Kaka Issa Michuzi,
Sisi wafanyakazi wa Hoteli ya Movenpick Royal Palm Hotel tunaomba utufikishie kilio chetu dhidi ya uongozi wa hoteli hii ambapo unatunyanyasa kiasi cha kutuona sisi wafanyakazi wazawa kuwa wote ni wezi.

Uongozi wa Hoteli hii unataka kumuajiri Meneja rasilimali watu (Human Resources Manager) raia wa Kenya kwa kigezo kuwa eti Watanzania ni wezi na wanalindana, kwa hiyo akiajiriwa meneja Mtanzania anawalinda Watanzania wenzie hata kama ni wezi, hivyo uongozi wa Hoteli hiyo umedhamiria kuajiri Meneja Rasilimali watu kutoka Kenya maana atakuwa hana mchezo na atawakomesha Watanzania kwa kuwa hawajui na hana undugu nao.

Angalizo wanalotumia ni Hotuba iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akifungua Hoteli ya Snow Crest kule Arusha, pale aliposema kuwa Watanzania waache udokozi, kwa sababu wawekezaji watakimbia. Kauli hiyo imechukuliwa na uongozi wa Hoteli hiyo kama tuhuma za moja kwa moja kuwa Watanzania ni wezi kwa hiyo hawafai na ndio maana wanataka kumleta Mkenya ili awatie adabu.


Meneja aliyekuwepo na ambaye ni Mtanzania amemaliza muda wake na anaondoka katikati mwezi huu na uongozi wake ulikuwa ni mzuri na unaozingatia haki, kama ni mtu kufukuzwa kazi alikuwa anafukuzwa kwa haki bila ya uonevu na hata migogoro ya kesi za madai katika mahakama ya kazi zimepungau kwa kiasi kikubwa kutokana na kuzingatia sheria za kazi.

Sasa hilo lilikuwa haliwafurahishi hawa wenzetu wazungu kwa kuwa wao walikuwa wanataka wakisema huyu simtaki hapa basi afukuzwe, kitu ambacho kilikuwa hakiwezekani. Nchi hii inaendeshwa kwa katiba na sheria na hata katika maeneo ya kazi zipo sheria zianazomlinda mwekezaji na mfanyakazi, sasa iweje mtu akurupuke na kusema huyu simtaki halafu afukuzwe kazi bila kuzingatia sheria wala taratibu za kazi, hivi inawezekana kweli?

Tunavyofahamu sisi, ni kwamba sheria za kazi zimeweka bayana kuhusiana na kazi zinazopaswa kufanya na wageni na zile zinazopaswa kufanya na wenyeji, na ninafahaku kuwa nafasi ya Meneja Rasilimali watu (Human Resources Manager) inatakiwa ishikwe na mzawa ambaye anazifahamu sheria za nchi vilivyo na sio mgeni.
Hivi mgeni anaweza kujua sheria zetu za kazi na za nchi kweli? Na kwa kushika hiyo nafasi ina maana kuwa hakuna Watanzania wazawa ambao wanaweza kushika hiyo nafasi, mpaka aletwe mgeni?

Je nini majaaliwa ya Watanzania wanaofanya kazi katika Hoteli hiyo, watatendewa haki kweli?

Baada ya baadhi ya Wafanyakazi kuhoji kuhusu suala hilo katika mamlaka zinazohusika wakianzia na chama cha wafanyakazi wa majumbani na mahotelini yaani CHODAWU walipewa ufafanuzi kuwa hilo haliwezekani kabisa kwa kuwa sheria iko wazi kuwa nafasi hiyo inatakiwa ishikwe na mzawa anayezijua sheria za kazi za nchi.

Sasa hivi baada ya kuona kuwa wafanyakazi wameshituka na wanahoji vigezo vinavyotumika ili kumleta Mkenya huyo, uongozi wa Hoteli ukiongozwa na Meneja Mkuu Msaidizi unasisitiza kuwa ni lazima huyo Mkenya aletwe hata kama itagharimu kiasi gani cha pesa kwani Money Talks.
Taarifa ambazo tunazo ni kwamba Kigogo mmoja amekuwa akitumiwa sana na Uiongozi wa Hoteli hii katika kuhakikisha kuwa wageni wanapata vibali vya kufanya kazi hapa nchini.

Kwa mujibu wa maelekezo ya mheshimiwa Raisi Jakaya Kikwete aliagiza kuwa haitakiwi Hoteli yoyote kuajiri wageni zaidi ya watano, kwani hizo nafasi zinapaswa kushikwa na Watanzania na wapo, lakini katika Hoteli hio kuna wageni Kumi wanaofanya kazi ambazo zingeweza kufanywa na Watanzania, na wengine wameishi hapa nchini zaidi ya miaka sita huku wakibadilisha nafasi za kazi kila kibali kikiisha muda wake.

Ukweli ni kwamba kuna kukinzana sana kati ya TIC na uhamiaji na haifahamiki kuwa ni nani mwenye mamlaka ya kuidhinisha wageni kupewa vibali vya kuanya kazi hapa nchini, uhamiaji wanawatupia mpira TIC na TIC wanawatupia mpira Uhamiaji.

Tunaomba mtufikishikie kilio chetu kwa wahusika watueleze kama hii ni halali na inakubalika ndani ya nchi hii? Ni sisi wafanyakazi Moevenpick Royal Palm Hotel Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 85 mpaka sasa

  1. Kwanza niwapongeza kwa hatua yeneu ya kutetea haki ya wa TZ.
    Poleni sana kwa adha mnayopata. Naona mheshimiwa JK naye aliamua kukandamiza wa TZ kwa kutumia visingizio vya wawekezaji. Kama watanzania ni wadokozi kwa nini hao wawekezaji hawawafikishi kwenye vyombo vya sheria?

    Pili, nadhani mngetusaidia wa TZ kama huyo kigogo angetajwa badala ya kuweka kapuni jina lake. kuendelea kufichaficha majina ya hawa vigogo ndo kunapelekea wao waendelee kupokea rushwa na kuzidi kutunyanyasa wa TZ.

    ReplyDelete
  2. Mmezidi kudokoa ndio! Yaaani mahali alipo Mtz lazima ubabaishaji, ujanja janja mwingi ndoto kumbwa za kuendesha RangeLover mshahara hauruhusu!
    Ili ufanikiwe katika maisha inatakiwa descipline ya hali ya juu wakati mwingine unatakiwa kusubiri, sacrifice nk. Ona bandari yetu gari kulitoa tu pale mbinde hata kama una kula doc. uwanja wa ndege pale ukikosea ukaacha laptop simu au camera kwenye bag umekwisha Nairobi tuna pita bila shida! Mombasa tunatoa magari bila matatiza! Sasa unajiuliza watz tunanini?

    ReplyDelete
  3. Ndugu wadada na wakaka wa Moevenpick ni kweli kwamba wafanyakazi wa kitanzania tumekosa uaminifu sana katika nafasi na majukumu ya kazi tuliyokabidhiwa. Tumekuwa wadokozi mmno na kila mtu aliyena nafasi fulani anataka awe kafisadi dagaa, awe na gari na awe na nyumba ndani ya mwaka mmoja! Sio siri bado watanzania tumejiweka katika hali ya kutaka kutawaliwa na imefika wakati viongozi wa makampuni wengi watatoka nje ya nchi wakati tuna watanzania wenye elimu na uwezo wa kuwa menejas wa kusimamia kampuni mbalimbali. Malalamiko yenu yana msingi lakini ukiangalia swala la kutokuwa waaminifu ni kweli, uzembe kazini, udokozi kwenye vyumba vya wageni, kwani wageni wengi wanalalamika wanapoacha vitu vyao hotelini wakirudi wanakuta mabag yao yamepekuliwa. Kingine ni pale wateja wanapotoa oreder ya vyakula na vinywaji usanii unatumika katika risiti na wanakuwa wanalipa gharama mara tatu ya gharama ya chakula na vinywaji. Kuna mambo mengi yanayoendelea katika hotel nyingi kiasi kwamba mtu unaogopa hata kulala hotelini ni bora hata kutafuta ndugu aliyekwenye mji huo ni salama zaidi.
    Inabidi watanzanie tubadilike sasa ujue mwajiri yeye anachotafuta ni faida sio hasara na anahitaji mtu mwaminifu ili kuendesha biashara sio wasanii wenye kurekebisha vitabu vya mahesabu kiaina. Binafsi ninaupongeza uongozi huo wa hoteli hii kwa kufanya uchanguzi wa kina na kubaini kwamba watanzania sio waaminifu katika sector nyingi ila hii itakuwa ni fundisho na mjirekebishe sio kulalamika.
    Blogu hii ni kioo cha jamii na sisi tunataka watanzania mjiangalie kutoka katika blogu hii kisha mfanye mabadiliko ya kimienendo ili muweze kufurahia matunda ya uhuru wa nchi yetu.
    Mungu ibariki Tanzania.
    Mdau USA

    ReplyDelete
  4. Mimi napinga vikali uamuzi wa Hoteli hiyo. Pamoja na hayo, nataka kuwaarifu Watanzania wenzangu kuwa tusipobadili desturi zetu za utendaji tutapoteza kazi zote. Mimi nina mifano halisi ambapo Watanzania wengi bado ni wazembe makazini, hawajali wateja, wana kauli mbaya na hawaheshimu kazi zao. Wenzetu kwavile wamekuwa katika mifumo ya soko huria kwa miaka mingi wanajua kuwa kuna competition katika labour market kwahiyo wanaheshimu kazi. Sisi bado tunazembea kazi kwavile wengi wetu tunaajiriwa kwavile tunamfahamu mtu fulani...jamani tubadilike...kazi zote zitachukuliwa na Wakenya na Waganda kwavile wao wanajua Customer service. Utakuta mtu ana-chat kwenye simu halafu wateja wamesimama kumsubiri...hivi hamuelewi kuwa hatuko katika Ujamaa tena? Kwa upande mwingine ngoja wamuajiri meneja toka Kenya mfundishwe Adabu..nilikuwa Tanzania mwezi wa 11 na kila kitu kinaudhi..watu hawajali kazi zao hata makampuni kama Precision ambao tulifikiri watabadili huduma za ndege bado ni wazembe. Nimekaa dakika 30 airport ati mhudumu amefunga ofisi kisa ameenda Msalani...ngoja kazi zote tu zichukuliwe labda vizazi vijavyo vitajifunza...!! Badilikeni acheni kulalamika. Mdau-USA

    ReplyDelete
  5. Mimi nimefanya kazi katika kampuni moja ambayo ilikuwa na mgogoro kama huo, kuajiri wakenya kibao. Mmoja watu ambae alikuwa mzalendo wa hali ya juu sana ali-report uhamiaji na jamaa walichukua hatua haraka sana. Wakenya wale walitiwa ndani na kufukuzwa nchini. Fanyeni hivyo hivyo. Najua wawekezaji wanapewa nafasi ya TIC ya kuajiri wageni wasiozidi 7. Nyie hesabuni tu idadi hio ya wageni, kama imezidi ripotini uhamiaji. Wengi wanatumia working permits wanazopata kwa njia zisizo halali.

