Rais Jacob Zuma akiwa na mai waifu zake wote watatu, mpya ni wa pili shoto

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 73 mpaka sasa

  1. ukichukulia alishawai kumbaka mwanamke ambaye inasemekana alikuwa na ukimwi na yeye kujietea kuwa alioga punde tu na maji ya vitunguu swaumu....ktk nch ambayo inaongoza kwa ukimwi afrika,sidhani km yeye ni mfano au anaweza kupigana vita na hilo gonjwa....atawaeleza nini watu

    ReplyDelete
  2. Michuzi si ana wake watano?? Wengine wawili wapo wapi?

    ReplyDelete
  3. Ankal vipi mbona umekomaa na Zuma? samahani wakina Hawa, lakini ukweli ni kwamba kama si baadhi ya dini kuweka ukomo wa kuoa na hali halisi ya maisha, basi mwanamume (kina Adamu)wanastahili kuoa wanawake wengi na mwanamke haruhusiwi kwani kwa mwaka mwanamke huzaa mara moja tu,je mwanamume kwa mwaka anauwezo wa kuzalisha mara ngapi?wastani kama kila tendo humpa mimba mwanamke na kama mwanamume akishiriki mara tatu basi kwa mwaka huyu mwanamume anaweza kuzalisha wanawake 1095! Hali hiyo ingeachwa iendelee bila dinina hali ya maisha kuingilia kati na hali ingekuaje sijui!

    ReplyDelete
  4. Hongera!!! Huo ndio udume.Angalia kinamama nyuso zilivyofurahi.Mzee Zuma kweli unawakilisha

    ReplyDelete
  5. haya sasa kama raisi atafanya kazi saa ngapi? na how wanawake atawashugulika saa ngapi?? ndio maana waafrika tupo nyuma kwa sababu ya mambo ya kishamba kama haya, kweli zuma anaona fahari kuwa na hawa wanawake wote???? poor those women too i think is because of money no love there
    true love is for two people only when it come to three people means to crowded

    ReplyDelete
  6. Mimi ni mwanamke lakini naona ni bora mwanamke aolewe na mumeo awe mke mwenza kuliko hawara, yaani the other woman. Maana huyo hawara hana kazi yoyote yeye ni kustarehe tu na mumeo wakati akiwa mke mwenzio anabeba majukumu ya mke yampasayo kumfanyia mume na wewe unapumzika. Akiumwa unajua utamuuguza, kuliko hawara, mumeo akiumwa wewe ndio wa kuuguza yeye anasumbiri apone akale mahanjumati!

    Kulikoni mwanaume anayetoka nje kama paka shume akirudi anafuta michuzi kwenye masharubu yake (samahani Mr. Michuzi namaanisha soups sio michuzi wewe). Maana hata hujui katoka kulala na nani? Yeye linajiendea tu lakini mkiwa mnajuana mko wako wenza unaweza hata kupiga simu kwa mke mwenzio ukamuuliza "hivi huyu mwehu yuko kwako huko au? Maana naona mpaka saa hizi sijamuona mitaa ya huku na leo alikuwa ana zamu ya kuja ya huku" Mnabana kisawasawa, na yeye anakosa muda wa kuruka ruka nje hovyo kama kishada kisichokuwa na mwenyewe!

    Mswahili!

    ReplyDelete
  7. Michu umemkomalia jamaa kinoma. Ni wivu tu au vipi?
    Haya mambo ya mke mmoja mume mmoja tumeiga tu. Mila na desturi zetu kidume lazima uwe na wake kibao. The Zumas wanastahili sifa kwa kutobabaishwa na utamaduni wa kigeni ambao unafanya watu wanaoa mke mmoja na kuibiaibia.

    ReplyDelete
  8. Watoto ni ni neema.Afrika tupo nyuma kwasbabu continenti halina watu.

    Makontinenti yenye watu ndio yenye neema ana elimu.

    Mzee Zuma wakilisha....

