utakaotolewa mahakamani. Bahati nzuri kwa HAKI mashahidi walikuwa wengi na wamejitolea kutoa ushahidi. Hawa maaskari wamenenepa kwa jasho la wananchi. Usii"preempt" kesi.
ReplyDeletehapana hawa walidhamiria kabisa. inawezekana hawakudhamiria kuua kama mdau unavyodai hapo juu lakini mazingira yanaonyesha walidhamiria japo kumjeruhi vibaya sana kama si kumpoteza kabisa. kwanini wambebe toka k'ndoni waende nae hadi kule walipoenda kutolea kipondo??. t'was intentional man!! hebu angalia sura ya huyo mtaalam hapo anaonekana na sura flani hivi haijatuliatulia. halafu wakati wanaendeleza libeneke la kipondo, huyo dada roda ndo alikuwa anashabikia kuwa wampe discipline marehemu. baadhi ya binadamu tumekuwa na roho mbaya sana.
ReplyDeleteMda wa P&T
Poleni familia ya wafiwa, Swetu RIP. Jamani jeshi na polisi ni serikali kazi yao ni kulinda usalama wa nchi raia na mali zao sio kuua, sasa sarikali isipoangalia haya mambo ya polisi na wanajeshi kuua raia wasiokuwa na hatia siku moja nchi yetu yenye amani na utulivu hii amani itaondoka wananchi watachoka kuvumilia kupoteza ndugu zao au rafiki zao. kitu kama hiki kilitokea Mbeya Kyela Mwaka jana polisi waliua kijana asiyekuwa na hatia, huyo kijana akuwa na support kama ya Swetu. Sasa ni lini viongozi wetu watajifunza? Au mpaka iwe too late? wananchi watakapoamua kuchukua sheria mkononi?
ReplyDeletetusiwalaumu tu watuhumiwa bali hata mwajiri wake anastahili lawama kwa kuwapa kazi na kutokuwafundisha askari jinsi ya kukaa na civilian kwa amani. kwa hiyo akina Fundikira shitaki huyo mwajili wake (serikali) mpaka ifirisike ndipo watajifunza jinsi ya kuwatia nidhamu hao askari japo malipo yake hayatalingana na ndugu yako aliyefariki.
ReplyDeleteENZI ZA NYERERE WANAJESHI WALIKUWA WANAKAA KAMBINI, HATA SEHEMU ZA WENZETU HUWA WANAKAA KAMBINI NA SHUGHULI ZOTE ZA STAREHE HUWA WANAPELEKEWA HUKO HUKO, HUU MCHEZO WA KUWA ACHA HURU NA KUKAA URAIANI, NA WANAKWENDA MAHALI POPOTE WAKATI WOWOTE WAKITAKA, KAZI YA JESHI NA POLISI NI KAZI TOFAUTI NA ZINGINE WANATAKIWA WAKAE PAMOJA KWA NIDHAMI NA KUFUATA MAAGIZO YA WAKUU ZAO, SASA WAJENGEWE MAJUMBA PAMOJA NA WAKAE PAMOJA KAMA WANAENDA NJE BASI KWA KIBALI, NA HIY NI NDIYO NI KAZI YA JESI NA POLISI ILIVYO, NA WAACHE KUONA KUWA WAO NDO SHERIA, WAO NI WATU KAMA WATU WENGINE. KWANI HATA KAMA MTU ALIWAKOSEA HAWAWEZI KUCHUKUWA SHERIA MIKONONI MWAO WANGEMKAMATA NA KUMPELEKA POLISI NA SHERIA KUCHUKUWA MKONDO WAKE, HATA HIVYO INAONEKANA WALIKUSUDIA KUMPIGA KULIKOPELEKEA KIFO CHAKO HATA KAMA ALIKUWA NA UGONJWA MWINGINE KWA KILE KITENDO CHA KUMCHUKUWA TOKA SEHEMU YA TUKIO NA KWENDA KUMPIGIA SEHEMU INGINE MBALI NA TUKIO, MWISHO HAWA NI WATUHUMIWA WA MAUAJI WANATAKIWA WALE MBINGU WANAPOKUJA MAHAKAMANI, PINGI JAMANI WAPIGENI PINGU HAO
ReplyDeletewaone kwanza hao wauaji, wamejaza vitambi tu kwa beer za bure za mess, kama beer moja sh 850 kaka michuzi, what do u expect? akili zenyewe zinakua zimejaa machicha tu, sasahivi wanaweka sura za huruma, watu wenyewe hawana hata mikwaruzo, watasema marehem aliwaprovoke vipi hadi wamchangie 3/4 in one? e bwana justice tunaomba ifanyike. NO MATTER WHAT, THERE IS NO REASON TO JUSTIFY THEIR ACT.. wanatutia hasira na sisi raia tuanze kuwakandamiza maafande mitaani mmoja mmoja.. ohoooo.. mh. davis mwamunyange uko wapi? kwanini hawa vijana wako wanatoa roho za watu kila mara na wewe huwakanyi? je, sisi raia tunapaswa kuwakimbia wanajeshi tunapowaona na kuwachukia badala ya kuwakimbilia tukidhani kuwa ndio salama yetu? hii inatumika kwa both jeshi la polisi na jeshi la wananchi au jkt.. na mapolisi nao wana mambo yao vile vile, wao zaidi ni ujambazi,KAKA MICHUZI, UKIANGALIA SANA UNAKUTA KUWA YOTE HII NI NJAA TU.. kwanini serikali ISIWALIPE VIZURI HAWA WANAJESHI WETU NA KUWAPA MALAZI MAZURI, MAKAZI, ETC ILI NA WAO WAWEZE KUPENDA RAIA NA KUTUMIKIA NCHI KWA MOYO MMOJA NA MKUNJUFU?