    Imefika wakati watanzania tuamke. Viongozi wote wa chama tawala na serikali wana sera ya kutetemekea wawekezaji na mataifa ya nje. Wanatoa kauli zinazotoa picha mbaya juu ya watanzania bila kujali madhara ambazo kauli hizo zinasababisha. Wanachojali ni kuwafurahisha tu wawekezaji kwa kuwatukana ndugu zao. Hii sio mara ya kwanza kwa viongozi wa kitaifa kuwambia wawekezaji na mataifa ya nje juu ya 'ubaya' wa watanzania. Tutafanya nini ni sisi wenyewe tuliwaweka madarakani?

    Kwa hiyo piganieni haki zenu. Sheria inasema asiajiriwe mgeni kwa kazi ambayo mtanzania anaweza kufanya. Hata ikibidi mgeni kuajiriwa kwa exceptions kama za wawekezaji au mashirika ya misaada, inatakiwa wawaandae watanzania kushika nafasi hizo mikataba yao inapoisha. Tumieni uhamiaji kuwadhibiti wageni wanaoajiriwa kinyume cha sheria.

    ReplyDelete
  6. Watanzania wanajua kulalamika lakini hii inatokana na malezi tuliyo pewa ya kijamaa, customer service kwetu tunaona kama tuna dhalilishwa. Nenda kwenye hotel yoyote na umkute receptionist , ana ongea kwenye simu na rafiki yake wala hajali kama kuna mgeni kasimama mbele yake. Waache waajiri wakenya so we can learn from them,

    ReplyDelete
  7. hata kama mtoto wako anakojoa kitandani sio jambo jema kupita njiani na kuwaeleza wageni kwani wageni watakimbia kumbe shida ni wewe. Shida inaanzia hapo wandugu

    ReplyDelete
  8. Maoni ya rais kuhusu udokozo ni ya kweli siyo tu kwa wafanyakazi wanaoajiriwa na wawekezaji.alichokosea Kikwete ni kushindwa kukiri kuwa udokozo unaanzia kwake yeye mwenyewe na mawaziri wake,benki kuu CCM katika uchaguzi na maofisa wengine wa serikali ngazi zote.Akisema watanzania wasiajiriwe kwa sababu ya udokozi inabidi tuagize rais na mawaziri kutoka nje.Uchaguzi unakuja utaona wanaojiandikisha kupiga kura ni watu mia moja laki CCM imeshinda kwa kura mia tatu,Sijui inabidi tuagize chama cha siasa toka nje?Suala la udokozo lipo nchi nyingi laki watanzania tumezidi,tunaiba sana na ni vizuri tumeanza kugundulika labda itatusaidia kubadilika.

    ReplyDelete
  9. watanzania kazikuwaajirindugujamaana marafiki hata kama hwanana ujuzi wa hiyo kazi. mkenya atawafaa sana

    ReplyDelete
  10. Acheni kulalamika Customer service zero, uwizi udokozi ndio mbele, rushwa ndio usiseme !! Ngoja jamaa aje awafundishe kazi msilete malalamiko, mnatakiwa mbadilike. Ndio maana wazungu wakiajiri hawaangalii vyeti vikubwa, wanaangalia uwezo,reference, cuatomer service etc. Sasa hapo bongo kila mtu ninayekutana naye anapiga masters mpaka za uchochoroni lakini huko kazini ni wizi mtupu, uzembe etc badilikeni !! kudadadek !!!

    ReplyDelete
  11. Watanzania ikiwa mtajirekebisha na kuthamini kazi zenu basi haja ya kuwaajiri wageni haitakupwepo. Hakuna sababu mwekezaji amwajiri mgeni kwa gharama mara tatu ya kumwajiri mtanzania kama hana sababu ya msingi. Sisi tukikosa kazi tunalalamika, tukipatiwa kazi tunringa na tunapenda kulalamika siku zote. Leo watu kutoka kenya, US, India, SA wanaletwa nchini na wawekezaji wengi - inamaana wawekezaji wote hawana akili? Jirekebisheni na msilalamike siku zote.

    ReplyDelete
  12. JAMANI SI KILA KITU ANACHOFANYA RAIS NI KIBAYA.TUMSIFU KWA KUONGEA UKWELI.MIMI NAPINGANA NA RAIS KATIKA MAMBO MENGI SANA,LAKINI HILI AMENIGUSA NA NAMPONGEZA SANA SANA.NI KWELI KABISA WATANZANIA NI WADOKOZI SANA.NDIO MAANA HATA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI WATU KARIBU WOTE NI WEZI.HII NI TABIA YA WATANZANIA.ETI "DEAL".NAOMBA WAWEKEZAJI WAONGEZE NGUVU.WAO WAMEKUJA HAPA SIO KUPATA HASARA BALI NI KUPATA FAIDA.SASA KWA NJIA HIYO WATANZANIA WATABADILIKA.WIZI SASA UMEFIKA MWISHO.
    MDAU
    WASHINGTON DC

    ReplyDelete
  13. Poleni kwa hayo yanayowasibu,ila mimi naona hakuna cha kulalamika km wadau wanavyosema hapo juu hesabuni wageni then mchukue sheria.Na kama pia wakati huyu mtu wa nyumabni alipokuwa madarakani na kulikuwa hakuna shida,so pia kwanini mwaogopa huyo mkenye kuletwa,kwani msianze kutafuta tabu wkt hata bado hayupo kazini,km wa kwanza alikuwa shwari basi km nyie mwajiamini na kazi zenu basi kila kitu kitaenda shwari,kwani hapo ni mahali pa kazi hivyo kazi kwanza then urafiki baadae km ni saa za mapumziko n.k..mimi sio ni tabu ila what i can say is let the guy come n see how things will be.nanyie mtie bidii kwenye sector zenu,hivyo kuepushe hata muajiri mwenyewe akiona kila kitu cha enda km before hata yy ataona aibu you never know.

    ReplyDelete
  14. mimi kama mtanzania sioni kosa lolote la mkenya kupewa kazi. Kosa liko wapi hapo? angepewa m-denmark jee? mngekasirika
    Mwafrika yoyote kama ana sifa na apewe hiyo kazi, maendeleo ndiyo yanapatikana hivyo, msituletee hizo.

    ReplyDelete
  15. Kwanza mie nina swali: Hivi kwa nini Hoteli hiyo inabadilisha jina mara Sheraton hotel, mara Royal Palm , mara Movenpick hotel, hivi kuna nini wadau werevu????

    Pili mie pamoja na kukemea wizi, udokozi, kuwepa kodi, kupata capital gains bila kuilipia n.k n.k Ningeishauri serikali kutafuta mbinu za kuelewa wawekezaji wanaendeshaje miradi yao.

    Njia mojawapo ya serikali kuwa na mkono wake kwa wawekezaji 'wajanja' napendekeza baadhi ya vyeo vya juu kikiwemo hicho cha Human resources manager vishikiliwe na wazawa.

    Sababu ya kupendekeza wazawa ni kuwa watakuwa macho ya watanzania kujua ni nini kinachoendelea ktk biashara za wawekezaji.

    Baada ya kuwadhibiti wawekezaji wa nje ili pande zote zipate manufaa(wawekezaji+watanzania), hili suala la kupunguza 'wizi' unaofanywa na wafanyakazi wa kitanzania jibu lake ni dogo sana.

    Kila mfanyakazi afanyiwe criminal record check polisi, hivyo kutakuwepo kumbukumbu na kama kutatokea uhalifu ni rahisi kumfuatilia mtuhumiwa. Na kumbukumbu hizo zitasaidia kupunguza tatizo hilo angalau kwa asilimia 95% , maana kwa asilimia 100 kitu hicho hakiwezekani.

    Pia ulinzi ukiimarishwa CCTV camera, uniform, logu-buku n.k tatizo hilo litamalizwa.

    Mie nilijua wawekezaji wamepata 'mtaji' kwa kunukuu vibaya dhana ya kauli ya mkulu wa nchi.