    ReplyDelete
  9. stop nyumba ndogoz!January 06, 2010

    ingawa sikubaliani na ndoa za wengi lakini pia wanaume wa siku hizi hata kama amekuoa wewe nje ana nyumba ndogo za kumwaga na kama ana pesa ndo kabisa nyumba ndogo ndo atafaidi kuliko nyumba kubwa, atajengewa nyumba atasafiri na mzee ukoo wake utatunzwa, na wewe mke utabaki huna cha kufanya, so really hamna tofauti. Na mbaya zaidi tumeshuhudia wanaume wakileta gonjwa ndani ya nyumba na nyumba ndogo akisikia tu jamaa mgonjwa bin hoi ndo kwanza anaingia mtini na akiambiwa ndo kwanza atamkana na kusema wala mi hata sikua na uhusiano nae! @ the same time nyumba kubwa ndo shuguli ya kuuguza inaanza mpaka kifo bila msaada wa nyumba ndogo, saa hizo nyumba ndogo keshahama mji, analetewa tu habari na mashoga kwamba jamaa kalazwa tena, nae anazidi kumkana, then jamaa anaachia ngazi na mama anaachwa hana cha zaidi ya kusubiri zamu yake huku akijua maskini watoto watabaki yatima siku si nyingi sababu ya starehe za baba yao, na mbaya juu ya mbaya, muda wote baba anauguzwa ,mke haruhusiwi hata kumhoji mume kwa maafa aliyoleta sana sana ndugu wa mume wanajiandaa kuja kurithi magari na nyumba. Iv seen this first hand and is really sad and upsetting! and is a very common trend, a lot of people can tell this same story!
    labda ingefaa akina mama waungane waamue kabisa leta ugonjwa ukianza tu kuugua unahama humu ndani nenda kaugulie nyumba ndogo labda itasaidia kina baba kufikiria mara 2 kabla hawajafungua zipu.
    inaudhi sana. mfyuu(msonyo)

    ReplyDelete
  10. Huu ndio mfano gani! Kiongozi wa nchi yenye Ukimwi kuliko zote duniani ana wake sita. Mtu wa kawaida mtaani hivi anaonaje hii? Na jamaa hapo juu wanasifia tu, HEBU JAMANI FIKIRIENI KWANZA KABLA YA KUROPOKA NA KUSIFIA.
    Afrika ni afrika tu, tutakaa hivi hivi, watu mnaona maendeleo kuwa na wake wengi. Udume ni kumuhudumia mke wako,kuwalea na kusomesha watoto wako ili nao wafanikiwe na maisha yao. Yaani wakati mwingine inaonyesha jinsi gani sisi Waafrika tupo nyuma DAAAH! WE ACHA TU.

    ReplyDelete
  11. inasikitisha sana.... hata alivyosimama na hao akina mama haina hata chembe ya mvuto, hapo tamaa mbele mapenzi nyuma, by the way hata hao wanawake vichwani mwao wanaamini nani anapendwa na huyo jamaa???? ni kweli kabisa kinachowabakisha hapo ni pesa tu na hakuna kingine, wananchi wanatoa kodi zao halafu raisi unatumia kupata wanawake wengi... duh!!!! kwani jamaa siyo hundsome sana kiasi cha kuwadatisha hao wanawake... it is just Rubish

    ReplyDelete
  12. Mwana upo na vakesheni ya muda huko bondeni.

    Angalia ujuba Raisi mademu wachovu. Hawanipi mimi niwape funzo la kuibua mademu wa maana??

    ReplyDelete
  13. UJINGA WA MWAFRIKA!!

    ReplyDelete
  14. Bora kaburu alichelewa kuwapa uhuru hawa jamaa wa bondeni, maana angewapa uhuru mapema mpaka sasa wanawake wa kuoa wangekua wameisha maana kila mtu angekusanya kila kukicha.

    ReplyDelete
  15. Huyo dada hapo juu anayejiita mswahili ndiokatoa ujumbe wa maana maana nafikiri anajua kukabana na haya mabwana ya siku hizi yanayoruka kama kishada alivyojisemea mwenyewe dada hongera kwa ujumbe naona wew unatokea uswaz kweli i mean "MTONI KWA MZIZI ALI" AU unatokea kule MWEMBE YANGA

    ReplyDelete
  16. Elimu ni kitu kizuri sana, sasa hawa wasouth walinyimwa elimu na makaburu sasa haya ndio matokeo ya kukosa elimu. Hapa tusubiri mpaka hiki kizazi cha kina Zuma kiishe na umbumbumbu wao ndio tuanze kuona watu wenye busara zao,

    ReplyDelete
  17. Why don't we just respect peoples' culture, choices and lifestyles. I like the pose and it seems they have been carefully arranged (left to right) in order of weariness, exhaustion and depreciation...