ReplyDeleteE bwana tunataka JUSTICE HAPA.. R.I.P SWETU...
Mdau Kinondoni
Tukumbuke kuna mwingine ametoroka. Sijui wanamtafuta au la. Kama mtu ni innocent kwa nini atoroke? Huyu alietoroka ana lake jambo ambalo linawazidi waliopo kwa logic tu....
ReplyDeletenaomba kuuliza hivi kwanini marehemu alipigwa hivyo alifanya kosa gani mpaka akapigwa hivyo????
ReplyDeletesomething fishy here,why him?tuangalie na upande mwingine wa shilingi,tuangalie na mazingira ya marehemu alipopata hicho kipigo je hyu mama na jinsi alivyo kweli aliweza kupiga,sijui ila i really doubt,farid
ReplyDeleteAnonymous:Thu Jan 28, 07:15:00 AM,Ninakujibu kwa sababu umeeuliza na unahitaji jib;Kwa mujibu wa watu walioshuhudia ugomvi huo,ulitokana na vitendo vya kibabe vilivyojitokeza baada ya kukwaruzana barabarani.Wanajeshi baada ya kukwaruzwa, marehemu alikuwa na gari yake lakini hakuwa anaendesha yeye.Inasemekana wanajeshi waliwafukuzia na baada ya kuwapata katika maeneo ya mataa ya manyanya.Aidha, marehemu ama mwenzake akateremka na Panga nakuwatishia waliokuwa wanawafukuzia. Wajeda wakatumia mbinu za medani wakilitwaa panga na kumkamata marehemu.
ReplyDeleteSasa nadhani tutoe maoni kulingana na maudhui hayo;kuuahakukustahili kabisa ni kosa kubwa sana.Ila tufahamu kuwa matukio mengi lazima yajadiliwa kwa hekima na busara, pia tujifunze kuwa ubabe kwenye matukio hautakiwi,ila mapatano yanakuja kwa hoja na kufikia muafaka, tumeona hata huko Burundi,Rwanda na Kenya, vita havikusaidia ila watu walikaa na kufikia muafaka ndo Serikali zao zinaendeshwa kwa usalama.
Ila hizo zote ndio athari za sheria kutochukua mkondo wake. Wanajeshi hujiona wao ndo wako juu ya sheria, na Tz mwenye kuwa mbabe zaidi ndiyo sheria humlinda ndo maana vijana waliibuka na Panga ili sheria iwalinde wawanyamazishe waliowagonga.
Sasa sisi tulio hai tujifunze hili ni funzo kwetu.Ila tumwombee kwa mwenyezi Marehemu apunguziwe adhabu ya kaburini. Amina
mh kazi ipo...kumbe kuna mjeshi mmoja kakimbia?kwa LIPI ASA?kuna walakini hapa
ReplyDeletesasa ata km ilikua ni ugomvi,wakatukanana nk ndo muue mtu?ivi kuna kosa gani hasa la mjeshi kuua raia?me nijuavo akiwa vitani mjeshi anaua adui tu
anyway ngoja tuone itapofikia kesi,ila tunasema ivi watu hawatanyamaa kimya patakuwa hapatoshi mtaani...wajeshi vs raia
ndo huu ubabe wa waziri afungia gazeti la raia linalotupa UKWELI wa madudu ya mafisadi..akili hii???
na ivi tulivo na viongozi vilaza/wabinafsi (%kubwa) watanyamaza tu
Pombe influence hiyo
ReplyDeletenaskia huyo dada ni mume wa mtu and that day alikuwa na huyo jamaa yake wa pembeni
ok, all in all, marehemu alishuka na panga na nini cjui,hakustahili kufa! wangempeleka police kwa kosa la kutishia,lakini wakaona wao ndo mahakimu wakampa kipondo hadi kumuua.is not fair at all.sheria ichukue mkondo wake iwe fundisho kwa wengine,
ReplyDeleteam nandy nawakilisha from tz.
