Habari zenu wana blog wenzangu!
Nikiwa mmoja ya wanablog kutoka www.kingkif.blogspot.com kwa kupitia blugu hii naomba nichangia japo kwa aya chache kuhusu ukumbe wa Kajuna son wa kijiji cha Habari na Matukio (www.kajunason.blogspot.com) ambapo mapema mwezi huu aliandika kwenye blogu mbalimbali .Hivyo basi , na mimi King Kif napenda kushare hili na ndugu zetu ili walifahamu hili.

Tangu nimeanza kublogu nina muda wa miezi tisa sasa ! Ni muda mfupi mno! Lakini kwenye muda huo kiduchu nimeweza kupokea e.mail nyingi sana kutoka hapa Tanzania na nnje ya nchi ambazo watu wanaomba niwatangazie mambo yao kupitia blogu yangu na nyingineziliomba niwatumie hata wamiliki wa blogu nyingine ambao ni marafiki zangu!Kwa bahati mbaya ama kwa makusudi mazima ni ni wachache sana ambao wanajua umuhimu wa kurudisha fadhila au hata kutuma mialiko ya matukio ambayo wanayafanya(hasa hapa Tanzania).

Hapa kwenye aya hii ninamnukuu Kajunason: "Jambo baya na la kusikitisha kabisa hawa watu pale unapopata nafasi ya kwenda utaambiwa hautambuliki kabisa kwa nini nisitambulike wakati unanitumia e.mail ili nikutangazie mambo yako ulinitambuaje? na leo nimekuja kwenye hicho kitu kuangalia kama kweli kimefanyika unasema haunitambui?".

Washiriki wenzetu , nimeamua kuandika e.mail hii ili kuweza kusema ukweli...haiwezekani ukanitumia tangazoau matangazo na kuomba utangaziwe concert, upigaji mnada , au tukio lolote harafu hautumi mwaliko inakuwa haina maana ninaomba tubadilike huu ni mwaka mpta 2010.

Ni mimi,
Kingkif wa
www.kingkif.blogspot.com
...ustarabu ...ni jambo jema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. weka ada ya matangazo. usitegemee undugu

    ReplyDelete
  2. Ndugu yangu unaonekana una matatizo makubwa sana ya kisaikolojia.
    unapofanya msaada siku zote usitegemee kulipwa fadhila,fadhila ni mtu mwenyewe atakapotaka na wala si lazima kama wewe unavoonekana kulazimisha sijui umeipata wapi kanuni hii.
    kama umeamua kusaidia vipi tena unalazisha fadhila ?
    cha muhimu andika kwenye blog yako kwamba unaposaidia na wao wanaosaidiwa walipe fadhila,ili ijulikane moja sio kuomba fadhila kinguvu hamna KANUNI HIYO DUNIANI.hakuna DINI wala KABILA lenye kuladhimisha fadhila.

    ReplyDelete
  3. Mi nadhani ulitaka kusema hutangazi biashara ya mtu hadi uione kwanza kama ipo au vipi. Vinginevyo sikuelewi kwani we huna shughuli nyingine za kufanya hadi unganganie mialiko ya unaowatangazia shughuli zao!?

    ReplyDelete
  4. Ninakumbuka miaka ya 70 kulikuwa na bendi ikiitwa Njohole Jazz Band ya Ifakara iliimba wimbo kama ifuatavyo "Tenda wema wende zako wowowo usingoje shukurani wowowo...

    Kikosi chote cha bendi hiyo kiliteketea kwenye ajali ya gari maeneo ya mikumi.

    Ni kweli fadhila haipaswi kudaiwa.

    ReplyDelete
  5. Weka Masharti bw. Kingkif. Mimi ninakusaidia kulibuni.

    MASHARTI YA TANGAZO

    "Atakayeomba tangazo lake Hususan la Mnuso litolewe kwenye blog ya Kingkif, anakubali kwamba tangazo likitoka automatically amemualika owner wa blog na ndugu zake wanne kunusa katika mnuso huo"

    ReplyDelete
  6. wewe bwana hiyo post yako nilishaiona siku za nyuma, kwanza mimi hata hiyo blogu yako siijui.Nadhani unatafuta kipato kupitia blogu
    weka masharti ya blogu kila mtu asome mfano "buy this place to advertise ur business" wataelewa

    ReplyDelete
  7. uroho unakusumbua tuu!! unamuonea gere mkuu wa nanihii sio ?? utajiju vidole havilingani

    ReplyDelete
  8. Mbona mnamshambulia King Kif peke yake wakati yeye kaendeleza tu hoja kwa kumuunga mkono Kajuna?!Shukuran haiombwi, lakini ni vema binadamu tukaishi kwa kushukuru kila tunapotendewa wema na wenzetu.David Kima,Marekani.

    ReplyDelete
  9. Ni haki yake Kingkif kuandika alivyoandika,si yeye pekee kwenye ulimwengu huu anayeumizwa kwa kutopewa shukurani.

    ReplyDelete
  10. kumbe ndivyo ulivyo bw. kif kuanzia leo mimi na ww basi

    ReplyDelete
  11. wanataka kula bila kuliwa? haiwezekani bwana walipe fadhila

    ReplyDelete
  12. Habari zenu wana blog wenzangu!
    Nikiwa mmoja ya wanablog kutoka kijiji cha Habari na Matukio (www.kajunason.blogspot.com) ningependa kushare hili na ndugu zetu ili walifahamu hili.

    Kwa mwaka 2009 tumepokea e.mail nyingi sana za kuomba watu watangaziwe mambo yao kupitia blog ila ni wachache sana ambao wanajua umuhimu wa kurudisha fadhila au hata kutuma mialiko ya matukio ambayo wanayafanya.


    Jambo baya na la kusikitisha kabisa hawa watu pale unapopata nafasi ya kwenda utaambiwa hautambuliki kabisa kwa nini nisitambulike wakati unanitumia e.mail ili nikutangazie mambo yako ulinitambuaje? na leo nimekuja kwenye hicho kitu kuangalia kama kweli kimefanyika unasema haunitambui?

    Wadau wetu nimeandika e.mail hii ili kuweza kusema ukweli...endapo unatuma tangazo na kuomba utangaziwe concert au tukio lolote harafu hautumi mwaliko inakuwa haina maana ninaomba tubadilike huu ni mwaka mpta 2010.

    Ni mimi,
    Cathbert Angelo Kajuna,
    www.kajunason.blogspot.com
    ...Everything Possible Through Peace and Stability...

    ReplyDelete
  13. Matatizo anayopata Kingkif kwa sasa, mimi nimeyapata mno wakati nafanya kazi ya uandishi wa habari kwenye miaka ya tisini mwishoni pale Nipashe.Mapromota wa hapa Bongo hizo ndio zao.Kingkif wazoee kisha wapuuze.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...