Mambo vp mzee?

Ebwana naomba msaada wako unitangazie, kiwanja kinauzwa Kibada, Kigamboni, Dar es salaam.

Size: 540 square metres
Kipo Block 15, Kibada, Kigamboni.
Kina title deed/hati ya kiwanja kwenye jina langu.
Kiko 200 metres from the main road.

Kama mtu ataitaji kukiona anaweza mpigia simu Anna Musa 0715 952667
Bei ni kuanzia Tshs 8,000,000. Makubaliano yanakaribishwa.

Hiyo picha ilipigwa September 2008

Asante sana.

Abdulrabih Nyoka
Email: abdul@kinyoka.co.tz
Mobile: +44 777 6311137
Manchester, Lancashire
United Kingdom.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mzee umeshaamka asubuhi hii!
    Habari za asubuhi? Mimi ndo ninajiandaa kulala ninapitia blogu yetu kisha nipige sala nipumzike.
    Ninakutakia kazi njema.
    Ni mimi mdau wa damu USA

    ReplyDelete
  2. kwa huyu ndau anastahili pongezi kwanza bei ni ya kawaida siyo mtu anakurupuka toka usingizini eti kiwanja ekari moja milion tzs 800 kweli unauza au unataja bei tu na huoni ufisadi mwingine kwa wa -tz halafu kiwanja kipo boko au kimara mwisho si bora anunue nyumba kariakoo kwa bei chini ya hapo na sehemu inalipa.wa-tz hachani kutuzingua kwenye blog ya ankal wetu

    ReplyDelete
  3. Mie nakushauri ukiuze kuanzia milioni 15 hadi 20mil hiyo milioni nane utapata hasara.Mahali hapo pameshakuwa hot cake sana.Najua utapata watu wengi kwa hiyo bei ila utajuta kukiuza after 3 months. Take my advice!!!

    ReplyDelete
  4. aisee ! are you sure hakijajengwa maana siku hizi kibada ni noma !!!

    alafu mbona cheap sana siku hizi vinaenda mpaka 30 m

    Amka !!!!

    mkazi wa kigamboni

    ReplyDelete
  5. Wabongo mnanishangaza, eti bei ndogo, sasa c mnunue nyie ili muuze kwa bei kubwa hiyo ya milioni 30! mnadhani mpaka kaleta tangazo hapa michuzi c keshatangaza na bado hajapata mtu? msiropokeropoke tu!

    Pedestrian hapa!

    ReplyDelete
  6. nyie mnaongea nini,kigamboni yote nasikia ishauzwa tayari jamaa nae naona anataka kuuza mbuzi kwenye gunia.

    ReplyDelete
  7. Asanteni kwa comments, ni sawa bei kwa sasa ni kuanzia 10 Millions to 15 millioni. Ila mi nimeamua kuuza kwa bei iyo ya Tshs 8 Millions, natumai mteja atatokea.

    Ni sehemu nzuri haijajengwa na ina hati , na imepimwa fresh na serikali.

    Kwa anayeitaji anaweza piga simu

    Anna Musa 0715952667
    au
    Abdulrabih +447776311137

    e-mail: abdul@kinyoka.co.tz

    ReplyDelete
  8. Jamani kuweni macho sasahivi si muda wa kununuwa KIWANJA KIGAMBONI sababu nasikia Soon inabebwa Kigamboni, Ndomana watu wanauza Nyumba zao kwa Speed huko. Mama Prisca.

    ReplyDelete
  9. hahahah mdau ameshashtuka...sis tuna viwanja kigamboni kama chako...ndio mana mnaambiwa mufuatilia mambo yanayoendlea kwa kina tz hasa juu ya kigamboni na kama mna mchango muchangie...inaeleweka serekali inataka kujenga mji wa ksasa kwa kauli yao..au kwa kauli ingine imeuzwa....je kama wewe raia ufanye nini usaidie....mdau serekali inataka kupelekwa mahakamani na wakazi wa kigamboni na huu mpango uko njiani kabla hata mwezi watatu...sijui kama atatokea mtu kukinunua ila atatokea baada ya wakazi kushinda kesi mahakamani na utakuwa sisdhani kama utaweza kuza tena....NA USHAURI WANGU NAPENDA KUTOA KWA YEYOTE KAMA ANAYEUJUWA KAMATI ILIOUNDWA KUIBURUZA SEREKALI YA MAFESADI MAHAKAMANI...NINGESHAURI VILE VILE WAFUATILIE KUPITIA AMNESTY INTERNATIONAL.....Asanteni na kazi njema

