Steven Charles Kanumba the Great
http://kanumbathegreat.blogspot.com/

Katika siku kama ya leo,miaka 26 iliyopita pale mkoani Shinyanga, alizaliwa kijana na kupewa jina la Steven. Hivi leo ni maarufu kama Steven Kanumba au kama mwenyewe anavyojiita wakati mwingine “The Great”. Kwa maana hiyo,leo ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Steven Charles Kanumba.
Happy Birthday!

Kwa mtu yeyote ambaye anafuatilia maendeleo ya tasnia ya filamu nchini Tanzania,bila shaka atakubaliana na mimi nikisema kwamba Kanumba ni miongoni mwa waigizaji wa filamu(Film Actors) ambao ni maarufu zaidi nchini Tanzania. Leo hii ni vigumu kuiongelea sanaa ya filamu nchini bila kumhusisha Kanumba kwa njia moja ama nyingine.

Kwa hivyo,haishangazi sana kuona kwamba,katika mwaka uliopita jina lake lilikuwa takribani la kudumu katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya mtandaoni,mitaani nk. Bila shaka unakumbuka jinsi
habari ya Kiingereza Vs Kiswahili ilivyozua mjadala wa kitaifa. Kila mtu akasema lake.

Baada ya mambo kama yale,mijadala kama ile,watu hupenda kujua what next? bongocelebrity.com ilimsaka Steven Kanumba ili kujua machache kuhusu mipango yake ya mwaka huu
Kupata mahijoano yake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. ankal unaweza kumzaa kanumba bila wasi wasi.

    ReplyDelete
  2. Naomba kuuliza hivi Kanumba ni Muislam au Mkristo au hana dini.Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  3. Happy Birthday to You Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania! May you See many many more!

    ReplyDelete
  4. Steven Kanumba, I wish you a Very Happy Birthday! God Bless You!

    ReplyDelete
  5. happy birthday kanuba wewe usiwajali binadamu kusema ndio zao kaza buti upo juu karibu unashika mwezi waaaaaaaa

    ReplyDelete
  6. Grown up, well done. Other guys hide their ages.

    ReplyDelete
  7. "HAPPY BIRTHDAY STEVE KANUMBA"

    ...usiangalie nyuma daima songa mbele na kipaji chako cha kuzaliwa kipaji hicho ulichopewa na Mungu binadamu hawezi kukiondoa kwa maovu ya chuki,fitna na wivu pekee....

    ...sherehekea siku yako ya kuzaliwa na wale wanaosonga mbele na wewe katika kuleta maendeleo ya watanzania wote,kazi yako tunaiona na inastahiri sifa zote....

    "NAKUTAKIA KILA LA KHERI"
    Mickey Jones Amos
    Denmark

    ReplyDelete
  8. SitakenchekeJanuary 09, 2010

    Michuzi kwa uchokozi tuu hujambo, unataka kuanzisha moto halafu wewe unakaa pembeni. Haya, HaPpi Bethidei ya kuzaliwa mdau Kunumba!

    ReplyDelete
  9. Mmmmmmh Mzee wa burudani.

    ReplyDelete
  10. Happy Birth Day Alfred - what your name again in ... the other movie, ...can't remember the title now - only that you really bullied that innocent wife of yours for not conceiving. Could somebody remind me please. Never do that again.

    ...and talking of bullying, just to let you know that some afendis were bullying me when you were born...

    ReplyDelete
  11. so what???

    ReplyDelete
  12. Tatizo ni hicho kiinglishi

    ReplyDelete
  13. Kanumba sio mbovu sana kwa ngeli
    The guy is good-trying hard especially kwa international interview
    Am proud sana na mtu huyu-Tupunguze matusi against him.

    Watch youtube clips Kanumba Sporah Show intervies

    http://www.youtube.com/watch?v=Iasicyrx5no&feature=related

    ReplyDelete
  14. Happy birthday Kanumba,

    Watu wakikutukana au kukusengenya vibayya, tusi moja wewe songa mbele kumi, utakuwa umewaacha nyuma yako hatua tisa. Na wala usifikiri hayo unafanyiwa wewe tu, binadamu ndivyo tulivyo hatupendi kuona mtu anaendelea, kwa kweli tuliokuona ukianza kuigiza kwenye kipindi cha Maisha, ukiwa mdogo leo hii umeendeleza kipaji chako mpaka kufikia hapo ulipo tunakupa hongera!

    Chukua constructive critism fanyia kazi ili uzidi kuimarika, matusi na rubbish zote tupa kwenye rubbish bin! Hiyo ndio zawadi yangu ya birthday kwako.

    Mswahili

    ReplyDelete
  15. kanumba movie yako ya saturday morning ni nzuri sana umejitahidi sana kaka afya njema dogo

    ReplyDelete
  16. Aaawwww!!! Happy B-day handsome.