    Mdau
    Mzalendo

    ReplyDelete
  16. hivi nyie mnaosema ooh watanzania wamezidi ,ooh sijui mkome kwa sababu ni wezi, ooh ngoja mje kufundishwa adabu na mkenya Je nyinyi ni watu wa taifa gani? manake mnasema nyie watanzania mmezidi kama vile wewe humo! Au kwa kuwa tu unabeba boxi au unaishi ugaibuni basi wewe si mtanzania na sasa unatukana ndugu zako? Eti nilikuja hapo Tanzania nikakuta abcd .. acheni ushamba. tatizo mtu akikaa Ulaya kidogo tu basi kila akija bongo ni malalamiko tu ooh joto sana, ooh vumbi , ooh sijui huduma mbaya.. utafikiri alizaliwa kwenye barafu .. ili hali labda kaondoka mwaka mmoja tu .. watu bwana?ukienda ulaya tu basi wewe kila jambo la bongo unalilalamikia na kuona walioko nyumba hawana akili. Mi niko Ulaya lakini naheshimu nyumbani na sio kuwa na ulimbukeni wa kujifanya kulaumu kila kitu cha nyumbani. Watu wanadai haki zao nyie ooh watanzania wezi..Kwani hapa Ulaya hakuna wezi? Haya magereza yao wamefungwa watanzania? Nyie tafuteni maisha heshimu kwenu ... tena wengine hata mkiwa hapa Ulaya na sa mko na wageni wa nchi nyingine au wazungu mnaongea mnaponda kwenu .. ujue wale watu wengine wanawadharau nyie mnajianika ooh you know Africa sijui hivi sijui vile mambo mabaya tuu .. acheni hizo..

    ReplyDelete
  17. msilalamiki kweli muna mikono ya kudokowa nakumbuka nimeshawai kula hapo wakati naitisha bill yangu waiter haliniambia kama nataka nimlipe hela cash hatanifanyia half price ama kama sitaki hanipe bill iliyokuwa print hikiwa kamili kilichotokea ni siri yangu lakini ni kweli hamuna uhaminifu

    ReplyDelete
  18. ukweli nikwamba watanzania wengi hasa serikalini wanafanya uzembe wa hali ya juu na maadili ya kutoa huduma kwa wahitaji huduma ni almost hayapo,watu wakipewa ofisi wanaziona kama zao,watafanya wanavyotaka na sio kufuata taratibu,ethics,na hata ubinadamu wa kutotaka kumpotezea muda mwenzio na rasilimali zake.
    huenda kweli kinachofanyika hapo sio sahihi lakini kwa upande wapili lazima tuangalie je huduma mnazozitoa mnazitoa kwa kiwango kinachostahili bila kuwekewa shinikizo na uongozi?au hadi mtishiwe ndipo mnafanya kazi inavyosttahili,maana kama ndivyo basi uongozi unajali mtu anayeweza wapeleka mnavyostahili kupelekwa,na kama ni mkenya shida iko wapi kama quality of service itakuwepo na hoteli itapata faida na nyie muendelee kulipwa chenu?
    mimi mwenyewe nikishika nafasi mahali popote nitahakikisha waliochini wanafanya kazi kwa discipline inayostahili,hata kama ni ndugu ilimradi amequalify na anafanya kazi kwa discipline ni sawa,ila kuleta uzembe unao cost watu muda,pesa,na hata usalama wao siendekezi ujinga huo.
    nakama nikiingia ktk ofisi watu wenye tabia za kubweteka na kujiona mungu wakanizengua mimi sina simile kupotezeana nao muda,nakusubiri mtaani nakutia adabu kisha nakukumbusha maana kuzungushana ktk vyombo vya sheria miezi 5 sina muda mchafu huo.
    nchi yetu itaendelea pale tu watu watakapo jua kuwa maendeleo hayaji kwa kubweteka ila kwa kuthamini kazi na muda.ofisini sio sehemu ya kuchat na kutia story,nikazi mtindo mmoja,mteja kaingia napokelewa anahudumiwa anaondoka thats it!!!iwe serikalini iwe private. sio mtu katoka mtwara anagandishwa siku 4-10 kilasiku anafuatilia jambo hilohilo na kupigwa tarehe za njoo kesho huku akitoka watu wanaendelea kutia story hadi watakapo muona tena kesho ndo wanajifanya wanatafuta file.
    ntawatia adabu sana,maana yote hayo nimepitia na kuzungushwa sana.najua uchungu wake.
    kama mko sahihi teteeni haki yenu,lakini kama nyie ndo chanzo fyateni mkia mkae kimya hakuna kuleta uzembe kazini.do your job get your right mind your business thats it!!

    ReplyDelete
  19. NDIO WATANZANIA TUMEZIDI NI WEZI!!!! WEZI MAJAMBAZI!!!!! CUSTOMER SERVICES ZERO!!! WIZI 100% UWIZI UNAANZIA SERIKALINI KWA WALIO JUU MAFISADI MPAKA VIBAKA BARABARANI. HAKUNA MSAFI HUKO. WACHA WAAJIRI WAKENYA. HATA MIMI NIKIJA KUWEKEZA HUKO SITAAJILI WATANZANIA HATA KAKA YANGU SIM-WEKI. TUACHENI TABIA ZA KULALAMIKA, TABIA ZA KUOMBA OMBA, TUANZE KUJITUMA NA KUFANYA KAZI KWA BIDII NA MOYO NA LOYALITY. TUTAPATA MISHAHARA MIZURI NA KUENDELEZA NCHI. NCHI ITAJENGWA NA WANANCHI WENYEWE. SISI WENYEWE, LAKINI TUKIENDELEA NA VIJITABIA VYA UDOKOZI MTASHANGAA NCHI INACHUKULIWA SI WAKENYA TU NDUGU ZETE WA JIRANI HAPO. HATA WACHINA, SOUTH-AFRICANS, HINDI TAYARI WAMECHAJINYANYULIA CHA KWAO, WAMAREKANI WAKO NJIANI, MTUTABAKIA VIBARUA TU KATIKA NCHI YETU WENYEWE. HATA HOUSE-KEEPING HATUTAPATA. TUACHE UWIZI!!! NDIO TABIA YETU. TUNAJUA SANA UDOKOZI. NO WAY AROUND IT.LOOK YOURSELF IN THE MIRROR BEFORE STARTING COMPLAINING.

    ReplyDelete
  20. NAWASHANGAA SANA WATANZANIA WANAOISHI NJE NDIO WA KWANZA KUSHABIKIA WAGENI TOKA NJE WACHUKUE KAZI ZA WATZ. Wengi hawajiulizi kwanini wana elimu na wanaendelea kuwa walinzi na kufuta wazee mavi kwenye hizo nchi wanazoishi. Kwanini hawajiulizi inakuwa ngumu kwa mtu wa nje kupewa kazi proffesional. WAPO WATU TOKA NJE KIBAO WANAOFANYA KAZI TANZANIA NA HAWANA HIZO SIFA. Ila ni aibu pia kwa Kiongozi mkubwa wa nchi kutoa tamko bila kujua madhara ya anachokisema. KIKWETE ALIJUA ANAWASAIDIA WATAZ KWA KUFANYA VILE KUMBE HAKUJUA KAULI ILE ALITAKIWA HAITOE WAPI. kazi sana.

    ReplyDelete
  21. Ndugu wafanyakazi, hongereni sana, kwanza nianze kwa kusema yawezekana kabisa tabia ya udokozi ipo na mbaya maana itatuharibia jina la watanzania! Maoni yangu ni kwamba mmefanya jambo la ujasili kuweka wazi kinachoendelea hivyobasi nadhani ni busara kutumia vyombo vya habari kama magazeti na pia kupeleka lalamiko lenu moja kwa moja kwa waziri na nakala kwa bodi zote zinazohusika (Ikiwezekana hata kwa Rais). Hii ni vita ya kulinda ajira za watanzania lazima tukomae tusikubali kuwa vibaraka na kuruhusu wageni wachukue kazi zetu na tujitahidi kujenga hoja kwa kurejea nini sheria inasema, na pia ni muhimu sana tuwe waaminifu na wachapa kazi wazuri ili hawa wawekezaji wasipate vijisababu vya kuajiri wageni, Ninawaunga mkono na Mungu awajaalie!
    Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  22. Nanyiii, suala dogo sana, kwani wa TZ mpo wangapi hapo. Hamna haja ya kulalamika, kimya kimya, akiajiriwa tu mnajiorganise mnampiga vibao viwili vitatu. Mnamuacha a week, mkiona mnoko wa kuleta ukabila, ubaguzi wowote aaaakh, piga tuu.

    ReplyDelete
  23. kwani uongo mnaiba mpaka vijiko vya hoteli

    ReplyDelete
  24. Kweli watanzania wengi wetu ni wadokozi.Ni vyema hata wakaajiri wageni wote, maana uaminifu utakuwepo kazini, uzembe utapungua na malalamishi yataisha.
    Cha msingi nyie wafanyakazi mnaolalamika ni bora mkaenda kutafuta kazi kwenye kampuni au sehemu nyingine kama mnaona hamtaki kuwa na bosi mkenya.Kazi ni nyingi mno sasa sijui kinachowafanya mng'ang'anie hapo ni nini kama sio huo udokozi wenu.Mtajikuta ni watu wa kulalamika kla mnapokwenda.Tuache ushamba wa-tz, kwani kuna maelfu ya watz wanafanya kazi nje ya nchi na wamepewa kutokana na uaminifu wao, sasa mnataka nao warudishwe ?

    ReplyDelete
  25. Asilimia kubwa ya wa sisi waTanzania tuna tamaa, njaa, wivu, vijicho, uzembe, uvivu na kiburi kazini, hasa kwenye mashiriki ya umma na serikalini. Kampuni nyingi zenye uongozi kutoka nje, au za waHindi zinafanikiwa, kwani wanajua jinsi ya kutubana. Sisi ni Hovyo na tunahitaji viboko na udiktekta kidogo. Ukweli unauma lakini ni ukweli.
    Lakini kamshahara kenyewe hakatoshi. tehe tehe tehe

    ReplyDelete
  26. I AGREE WITH SOME COMMENTS REGARDING UZEMBE KAZINI...ALL BECAUSE OF UJAMAA IN MY OPINION...SIKU ZILE WAKATI UJAMAA WAS INTRODUCED IT SOUNDED VERY GOOD...JUST LOOK AT OUR POLITICIANS...ALL OF THEM ARE WAZEMEBES...THIS IS WHY WE ARE NOT PROGRESSING...BUT WE TANZANIANS ARE NOW PAYING THE GENERATIONAL PRICE...
    DO NOT LOOSE HOPE AND I AM SURE THERE ARE MANY MANY TANZANIANS WITH EXCELLENT CUSTOMERS SERVICE WHO CAN DO A VERY GOOD JOB A BEING A MANAGER...GOOD LUCK

    ReplyDelete
  27. IT'S OK KUAJIRI HR KUTOKA KENYA.

