Misaada yetu ya kwanza tuliyokusanya siku hizi mbili itakabidhiwa kesho (Ijumaa) Kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu cha Tanzania Mstahiki Meya wa Jiji la Dar-es-Salaam Alhaji Adam Kimbisa leo Ijumaa majira ya saa kumi hivi (kama muda haujabadilika) ofisini kwake Karimjee Hall jijini Dar.

Tunatumaini hii itakuwa ni hamasa ya kuwahakikishia watanzania wenzetu kwamba katika hili tuko makini na tunataka kuonesha kuwa tunaweza.

Taarifa ambazo bado zinaingia zinaonesha hali bado haijatulia hasa huko Kilosa kwani mto unazidi kufurika na watu wengi zaidi wanazidi kuathirika na hivyo misaada yetu inahitajika zaidi leo hii.

Kwa wale walioko Marekani unaweza kuchangia kupitia
Paypal ya mtandao wa mwanakijiji.com (fedha zilizochangwa siku hizi mbili, tayari zimeshatumwa Tanzania ziunganishwe na misaada mingine). Kwenye mtandao huo unaweza kutumia kadi za Kibenki kwa njia salama kabisa (secure transaction).

Huenda mmojawapo wa mawaziri atakuwepo kuwasilisha michango yetu hii kwa Red Cross akionesha mshikamano na umoja.
Join now; be part of change,
don't wait for change to happen, you'll wait unchanged!

Taarifa zaidi baadaye:

KUCHANGIA MAAFA YA HAITI NA MAFURIKO YA TANZANIA:

Kama uko Marekani.. unaweza kusaidia waathirika wa Tetemeko la ardhi Haiti:

Text "Haiti" kwenda namba "90999" to put a 10 dollar donation on the phone that will go to the Red Cross

Kama uko Tanzania .. unaweza kuchangia waathirika wa mafuriko wa Tanzania:

Text "TPN" kwenda namba 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Na utachangia Shs 150.00 kwa siku thelathini; sawa na 4500Ths!
Hii ni sawa na kuchangia dola 3.46 kwa mwezi!!

the amount raised will be contributed to the Tanzanian Red Cross Society

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Uncle Michu, naungana na ulimwengu mzima kuwapa pole wenzetu wa Haiti kwa msiba huu mkubwa, lakini tukiwa tunahamasisha kuwachangia hawa wenzetu wa Dunia ya Tatu kama sisi, pia tukumbuke kuna familia lukuki za Kitanzania pia hazina makazi baada ya kukumbwa na NATURAL DISASTER pia mafuriko. mchango huu wa Watanzania umekuwa ni mdogo kiasi kwamba nimeatamani kulia baada ya kupiga hesabu kuwa kwa mwezi mzima, mchango wangu utakuwa ni sh 4500/- tu za Kitanzania, baada ya kukatwa kwenye simu yangu. so tuwakumbuke na hao pia jamani.

    ReplyDelete
  2. Huyo msajili anayechukua hizo 250 za uasijili si angezisamehe tu ili hela yote iende huko. Macredit company yote hapa leo yametangaza kuwa kama unachangia hela kwenda Haiti no fees.

    Na hao wangeiga mfano huo pia. Sio mfano wa kusaidia tuwe nao wananchi lakini makampuni makubwa ndio yatajirike hapo...Nao wafuate uzalendo.

    ReplyDelete
  3. poleni sana watu wa haiti na watanzania wote waliokumbwa na mafuriko. but nina swali moja hivi tanzania tuna ubalozi nchini haiti. na kama upo je upo kwenye hali gani mpaka sasa au kuna watanzania wanaoishi haiti nazani hili serikali inabidi wafuatilie kwa makini kama kuna wanatanzania wanaoishi haiti ili kujua kama wapo hai

    mdau
    asiependa anayechukia ufisadi

    ReplyDelete
  4. What happened in HAITI is a disaster on a Biblical scale. These people need help, help now and for long time to come, I am glad America is taking a lead on this. NA HUYO KIMBISA VYEO VYOTE VIWILI ANASHIKILIA YEYE TU SI AACHIE WENGINE KIMOJA, TUANCHE HII TABIA YA KUKUMBATIA VYEO VINGI KWANI INAJENGA TABIA YA KUKOSA WATU WAZOEFU KATIKA NYANJA MBALIMBALI KAMA MTU MMOJA ANASHIKILIA VITU VYOTE PEKEE, SASA WENGINE WATAPATA WAPI UZOEFU

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...