Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Prof. Mark Mwandosya (kulia), akiwa na Balozi wa Israel Tanzania Mhe. Jacob Keidar (katikati )alipomtembelea Waziri Mwandosya kuzungumzia jinsi Israel itakavyosaidia kuijingea uwezo Sekta ya maji na Umwagiliaji nchini.Kushoto ni Mhandisi Benjamin Arbit
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Mark Mwandosya, Januari 8, 2010 amefanya na mazungumzo na Balozi wa Israel Tanzania Mhe. Jacob Keidar ofisini kwake Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yalihusu ukamilishaji wa muundo (flamework)wa ushirikiano kati ya Tanzania na Israel katika sekta za Maji na Umwagiliaji.

Makubaliano ni kukamilika kwa rasimu((draft) ya kwanza ya waraka muundo ifikapo mwezi Machi, 2010. Waraka huo ni muhimu katika utekelezaji wa makubaliano ya pamoja katika mambo yafuatayo:-

(1)Uanzishwaji wa kituo cha Utafiti wa masuala ya Umwagiliaji.

(2)Kuzijengea uwezo sekta za Maji na Umwagiliaji
(3)Kubadilishana utaalamu na Wataalam
(4) Uhamasishaji wa kilimo cha umwagiliaji kwa njia ya matone.
(5)Uwekezaji katika sekta za Maji na Umwagiliaji.
Katika ziara hiyo, Mhe. Balozi aliambatana na Mwakilishi wa wafanyabiashara wa Israel Mhandisi Benjamin Arbit ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya SBI International Holding AG Africa Kampuni inayoshughulika na kazi za ujenzi wa miundo mbinu mbalimbali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ha! Ina maana hatimaye Tanzania tumekuwa na ubalozi wa Israel nchini au bado tunashirikiana kupitia ule wa Nairobi? Kwa ajili ya baraka za Bwana Mungu wa Israel (The Lord God of Israel) tunahitaji sana kuwa na uhusiano mzuri na Israel kama taifa. Biblia inasema juu ya taifa la Israel katika Zaburi kwamba 'nitamlaani anayekulaani na kumbariki anayekubariki' na pia inasema 'ombeni amani kwa ajili ya Israel, amebarikiwa yule akutakiae (Israel) mema'. Makosa yaliyofanyika katika utawala wa awamu ya kwanza wa kuvunja uhusiano na Israel yalikuwa ni ya hatari sana katika ulimwengu wa roho. Mungu ibariki Tanzania tusirudi huko. Shalom Israel. Peace be unto you!

    ReplyDelete
  2. Duh! ndo leo najua kuna Ubalozi wa Israel nchini Tanzania. Umeanza lini? Passport zinapatikana hapa?

    ReplyDelete
  3. haya ndiyo mambo tuanayotaka. nchi yetu ni tajiri sana,ardhi ipo mito ipo lakini watu wanakufa njaa na umaskini unawaua hii ni aibu kubwa sana kwa taifa lenye baraka kama tanzania.kuna watu wanatamani wangekuja tanzania wakageuza huo ufukara into gold.
    myahudi sio mchezo ukitaka kujua watu ambao wanaweza kuugeuza mlima kuwa shamba basi ni wayahudi hapo nyosha mikono juu.
    nchi yetu inahitaji mechanised agriculture na hii inatosha kabisa kufuta umaskini lakini utakuta miviongozi inapanua ufisadi tu kutanua mitumbo ikifyema mabilioni ya fedha wakati fedha hizo zingebadili angalau maisha ya familia 100 nchini.
    umefika wakati watu waamke watizame mambo ktk angle tofauti na waliyozoea,sio lazima wote wakajazane kariakoo,city center manzese n.k kuna sehemu zinaweza kufanywa zikawa nzuri tu na zikazalisha na pesa ya kutembelea utakako ikawepo always.
    huku ulaya baadhi ya sehemu wanamiezi 4 tu ya kuzalisha chakula na hawalii njaa hata siku moja,hii ni kwasababu wanatumia mechanised agriculture sio kilimo cha jembe lamkono na kutegemea nvua.