    ReplyDelete
  18. Waislamu wana raha sana.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  19. Huyu jamaa kweli ana taste ya ajabu..mbona wote wamefanana tu? Ukiamua kuoa wanawake wengi wengine wanatakiwa wawe warefu, wembamba, wafupi mchanganyiko sasa wote ni kitu kimoja tofauti iko wapi?-Mdau-USA

    ReplyDelete
  20. WEWE ANON WA: Tarehe Tue Jan 05, 11:22:00 PM, Mtoa Maoni: Anonymous

    Wake zake wawili walishakufa. Haijulikani kama ilikuwa ni miwaya au ni gonjwa zipi ziliwapeleka kuzimu. Lakini kwa kweli: kiongozi kama huyu wa nchi kubwa Africa na duniana, hatakiwi kuonyesha mfano mbaya namna hii. Pamoja na kwamba inasaidia sana katika familia kuwa na wake wengi, lakini mimi binafsi sipendelei tabia hii. Ni mbaya sana na IKOME.
    Nawasilisha

    ReplyDelete
  21. Ovyo! wanaume wa kiafrika hakuna kingine wanachofikiria! Kuongeza wake badala ya maendeleo.

    ReplyDelete
  22. wee anony wa jan 06,12:18 unajua maana ya mke na hawaraa? je unajua tofauti zake? basi kwa kifupi ni hivi mke ataendelea kuwa mke na hawara ataendelea kuwa hawara hata mume akioa wake 5 hawara ataendelea kuwepo na humo ndani ya ndoa watagombania kile ambacho mke mmoja angepata huku hawara akila kama kawa share yake,naona umenielewa vizuri sasa.

    ReplyDelete
  23. raisi ZUMA soma biblia agano la kale kuwa kwa asili MWENYEZI MUNGU aliumba ADAMU na mke mmoja HAWA,swali je Mungu anabadilika?

    ReplyDelete
  24. zuma hauna tofauti na waafrika wengine mtu akipata pesa anafikiria kuongeza second wife

    ReplyDelete
  25. hata mfalme sulemani alioa wake wengi ila mwisho alikiri kuwa huo ni ubatili tu

    ReplyDelete
  26. zuma ni mkwale tu

    ReplyDelete
  27. raisi gani anawaza kuoa tu badala ya kujenga uchumi ndio maana afrika kusini maisha ni magumu kwa raia wake hadi wanaanza kufukuza na kuua wageni hata walio wasaidia wakati wa makaburu

    ReplyDelete
  28. mtoa maoni unayefikiria kuoa ili kuongeza watu nakupa pole sana maendeleo ya nchi yanakuja kwa kujikita kwenye shule hasa sayansi na kamwe sio watu afrika watu wanakufa njaa kila siku

    ReplyDelete
  29. zuma na mfalme mswati tamaduni zenu zimepitwa na wakati hii sio karne ya tano hapa!ndio maana nchi zenu zipo karibu

    ReplyDelete
  30. zuma angalia ukimwi ok

    ReplyDelete
  31. bi mkubwa wa kwanza kulia hana raha kabisa

    ReplyDelete
  32. zuma hata kama hauna dini je ni kwanini Mungu toka mwanzo hakuumba ADAMU NA WAKE WATATU kama wewe unavyofanya?

    ReplyDelete
  33. hivi afika ya kusini mnaongozwa na sheria gani?hatushangai ya zuma kwani nchi ya afrika kusini ndoa za mashoga ni ruksa!

    ReplyDelete
  34. nimefahishwa na ano 1218 kwa kweli umenena.habari ndo hiyo chamsingi ni uadilifu wa mwanaume lakini wanaume tulio wengi tunacheat,angalia akina tiger wanavyoabika ukweli ndo tuko hivyo.ni vyema kwa wanawake wakajijua wakiwa wawili ni rahisi kumdhibibiti mzee.awezi kuwa na ujanja,swala la mwanaume kuwa na mwanamke mmoja kwa africa aliwezekani.kungekuwa na cctv aibu ingewakuta wengi .africa kuna interaction,ni mia kwa mmoja kwa kweli,kwa ulaya ni rahisi kutokana na life style

    ReplyDelete
  35. black tupo more active mila ya mke mmoja ni ya wazungu ambao wenyewe ni inactive kwenye majamboz so wenyewe wako comfortable na hali hiyo,kwanza huyo mmoja hawamtoshelezi,wake wengi for black.utabana asioe lakini nje anahalibu,bola muwe wawili kuliko kumi

    ReplyDelete
  36. Mimi ni mwanamke pia, kwakweli mswahili umenikuna sana na comment yako. you are very right

    ReplyDelete
  37. Haya mambo hata bongo yapo, mimi namjua waziri mmoja wa bongo jina namhifashi, kesha oa mara tano, lakini jamaa ana watoto kumi tu.

