Ankal salamaleko...
Mie bwana nina kadukuduku kadogo maana hapa Kigoma kuna wakandarasi wanaojenga barabara zetu za hapa mjini mojawapo ni barabara iendayo katonga ina jengwa na mkandarasi fulani chini ya usimamizi mzito wa TANROADS- Kigoma lakini cha ajabu ni kwamba haina cha mfereji wa maji ya mvua wala daraja (Storm water drainage system) ili kupitisha maji kutoka pande mbili za barabara hii na ukizingatia ni masika na kuna mvua za el-nino.
Hofu yetu kwamba wamepandisha tuta la barabara na kukosekana kwa daraja au karavati kutasababisha yumba za upande wakushoto( Ambazo nyingi zao ni Kambi ya Polisi) mwa picha hiyo hapo juu kukumbwa na mafuriko
Nawakilisha
Mdau Kigoma

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Barabara bila ya mfumo mahususi wa maji mvua (stormwater system) ni kawaida Tanzania. Hawa TANROADS, Wizara ya Ujenzi, wahandisi ujenzi, washauri ujenzi, wakandarasi na wadau wengine hawatilii maanani kabisa. Barabara nyingi nchini kwetu hazidumu kwasababu ya kukosa mfumo mzuri wa kuondoa maji ya mvua. Mhandisi yoyote yule wa ujenzi anajua kuwa 'base course' ikinywea maji, rami inabomoka.......cha ajabu hakuna cha maana kinachofanyika wakati wakusanifu na kujenga hizi njia za magari.
    swali ni kwamba nani alaumiwe na nani arekebishe hii tabia. Je tunahitaji wazungu watusaidie kusanifu mifumo ya maji mvua kwenye barabara zetu?

    WADAU INABIDI TUWAJIBIKE.

    mdau mhandisi chipukizi

    ReplyDelete
  2. Mimi siyo mtaalamu wa mambo ya ujenzi, lakini "common sense" inaniambia muhandisi huyu aliyehandisi barabara bila kuzingatia jinsi ya mifumo kuondoa maji ni muhandisi mpumbavu. Huu ni mfano mmojawapo unaoonyesha kwanini hatuendelei.

    Hawa ndiyo wasomi wetu na wasomi hawahawa ndiyo wanaosema
    "yessi..., of koz; how ken yu develop without english? angalia kenya wenzetu, ol dhea edukeshen sistim iz in english...., we masti chenji it in english ili kusaidia soko letu la ajira".

    ReplyDelete
  3. Mkuu Michuzi mimi ni mhandisi na naomba kabla wadau hawaja lalamikia sisi wahandisi watuulize ni kiasi gani cha fedha tumepewa kwa ajiri ya barabara hii na je pesa waliyotoa wanasiasa (wabunge na waziri) inalingana na tuliyoomba kwa ajiri ya barabara husika?

    Kama jibu ni pesa imetolewa kidogo je tuikatae irudishwe hazina? au tujenge kulingana na pesa iliyotolewa??

    ReplyDelete
  4. Minadhani ninaweza kukubaliana kiasi Fulani na muhandisi huyo. Ni kweli kwamba viongozi na wanasiasa wanakwamisha jitihada nyingi za maendeleo katika kila idara za serikali. Ni wepesi kutetea masilahi yao binafsi nakusahu nafasi ya utumishi wao kwa uma na watumishi walioko chini yao. Sidhani kama malipo ya wabunge na mawaziri yamekwisha cheleweshwa kama ilivyo kwa watumishi wengine. Viongozi hao, mawaziri na wabunge malengo yao ni kuichuma serilikali tu. Kwanza hawataki kutambua na kutekeleza mawazo ya wataalamu. Wana kwaida ya kuwasahau wataalmu tulionao katika swala zima la kuleta maendeleo na kutopitisha makadirio ya matumizi ya mahitaji ya miradi. Kwa sababu ya utaalamu wa wizi waliona viongozi watadai hakuna pesa za miradi husika ili waweze kupata pesa nyingi za kuiba. Kama kweli nchi haina pesa,hizo za ufisadi zimetoka wapi. Viongozi,mawaziri na wabunge acheni kuwadangaya watanzania, mnayoyafanya yanatambulika kwa matendo yenu wenyewe. Dawa ni moja, kuwatoa madarakani viongozi walio kaa madarakani muda mrefu ili wasiendelee kuharibu.

    Na nyie wahandisi na mainjinia, hiyo isiwe kisingizio kutengeneza barabara bila matoleo ni kutaka maji yakusaidie kubomoa barabara mnazo tengeneza. Poleni na changa moto mnazopata toka wanasiasa na viongozi.

    ReplyDelete
  5. MDAU SI HATA UMSALIMIE UNLCLE KI KABILA CHENU KULIKO HIVI? SALAMALEKO NDIYO NINI? SEMA ASSALAM ALEYKUM SIYO SALAMALEKO INA KUJA MAANA NYINGINE ANGALIA USIJE UKATUKANA BURE, USILOLIJUWA ULIZA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...