Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akisalimiana na Katibu Mku wa CUF Seif Sharif Hamad,alipowasili katika uwanja wa Mkutano wa Makombeni jana Mkutano ulizungumzia zaidi umoja na utulivu Nchini,katika kusherehekea miaka46 ya Mapinduzi Zanzibar.
Wananchi wa Makombeni Mkoa wa Kusini Pemba, wakimsikiliza Rais Karume alipozungumza nao wakati wa Mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa mpira Makombeni,miongoni mwa shamra shamra za miaka 46 ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,akikata utepe ikiwa kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya MKoani,Makombeni Pemba,katika kusheherekea miaka 46 ya Mapinduzi ya ZanzibarRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(wapili kushoto) na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Machano Othman Saidi,(katikati) pamoja na Viongozi wengine,wakitembea katika Barabara ya mkoani,Makombeni,iliyojengwa nguvu za Serikali, mara baada ya kuizindua,ikiwa ni sherehe za kuadhimisha miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Amani Abeid Karume,(wapili kushoto) na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Machano Othman Saidi,(katikati) pamoja na Viongozi wengine,wakitembea katika Barabara ya mkoani,Makombeni, iliyojengwa kwa nguvu za Serikali mara baada ya kuizindua,ikiwa ni sherehe za kuadhimisha miaka 46 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Picha na mdau Ramadhani Othman wa Ikulu, Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. HAWA JAMA NISHAONA WANATAKA KUVUNJA VYAMA VINGI NDIO MAANA,HAIWI HADI MKUTANO WA CCM NA CUF WAHUDHURIE.
    Mbona hawaelezi nini kimezungumzwa na wanakusudia nini mbona kila kati wapo pamoja ndio upinzani gani huu?

    ReplyDelete
  2. mchangiaji inaonesha unaufahamu mdogo sana kuhusu siasa za ushindani, kwako wewe ushindani ni sawa na kupigana na kutosalimiana! ushindani wa siasa ni tofauti of idea and idology katika kuleta maendeleo ya nchi only na hio haina maana kuwa watu wasizungumze au wasikutane. now zanzibar ndio wanajenga "harmonized democracy" ambayo ndio inayotakiwa na sio "hatered democracy". hongera karume hongera maalim seif.
    ndugu wakigombana chukua jembe ukalime! kesho watapatana
    ZANZIBAR DAIMA

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji "Tue Jan 12, 02:08:00 PM". Nakubaliana na ujumbe wako asilimia 100. Lakini mara ijayo itakuwa vema kama ukiweka ujumbe wako kwa lugha moja - ikiwezekana kiswahili. Haipendezi sana kuchanganya lugha na kama mchangiaji wa kwanza hajui kiingereza, ujumbe wako mzuri "haujamfikia". Najua ni ngumu mara nyingine lakini sio mbaya kujaribu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...