    ReplyDelete
  38. Jamani mnaomshambulia Zuma kwa kweli mnamuonea. Kwani kuna mtoa maoni hapo juu kajiita mswahili amesema ukweli na pia kama Mkristo kuna aya ktk biblia kama siyo Elia au Esaya inasema waliondokea wanawake saba wakaenda kwa mtu mke na mume mmoja wakimuomba mke wake na wao waitwe kwa jina la mume wake huyo aliyeolewa. Hivyo nafikiri hata sensa ya dunia ya Shirika la Kimataifa la Watu inasema duniani wanawake wanne ni sawa na mwanamme mmoja. Hivyo na imani Zuma kaanza kuonesha mfano. Wananwake wamekuwa wengi kiasi ndiyo wanaongoza hata katika biashara ya usagaji au ndoa za jinsia moja.Kuliko wasio ridhiki. Ni imani yangu kuwa itafikia siku wanawake wataandamana wakitaka sheria na imani zisizoruhusu ndoa za mwanamme mmoja na wanawake kumi ziruhusiwe ili kuondoa suala la nyumba ndogo. Kaka mswahili

    ReplyDelete
  39. idadi ya wake ambao tayari alikwishaoa ni watano,mmoja alikufa kwa ajali na mwingine wameachana-Dlamini Zuma na watatu waliobaki ndio hao mnaowafahamu.

    ReplyDelete
  40. NI BORA YA ZUMA KAFANYA WAZIWAZI KULIKO KIRAISI UCHWARA KINAONGEZA MKE KIMYAKIMYA NA KUWAPA NYAZIFA ZA JUU HAWALA ZAKE WA ZAMANI

    ReplyDelete
  41. KELAND PRIMARY SCHOOLJanuary 06, 2010

    Duuh Rais Mzima ,anatudhalilisha waafrica, hiyo mila yakuoa wake wengi imepitwa na wakati

    ReplyDelete
  42. Ni ubatili mtupu na unafiki wengine unaochangia hoja hapa.
    Nyie wanawake mnasapoti hali hii mkijidai ni waaminifu sana na kuwasema wanaume kuwa huwa na nyumba ndogo!! Wale wanaosubiri mzee atoke kwenda kazini nao wanachomoka na kutinga guest je? Ndiyo uaminifu huo? Nyie mliojaaliwa kufanya kazi mnasingizia kwenda shift za usiku kumbe mnakwenda kwa mabuzi vipi? Hakuna aliyemwema wa kumsema mwenzake hapa, La msingi ni kwamba turekebishe tu tabia zetu na tuwe waaminfu wote.
    La kujadili hapa ni vipi jamaa anakomalia kuoa tu badala ya kufikiria kujenga nchi. Asijivune lolote kuwa wameendelea, washukuru kuwa maendekeo yanayoonekana yalifanywa na makaburu. Bahati kwamba kaburu alidhani waafrika hawataamka na kudai uhuru wao. Wangefunuliwa kama walivyoachiwa Waingereza hii bongo, nadhali hadi sasa wangekuwa bado kwenye vibanda vyao vya round kama viota vya ndege mnazi.
    Hii ni awamu ya kwanza, jamaa kavuta demu, subirini awamu ya pili ataongeza demu mwingine. Ndiyo ushujaa wa kiafrika. Fahari ni kuoa.
    Atakoma pale watakapoanza ku-riot wazulu wake wakidai kuchoshwa na hali ngumu.
    Namsikitikia sana, ......aah, yaani president mzima nanogewa tuuu. Lini atafikiria maisha ya watu wake wakati kila wakati atakuwa anabanwa kutimiza haja kwa mwenye zamu.
    Maah, UCHAFU mtupu.

    ReplyDelete
  43. Facts: Mzee Zuma ana watoto 19. Mpaka sasa ameshaoa wake watano officially. Mke wa 1- huyo bibi kizee kwenye picha kulia. Mke wa 2 - walidivorce 1998 (ndio waziri wa mambo ya ndani katika cabinet yake). Mke wa 3 - alijiua (suicide, mwaka 2000. Mke wa 4 - pichani kushoto. Mke wa 5 - pichani, pili kushoto, ndio huyo mpya.

    Mzee Zuma ametoa mahari kwa binti mwingine anategemewa kuwa mke wa 6!

    ReplyDelete
  44. mbona mnamponda zuma. wakati baba yake nyerere alikuwa rais wenu aliowa wake wengi

    ReplyDelete
  45. WE KELAND HAPO JUU INABIDI UBAKI HAPO HAPO ULIPO USOMESHWE ZAIDI, HUFAI.

    KWAMBA ZUMA ANADHALILISHA WAAFRIKA, HOW?? WANAODHALILISHA WAAFRIKA NI WALE WANAOACT UZUNGU.

    WAZUNGU SIYO KIPIMO CHA MAENDELEO YA MWAFRIKA. WAAFRIKA TUTAENDELEA KUBAKI WAAFRIKA TU SIKU ZOTE.

    OF COURSE KUNA SUALA LA KWENDA NA WAKATI LAKINI SIYO KUUKANA UAFRIKA.

