Ubalozi wa Tanzania nchini UAE ulifungua kitabu cha maombolezo ya kifo cha Simba wa Vita Mhe. Rashidi Mfaume Kawawa tarehe 5 na 6 Januari, 2010, Ubalozini, Abu Dhabi. Waliokuja kutia saini kitabu hicho ni pamoja na Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa UAE, Mabalozi, wawakilishi wa Mabalozi na wadau wengine. Pichani juu mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje nchini UAE, Balozi Saeed Hamdan Al Naqbi, akitia saini kitabu cha maombolezo huku Kaimu Balozi, Bw. Athumani W. Beleko na Afisa Itifaki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje Bw. Zaigal wakishuhudia.
Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje akimpa mkono wa pole Kaimu Balozi, Bw. Athumani W. Beleko baada ya kusaini kitabu

Balozi wa Nigeria, Mhe. Bashir Yoguda, akitia saini kitabu cha maombolezo.
Balozi wa South Africa, Mhe. Abba Omar, akitia saini kitabu cha maombolezo huku Kaimu Balozi, Bw. Athumani Beleko akishuhudia.
Balozi wa Senegal, Mhe. Abdourahmme Diof, akitia saini kitabu cha maombolezo

Mwakilishi wa Balozi wa Morocco akitia saini kitabu cha maombolezo
Mwakilishi wa Balozi wa Russian Federation akitia saini kitabu cha maombolezo huku Afisa wa Ubalozi Bw. Setebe akishuhudia








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...