    KWANZA, TAYARI TUMEISHAINGIA KWENYE SOKO HURU LA AJIRA LA JUMUIYA YA AFRIKA YA MASHARIKI. KAMA MKENYA NDIO ANAFAA KWENYE HIYO KAZI KWA SASA BASI NA AJE TU.

    PILI, KUONGEZA UFANISI KAZINI ILI KUACHANA NA ILE HALI YA KUTOJITUMA MIONGONI MWA WAFANYAKAZI WENYEJI.

    TATU, KUONGEZA USHINDANI.

    NNE, KUPUNGUZA AU KUONDOA KABISA TABIA YA WIZI.

    WATANZANIA TUJIFUNZE, NI KWELI TUNA KERO SANA MAKAZINI ESPECIALLY TUNAPOKUWA NI WAMATUMBI TUPU. ACHENI TABIA YA ULALAMISHI FANYENI KAZI. SIDHANI KAMA HUYO MKENYA ANAKUJA KUWATIMUA WATU WANAJITUMA KAZINI.

    KUWENI NA CONFIDENCE.

    ReplyDelete
  28. Ukitaka kujua adha ya tabia zetu za uvivu na udokozi anzisha biashara yako binafsi, utajuta na kujua kwanini makampuni mengi yanapenda kuajili wageni. Ni lazima tubadilike, kwa hili siwaungi mkono wafanyakazi wa Movenpick. Nilikuwa na timu ya Ivory Coast kwenye training session, wamelalamika vyumba vya kubadilishia nguo vichafu!, vyoo vichafu unampigia muhusika yuko nyumbani!. Ndiyo maana tunaogopa EAC kuruhusu free mobility of labour kwani sisi wavivu na wadokozi. kwani wakenya wana macho mangapi?, miguu mingapi?.

    ReplyDelete
  29. jamani wantanzani tunalalamika kila siku ilhali kazi hatuwezi kutokana na madili yetu mabaya ya kuiga mambo ya kifisadi.customer service kweli haiyo na watanzania wanao kimbia uhamiaji huwa ndio wale wakudokoa.
    Kaka , dada mtanzania kazi kujituma sio kulalamika eti wakenya. waganda blah blah nyingi fanya kazi.

    Ila movenpick kweli nyie wadokozi haswa kwenye swala la menu ya chakula cha mchana....

    ReplyDelete
  30. sawa kabisa tunalindana sana hakuna tena kujuanajuana, shule nzuri kazi nzuri,heshima kazini muhimu,kwani mmesahau yaliyotokea benk kuu?? au bima'wacheni majungu nyie fanyeni kazi mujenge taifa leni,hakuna tena kulindana mambo hayo yalipitwa na wakati angalieni mbele sawa jamani

    ReplyDelete
  31. Ndiiyo. Watz ni wezi sana. Hata mabenki yanashindwa kutangaza lakini yanalizwa sana. Ushauri wangu ni kuwa tumieni chama chenu cha wafanyakazi kama mnacho halafu wao waiulize menejimenti ieleze huo udokozi umefanywa na nani na mara ngapi.
    Mkipata picha kamili ya tatizo Basi wao kama wanawajua hao wadokozi kwa majina basi wawapeleke mahakamani. Otherwise utakuwa ni uzushi tu

    ReplyDelete
  32. Kama nyongeza, unapomuibia muajiri wako unategemea akukenulie meno? Hiyo ndo hasara ya mambo ya kujuana makazini...mimi naamini kabisa kuwa huyo jamaa wa HR anawalinda aliowaingiza hapo na wala si ajabu wengine wanampa ngono..kwani hatuwajui wabongo bwana? Hebu acheni kulalamika...I love the move hii Hoteli inayochukua..fanyeni kazi, kuweni waaminifu au vibarua vitaota ndago. Mdau-USA

    ReplyDelete
  33. MDAU LONDONloJanuary 08, 2010

    HEE NYIE MNALALAMIKA KUAJIRIWA WAGENI WAKATI RAIS MWENYEWE KESHASEMA WATANZANIA NI WEZI? ACHA MOVEN PICK HATA UBALOZI WA TANZANIA LONDON MARECEPTIONIST NI WATHAILAND, KWA KIFUPI SELIKALI HAIJALI NANI AFANYE KAZI WAPI ILA INACHOZINGATIWA NI NANI MWIZI MMAKONDE AU MCHINA? KAMA MWIZI NI MMAKONDE BASI MCHINA ANAPEWA MDARAKA FULL STOP.

    ReplyDelete
  34. Watanzania wavivu na wanapenda kulalamika tu. Hadi Raisi, Mkapa na sasa Kikwete wamesema ukweli watanzania ni wavivu na wanapenda mteremko. Sasa kama wewe sio MWIZi una wasi wasi gani hata wakiajiri mtu toka sayari ya saba au mwezini? Fanya kazi yako usianze ooh wanasema sisi wezi etc? Kama mtu sio mwizi huwezi kuwa na wasiwasi kwani upo kwenye mikono safi

    ReplyDelete
  35. MOVENPICK HONGERENI SANA lazima muwanyoroshe hawa waTZ hawana uaminifu ni kweli, na JK kawapa black and white....toka ukifika airport mpaka uswazi ni ubabaishaji/usanii tuu watu hawajali muda,hawaheshimu kazi,kazi porojo na majungu.
    UONGOZI MOVENPICK fukuza wazembe wote ajiri wakenya/waganda wanaojua kazi ni nini.
    JK wape shua hao kazi udokozi tuu,mtu anataka shortcut za maisha.
    Hongera MOVENPICK KWA KAZI NZURI MNAYOIFANYA YA KUONDOA UOZO HUO.
    Mdau wa Mbezi Beach.

    ReplyDelete
  36. kwakweli nimefurahishwa na hili jambo la kuajiri wageni badala ya watanzania.sababu ni kama ambazo wenzangu wameongelea hapo juu mimi pia nilikuwa Tanzania mwezi wa 11 kwa kweli ni aibu tupu.Kama ofisi za manispaa ni uozo mtupu yaaani watu ni wavivu hawapendi kufanya kazi,wanamishauo ya kishamba,kwa upande wa banks ndio kumekufa kabisa, mpaka mtu huwezi kukasirika tena unaamua kusema hii nchi sasa basi.Halafu eti mnalalamika?wakati mnajijua nyie ni wavivu na wezi mnapenda shortcuts.Mimi naandika barua nyingine iende serikalini waongeze idadi ya wafanyakazi wageni ifikie 15 au zaidi,its about time,mnatakiwa muamke na mfanye kazi kwa bidii kusudi hata hao wawekezaji wenyewe waone,sio kulalama tu.

    ReplyDelete
  37. Mimi sishangai kwani mweshimiwa Rais Kikwete analijua hilo la udokozi na wala sio siri mbongo usipodokoa unaonekana mjinga wabongo kuiba ndio ujanja!!!hata serikalini wizi ni mkubwa sana rushwa vyote hivyo waache wamuajiri mkenya mjifunze na bado wakenya watachukua kazi nyingi sana bongo huu ni mwanzo tu
    Suluisho ni nini????/
    mimi naona uongozi wa juu unatakiwa kuwa siriasi kwa mfanua wakati wa nyerere rushwa ilikuwepo lkn haikuwa ya wazi hivyo saa ingine mtu unazikimbia pesa kwa sababu mchonga alikuwa siriasi

    to be continued....

    ReplyDelete
  38. WATANZANIA FANYENI KAZI ACHENI MAJUNGU LA SIVYO KILA SIKU MTALETEWA WAGENI KUWAONGOZA KUTOKANA NA TABIA ZETU CHAFU.KAMA JK ALISEMA KUWA TUNA VITABIA VYA UDOKOZI BASI TUNA HAKI YA KULETEWA WAKENYA NA MATAIFA MENGINE.EBU NINYI WAFANYAKAZI FIKIRINI..LEO NAANZISHA BIASHARA YANGU LAKINI WATU HAWAFANYI KAZI INAVYOTAKIWA( KWA TIJA) ILI MRADI TU WANARIPOTI KAZINI HAKUNA 'CREATIVITY" MNATEGEMEA NINI? LAZIMA UTAFUTE WAFANYAKAZI WATAKAOLETA TIJA NA MAFANIKIO KWA KAMPUNI NA SI VINGINEVYO.NAELEWA HALI HALISI KAMA MTANZANIA LAKINI UKWELI UPO PALE PALE 'YOU NEED TO DELIVER AND NOTHING ELSE' SIYO SIRI UJAMAA UMETULEMAZA KWA MUDA WOTE HUO.

    ReplyDelete
  39. Nyoooh na mkome kwa wizi.Nashauri pia zoezi hili la kuajiri Human Resources Managers wa kigeni pia lifanyike bandari(TPA),Polisi, mamlaka inayoendesha viwanja vya ndege,DAHACO,Posta,Reli,Tazara,Uhamiaji bila kusahau TRA.Mashirika yote haya yanahitaji kufanyiwa restructuring na kufukuza wazembe wote, wezi, wabadhirifu na wala rushwa bila kumwogopa mtu kutokana na cheo chake au nafasi yake katika jamii. Cha kushangaza ni kwamba mbona wenzetu wa Rwanda hivi majuzi tuu wamefukuza kazi watu zaidi ya elfu tatu bila kujali wao ni nani kwa mambo kama hayo ya kifisadi, sisi tunashindwa nini? Watanzania lazima tuondokane dhana zilizopitwa na wakati kwamba kila mtu anakula kazini kwake. Inashangaza kuona miezi michache iliyopita raisi wetu alipotembelea bandari ya Dar es salaam alisema anakijua wafanyakazi wanachokifanya (akimaanisha wizi)na bado mpaka leo hakuna hatua yoyote aliyoichukua kurekebisha hali hiyo!! Hivi tutafika kweli?

