Katika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.
Happy Birthday!
Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.
Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.
Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? bongocelebrity.com ilimsaka Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu
Kupata mahijoano yake
ankal unaweza kumzaa kanumba bila wasi wasi.
ReplyDeleteNaomba kuuliza hivi Kanumba ni Muislam au Mkristo au hana dini.Naomba kutoa hoja.
ReplyDeleteHappy Birthday to You Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania! May you See many many more!
ReplyDeleteSteven Kanumba, I wish you a Very Happy Birthday! God Bless You!
ReplyDeletehappy birthday kanuba wewe usiwajali binadamu kusema ndio zao kaza buti upo juu karibu unashika mwezi waaaaaaaa
ReplyDeleteGrown up, well done. Other guys hide their ages.
ReplyDelete"HAPPY BIRTHDAY STEVE KANUMBA"
ReplyDelete...usiangalie nyuma daima songa mbele na kipaji chako cha kuzaliwa kipaji hicho ulichopewa na Mungu binadamu hawezi kukiondoa kwa maovu ya chuki,fitna na wivu pekee....
...sherehekea siku yako ya kuzaliwa na wale wanaosonga mbele na wewe katika kuleta maendeleo ya watanzania wote,kazi yako tunaiona na inastahiri sifa zote....
"NAKUTAKIA KILA LA KHERI"
Mickey Jones Amos
Denmark
Michuzi kwa uchokozi tuu hujambo, unataka kuanzisha moto halafu wewe unakaa pembeni. Haya, HaPpi Bethidei ya kuzaliwa mdau Kunumba!
ReplyDeleteMmmmmmh Mzee wa burudani.
ReplyDeleteHappy Birth Day Alfred - what your name again in ... the other movie, ...can't remember the title now - only that you really bullied that innocent wife of yours for not conceiving. Could somebody remind me please. Never do that again.
ReplyDelete...and talking of bullying, just to let you know that some afendis were bullying me when you were born...
so what???
ReplyDeleteTatizo ni hicho kiinglishi
ReplyDeleteKanumba sio mbovu sana kwa ngeli
ReplyDeleteThe guy is good-trying hard especially kwa international interview
Am proud sana na mtu huyu-Tupunguze matusi against him.
Watch youtube clips Kanumba Sporah Show intervies
http://www.youtube.com/watch?v=Iasicyrx5no&feature=related
Happy birthday Kanumba,
ReplyDeleteWatu wakikutukana au kukusengenya vibayya, tusi moja wewe songa mbele kumi, utakuwa umewaacha nyuma yako hatua tisa. Na wala usifikiri hayo unafanyiwa wewe tu, binadamu ndivyo tulivyo hatupendi kuona mtu anaendelea, kwa kweli tuliokuona ukianza kuigiza kwenye kipindi cha Maisha, ukiwa mdogo leo hii umeendeleza kipaji chako mpaka kufikia hapo ulipo tunakupa hongera!
Chukua constructive critism fanyia kazi ili uzidi kuimarika, matusi na rubbish zote tupa kwenye rubbish bin! Hiyo ndio zawadi yangu ya birthday kwako.
Mswahili
kanumba movie yako ya saturday morning ni nzuri sana umejitahidi sana kaka afya njema dogo
ReplyDeleteAaawwww!!! Happy B-day handsome.
ReplyDeletenamjua vizuri kanumba nimekua nae nimesoma nae kule shy ni jirani yetu, ni age mate wangu, umri wake sio 26 ni 34!! muulizeni vizuri
ReplyDeleteWewe unaesema unamjua vizuri Kanumba na umri wake ni miaka 34 kweli unanishangaza. Mimi nina miaka 40 na nikiwa tayari nina watoto nimemuona Kanumba anaanza kuigiza kwenye kipindi cha maisha, akiwa na machunusi kibao usoni, namaanisha akiwa teenager anayeanza kubalehe, very young, nakumbuka mchezo wake wa kuigiza uliompa umaarufu ni ule alioigiza kama mtoto wa mzee Kipara aliyemposa mtoto wa Mhogo Mchungu Dida, wakati huko kijijini kwao familia hizi mbili zilikuwa na bifu la nguvu.