    KUWENI NA CONFIDENCE, INATIA KINYAA!!

    ReplyDelete
  46. hongera zuma yaani una totoz bomba dah!!kula bata m2 wangu.unanitamanisha maana ni enjoyment kwa kwenda mbele.bora umehalalisha kuliko ungetiger wood

    msemakweli

    ReplyDelete
  47. Kuna mtu ameuliza hapo juu kuwa kama mie ni mswahili wa Mtoni kwa Azizi Ali au Mwenge Yanga, haswa umegota mahala pake ingawa sio maeneo hayo lakini naweza kukwambia ni kati ya maeneo hayo mawili. Wakujua Temeke mwisho? Wakati tuko wasichana wadogo wavulana/vijana wa kutoka uzunguni walikuwa wanakuja kula mahanjumati uswahilini kwetu, lakini out wanatoka na vipura vya kwao uzunguni. Maana mahanjumati yote yako uswahilini ya mezani na kitandani. Na hata sasa mashangingi na makruza yanapaki huku uswahili kwetu kula mahanjumati mchana, usiku yanarudi kulala uzunguni kwao!

    Hao wanaobisha kwa kweli hawataki tu kukubaliana na hali halisi, ni nani siku hizi anafuata dini kwa vitendo tena 100%? Nimesema ni bora awe na wake humo ndani kuliko kujidanganya niko peke yangu kumbe mko kumi na mbili.

    Na asikudanganye mtu mwanaume akiwa na mke zaidi ya mmoja ambao wote wana majukumu ambayo wanahitaji kutimiziwa ya kimwili pia, saa ngapi atakwenda kwa hawara? Fikiria ana wake 3 au 4, na kila mwanamke ana zamu ya siku 2 au 3 hapo. Na wote mnajuana. Kwa hiyo kila nyumba atakayokuwa na zamu, yule mke mwenye atataka haki yake ya unyumba. Kwa hiyo kwa muda wote yeye anazunguka kama pia kutoa huduma, na kama mke hawezi kutoa unyumba kutokana na na kuwa yuko kwenye siku zake, anaweza kubadilishana zamu na mke mwenzie. Sasa hiki kishada, kitapata wapi nafasi ya kutoka na kuzurura hovyo kama hakina mwenyewe?!!!

    Cha muhimu na msingi ni maelewano baina ya nyie wanawake, na pia kupima afya zenu, kwani hakuna kuoana bila kupima afya. Na kwa kuwa mko zero grazing, basi hamna wasiwasi wa kupata maradhi. Kuwa kiruka njia au kutembea ovyo nje ya ndoa ni tabia tu ya mtu haitokani kama ameolewa au hajaolewa. Lakini mkiwa wote tabia zenu safi, mmeridhika, na mmetosheka, na mna mcha mungu, basi hakuna wasi wasi ndani ya nyumba yenu. Lakini nakwambieni, kimaumbile mwanamke anaweza kukaa muda mrefu bila hata kufikiria tendo la ndoa, lakini mwanamume, mpe miezi mitatu akae tu hivi hivi aweza stahamili hiyo miezi mitatu baada ya hapo atakamata hata mwendawazimu, kwani yeye katika suala hilo keshakuwa "mwehu", hawezi stahamili.

    Mie mume wangu siku ya zamu yangu nampa mahanjumati ya nguvu, namkaba asubuhi kabla hajatoka, akitoka ameshiba haswa, na akirudi dozi kama kazi. Lakini namwambia, ukitaka kuongeza mke wa tatu ruksa tena ntakusindikiza kupeleka posa! Maana hata kuongeza wa pili nilimruhusu! Sasa anajifikiria hawa wawili demand yake iko hivyo, akija huyo wa tatu je? Na tatizo lingine linalotuponza kina dada wengi ni kudengua? Mtu ameshikwa anataka mahanjumati asubuhi unamdengulia, akienda ofisini anakutana na wenzio mimacho wamerembua kama komba mlevi au bundi, tena mapaja nje, si ndio anaenda kumalizana naye lunch time!!

    Mswahili

    ReplyDelete
  48. Mimi naona mwenye raha ni huyu wa mwisho akishaongezewa mwenzake ndio naye ataanza kukunja uso au kucheka kinafiki kama wenzake.

    ReplyDelete
  49. GO ZUMA GO ZUMA... GIMME EM WHAT UR FATHER GAVE YA!

    ReplyDelete
  50. Served as Deputy Chief Representative and later Chief Representative of the ANC in Mozambique until 1984, the year of the signing of the Nkomati Accord between the Mozambican and South African governments.