    ReplyDelete
  40. ni kweli mmezidi wizi na rushwa mnadhani ni haki yenu
    rusha na wizi wa mali za umma tanzania sasa hivi ni maisha ya kawaida na haki ya msingi ya mtanzania yoyote (i.e. vigogo na wananchi pia)

    ReplyDelete
  41. Wafanyakazi,

    Nitafikisha kilio chenu kwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya Wakurugenzi amabaye ni rafiki yangu.

    Mimi nipo nanyi.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  42. Mnalalamika ni nini hili ni treila tuu subiri muvi lenyewe EAC itakapoingia rasmi mwezi wa saba

    ReplyDelete
  43. Mimi naunga mkono uongozi ulete meneja toka kenya,kwa sisi itatusaidia kujifunza kuheshimu kazi pamoja na uchapakazi.Sisi wabongo tunajulikana Dunia nzima kama sisi ni wapiga domo sana,wavivu na sio waaminifu katika kazi,ni time sasa ya kukubali udhaifu wetu na kujaribu kujirekebisha.
    Na mukitaka kuthibitisha kuwa hoja za uongozi zina uzito,MICHUZI nenda movienpick ukawahoji jamaa,wenyewe pia wameshachuchoka.
    MDAU ISTANBUL

    ReplyDelete
  44. Well said avove mchangiaji...It's very tru wakenya( I mean most of them) wakiwa job hawana mashauzi ya kijinga. Swala la kwenda hotelini unamkuta dada wa kibongo ana zero customer service skills utasikia kutapika.
    Watanzania tufungue mamcho na tulearn kwa wenzetu tuache lawama. Kama mtanzania anaqualify apewe but kumnyima mkenya anayequalify kwa madai kwamba tunatakiwa kuhire wabongo mimi sikubaliani nayo
    Na sio kwamba watanzania wenye exposure hawapo bali ni wachache sana na kwa ujumla CUSTOMER SERVICE bongo ni jambo lakuangaliwa kwa kina kikubwa saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana

    ReplyDelete
  45. Ubabaishaji tumezidi, lakini sio kigezo chakunyanyasika, anaye babaisha atimuliwe, pia tusilaumiane sana watanzania nakutukuza wengine. Wote binadamu tu, 2nakosea ila tuwe wepesi kujirekebisha. Pia tuache kujumuisha mambo(generalization) like huyo anonymous wa Tarehe Fri Jan 08, 05:58:00 PM hapo juu - NANI KAKWAMBIA AIRPORT ZA KENYA MIZIGO HUA SALAMA? unabahati kama hujalizwa hapo au ukomakini na jinsi unavyofunga mizigo yako. WATANZANIA TUNAWEZA, NDIO TUNAWEZA, MSIJIKATISHE TAMAA KIRAHISI WANDUGU. Na muwekezaji akileta ujinga kwakweli inabidi ashughulikiwe tu, vivyohivyo na kwamfanyakazi. It should be a WIN-WIN ENVIRONMENT. HAPPY NEW YEAR WAPENDWA WATANZANIA

    ReplyDelete
  46. NINAKUMBUKA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA TATU MZEE MKAPA ALISEMA KUWA TRENI YA UTANDAWAZI INAPITA KWA HIYO KAMA HAMTAPANDA BASI MTAACHWA.
    SASA HALI IMEANZA KUJITOKEZA, WAWEKEZAJI (INVESTORS) WANAHITAJI MAREJESHO KUTOKA KATIKA MITAJI YAO WANAYOWEKA. KAZI YA KUHAKIKISHA KUWA INVESTORS WANAPATA MAREJESHO YAO IMEKABIDHIWA KWA BOARD OF DIRECTORS NA MANAGEMENT TEAM. KWA HAKIKA KAZI HIYO SI RAHISI KWANI INAHITAJI BOARD NA MAMAGEMENT KUWEKA MIKAKATI AMBAYO ITAWEZA KUFANYA KAZI NA KUKIDHI MATAKWA YA WALE WALIOWEKA FEDHA ZAO.
    TUKIANGALIA SUALA LA MOVENPICK, INVESTORS WAMEWEKA PESA ZAO WAKITARAJIA KUPATA MAREJESHO KUPITIA KWENYE DIVIDENDS AMBAZO ZINAPATIKANA BAADA YA HOTELI KUTENGENEZA FAIDA. FAIDA HAIWEZI KUPATIKANA BILA YA KUWA NA WAGENI NA WATEJA WATAKAOTUMIA HUDUMA ZA HOTELI HIYO. HOTELI SI UZURI WA JENGO NI PAMOJA NA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA WAFANYAKAZI IKIWEMO KUWANYENYEKEA WAGENI, UAMINIFU NK. TABIA YA KUKOSA UAMINIFU MIONGONI MWETU IMEKUWA NI KERO KWA WAGENI NA HATA WAWEKEZAJI. WAPO WATANZANIA AMBAO NI WAFANYAKAZI WAZURI TU NA NI WAAMINIFU KABISA, LAKINI BADO KUNA BAADHI YA WAFANYAKAZI SI WAAMINIFU KATIKA HOTELI HIYO YA MOVENPICK NA BAADHI YA SEHEMU NYINGINE ZA HUDUMA.
    HATA MIMI LEO HII UKINIPA KAZI YA KUSIMAMIA HOTELI ZETU AU MABENKI SINTOSITA KUWAAJIRI WATU WAAMINIFU NA WACHAPA KAZI BILA YA KUJALI WANATOKA SEHEMU GANI YA DUNIA HII, KWANI UKIMCHELEA MWANA UTAKUJA KULIA MWENYEWE.
    WITO WANGU KWA WAFANYAKAZI WA MOVENPICK, WAFICHUENI WALE WOTE WASIO WAAMINIFU NA WAZEMBE HALAFU MUONE MWAJIRI WENU KAMA ATAPOTEZA TENA IMANI NA NINYI.

    ReplyDelete
  47. Hakuna haja ya kuogopa kama unafanya kazi yako sawa sawa, hata aje nani hawezi kukuonea, sasa unapokuwa mahali umekaa kiufisadi + longo longo ndio unaanza kutetemeka uongozi unapobadilishwa, mimi nafanya kazi nje lakini bosi wangu kutoka europe aliyeshafanya kazi bongo miaka ya zamani aliniambia kuwa TZ wizi upo sana alishangaa kuona watu wanaipa vipakti vidogo vya majani ya chai ....ushauri - Kulalamika hakusaidii, chapa kazi na wewe utakuwa kama huyo mkenya!

    ReplyDelete
  48. Ndugu zangu poleni! Pili hakuna namna ya kumlaumu Rais kwa tazamio alilolitoa kwenye ufunguzi wa hotel ya crest.
    Jambo la muhimu ni kuhakikisha kwa mujibu wa sheria za uajiri iliyowekwa kwa kampuni na wawekezaji ndani ya nchi yetu kuwa meneja rasilimali (human resource manager) anapaswa kuwa mtanzania inapaswa kufuatwa.

    Hili sio suala la kualaza damu hadi pale haki ya mtu inapokanyagwa ndio tuanze kulalamika. Ushauri wangu ni kujitahidi kuwazuia hao watu wasijeari mtu ambaye si mzawa kuchukua nafasi ambayo kisheria haruhusiwi.

    Iteni vyombo vya habari vije kuchukua habari yenu kutokea hapo kazini kwenu, hakikisheni mnatoa taarifa serikalini (wizara ya kazi) kuhusiana na hili na muwe wamoja. Yeyote atakayejitoa ataharibu uwezekano wa haki kutendwa dhidi yenu. Natumaini utweza kuendelea kutujulisha yanayoendelea kujuri kwenye suala hilo.

    Thanks

    ReplyDelete
  49. sioni sababu ya watanzania kuendelea kutegemea wawekezaji kutoka nje na hali kuna watanzania wanaweza kuendesha nchi tena wengi sana tatizo la hayo yote ni serikali yatu urasimu umezidi, na uzalendo umeachwa je kuna watu wadokozi kama wawekezaji kutoka nje, kila baada ya miaka mitano wanabadilisha mikataba au kukwepa kulipa ushuru serikali au wanafikiri hajui,pia sioni sababu ya kumuajiri mkenya, wakenya wamezidi tanzania warudi kwao wakaihamamisha serikali ya moi iongeze nafasi za ajira ili waachane na umachinga katika nchi za watu,serikali iingilie kati suala hilo.

    ReplyDelete
  50. Mkenya atatokomeza vipi udokozi?
    Kama ni kweli kuna udokozi sugu wafukuzeni hao vidokozi lakini msitukane watanzania wote, hii ni aibum hata Kenya mbona kuna vibaka na malaya wachafu wa barabarani wanaoganda watalii na kuibia watalii?
    Solution,
    Wekeni camera halafu lipeni wafanya kazi mishahara mizuri. Na pia mwizi akibainika afukuzwe kazi.
    Eti watanzania wezi,
    Sema tanzania kuna wizi kwenye mahoteli unaosababishwa na wafanyakazi wenye tamaa na wasio na maadili ya kazi.

    ReplyDelete
  51. wizi hata ulaya upo. sisi tumeiba sana tena viongozi wa mission ni wazungu wenyenwe. tulikuwa tunafanya na wataliano wa wasipanish, wewe acha tu, mimi nilikuwa mgeni sijui kuiba wenzangu wakanifuata na kuniambia "maza faka" this is not your father's hotel. waakanza nifundisha kuiba na kuangalia kamera kama iko upande gani. ila sisi tulikuwa na siku za kuiba si kila siku tu. tulikuwa tuna gawana naye tajili. Ijumaa ndio ilikuwa siku ya mavuno. tunaleta mpaka bia zetu anapewa bar tenda kuziuza. tukimaliza za kwetu ndiyo tuna uza za hotel na kuwaliza vile vile. Mbongo nilikuwa peke yangu. kwa hiyo huwezi kusema eti watanzania tu ndiyo wezi, si kweli. watu wote wana iba sana tena humu kwenye mahoteli usiombe.
    mdau UK.