ReplyDeleteHata hivyo akiwa 26 au 34 inahusu nini? Wakati age is nothing but a number? Wivu unakusumbua eti tumekuwa wote so what ndio keshakuacha hivyo mwenzio yuko level nyingine.
Kanumba wakatae, wakubali uko juu mno...nyota yako yang'ara ...nakufananisha na yesu alipigwa mawe na walimtemea mate...nataka ujue mungu anamakusudi yake lakini wanakuchongea barabara utazijidi kuwa juu watu wachache hawapendi kuona unapata nawanadharau moview zakibongo kwhy wakiona mafanikio yenu wanatafuta mawe namisumari... Uko juu huu mwaka mpya naamini umejiandaa vyakutosha muweke mungu mbele kwn wasanii hampendani pia wapo wanaochangia kupanda mbegu mbaya juu yako kukuangusha wewe si the great tu more than the great...kikulacho ki....
ReplyDeletekanumba tafuta A.K.A nyengine si THE GREAT ni mungu pekee ndio mwenye sifa hio,usivimbe kichwa kaka si denzel washington wala will smith wala mastaa wengi wenye akili zao timamu kujipachika jina hilo okeeee?ijekua wewe kaka?no the great is only ALLAH,GOD,MUNGU,JAH NK HAYO NI MAJINA YAKE TU MKUBWA WA WAKUBWA....MDAU,GREECE
ReplyDeletehappy bday steven,
ReplyDeleteulieuliza kanumba ni mkristo anaabudu AICT
mhh watu kwa kuchonga tuu ndio kazi yao kijana wa watu anajitaidi lakini pia munamtowa makosa na huyu anayesema machunusi kibao ni roho mbaya na wivu ,kanumba mimi nakufagilia hile mbaya wewe songa mbele jiite jina lolote unalopenda na kila mtu ana haki ya kujiita anavyopenda so what unayelalamika kwani umekatazwa wewe kujipachika jina ,lugha haijalishi yeye kujuwa englisg sio issue kwani wewe ulizaliwa na kukijuwa mwaya ukija UK nitafute weka kwenye blong safari yako nitakupa number ya simu watoto wangu wanakufagilia kweli waaaaaaa
ReplyDeleteHivi hamchoki? Kumpiga madongo mtoto wamwenzenu? Nani mkamilifu kwakila jambo anyooshe kidole tumuone. Kanumba, kanumba, kanumba, kanumba..... Mtoto wawatu asipumue? Imekuwa kosa kuwa maarufu? Kwn wasanii wangapi wanajua kiinglish? Nini wasanii wewe je unaeponda unajua au unaongea tu? Nyambaf....
ReplyDeleteWewe unaepinga age ya kanumba unadhani umri ndio kigezo cha mafanikio? Inakusaidia nini? Pia kusoma nae haina maana moja kwa moja kuwa mlikuwa mnalingana kiumri. Hata hivyo watu huwa hatusomi tu comments tunafikiri pia. Mimi mwenyewe nina 34 na naelewa huyo hawezi kuwa agemate wangu maana nimeanza kumwona akiigiza akiwa mdogo zaidi ya mimi niliekuwa naangalia tamthilia zile.
ReplyDeleteHappy Birthday Kanumba though you don't look 26.
ReplyDeleteme na wengine wetu wengi tu huwa sipendi picha za kiswahili maana nyingi hazina mtiririko na kuiga kwingi
ReplyDeleteila siku moja niliwekewa movie yako ile uloigiza na wema sepetu..khaaa sikuamini kabisa
toka siku iyo natafutaga movies zako basiiiii
hongera kaka kwa kuinua soko la movie na kufanya wabongo tupende chetu
happy bilated b'day dogo
Ni lini sisi binadamu tutakubaliana na kuiona kazi ya mtu inapendeza? Nasema hivyo kwa sababu wivu ni mwingi bila kumpa mtu changamoto ya alichokifanya. Ina maana wewe pia hupendi wala hutaki maendeleo???? Sababu wengi wanaongeeea visivyo ili mradi achafue tu jina lako. Mungu hapendi hivyo na ndio maana wewe na roho yako mbaya utaadhibiwa na huoni maendeleo yako. Fanyeni mema na yatabarikiwa acheni sana kuchonga. Kanumba unatupa sifa endelea baba don't mind. Give Up.
ReplyDelete