    ReplyDelete
  10. BWANA NYOKA UNA ROHO NGUMU KWELI KWELI!!!
    UNAUZA PORI!!!
    MAJI YA BOMBA YAPO?
    UMEME JE?
    BARABARA AU UNAINGIA KWA HELIKOPTA!!!
    KIMEPIMWA?
    ASALAAM ALEKHUM NA HIYO MINAZI NA NYASI UNATAKA FIDIA PIA?
    HAYA BWANA.

    ReplyDelete
  11. Buyer beware. Kibada kuna maji mengi sana ya kisima ambayo ni masafi ... unakunywa laivu bila kuchemsha wala kupiga mionzi.

    DAWASCO wameshafanya survey na hilo eneo wamelinunua ili wachimbe visima vya maji kwa ajili ya Kigamboni na maeneo mengine ya Dar es Salaam.

    Kuwa makini usije uziwa mbuzi kwenye gunia.

    ReplyDelete
  12. Hallo ankal Mithupu,

    Enyi Wadanganyika Kigamboni Inauzwa,Kuanzia Ferry mpaka Kibada sasa sijajua kwa nini huyo mdau anataka kuwaingiza watu mkenge! Me Nimekaa Kigamboni Kuanzia Mwaka 1984 mpaka leo nakaa kigamboni,Mjimwema sasa wadau kuweni makini sana na huyo m2 angesema kiwanya kipo Kisarawe na mwasonga ningewashauri kununua..
    Kuanzia mtaa wa ferry,kigamboni,tungi,kibanebane,mjimwema mpaka kibada inauzwa kwhyo wananchi msiingie mkenge...
    Ni Mimi Mkazi wa Kigamboni.

    ReplyDelete
  13. Jamani kuweni macho saana ni juzijuzi nimetoka Bongo issue ya viwanja kigamboni ni matatizo tupu inachukuliwa yoote nina madaktari wenzangu wamejenga maeneo hayo hayo wako wanalia ile mbaya na walijenga mahekalu sio mchezo. Pia eneo kubwa linachukuliwa na jeshi na hiyo imeshapitishwa. Hao madaktari walinunua miaka mitano iliyopita tena kwa bei kubwa zaidi ya hii anayosema kwa sasa. Kuwa chonjo mtalizwa saana.
    Mdau kwa sasa USA.

    ReplyDelete
  14. nyoka mambo vp mwana? kumbe uko hap man city!!! tutafutane kaka. vp kikapu umeacha cku hizi manake ulikuwa unakicheza sana pale mzumbe sec

    ReplyDelete
  15. ngoja tufatilie kwa ukaribu hii habari ya serikali vs kigamboni.

    maana raia apa mnachonga sana

    ReplyDelete
  16. Mie ni mdau nipo nje ya nchi na ninafanya kazi katika ofisi moja ya serikali ya Tanzania huku nje (ubalozini) na pia ninamiliki viwanja viwili hapo Kibada. Ukweli ni kwamba zipo hizo tetesi kwamba serikali imeliuza eneo hilo kwa wawekezaji tena wapo wengine wanaodai eti serikali imeliuza eneo hilo kwa George Bush, yoote hayo ni uongo mtupu. Nimefuatilia hilo swala kwa rafiki zangu serikalini hasa wizara ya ardhi na Ikulu na nimethibitisha kwamba ni uzushi. Haiwezekani serikali ikatoa title deed ya kiwanja na pia ikatoa kibali cha ujenzi katika ardhi ambayo tayari wamepanga kuiuza kwa mwekezaji. Sehemu zenye matatizo ni zile ambazo hazijapimwa na serikali na ikatokea mtu akauziwa na wenyeji wa huko Kigamboni. Kama umenunua ardhi yako kutoka kwa wenyeji wa kigamboni, ardhi ambayo haijapimwa na serikali, then wewe utakuwa na matatizo. LAKINI VIWANJA VYA KIBADA HAVINA MATATIZO. Bwana Nyoka, nitawasiliana na wewe ili tuongee kuhusu hiyo bei.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...