    Served on the ANC's Military Committee and Political Committee when formed in the mid 80's.
    Appointed Head of the Underground Structures and shortly thereafter, Chief of Intelligence at the ANC Head Office in Lusaka, Zambia (1987).

    He was one of the first ANC leaders to return to South Africa to begin the process of negotiation, following the unbanning of the ANC (1990).
    Instrumental in organising the Groote-Schuur Minute between the FW de Klerk Government and the ANC that reached important decisions about the return of exiles and the release of political prisoners (1990).

    Elected Chairperson of the Southern Natal and took a leading role in fighting violence in the region, this resulted in a number of Peace Accords involving the ANC and the Inkatha Freedom Party (IFP) (1990).

    Elected the Deputy Secretary-General of the ANC during the National Conference held in South Africa after the unbanning of the organisation in 1991.

    Deployed in KwaZulu-Natal because he felt that he had a role to play in bringing about peace and stability in the then highly volatile region (1994).
    Nominated as the ANC candidate for the Premiership of the KZN Province (1994).

    His strategic thinking and conflict resolution skills played a pivotal role in ending conflict in KwaZulu Natal and the then PWV region, where state-sponsored violence was tearing communities apart.

    Appointed Member of the Executive Committee (MEC) of Economic Affairs and Tourism for the KZN Provincial Government (1994).
    As MEC, he worked hard to develop the tourism industry in the province. He created a good working relationship between business, labour, and worked tirelessly to facilitate new investments in the KwaZulu Natal economy.

    Elected National Chairperson of the ANC and Chairperson of the ANC in KZN (December 1994).
    Executive Deputy President of the Republic of South Africa (17 June 1999 - 22 June 2005).

    Leader of Government Business in the National Assembly (June 1997).
    Started the process of promoting positive values through the launch of the Moral Regeneration Movement.

    Deputy President of the ANC (December 1997).

    Chairperson of the South African National Aids Council.
    Chancellor at the University of Zululand.
    Patron of the Jacob Zuma Bursary Fund (1998).
    Patron of the Peace and Reconstruction Foundation.
    Patron of Albert Luthuli Education and Development Foundation.
    Played an important role as mediator and facilitator of peace on the continent especilly in Bulundi and Democratic Republic of Congo (DRC).
    Awards/Decorations/Bursaries

    Honoured with the Nelson Mandela Award for Outstanding Leadership in Washington DC, US. (1998)
    Received an Honorary Doctorate of Literature from the University of Fort Hare (2001)
    Received an Honorary Doctorate of Administration from the University of Zululand (2001)
    Received an Honorary Doctorate of Philosophy from Medical University of Southern Africa (2001)
    source; http://www.anc.org.za/people/zumaj.html

    ReplyDelete
  51. Applause for recognition of polygamy in Republic of South Africa:
    It was with great applause on Sunday that rural villagers outside Nelspruit, South Africa, responded to the news that polygamy is now officially recognised. The Customary Marriages Act was explained to about 100 residents of Daantjie tribal trust, after it came into effect on November 15, 2000.
    "This is the emancipation of black women whose status was relegated to the background," said national deputy director general in the South African Department of Justice and Constitutional Development, and legal services head, Simon Jiyane.

    He said the Act marked the demise of the colonial order and that couples could now register polygamous marriages at home affairs offices and be issued a marriage certificate. He said it was important that men support the Act and that traditional healers ensured their subjects were familiar with it.

    The main objective of the Act is to extend full legal recognition to marriages entered into in accordance with customary law or traditional rites by bringing women and children into the protective realm of the constitution.

    The main objective of the Act is to extend full legal recognition to marriages entered into in accordance with customary law or traditional rites by bringing women and children into the protective realm of the constitution.

    The main objective of the Act is to extend full legal recognition to marriages entered into in accordance with customary law or traditional rites by bringing women and children into the protective realm of the constitution.

    A husband in a customary marriage who wishes to enter into a further customary marriage with other women after the commencement of this Act must make an application to the court to approve a written contract that will regulate the future matrimonial property system of his marriage, Gillwald announced.

    conclusion:
    Good Law.

