eneo la mapumziko hoteli ya Giraffe Ocean View

Hoteli ya Giraffe Ocean View ambayo ni kati ya hoteli maarufu hapa jijini Dar es Salaam imejizatiti kuendelea kuwa kiota cha maraha kisichokuwa na matukio ya wizi ama uporaji ndani na nje ya hoteli hiyo ambayo hupokea wageni wengi kwa ajili ya mikutano mbalimbali.
Msemaji wa hoteli hiyo ambayo inajivunia vivutio kibao wakati wa wikiendi na sikukuu kiasi cha kusababisha hata maeneo ya maegesho kutotosha, ameiambia Globu ya Jamii leo kwamba wanajivunia rekodi ya hali ya usalama wa mali na watu kwa kipindi chote cha mwaka 2009 hadi hii leo.
"Wingi wa wageni hapa Giraffe inadhihirisha hali hiyo na pamoja na wateja kulazimika kuegesha magari yao katika maegesho ya jirani na hoteli tunawahakikishia usalama wa hali ya juu.
"Kutokana na huduma nzuri za hoteli hii na wateja kufurahia mandhari yake na upepo mwanana wa bahari ya Hindi kiasi cha kufurika hapo inatulazimu kuhakikisha kuwa mali na usalama ni wa hali ya juu.
"Katika kuhakiisha hilo tumeajiri kampuni yenye uzoefu na viwango vya juu katika masuala ya ulinzi inashirikiana na uongozi wa hoteli katika kuhakikisha kuwa ulinzi umepewa kipaumbele", alisema.

Tamko lake hili linakuja baada ya maeneo ya Kunduchi ambako iko hoteli ya Giraffe Ocean View Hotel kutajwa katika orodha ya maeneo hatari kwa vibaka hasa nyakati za usiku.
Amesema ingawa hoteli hiyo haikuhusishwa na tuhuma za vitendo vya hujuma kwa wateja wake ambavyo yenyewe haiwezi kwa namna moja au nyingine kufanya hivyo, hawawezi kukaa kimya kwani wao ni wadau wakuu wa eneo hilo.
"Hivi tunavyoongea yapata mwaka mmoja sasa Hotel hii haijawahi kupokea taarifa za wizi kutoka kwa wateja na hakuna taarifa hizo katika vituo vya usalama kama nasi tunafurahia hilo na tunaomba ushirikiano wenu katika kutupatia taarifa zitakazotuwezesha kuendeleza hali hii ya usalama hapa hotelini", aliongezea.
Amesisitiza kwamba huenda vitendo vya uhalifu vilikuwepo miaka ya nyuma kabla ya hoteli kufunguliwa, na kwamba hivi sasa utawala kwa kushirikiana na vyombo vya dola pamoja na ulinzi wake yenyewe hali iko shwari.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Maeneo yote ya pwani ya Kunduchi hayana usalama kabisa na ni aibu kubwa kwa Taifa letu hasa wanapoporwa wageni. Mie nilishuhudia mwenyewe tukiwa Kunduchi beach hotel, mgeni wetu mmoja alipoamua akafaye jogging beach mida ya asubuhi kama saa moja kasorobo hivi, aliporwa simu yake kweupee na vibaka akabaki anashangaa! Tena akatuambia wazi kuwa pwani ya Mombasa iko salama zaidi ndio maana watalii wanajaa huko.

    Inawezekana kukawa na usalama ndani ya hoteli, lakini wageni hawaji kujifungia vyumbani, kama ni vyumba na vitanda hata makwao wanavyo.wanataka kuenjoy beach kuona jua likizama na kuchomoza, na kuogelea time yoyote ile. Sasa kama hakuna uwezekano huo kwanini wasiende Mombasa?

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli tusijitetee kwa vijisababu visivyo na research kamili pwani ya kunduchi si salama. Angalia maeneo yote na fanya mikakati na majirani kuzuia si, sawa ndani ni poa wakitoka hatua mbili noma. jiungeni mrekebishe au fatilia msaada kwa vyombo husika

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...