Ndugu Anon wa 04:51. Hata enzi za Mwalimu, kulikuwa wanajeshi wachache wanawapiga raia. Tuulize sisi tuliowahi kuishi Nachingwea na Tabora miaka ya 60 na 70 na 80. Tatizo hili limeshamiri katika nchi nyingi za Kiafrika kwa sababu mwamko wetu wa haki za uraia uko duni. Wakoloni ndio waliojenga dhana katika nyoyo zetu kuwa "uniform is power" wakati wa enzi za ukoloni ambapo wenyeji hatukuwa na haki yoyote. Ni juu yetu sisi kuondokana na mawazo hayo ya kikoloni kwa kuelimishana kuhusu umuhimu wa kuheshimiana na kusaidiana. J. Njau.(age 62).
ReplyDeleteHUYO RHODA HANA CHA UINNOCENT WALA NINI!?
ReplyDeleteNIJUAVYO MIMI MWANAMKE ANA HURUMA SANA,ANGETETEA WAKATI WANAMPIGA HASA UKIZINGATIA KOSA LENYEWE NI LA KIPUUZI LABDA INGEKUWA MAREHEMU KAMJERUHI MMOJA WAO HAPO TUNGESEMA NI HASIRA ZA MWENZAO KUUMIZWA,LKN ETI GARI IMEKWARUZWA ETI SIJUI KAWATUKANA,NDO APIGWE KM MBWA MWIZI?
MIMI NI MWANAMKE LKN NIKIONA MTU ANAPIGWA HATA KAMA IWE NI MWIZI MWILI HUWA UNANISISIMKA NA KUONA HURUMA,MPK HUWA NAPAZA SAUTI JAMANI MUACHENI MPELEKENI POLISI.
SASA RHODA MWANAMKE GANI ASIYE NA HURUMA?
PIA NAHISI WAHUSIKA WOTE WALIKUWA TUNGI NDO MAANA WAKAKOSA BUSARA WALIKUWA WANATOKA WAPI USIKU WOTE HUO?NA MAREHEMU ALIKUWA TUNGI ZAIDI YA WAJEDA NDO MAANA WAKAMSULUBU WATAKAVYO,NA MTU AKIWA TUNGI BWANA DAMU INAFLOW KINYAMA,USIKUTE ILIVUJIA NDANI.
POMBE ZIMEWAISHA SAA HZ WAPO KWA PILATO NYUSO ZIMEWAPALAMA KWA MAJUTO..SANA SANA WANAWAZIA FAMILIA ZAO BAADA YA WAO KUSWEKWA NDANI..
TUJIFUNZE KUSEMA NA HASIRA ZETU WAUNGWANA,UBABE HAUSAIDII.
WATU WENGI WANATEMBEA HUMU MJINI LKN WAGONJWA,KUPIGANA HOVYO KUTAKULETEA KESI BUREE..
MI NILISHUHUDIA UGOMVI BAR,UBISHI WA POOL TABLE MTU KAMPIGA KICHWA MWENZIE KADONDOKEA KISOGO BAADAE TUNAAMBIWA KAFA..UNAONA HAPO KISA POOL TABLE KAFUNGWA WASH ANAENDA KUWEKWA SELO..
HUYO SWETU SIMJUI LKN NILIPOONA PIC YAKE WKT YUPO ICU MPK ANATISHA,MASKINI KUJA KUONA PIC YAKE HUMU KBL HAJASULUBIWA,KWA KWELI ALIKUWA HANDSOME.
MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI
Mnasema marehemu alishuka na panga, mbona hao wajeshi hawana hata jeraha moja hapo? wapo poa kabisa sasa hilo panga ndo wao walimkatakata nalo marehemu? wao km wajeshi kwa nini wasimkamate na kumpeleka polisi wakachukua sheria mkononi, haifai hiyo.halafu wala hawana sura za majuto hapo kwenye picha wanaoneka wameridhishwa na kitendo hicho.