    ReplyDelete
  4. Flamework
    Tunakazi jamani

    ReplyDelete
  5. hakuna flamework, mnapotuma materials kwa Michuzi mzifanyie proof reading. mnaji-expose sana ndugu zangu, hivi vitu havifutiki hapa.

    ReplyDelete
  6. Habari Michuzi,
    Kwanza samahani kwa kuweka ombi hili hapa. Siku nyingine nitakutumia email. Nimeona habari njema kwenye tovuti ya IPP media kuhusu ukamatwaji wa nyavu haramu za kuvulia samaki. Operesheni iliyoendeshwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. John Magufuli. Ninaomba uweke habari hiyo kwenye blogu yako ili watanzania waone kuwa tuna viongozi wanaofanya kazi na wenye nia ya kuleta maendeleo. Pia iwe changamoto kwa mawaziri na viongozi wengine. Kama Rwanda wanavyopiga hatua, na sisi tunaweza kama tukiwa na viongozi wa kutosha kama Dk. Magufuli.
    Mdau

    ReplyDelete
  7. Hivi huu Ubalozi wa Israel Tanzania ulirejeshwa lini? Msaada kwenye tuta tafadhali

    ReplyDelete
  8. Hawa si binadamu na wala si wakuamini kabisa hivi wapo nchini wanafanya ujasusi hawakai sehemu bila hivyo, watu wabaya sana hawa wamekaa kama wanyama hawana uaminifu kabisaaa.

    ReplyDelete
  9. Mheshimiwa Mwandosya hongera sana. Israel ni nchi ambayo ina utaalamu mzuri wa kilimo cha umwagiliaji kinachofahamika kwa jina la drip irrigation. Umwagiliaji huu una hakikisha maji yanatumika economically hata kwenye sehemu zenye ukame kilimo hiki kina tija. Mimi nilifika Israel sehemu za Galilaya nilienda kwenye shamba la ndizi la mzazi wa rafiki yangu na nikajionea. Nchi yetu kwa water resources tulizo nazo pamoja na uwingi wa ardhi tunaweza tukawa exporters wakubwa wa ndizi. Kwa spirit ya kilimo kwanza, Mheshimiwa you are in the right track. I just hope wadau wote watakuunga mkono. Hongera sana mkuu.

    ReplyDelete
  10. wewe unaye piga porojo za ujausui unadhani kwa dunia ya sasa ujasusi unashindikana kufanyika kwa teknolojia zilizopo?labda bado uko dunia ya mabonde kwinama,kama hupendi kufanyiwa ujasusi basi uwe na gharama za ajabu za kuzuia teknolojia inayoweza kukusoma na kukamata habari na picha zako vinginevyo unasema usichokijua.

    ReplyDelete
  11. MAMBO YA MTO NILE TU HAYO

    ReplyDelete
  12. ....Prof Mwandosya mi namkubali sana...lugha ya picha tu inaonesha anaongea vitu vyenye AKILI apo....ata POZI alokula apo linaonesha ana-KONFIDENSI na anajua ANACHOONGEA!

    ReplyDelete
  13. YAANI TANZANIA NI KICHWA CHA MWENDAWAZIMU KILA KITU KUSAIDIWA ISIPOKUWA WIZI TUMEJAALIWA HATUITAJI KUFUNDISHWA. HAHA HA HA AHA AHE

    ReplyDelete
  14. Anony hapo juu acha kuropoka israel watoke kwao huko kuja kuifanyia ujasusi tanzania mna nini nyie???? Hao tumewafuate wenyewe kwa shida zetu tena bora wamekuja watufundishe jinsi ya kutumia maji yetu vizuri tuna mito kila kona ya nchi hii lakini bado tunakuwa masikini wa kutupwa na njaa juu, jambo la aibu sana hilo Hongera prof mwandosya kwa kufikiria kuondoa hii aibu hapa kwetu

    ReplyDelete
  15. woooo wooooo woooo mweee ni kweli?tuna ubalozi wa ISRAEL tanzania au nimeona vibaya?msaada ata mimi nijue umeazishwa lini mbona hatujawai sikia ilhal tupo bongo now?

    mweee kama ni kweli na ibarikiwe tanzania na israel na aliyeurudisha atapata rehema za Mwenyezi

    i wanted this thing for ages now lol..annon #1 well said dear

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...