Jumuiya ya Watanzania Uingereza inasikitika kutangaza kifo cha Dada Sophia Hayumu (Mke wa Gerald Lusingu ) kilichotokea leo mchana Berskshire.
Msiba upo :
15 Whitenights
Reading RG6 7BY
Utaratibu wa kusafirisha mwili wa marehemu unaandaliwa chini ya Mwenyekiti wa kamati ya kusafirisha mwili, Sheikh Ali Sungura.

Tanzania Association inaomba watanzania kutoa michango kwa ajili ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda Tanzania kwa ajili ya mazishi.

Tafadhali tuma mchango wako kwa mshika fedha wa kamati :
Ndugu M Upetu
Sort Code:207106
Account:80585114
Barclays Bank


Namba ya M Upetu:07501083328


Kwa maelezo zaidi wasiliana na Sheikh Sungura:07960319156

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Poleni sana ndugu zangu hapo Reading. Pia nampa pole mfiwa mungu ampe nguvu na uvumilivu.

    ReplyDelete
  2. Pole sana kaka Gerald, ni mipango ya Mungu, tupo pamoja kaka katika kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu na marafiki kwa pengo hili kubwa. Mungu amlaze mahali pema.

    ReplyDelete
  4. Inna lillah wa inna ilaihi raajiuun. Tunamwomba Allah awape subra wafiwa...

    ReplyDelete
  5. POLE SANA KAKA GERALD NA FAMILIA KWA MSIBA HUO MKUBWA ULIOWAPATA, HATUNA JINSI KWANI YOTE NI MIPANGO YA M'MUNGU, KWANI YEYE NDIYE MPANGAJI WA YOTE, CHA KUFANYA NI KUMUOMBEA DADA YETU, M'MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, MBELE YAKE NYUMA YETU, KAKA GERALD M'MUNGU AKUPE MOYO WA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU. POLE SANA KAKA GERALD. MUNGU ATAKUSAIDIA. USIFE MOYO TUPO PAMOJA NAWE. MDAU N.S

    ReplyDelete
  6. rest in peace sophy.. mungu awape nguvu familia ya marehemu.. na si pia tutawaweka ktk dua zetu za kila siku.AMIN..inna lillah wainna illah raj'iuuun.

    ReplyDelete
  7. Roho ya marehemu Sophy na marehemu wote waliotutangulia wapate rehema kwa Mungu wapumzike kwa amani Amen.

    ReplyDelete
  8. pole mpendwa sophy m/mungu aipumzishe roho yako pema peponi amen.tulikupenda na tutazidi kukupenda daima upumzike kwa amani amen.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...