ReplyDeleteNimegundua Misupu yuko biased nilitoa maoni yangu kama mwanasheria lakini hakuyaweka. Najua sijui hata haya yatapita. Nilitaka niwaeleze watu kuhusu msimamo wa kesi hii kisheria lakini kwa sababu Misupu yuko biased labda kuna undugu na wafiwa hakuyaweka. Na haya maoni husiweke ukipenda. Lakini napenda nikuuleze kuweka maoni ambayo yanawahukumu watuhumiwa na kuacha upande mwingine hujatenda haki
ReplyDeleteThis and many other like incidents to me they are greetings from the army.
ReplyDeleteGross indiscipline?? i don't know. Dissatisfaction?? not sure. A tip of ice bag?? may be.
Mithupu maoni yoyote yanayoonyesha upumbavu wa rais huwa hayatundiki. Ingawa kama kweli tunataka kupiga hatua basi rais wetu na wananchi wote lazima wawe tayari kuambiwa ukweli.
ReplyDeleteMithupu, mtu akituka, usitundike. Mtu akitoa maoni maridhawa hata kama huyapendi au yatamuuzi ndugu yako "mtukufu rais", kama hakuna matusi ndani yake basi unalazimika kuyatundika. Ingawa blog ni yako, lakini wewe mwenyewe umeamua kuifanya kuwa ya jamii, kwa hiyo isiwe ya CCM tena.
Au kama hilo ni gumu sana basi vyama vya upinzani navyo inabidi vianzishe blog zao ili mawazo/maoni m-badala nayo yawafikie walengwa.
Wewe anony hapo juu unaejitia mwana sheria, naona hata hiyo sheria yenyewe huijui,hata iweje mtu hatakiwi kumuuwa mwenzie kwa ajili ya kukwa ruziana magari tu, wewe wala sio mwasheria na wala hujasoma yeyeto,wewe ni mcharuko mkubwa we,na hao labda ni ndugu zako, lakini nina kuonya ya kwamba, labda nikujue lakini nikikujua, nitatafuta ungovi na baba yako au ndugu zako halafu nimuuwe mmoja, hapo ndipo utajua uchungu wake. Na pia kwa taarifa yako basi Mimi,Michuzi, Swetu,Chelu, Norman Wage,Mgalula,Chindakta,Mwinyi Mangara, Sabri kina Makuka, Hujati kina Rumelezi na wengine wengi mchezo wetu mmoja, tumekulia Agrey pale, watoto wa mjini,na sheria tunazijua, na kwa hili wala halihitaji kwenda shule, wala kuwa mtoto wa mjini, hiyo ni mada kesi tu,wewe ni mcharuko tu, na kama ni lawyer, basi wewe tutakwita criminal lawyer.
ReplyDeletebinafsi toka mdogo nina allergy na izi mutu zinazovaa migwanda-gwanda na kubeba bunduki,,sijui kwanini!!
ReplyDeleteila nachojua ni ubabe ubabe tu kwa raia na kutishia maisha yetu thts why IMANI kwao imekwisha kabisa,,uwa nafikiria unajua wanamsongo wa mawazo hawajaenda vitani kuua watu/kumwaga damu maana ndo wanavofundishwa kambini KUUA,,,mayb rais iwepo ratiba maalumu kuwatuma kutumia vita vya wenzetu,kulinda amani au majanga kama HAITI...ili waweze punguza mawazo na KUTOUA RAIA,,,
INASEMEKANA WALIKUWA WANNE WAWILI WAKO WAPI??? KESI YANINI?? WAACHIWE TUU WATOKE NJE NA WAO WAPATE MKONG'OTO WA KISAWASAWA MPAKA WAFE.
ReplyDeleteWANAJESHI WANAFIKIRI SHERIA HAIWAGUSI. KULA BURE KULALA BURE HALAFU WANANCHI HAOHAO WANAOWALISHA KWA HELA YA SERIKALI MPAKA MNAVEMBEWA MATUMBO MNAWANYANYASA. TUMEWACHOKA!!! MNALOFANYA HALIONEKANI KAZI KUAMBUKIZANA UKIMWI TUU!!!
inaonekana aliyekuwa anafanya sifa wakati wa kumpiga huyo SWETU ni mpenzi wa RHODA so alikuwa anaonyesha uhodari mbele ya mpenzi.C UNAJUA TENA UKIWA NA MPENZI UNAVYOKUWA NA SIFAA!!!!!!!
ReplyDeleteBY MIMI