
KAMPENI YA PAMOJA YA KUCHANGIA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU KATIKA JUHUDI ZA KUSAIDIA MAELFU YA WAATHIRIKA WA MAFURIKO SISI NI NANI:
Ushirika wa wanachama wa mitandao ya kiintaneti ya JamiiForums.com, Mwanakijiji.com, na
Utangulizi:
Hadi hivi sasa watu wapatao 40,000 ambao kati yao 10,000 hivi hawana makazi wameathirika na mafuriko yaliyoanza siku ya Krismasi 2009 na kuendelezwa na mvua zinazonyesha sehemu mbalimbali nchini. Athari nyingine kubwa ya mafuriko haya ni kusababisha milipuko ya magonjwa, vifo na madhara kwa wanyama na uharibifu mkubwa wa mazao.
Hadi hivi sasa watu wapatao 40,000 ambao kati yao 10,000 hivi hawana makazi wameathirika na mafuriko yaliyoanza siku ya Krismasi 2009 na kuendelezwa na mvua zinazonyesha sehemu mbalimbali nchini. Athari nyingine kubwa ya mafuriko haya ni kusababisha milipuko ya magonjwa, vifo na madhara kwa wanyama na uharibifu mkubwa wa mazao.
Hadi hivi sasa Mikoa iliyoathirika ni pamoja na Morogoro, Dodoma, Mwanza, Shinyanga, na maeneo ya Ruvuma. Kuna uwezekano wa idadi ya mikoa iliyoathirika na wahanga wa mafuriko kuongezeka. Uharibifu mkubwa vile vile umetokea kwenye miundo mbinu ambapo barabara, madaraja na majengo mbalimbali yameharibiwa.
Kampeni hii basi inalengo la kukiwezesha chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kuweza kufikia wahanga wa mafuriko haya na kutoa misaada inayohitajika kwa haraka kama mahema, vyandarua, vyakula, madawa, nguo na mahitaji mengine ya kibinadamu. Tunataka kuchangisha si chini ya shilingi bilioni moja ndani ya muda mfupi uwezekenavyo kabla athari zaidi hazijatokea, tukizingatia kuwa hatuwezi kutegemea misaada ya kigeni hasa kwa vile mafuriko haya yamekumba nchi jirani vile vile na kuwa hali ya uchumi imepunguza uwezo wa nchi nyingi kutoa misaada.
Kuwasiliana
Mratibu wa Kampeni ya Kuchangia Chama cha Msalaba Mwekundu
Bw. Sanctus Mtsimbe -
Rais wa TPN
Simu: 0715 740 047
Email:
JINSI YA KUCHANGIA:
Tumebuni njia mbalimbali za kuweza kuchangia vitu kama vyandarua, maboksi ya maji safi, nguo, madawa (ambayo hayajapita muda au kufunguliwa), mahitaji ya watoto na kina mama n.k.
Tumebuni njia mbalimbali za kuweza kuchangia vitu kama vyandarua, maboksi ya maji safi, nguo, madawa (ambayo hayajapita muda au kufunguliwa), mahitaji ya watoto na kina mama n.k.
A: MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
P.O. Box 1133 Dar es Salaam
Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843
Email:
logistics@raha.com B: KUTUMIA MTANDAO WA WANATAALUMA WA TANZANIA (TPN).
Hivyo TPN itakusanya michango yetu kwa njia mbalimbali hapa chini na kuiwasilisha kwa TRCS na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kampeni hii.
2. Kuingiza Benki au kuhamishia fedha benki(bank deposit and transfers): · Jina la Akaunti: Tanzania Professionals Network, · Jina la Benki: CRDB Bank ; Tawi: Lumumba · Jiji: Dar Es Salaam; Nchi: Tanzania · Swift Code: CORUTZ TZ · US $ (Fedha za kigeni) A/C No: 02J1 007 608 900; · TZS A/C No: 01J1 007 608 901
C: KUTUMIA MITANDAO YA SIMU
3. M-Pesa (Vodacom): 0768 777 888 4.
Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88 5.
Zap (Zain) 0784 00 88 99
6. Michango ya kutumia makato ya kila siku ya Airtime za simu: “Changia Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili.
7. Western Union — Tuma kwa jina la:
Mr. Emmanuel Mmari;
TPN Finance and Administrative Manager;
Dar Es Salaam;
Tanzania.
uma nakala ya MTCN kwa
president@tpn.co.tz na mwanakijiji@jamiiforums.com ili kuweka rekodi sahihi. 8: Michango ya vitu mbalimbali: Ofisi za TPN —
Barabara ya Nyerere;
Jengo la TOHS;
Ghorofa ya kwanza,
karibu na TBC (RTD) Radio.
Piga simu 0715 740 047
kwa kupata msaada wa kuja kuchukua vitu kama huna usafiri.
....sio tuchangie harusi tuu!
ReplyDelete