    ReplyDelete
  52. watu wanapowekeza hawategemei upumbavu wa kudokoa, na kama jamaa wanataka kubadilisha uongozi kwa madai hayo basi kuna ukweli, tuache wizi,kama ujui uchungu wa kuibiwa uliza walio ibiwa. nchi inanuka wizi na sheria hakuna, na hayo ndio matokeo. pum.........v

    ReplyDelete
  53. msilalamike hapa ni kweli kabsaa wafanyakazi wa mahotelini mmezidi udokozzi saana wezi wa glasi wezi wa vijiko wezi wa uma wezi wa sahani wezi wa vikombe wezi wa sukari wezi wa mashuka wezi wa sabuni wezi wa mataulo wezi wa maforonya hadi toilet paper nyinyi ni wezi wa kila kitu kitakachokaa usawa wa kuiba bado hamjabambika bei za uongo nyinyi ni machori msilalamike naandika hapa kuna watu wapo hoteli moja bomba kuliko zote hapo dar wanakwiba pale bar level 8 kama hawana akili nzuri msilalamike nyinyi ni machoriiiiii tuu kama yale mengine ya pale JKN hamna tofauti ng'o tofauti yenu ni vitengo tofauti. my michuzz fikisha hii nzima nzima bila zengwe
    manka wa canada

    ReplyDelete
  54. huyo anayesema watanzania tumezidi udokozi kwani hajui mtoto wa nyoka ni nyoka hawezi kuwa mbuzi, kwani hao viongozi wa juu serikalini sio wadokozi tena wa kodi zetu walala hoi? mafisadi wakubwa sasa kwa nini na sisi huku chini tukipata nafasi tusiibe? kwanza hayo makampuni ya nje ndio ya nambari 1 kukwepa kodi na kunyanyasa wazawa, kwani hamjui kwa mfano makampuni ya madini hasa kule shinyanga mikataba yenyewe mibovu wanakwepa tu kodi kazi yao ni kuvuna tu dhahabu na kuwalipa wazawa mishahara mbuzi na wao kujilipa madola, mi naona ukipata chance we fanya kweli.

    ReplyDelete
  55. tena nyinyi mkome kulalamika humu ndani mmesikia?mna huduma mbaya kuliko mahotelier woote duniani mna nyodo kama wafanyakazi wa TRA tena nyinyi mkiona wazungu mnawakimbilia mkiona weusi wenzenu mnawanyari wee tabia hii iko pale sea cliff hotel kisa ni hivyo vitipu ndo vinawazingua wakati na sie tunawakatiaga tip za nguvu mnajidai sana bora mnyooshwe na wageni mjifunze maadili ya kazi mara mje kuhudumia mezani mmenuna ebo mambo yenu ya nyumbani huko huko pale ni ku smile tuu na mgeni watu tumekuja kutumia fweza zetu tunakutana na limtu limevimba kama chura mwenye mimba hatupendi huduma chafu chafu fanyeni kazi zenu kwa kujituma mtapata tip tuu mliomba kazi wenyewe maji ukiavulia nguo huna budi kuyaogaaaaaa!!!!

    ReplyDelete
  56. Kelele za chura hizo. Nchi ishachuliwa na wawekezaji, ooo hoo!

    ReplyDelete
  57. Mimi nasema: NDIYO kabisa Wafanyakazi wa MAHOTELI ni WEZI wakubwa.
    Hizi njaa njaa za Elf10,20 ndizo zinaleta image ya nchi nzima.
    NAPONGEZA: Hatua ya kuleta WAGENI wawe mameneja ili wabongo wajue umuhimu wa ku-behave.

    MAAMUZI mazuri kama hayo yakifanywa kwenye jeshi la Polisi na hata kiongozi MKUU wa nchi akiwa MUAJILIWA toka nje..huenda TUTAZINDUKA.

    ReplyDelete
  58. US BLOGGERSJanuary 09, 2010

    SINCE IM A LAW BY PROFESSIONAL IM HERE TO ANNOUNCE THAT YES AN EMPLOYEE CAN BE FIRED UP FOR NO REASON WHAT SO EVER, IT IS ONLY DEPEND ON YOUR CONTRACT, I MEAN CERTIFICATE OF CONTRACT. MANY HOTEL WORKERS, BARMAIDS AND HOUSE KEEPERS ARE EMPLOYED WITHOUT THIS CERTIFICATE THEREFORE CAN BE FIRED UP WITHOUT JUDGEMENTS AT ALL. THE ONLY PERSON KNOWS IS GOD NO BODY ELSE. AS FAR AS STEALING IS CONCERNED THIS IS KNOWN ALL OVER THE WORLD THAT WE ARE THIEVES SO INVESTERS KNOWS THIS BEFORE EVEN THEY GET INVESTMENTS SO I DONT THINK THIS IS CUMBERSOME AT ALL. AFTER ALL IT IS BETTER THAN BEING BURNT FOR STEALING LIKE THE DUDES OF KARIAKOO ARE DOING TO OTHER HUMAN BEINGS BURN THEM WHILE THEY WERE ALIVE IN PEACE, SO I THINK WE ARE OKAY IN THAT PART.

    ReplyDelete
  59. NA BADO, WATANZANIA WASIPOKUWA MAKINI NA KUJIREKEBISHA WATAJUTA KUZALIWA TANZANIA.

    UZEMBE KAZINI, UJANJA UJANJA MWINGI, KUTOFUATA SHERIA HAVITATUPELEKA POPOTE.

    ReplyDelete
  60. Mim naona kwa watanzania sio udokoz tu pia ni wazembe sana,nina mfano mmoja kuna siku nilienda benk ya NBC coorporate nikakuta foleni ndefu sana mpaka watu wengine wamekaa kwenye mabench kusubiria foleni,katika ile benk kuna counter zaid ya nane lakini cha kushangaza ni counter mbili tu zilikuwa zina watu wanaotoa huduma nakuambia niliganda pale kuanzia asubuh saa 4 nikaja kupata huduma saa 8,na wale wahudumu wawili waliokua pale walikua wanamhudumia mteja kama hawatak kwa sabab walikua wanachukua mda mrefu sana kwa kila mteja.Na ukiuliza hamna jib la maana unalopata.Kwa hiyo watanzania shida yetu tunafikiria namna ya kufanya ufisadi tu hatujitum kwenye kaz ni wazembe.

    ReplyDelete
  61. SASA NYIE WATOA HOJA NAWAAMBIA KENYA NDIO KUNA MAFISADI PAPA HAPA TZ NI CHA MTOTO KAMA HAO MOVENPIC WANAONA WAKENYA WAAMINIFU NA WACHAPA KAZ WAMECHEMSHA.

    ReplyDelete
  62. KWA NINI HOTELINI NDO WALETWE WAGENI TU.BASI HATA VINGUNGE WA NCHI WAJE TOKA KENYA KWANI HATA WAO WAMEJAA WEZI TENA WAKUBWA.LOOOOO

    ReplyDelete
  63. Mimi ni mtanzania na naipenda nchi yangu. lakini kama nikianzisha kampuni siko tayari kuwaajiri watanzania, kwanza ni wadokozi(wezi) wazembe, wababaishaji na si waaminifu. hilo tukubali na wawekezaji wengi sana wanalijua hilo na siwalaumu.kwa hivyo tuache kulalamika na turekebishe tabia zetu

    ReplyDelete
  64. China viwanda vinatengeneza maziwa ya watoto wenye sumu, serikali ya China na wachina hawasemi tuwaite wageni ili kutatua matatizo hayo mabaya kabisa.

    China wanatatua matatizo hayo kwa kufuata sheria na uzalendo wa kuipenda China, kwa kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa.

    Naungana na mdau Mzalendo kuwa Tanzania hatuna uzalendo na ndiyo maana tunatafuta njia za mkato kwa kuajiri wageni na kukumbatia wawekezaji wa nje hata pale ambapo tunauwezo wa kutatua masuala ya 'wizi', udokozi n.k

    Sasa badala ya kuimarisha ulinzi na usalama, sie tunakimbilia kuwakabidhi ofisi, viwanda, migodi, mashamba wageni ili watutatulie matatizo?!!

    Marekani kutokana na uroho wa mfumo wa kiuchumi wa kibepari uliopelekea mabenki yao kuyumba na baadhi kufa, hawakutafuta dawa kwa kuwaajiri wakomunisti toka Urusi, China au Korea ya Kaskazini.

    Marekani pamoja na sera zao za kibepari waliamua kufuata angalau kwa kipindi kifupi 'ushoshalisti' yaani serikali kutumia pesa za walipa kodi kunusuru 'mabenki binafsi', yote ikiwa ni kuinusuru Marekani uchumi wake usianguke au kuchukuliwa na wageni.

    Hivyo dawa mujarabu ya tatizo ni uzalendo za dhati kwa kufuata sheria na usalama, ili kunusuru taifa lisiibiwe na wageni kama mdau Mzalendo alivyobainisha.

    Mdau
    Jijini London

    ReplyDelete
  65. Mimi nimefurahishwa na hili jambo pamoja na comment za wadau wanaokubali wageni waje kutufundisha kuthamini kazi. Nilidhalilishwa na watanzania wenzangu pale "Dar" Airport kama vile mwizi au mzamiaji wakati wageni wanapita hata hawathubutu kukagua passport zao, then wananiomba nawaachie fedha kidogo. Yaa mijutu pale Airport imekaa kuomba rushwa na kuiba mizigo ya watu. Heri na pale waje wageni.