    ReplyDelete
  52. Mbona kuwalaumu wanaume wa Kiafrika kwa kupenda ngono? kwani hiyo ngono wanaifanya wenyewe? Kwani hao wanawake wamelazimishwa na nani? Si walipoingia walijua jamaa tayari anamke? Na ninyi mabinti zetu kwa kupenda dezo...!! ndo maana mnaishia kuolewa wengi..Lol....give us a break wanaume wa Kiafrika. Mdau-USA

    ReplyDelete
  53. Sijajua kwanini wanawake wakiwa ndani ama nje ya ndoa wanahofia mwanaume akianza kuugua itakuwaje ama mwanaume akifa urithi utakuwaje ndugu wa mume watagombea mali au la, huu ni umasikini tu, na nionanvyo mimi ndoa ni mfumo wa kale wa maisha mi naona nchi zilizoendelea mtu yoyote akiugua anafia hospitali , nursing home ama care home , biashara finish ukitaka urithi nenda kwa lawyers wa mhusika , urithi mwingine unaenda watoto (wawe wangapi),charity,mbwa,mafarasi etc acheni njaa zenu wadau

    ReplyDelete
  54. biblia inasema kuwa toa boriti kwanza kwenye jicho lako kisha toa kibanzi kwenye jicho la mwenzio nashangaa sa wabongo kumuandama zuma wakati tz ndio dili kubwa

    ReplyDelete
  55. katika amri 10 za mwenyezi MUNGU AMRI YA 9 inasema USITAMANI MKE WA JIRANI YAKO na sio usitamani wake za jirani yako hivyo maraisi kama zuma ni watu wanaoendekeza mira za long time

    ReplyDelete
  56. mimi ni mwanamke naomba nasi wanawake tuweze kuolewa na waume zaidi ya mmoja ok

    ReplyDelete
  57. jamani afrika kusini ndio nchi inaongoza kwa UKIMWI hapa duniani

    ReplyDelete
  58. hata mwanaume mmoja akioa wanawake 10 hawaishi kamwe

    ReplyDelete
  59. jamani huko afrika kusini kama kuna wanawake wengi mbona wanaume wanaoa wanaume wanzao na wanawake wanaoa wanawake wenzao?

    ReplyDelete
  60. zuma una watot 19 je unwakumbukwa wote majina?

    ReplyDelete
  61. bora zuma watoto wako watasoma shule huku tanzania watoto wengi wa ndoa za mitala HAWASOMI SHULE kwani wazazi hawana uwezo wa kuwasomesha hivyo wamebaki kuwa vibaka wanatusumbua kweli hapa dar

    ReplyDelete
  62. kama kuna mwanaume alistahili kuwa na wake wengi hapa duniani ni adamu

    ReplyDelete
  63. ila nakumbuka zuma alikuwa na kashfa ya kubaka ila kwa kuwa ni kigogo

    ReplyDelete
  64. VICTOR KILEOJanuary 06, 2010

    ZUMA ANA PESA NI HAKI YAKE AKAMATE NGOMA NYINGI NASIKITIKA ANAKAMATA NZEEE NZEEE AMA KUUU KUUU LAKINI YEYE MWENYEWE VIAGRA MTU KWA HIYO POA TU. HIVI NI NANI MICHUZI AMA NI NANI SIJUI ANA MKE UGANDA TANZANIA KENYA NA BURUNDI? NIMEMSAHAU LAKINI ANATEMBELEA SANA HIYO MITAA. ZUMA TAFUTA VIJANA UTA ENJOY ZAIDI

    ReplyDelete
  65. WAMAKONDE WANASEMA: CHAUMBILE NNUNGU CHA KUMEMENA. Yaani "ALICHOUMBA MUNGU UNAKULA TU", hata jiwe? "JIWE TUNACHEMUSHA NA KISHA TUNAKUNYWA SUPU YAKE".

    Mzee zuma, wewe memena tu bwana, hawa wanaochonga wakitaka wakakushitaki mahakama ya kimataifa "THE HAGUE".

    Hivi nyie akina dada mnaosema jamaa anaoa kama kuku, nyie wenyewe katika maisha yenu, mmememenwa na njemba ngapi?

    TAFUNA TAFUNA BABA ZUMA.

    HAPPY NEW YEAR ALL.
    mzee wa kumemena
    UK

    ReplyDelete
  66. KUmbe Zuma kama mimi.

    Safi sana. Bila ya kuoa zadi ya mmoja wanawake waliozidi watachezewa na midume wahuni?

    Dawa ni kuoa zaidi ya mmoja.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  67. Acheni kujipa moyo, hao watoto wa mitaani wanosumbua kama mnavyodai na kuzurura hovyo hawatoki kwenye ndoa zetu za mitala, kwa sababu watoto wetu wamitala wanazaliwa ndani ya ndoa na wanatambulika kisheria na hata familia nzima inawatambua kuwa huyu ni mtoto wa mke mkubwa na yule wa mke mdogo. Na kama baba ana msimamo wote wanalelewa nyumba moja. Zamani mlikuwa mnasingizia kuwa wanawake wanaoolewa mitala wanazaa watoto wengi lakini imekuja kugundulika ni vice versa wanazaa watoto wachache kuliko walio wengine.