    ReplyDelete
  17. namjua vizuri kanumba nimekua nae nimesoma nae kule shy ni jirani yetu, ni age mate wangu, umri wake sio 26 ni 34!! muulizeni vizuri

    ReplyDelete
  18. Wewe unaesema unamjua vizuri Kanumba na umri wake ni miaka 34 kweli unanishangaza. Mimi nina miaka 40 na nikiwa tayari nina watoto nimemuona Kanumba anaanza kuigiza kwenye kipindi cha maisha, akiwa na machunusi kibao usoni, namaanisha akiwa teenager anayeanza kubalehe, very young, nakumbuka mchezo wake wa kuigiza uliompa umaarufu ni ule alioigiza kama mtoto wa mzee Kipara aliyemposa mtoto wa Mhogo Mchungu Dida, wakati huko kijijini kwao familia hizi mbili zilikuwa na bifu la nguvu.

    Hata hivyo akiwa 26 au 34 inahusu nini? Wakati age is nothing but a number? Wivu unakusumbua eti tumekuwa wote so what ndio keshakuacha hivyo mwenzio yuko level nyingine.

    ReplyDelete
  19. Kanumba wakatae, wakubali uko juu mno...nyota yako yang'ara ...nakufananisha na yesu alipigwa mawe na walimtemea mate...nataka ujue mungu anamakusudi yake lakini wanakuchongea barabara utazijidi kuwa juu watu wachache hawapendi kuona unapata nawanadharau moview zakibongo kwhy wakiona mafanikio yenu wanatafuta mawe namisumari... Uko juu huu mwaka mpya naamini umejiandaa vyakutosha muweke mungu mbele kwn wasanii hampendani pia wapo wanaochangia kupanda mbegu mbaya juu yako kukuangusha wewe si the great tu more than the great...kikulacho ki....

    ReplyDelete
  20. kanumba tafuta A.K.A nyengine si THE GREAT ni mungu pekee ndio mwenye sifa hio,usivimbe kichwa kaka si denzel washington wala will smith wala mastaa wengi wenye akili zao timamu kujipachika jina hilo okeeee?ijekua wewe kaka?no the great is only ALLAH,GOD,MUNGU,JAH NK HAYO NI MAJINA YAKE TU MKUBWA WA WAKUBWA....MDAU,GREECE

    ReplyDelete
  21. happy bday steven,
    ulieuliza kanumba ni mkristo anaabudu AICT

    ReplyDelete
  22. mhh watu kwa kuchonga tuu ndio kazi yao kijana wa watu anajitaidi lakini pia munamtowa makosa na huyu anayesema machunusi kibao ni roho mbaya na wivu ,kanumba mimi nakufagilia hile mbaya wewe songa mbele jiite jina lolote unalopenda na kila mtu ana haki ya kujiita anavyopenda so what unayelalamika kwani umekatazwa wewe kujipachika jina ,lugha haijalishi yeye kujuwa englisg sio issue kwani wewe ulizaliwa na kukijuwa mwaya ukija UK nitafute weka kwenye blong safari yako nitakupa number ya simu watoto wangu wanakufagilia kweli waaaaaaa

    ReplyDelete
  23. Hivi hamchoki? Kumpiga madongo mtoto wamwenzenu? Nani mkamilifu kwakila jambo anyooshe kidole tumuone. Kanumba, kanumba, kanumba, kanumba..... Mtoto wawatu asipumue? Imekuwa kosa kuwa maarufu? Kwn wasanii wangapi wanajua kiinglish? Nini wasanii wewe je unaeponda unajua au unaongea tu? Nyambaf....

    ReplyDelete
  24. Wewe unaepinga age ya kanumba unadhani umri ndio kigezo cha mafanikio? Inakusaidia nini? Pia kusoma nae haina maana moja kwa moja kuwa mlikuwa mnalingana kiumri. Hata hivyo watu huwa hatusomi tu comments tunafikiri pia. Mimi mwenyewe nina 34 na naelewa huyo hawezi kuwa agemate wangu maana nimeanza kumwona akiigiza akiwa mdogo zaidi ya mimi niliekuwa naangalia tamthilia zile.

    ReplyDelete
  25. Happy Birthday Kanumba though you don't look 26.

    ReplyDelete
  26. me na wengine wetu wengi tu huwa sipendi picha za kiswahili maana nyingi hazina mtiririko na kuiga kwingi

    ila siku moja niliwekewa movie yako ile uloigiza na wema sepetu..khaaa sikuamini kabisa
    toka siku iyo natafutaga movies zako basiiiii

    hongera kaka kwa kuinua soko la movie na kufanya wabongo tupende chetu
    happy bilated b'day dogo

    ReplyDelete
  27. Ni lini sisi binadamu tutakubaliana na kuiona kazi ya mtu inapendeza? Nasema hivyo kwa sababu wivu ni mwingi bila kumpa mtu changamoto ya alichokifanya. Ina maana wewe pia hupendi wala hutaki maendeleo???? Sababu wengi wanaongeeea visivyo ili mradi achafue tu jina lako. Mungu hapendi hivyo na ndio maana wewe na roho yako mbaya utaadhibiwa na huoni maendeleo yako. Fanyeni mema na yatabarikiwa acheni sana kuchonga. Kanumba unatupa sifa endelea baba don't mind. Give Up.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...