    ReplyDelete
  66. mimi ni mteja mzuri sana wa hotel ya moven pick, na kama wanataka juajiri mkenya itakuwa bora sana kwa hotel kwa sababu wanakusa sana biashara, nitakupa mfano, ukienda moven pick hasa kule garden (coffee bar ourside) unaweza ukaka sasa nzima na hakuana anayekupa huduma, ukiwa umekaa karibu na mzungu utakuwa na bahati ya kuhudumiwa kwa shida sana, hiyo tu inaonyesha wafanyakazi hao walivyo na ubakuguzi wa susevu wageni wao. sasa ukipata huduma kupata bili ni kazi nyigine tena, utaita mpaka utachoka na anaweza akaja akakupa bili ya mdomo (imagine hiyo ni hotel ya kitalii) baada ya kuleta risiti, sasa hapo ndio wanapoiba uwape kashi ya mdomo ili aweke kwenye mfuko wake. wantanzania inabidi tuamuke sasa tuelewe kwa nini wakenya wana weza??? kwanza hutuna lugha zuri (customer services is very poor

    ReplyDelete
  67. Mmiliki wa Hotel ana uwezo wa kuajiri mtu yoyote anayetaka. Anaweza pia amua kufunga biashara na kufanya hiyo Hotel ikawa Nursing Home and nothing you can do about it.

    Tabia ya sisi wabongo sio tu udokozi na kutaka kuhongwa bali pia very poor customer service kila unapokwenda. Unaenda kuchukua hela Bank utaona tellar anakuzungusha ili umpe rushwa wakati hela ni jasho langu.
    Mnataka kuajiriana kwa kujuana ili mpate urahisi kwenye sick leave wewe kazi yako ni kujifanya tu mgonjwa, Oooh kuna msiba wa mtoto wa dada ya jirani yangu. Kuchelewa kazini kama ni mwanzo wa shifts au during breaks, kuwahi kutoka kabla ya muda, breaks za ajabu ajabu, kuvuta sigara, kuongea kwenye simu, na biashara zozote ukiwa kazini Mkenya atazimaliza.
    Welcome to the World wenzenu ndivyo tunavyoishi. Wakubwa kila siku wanabadilishwa Ukipata Mkenya mbona ingekuwa raha? Performance yako ndiyo inakulinda, uko kazini ontime, tunachelewa kutoka kumalizia chochote ambacho hakikuisha. Kuanzia sasahivi akija mgeni toeni super customer service kuanzia mlangoni anapoingia. Huyo ndiye anayewalipa mishahara yenu.

    ReplyDelete
  68. PIA TATIZO NI RAIS NA HOTUBA YAKE, HIYO NI MATOKEO YAKE

    ReplyDelete
  69. we mdau hapo juu usituletee ishu za china na maziwa ya sumu humu ndani kwani umesikia viwanda vyoote vya chinavinatengeneza maziwa ya sumu? ile ilikuwa ni bahati mbaya tuu inawezatokea popote ulimwenguni na ndo mana kiuchumi wako juu sanaaaaaaa huko kwetu ni kweli huduma nyingi sana ni mbovu kupindukia manesi ndo usiseme wao walitakiwa wawe mapolisi tena wa ffu na sio wauguzi wana kauli chafu na mbaya kwa wagonjwa huko hotelini nako ni hivyohovyo wanafanya wanavyotaka wao hadi msukumwe kama mbuzi mkiletewa wageni mnakuja juu ili iweje wavivu wakubwa bin wezi mtatia akili mwaka huu na bado mtatawaliwa kwa umbumbumbu wenu afadhali basi ingekuwa ni hoteli moja ndo yenye matatizo haya ya udokozi na uvivu wa kijinga hapa ni yote ufisadi ufisadi tuu na majungu na kauli mbofumbofu sisi hapana penda kabisa nendeni tu hapo kwa majirani kenya mahoteli yao ya kitalii utapewa huduma hadi utajihisi we ni mfalme huku kwetu hamjali mnajali mda wa kutoka kazini na mihuduma yenu mibovu hongera saana kwa kuleta wageni waje wawafundishe kazi na utu

    ReplyDelete
  70. Lieni tu na musipobadilika mutajikuta hamna kazi kokote nchini mwenu, wakazi wengine wa Afrika Mashariki watazikamata nafasi zote!It is time to style up the EAC is now free..open to all and sundry!..jobs and workpermits.

    ReplyDelete
  71. KWANZA NAPENDA KUWAPA POLE WATANZANIA WENZANGU AMBAO SIYO WEZI NA WAMEJIKUTA WAKIHESABIWA KWENYE HILO KUNDI LA WEZI.
    KWANZA KABISA NI KWAMBA RAIS WETU MWENYEWE KESHA TAMKA HILO MAANA ANAJUA NA YEYE NI MTANZANIA 100% NA SIYO RAIA MGENI"" SO HAPO NI SISI WATANZANIA KUJIPA MOYO NA KUAMKA ILI KUPIGA WEZI , UKIMUONA MWENZIO KAIBA ,MSTAKI ILI ASHIKWE NA KUPOTEZA KAZI YAKE MARA MOJA. WIZI HAURUHUSIWI MAHALI POPOTE, HASA KAMA VILE MAHOTELINI, HAPO HOTELINI NI MAHALI AMBAPO PANA KUWA NA WAGENI WENGI WA KILA NCHI NA MALI ZAO ZA THAMANI NYINGI KWAO, NA VILE VILE KUIBIWA MALI YAO WAKIWA KWENYE HIYO HOTELI NA KWENYE NCHI YETU, NI AIBU KWA SERIKALI YETU NA PIA KWA HIYO HOTELI NA KUSABABISHA UAMINIFU WA HIYO HOTELI NA MWISHO WAKE KUTOKUWA NA WATEJA NA HOTELI KUFUNGWA NA WOTE KUPOTEZA KAZI ZAO.
    MIMI NAKAA LONDON UK. NA NAFANYA KAZI UK NA MIMI NI MTANZANIA, SASA HEBU FIKIRIA KAMA WAZUNGU WASEMA HATUWAPI KAZI WATU WASIO WANCHI YETU YANI WAINGEREZA AU HATUWAPI KAZI WATU WEUSI?? INGEKUWAJE??? KWA HIYO KUMPA NAFASI YA KAZI MTU YOYOTE SIYO LAZIMA AWE MZALIWA WA HIYO NCHI, NI BORA AWE NA CV NA CV YAKE IWE INA YOTE AMBAYO YANAHITAJIKA NA VILE VILE AWE NA HAKI YA KUFANYA KAZI KATIKA HIYO NCHI" SO NYIE WAFANYAKAZI WA HAPO MOVENPICK WACHENI KULALAMIKA KWA JAMBO MNALO LIJUA NA MNALOLIONA KILA SIKU. WEZI""" NA MIMI MWENYEWE NILIKAA HAPO NA NILIFURAHI SANA KWA KAZI YENU NZURI HASA KWA MAPOKEZI YENU NA VYAKULA"" NYIE WANYENI KAZI KWA UANGALIFU BILA WIZI WA AINA YOYOTE NA MTAJIKUTA HATA MKIONGOZWA NA MZUNGU ASIYE JUA HATA KISWAHILI MTAJIKUTA MNAKAZI NA KURURAHIA MNAPOFANYA KAZI, KWA AJILI YA UAMINIFU WENU""
    GOD BLESS YOU ALL AND HAVE GREAT NEW YEAR"

    ReplyDelete
  72. Ndugu watanzania.
    Sasa wakati umefika tufungueni macho na kuangalia mbali. Hatutaishi milele kwa kutegemea rushwa na kutofanya kazi kwa bidii. Hapa siongelei wahusika wa hoteli ilioyoogelewa kwenye hii blog bali ni sekta zote. Watu wote wanaofanya kazi, ni wachache sana wanaofanya kazi kama inavyotakiwa. Hakuna performance appraisal na kama zipo kwenye kazi zinakuwa handled kiundugu. Kwa dunia ya sasa (globalization) kujuana hakutakuwa na nafasi ila utendaji wa kazi. Jingine ni kwamba inabidi tutambue kwamba kila kampuni inayo funguliwa inakuwa na main objective ambayo ni to make profit and realize growthy. Hakuna mwenye kampuni yeyote atakaye kukubali kuwa na manpower yenye uzembe na tabia za ubabaishaji. Hapo kwetu mtu akiwa competitve anonekana mkuda na mnoko kwasababu tumezoea kutofanya kile kinachotakiwa.

    Vilevile napenda kumkemea mtoa maoni mmoja kwenye forum hii aliye sema kwamba watanzania walionje wasomi wanawaosha wazee wakati wangeweza kufanya kazi za maana. Kwanza kabisa nchi kwa mfano ulaya au marekani, kila mtu anafanya kazi aliyo isomea mradi awe competitive enough. Vileviel watu hawachagui kazi, wewe unasema mwosha wazee, lakini kodi yake indiyo inakuja kusaidia hapo nchini baada yakuwa serikali haijitosherezi kugharamia bajeti. Leo hii unaona kwamba hiyo siyo kazi.Tayari hata wewe umeisha itegemea hiyo senti ya kuosha wazee mavi huko ulaya.
    Mfano mzuri ni kwamba, kunawatanzania wengi ambao wako nje na wanafanya kazi nzuri tu ambapo wazungu hawanakazi. Swala la msingi ni kwamba mtu anafanya kile anachotegemewa kufanya na siyo kupiga porojo na kudokoa dokoa, nikiwa na maana ya stakeholders wote including haki za wateja, mwajiri na raia wasio kuwa na hatia.
    East Africa Union indiyo itatufundisha adabu. Na ninaomba mungu matokeo yake yaanze kuonekana kwenye sekta zote maana wantanzania watajifunza nini maana ya customer care na customer service. Maendeleo yatakuwa maendeleo pale kilamtu atakapoweza kumpeleka mwanawe shule,(hapa sisemi shule nzuri maana shule zote zinatakiwa kuwa nzuri siyo kama tulizo nazo sasa shule nzima walimu wawili)kulala kwenye nyumba bora, kupata maji safi, usafiri, na huduma nzuri za afya kwa kila mtanzania.
    acheni kulalamika fanyeni kazi kwa bidii. Hata mkilalamika haitawezekana kukwepa kutawaliwa na wageni toka Kenya,Uganda nk. mpaka pale mtakapo kubali kufanya kazi kwa bidii.
    Mtanzania ishie nje.