    Sasa source ya hao watoto mnao waita wanawasumbua mitaani ni watoto ambao baba zao wanashindwa kuwapeleka kwenye familia zao kwa kuwa wamezaliwa kwa mahawara! Na anaogopa akimpeleka kwa mkewe litazuka zogo. Vile vile huyo hawara yeye akishazalizwa thamani yake inashuka anatafutwa spring chicken asiwe ya na makelele ya watoto na huduma inahamia huko. Hiyo source ya kwanza.

    Source ya pili ni watoto ambao wametoka kwenye ndoa zenye migogoro zilizovunjika kwa sababu baba ana nyumba ndogo/hawara. Mama keshajua hiyo siri kaona kadhalilishwa anaamua kubeba mizigo yake kichwani kurudi kwao,ama anawaacha watoto hapo kwa mumewe, au anakwenda nao kijijini ambako wanamtoroka kurudi mjini kwa kutokuzoea tabu za kijijini. Na hao wanaobaki na baba zao kutokana na mateso ya mama wa kambo, pengine hicho kibanda hasara (nyumba ndogo/hawara) ndio kimeingizwa ndani, basi ataona hao watoto ni nuisance, atawatesa mpaka watakimbilia mtaani kwenda kuwa omba omba.

    Mie niko nyumbani kwangu na mume wangu na watoto wangu wawili au watatu, na mke mwenzangu yuko kwake na watoto wake wawili, na baba yao yupo na wanatambulika kuwa ni watoto wa familia hii, kitakachowapeleka huko mtaani ni nini??

    Kama ni suala la kusema ni umasikini hata basi familia zenye mke mmoja zote zingekuwa matajiri, familia za wake wengi ambazo ni minority wangekuwa masikini na Tanzania isingekuwa ya tatu kutoka mwisho kwa umasikini. Tena kwenye familia ya mke mmoja ni rahisi sana watoto kwenda mitaani hasa baba akipata "kibanda hasara" halafu anamalizia pesa zake zote huko bila kukumbuka huduma ya mke na watoto wake nyumbani, na kama mama hana kibarua basi watoto wataishia mtaani maana hawawezi kustahamili njaa!!

    Mswahili

    ReplyDelete
  68. Mwenye makosa ni nani? ZUMA AU WAKRISTU?

    ReplyDelete
  69. Haa haa haaa. Kuna mtoa maoni mmoja ametoa maoni kwamba yeye ni mwanamke angependa kuolewa na wanaume wengi. Ndio wenzio wanavyofanya hivyo, sema ndoa zao na wanaume wengine ni bubu. Anika mawasiliano yako globuni, utapata wanaume wa ziada ushindwe mwenyewe.

    ReplyDelete
  70. Mi naomba kuuliza, kuna mdau anasema yeye anataka kuolewa na wanaume wengi(Mitala).

    Je huyo mama aliye na waume wengi atatambua vipi baba wa watoto zake? na pia huyo mama ataweza kuwatunza waume zake pamoja na watoto?

    Maana ya ndoa ya mwanaume na mwanamke ni kuweza kutambua mtoto baba yake ni nani, ili baba aweze kuwajibika kwa nguvu zote kuwatunza watoto wake pamoja na wakeze.

    Nawasilisha

    Mdau
    Mzulu Mjadi

    ReplyDelete
  71. nakumbukuka JABALI LA MUZIKI HAYATI MARIJANI RAJABU alikaa chini na kutunga wimbo WIMBO UKEWENZA mimi naomba kaka michuzi utuwekee ule wimbo ili watu wausikilize ujumbe uliomo na hapo watakubaliana naye kuwa ukewenza ni hatari ukikuta mke mwenzio hana imani,naitwa HANIFA nipo usa

    ReplyDelete
  72. katika agano la kale tunasoma kuwa ibrahimu na sulemani ni kati ya mitume na manabii ambao walioa wake wengi,swali je walioa kwa kwa maagizo ya wapi?naomba mtu anisaidie mstari au aya iliyoruhusu kuoa wake wengi wakati huo katika agano la kale,na je walitakiwa kuoa mwisho wake wangapi kwa mujibu wa maandiko ya wakati wa torati?walifanya hivyo wakiwa kama binadamu wengine tu

    ReplyDelete
  73. Wengi mnazunguka mbuyu tuu! Ukweli wa maandiko na hasa kwa sisi tunaomini Biblia, mungu alimuumba mwanaume mmoja Adam na mwezi wake Hawa.
    Period, mengine yote ni utashi mbovu wa kibinadamu.
    MFUMO DUME HUO !
    Wanawake tutaendelea kuwa mbumbumbu hadi lini wenzangu !

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...