Mashindano ya kuwania kombe la mapinduzi ya yanayodhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania yanatarajiwa kutimua vumbi kesho katika viwanja vya Mao Tsetung na Uwanja wa Karume Jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Mashindano hayo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Soka Cha Zanzibar (ZFA), Nassoro Salim Eljazeera alisema kwamba kila kitu kiko tayari kwa mapambano hayo.

Katika mashindano hayo, timu za Miembeni na Zanzibar View zitapambana katika uwanja wa Mao Tsetung wakati Simba na na Malindi zitachuana Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Karume.

Aljazeera alisema Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Dk Mwinyi Haji Makame ndiye atakayekuwa mgeni rasmi katika mchezo wa ufunguzi katika uwanja wa Mao Tsetung.

Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza alisema kampuni yake imedhamini mashindano hayo kwa zaidi ya Shilingi milioni 68.

Alifafanua kuwa udhamini huo unajumuisha vifaa vya michezo na fedha taslim.
Rwehumbiza alisema mashindano haya yanajumuisha timu za Tanzania bara na visiwani na kushindana kama ligi zikiwa katika kundi moja, alizitaja timu hizo kuwa Simba,Yanga,Mtibwa zikitokea Tanzania bara,na Tanzania Visiwani ni Malindi,Miembeni,Mafunzo na Ocean View.

Kwa mujibu wa Aljazeera fainali ya mashindano hayo ambayo yanalenga katika kuadhimisha siku ya mapinduzi zitafanyika tarehe 12 mwezi huu katika Uwanja wa Gombani huko Pemba na mgeni rasmi ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Aman Karume.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Vipi, Vodacom hawakutoa pesa ili mechi zirushwe kwenye Luninga? George, namna gani hii!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...