    ReplyDelete
  73. Hehehe, naona jamaa wamejiloga kuweka malalamiko yao blogini!! Hapo Movenpick si ndio mnajulikana kwa buffet za bei poa?? mteja akija kula buffet mnamtoza bei poa halafu hamuiingizi kwenye mahesabu ya siku?? kwa kweli katika hospitality industry tuko nyuma sana na hio idara ya hr ndio inayonyoosha watumishi kwahio mimi kama mtanzania ningeajiri mkenya bila ubishi. unajua sisi wabongo vitu vingi tunachukulia for granted, nimewahi kuingia kibo bar nikaagizia soda nikaambiwa 2500/- na ilipokuja time kuagizia ya pili nikaambiwa 3500/- sasa tofauti ya huyo barman na yule kibaka wa posta mpya ni nini? jana nilikuwa kempinski nikaagiza rum and coke jamaa akanitilia kwenye glasi ya wine, ile kumuambia jamaa ananishangaa nalalamika nini, sasa kama kinywaji kinagarimu 15,000/- kwa glasi moja is it too much for me to ask for a proper glass?? sasa kwakweli details kama hizo mbongo anaona poa tu wakati mtu unaingia 5 star hotel and you expect 5 star service kama mshahara haukutoshi au nyumbani kwako kuna mafuriko mimi hio hainihusu! We need to wake up maana hata kazi ya kuuza maduka town siku hizi zinachukuliwa na wahindi wa india.

    ReplyDelete
  74. o my god sasa tunaelekea kuharibu taifa letu eti anataka kuajiliwa mkenya coze mtanzania ni mwizi oh lord sasa ndiyo mnataka kuharibu kabisa mwelekeo wenyewe wakenya hawafai kabisa rushwa mbele tunaumia na polisi,mahakama.hospitali kwa rushwa sasa tunaletwa wataalamu wenyewe kutoka kenya hawa hawajifichi rushwa kwao ipo wazi na ndiyo iliyochangia kuuwa uchumi wao, sasa upo uwezekano mkubwa kuwa madhara yaliyokuwa mwanzo yanaweza yakawa madogo kuliko hiyo mnalotaka kulifanya, huyo mkenya huyoo akipewa tu mmekwisha, rushwa ipo kwenye damu

    ReplyDelete
  75. tena msilalamike ati kauli ya raisi sijui nini ile kauli ilikuwa fair kabisaa kwani raisi yeye ni mgeni nchini asijue mambo yanayotendeka ndani ya nchi anayoiongoza?? alisema wazi kwa nini afiche??? kila leo mr president yuko huku na kule kutuletea wawekezaji wakija nyinyi mnataka muwalize si ununda huo ni kitu gani?? mdau hapo juu ni kweli pale movenpick hasa pale kibo bar ni majambazi wakubwa tofauti hawavunji nyumba wao kwa kubambika bili ni namba moja tanzania yani kuna siku tulikuwa watano tu bia mbili mbili na wine mbili mbili vile ilikuwa usiku wakazani tumelewaaa wakatupa bili ati ya laki na siti na tano tukaja juu sana wakasema ati wataipunguza hadi elfu tisini yani niliudhika ile siku hadi basi yaani ile bili ilikuwa na whisky brandy yani vitu ambavyo hatukunywa yani kibo bar ni wezi wezi wakubwa wanajua sana kuchomekea bili pale wadau mkienda pale kila ukiagiza ita na bili manake unaweza ukaadhirika hivihivi kwa ajili ya wizi wao wa macho utakuwa na fifty mfukoni utaletewa bili ya laki ndo utakoma mnaletewa huyo HR kutoka kenya manake tabia zenu mbaya zilizoota mizizi zinajulikana mkome kulalamika uongo wezi nyinyi mshaliza saana watu lazima mzibitiwe msiharibu biashara za wenzenu meno ya mwenzio kutafunia mchanga enhee!!! bora mmeleta hii mada huku mmesutwaa mlizani tutatetea ujinga humu wakati mshatuliza?? acheni wezi wa hapa na pale. KIKWETE OYEEEEE!!!!

    ReplyDelete
  76. Hayo ndio madhara ya ten percent

    ReplyDelete
  77. Awe mkenya, mganda au Mnyarwanda. It does not matter. la msingi ni kwamba watu watoe huduma bora. competition ndiyo itatufundisha uwajibikaji na utendaji ulio bora. Hakuna mwekezaji atakayekuja anadai anataka mkenya au mganda, atatafuta mtu anaye faa kufanya kazi na kama hatuwezi kufanya kazi kama inavopaswa sioni sababu ya kulitia hasara kampuni wakati kunamtu anayefaa kufanya kazi bila ubabaishaji wa kibongo. Ni haibu tupu inabidi tubadirike. Nenda kwa majira Rwanza (ni juzi tu wametoka vitnai) uone watu wanavyo wajibika na hakuna upuuzu wa kitu kidogo.
    Tuache lawama tufanye kazi na kuendeleza taifa letu.

    ReplyDelete
  78. yani wee annon ulosemea EAC mbona kweli????

    jamaa jirani asa hawa wa-K wana chuki za kuua mtu tena wanatuchukia kinoma,,,yani mbona itakuwa kuchapana makofi tu umo maofisini na wapi sijui??

    me nilikua nao tena mahali pa kiroho/dini ila huwezi amini jamaa chuki chuki tuu,na wanachonga hao?huwezi amini tulichuniana tu na wako SO SELFISH KINOMA

    ngoja waje bongo,,,tutakomaa nao adi kieleweke
    poleni sana wafanyakazi,na kweli uyo HR mkenya akija hapo ni balaa either +ve au -ve!!! na -ve ndo kibao

    ReplyDelete
  79. NGOJA MTANDIKWE BAKORA TU...! MMEZIDI WABONGO...UVIVU NA WIZI TU..!!NIMEWAAMBIA UJAMAA UMEKWISHA LAKINI INAONYESHA INAINGILIA SIKIO HILI NA KUTOKEA LA PILI...NDO SOKO HURIA HILOOOOOOOO....KUFA HAMFI ILA CHA MOTO MTAKIONA...!!

    ReplyDelete
  80. Mtanzania anayeona kwamba tunafanya vizuri ni yule ambaye hajatembelea mataifa mengine na kuina tofauti. Hatuna kitu ndugu zangu. Tukila nyamachoma na bia na kuendesha saloon basi tumemaliza. Hivi ni sekta gani ambayo mtu anaweza kusema tunategemea kutuletea economic development bila reform ya hali ya juu?? madini? Utalii? misitu? kilimo? viwanda? wewe niambie. Hakuna kitu. Lasilimali tunazo kibao ila panning hakuna na vilevile hakuna accountability. Nasikitikia vizazi vyetu huko mbele ndio wataumia kufanya kazi ya ziada wakati sis tupo sasa hivi tunapiga porojo tu.
    Mimi nawatakia kila la kheri. Tukae tunaelewa kwamba mambo nimabaya. (ukiwa kwenye chumba yenye upungufu wa hewa huwezi kujua kwamba kuna upungufu wa hewa mpaka mtu anayetoka nje kwenye hewa safi na yakutosha ndiye atakaye kustua kwamba hewa haitoshi)
    mwenzenu RB.

    ReplyDelete
  81. hii topic ni interesting, mnaonaje tukianza kuwa wazi bila kukaa anonymous? Maana sioni kwanini tujifiche kama twaongea ukweli ni hoja tu.

    ReplyDelete
  82. Tuongee ukweli wakenya ni wanafiki kinoma, maswala ya kazi hata ufanye mpaka uvunjike mgongo watakuundia majungu tu. Na kwakuwa wakija huku wanakuwa katika ubosi bosi fulani wa saizi ya kati watakufanyia hila tu. Siko specific kwa issue ya Movenpick niko general to the topic.

    ReplyDelete
  83. Watanzania,
    Nadhani la msingi ni kuwa na uongozi mzuri kwenye sector zote swala la kuwa mkenya au Mnyarwanda siyo muhimu kwa sasa. Ujamaa umeisha jamani. La kuchekesha ni pale juu mwanzoni mwa Blog hii jamaa wa Movenpick anadai kwamba wakimweka mkenya hatakuwa na mchezo. Kwa kauli hii inaonyesha wazi kwamba watanzania wanamchezo kazini hahaha.
    Tanzania system nzima imharibika. Mfano ni shirika la posta. Huwezi kutuma kifurushi kwa njia ya kawaida kikafika. Na ukukituma kwa register bado wanadokoadokoa. Jama hatuwezi kukaa tunaficha ukweli.
    HII NI SAWA NA KUFUNIKA MOTO KWA NYASI UKIDHANIA UTAUZIMA.
    rB.

    ReplyDelete
  84. Ebwana, kuna ndugu yetu anatambilika kwa nina la Msemakweli, alitoa maoni yafuatayo hapo hawali kwenye sakata hili.

    namnukuru:-
    Watanzania wavivu na wanapenda kulalamika tu. Hadi Raisi, Mkapa na sasa Kikwete wamesema ukweli watanzania ni wavivu na wanapenda mteremko. Sasa kama wewe sio MWIZi una wasi wasi gani hata wakiajiri mtu toka sayari ya saba au mwezini? Fanya kazi yako usianze ooh wanasema sisi wezi etc? Kama mtu sio mwizi huwezi kuwa na wasiwasi kwani upo kwenye mikono safi

    Nadhani hii ni point nzito na inatosha sana kutuelewesha watanzania kwa ujumla.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...