JULIET SHANGWE MBEYELA
(Alizaliwa 1977—Alifariki 2009)

Kwa niaba ya familia ya Zakaria Maftah na ya Elizabeth Mbeyela, naomba tutoe shukrani zetu za dhati kwa ndugu, marafiki, majirani na wote waliojitokeza kutufariji na kujitoa kwa hali na mali wakati tulipofikwa na msiba wa kufiwa na binti yetu mpendwa
JULIETH SHANGWE MBEYELA.
Kifo chake kilisababishwa na ajali ya magari iliyotokea huko Muscat nchini Oman, tarehe 31 Desemba 2009. Si rahisi kuwashukuru wote kwa kuwataja majina lakini itoshe kueleza kuwa tunatambua moyo wenu wa upendo mliotuonyesha tangu tulipopata taarifa ya kifo hadi siku ya maziko tarehe 08 Januari 2010 yaliyofanyika Kinondoni.

Aidha shukrani za pekee ziwaendee wafuatao:
• Mheshimiwa Hussein S. Khatib, Balozi wa Tanzania nchini Oman,
• Ndugu Saidi Shwaibu Mussa Minister Counsellor
• Ndugu Abdallah A. Kilima First Secretary and Head of Chancery
• Na watumishi wa Ubalozi na familia zao.

Msaada ambao Ubalozi ulitupatia wakati tulipokwenda Muscat kuuchukua mwili wa marehemu Julieth ulikuwa wa thamani kubwa. Ubalozi huo ulijitoa kutusaidia kupitia katika hatua zote mpaka kuusafirisha mwili na sisi kurudi nyumbani Tanzania. Msaada huo ulitufariji sana. Hatuna maelezo ya ziada ila kuwashukuru. Asanteni sana na ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye atakayewalipa mema hayo.
Shukrani nyingine ziwaendee menejimenti na watumishi wa Oman Air kwa kuwa karibu na sisi wakati wote wa msiba na kuyarahisisha makazi na maisha yetu siku zote tulipokuwa Muscat.

Wengine ni Watanzania wanaoishi nchini Oman pamoja na wananchi wa Oman ambao wana asili ya Tanzania. Tunawaambia nyinyi nyote shukrani jazira na Mola inshallah atawajaza yaliyo mema kwa wingi unaostahili.

Aidha tunaushukuru uongozi na watumishi wa Ofisi ya World Health Organisation Tanzania, kwa msaada mliotupatia wakati wa maziko ya mpendwa wetu Julieth. Shukrani hizi pia ziwaendee watumishi wa Air Tanzania.

Pia tunawashukuru washirika wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Muhimbili chini ya uongozi wa Mchungaji Monica Lugome na Mwinjilisti Raheli Mbisa kwa sala na dua zao ambazo zilitutia nguvu kabla na siku ile ya maziko.

Sisi tulimpenda sana Julieth lakini
Mwenyezi Mungu amempenda zaidi,
Jina la Bwana lihimidiwe
Amen

Imetolewa kwenye Blog ya Michuzi na Patrick Tsere

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. Poleni sana na Mungu awape nguvu.

    ReplyDelete
  2. huyu Julieth ni yule aliyesoma secondary ya jangwani?
    RIP na poleni wafiwa, Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  3. May her soul rest in peace. Amen.

    ReplyDelete
  4. What a Beautiful young woman.Rest in peace.my heart goes out to the family.

    ReplyDelete
  5. Juliet alimalisoma form 5 na 6 Jitegemee Secondary siyo Jangwani.

    ReplyDelete
  6. Poleni sana familia ya marehemu Jullie.
    Nilimfahamu marehemu wakati tulipokuwa Air Tanzania na baadae yeye na mfanyakazi mwingine walihamia Oman Air. Mara ya mwisho kuonana na Jullie ni zaidi ya miaka 5 iliyopita kwani nami kama alivyokuwa marehemu Jullie niliondoka Air Tanzania kwenda nje katika harakati za kupambana na maisha.
    Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu Jullie.

    ReplyDelete
  7. Je wadau,huyu ni dada yake Fadhili Mbeyela niliyesoma nae kinondoni?

    ReplyDelete
  8. RIP Shoto...

    ReplyDelete
  9. Rest in Peace Julieth (Shoto) Mbeyela. Unakumbukwa na wadau uliosoma nao Manow Lutheran Junior Seminary huko Tukuyu Mbeya kuanzia form one mpaka four. Unakumbukwa kwa jinsi ulivyokuwa smart na kutokuwa na makuu na watu. Wewe ni mdau wa tano kati ya waliosoma manow waliokufa kwa ajali. Waliokutangulia ni Omary, Neema, Gwakisa a.k.a bonge, Peter Mpayo a.k.a Pierre na sasa ni wewe.
    We hate you ajali. Mwakalebela

    ReplyDelete
  10. kila siku uwa najiuliza kwanini mungu uchukua kizuri mapema jamani,nimeumia kweli jamani binti mdogo kabisa mwenye alikuwa namalengo yake mengi tu,kweli kazi ya mungu aina makosa ,mungu akupumzishe mahali pema peponi ,tulikupenda ila mungu kakupenda zaidi

    ReplyDelete
  11. My heart leaped a beat when I read the msg "Mary, mtoto Julieth hatunae tena.." the clock stop! the day was dark, I wished I was home to mourn with the rest of family and friends.

    Julieth,s picture, testmonies... reflects her inner beauty, she was such a kind, tender,...
    a wonderfull soul.

    To her mother Eliza: The loss is great, and will never get a substitute, one day your heart of a mother might heal but the scar will be there for life! You know, we never get over it but we learn how to live with the fact!

    GOD is our secret, HE is love, HE gave us the capacity to creat, overcome, endure and to be greater than our sufferings. May He be there every minute to give you peace not of man but of angels, He will hold you when we fail with our human arms.

    May HE hear your prayers and give you the ability to hear HIM back in whatever language you best understand. Stay strong honey, we are all with you.

    RIP daughter Julieth
    Msalato girls, Mazengo boys 1970s mpo?!

    ReplyDelete
  12. R.I.P Shangwe!

    ReplyDelete
  13. Rest In Peace my friend Shoto! we are all in the same route.I remember the old good days when we were young when we were going together at Upanga primary School and going home while deciding whether we should go at your home or mine first while singing "Don't be cruel...." by Bobby Brown.I will keep the memories of your kind heart,love,determination always encouraging. May God give grace to mama and your brother to hold on at this trial moment.

    ReplyDelete
  14. was real beautiful....rest in peace...

    ReplyDelete
  15. Ndugu yangu Anon wa Jan 14 12:59:00pm. Umeuliza kama Msalato na Mazengo wa 1970s wapo. Inaelekea wapo kwa sababu huyo alietoa hiyo notice Mr Patrick Tsere alikuwa miongoni mwa wana Mazengo 1970 na 1971. Kwa hiyo wapo. Maana mama mfiwa si ndiye alikuwa dada yetu pale Msalato kipindi hicho? Ama kweli miaka imeenda.

    ReplyDelete
  16. Oooh My God!! I cant believe it,kumbe huyu ndiye julieth , namkumbuka baada ya kuona picture yake, Nilisoma naye upanga primary school lkn alikuwa amenizidi darasa moja, alinisaidia sana nilipokuwa bullied wakati nimeahia shule ile kutoka shule nyingine,She was so caring, kweli wema hawana maisha,eeh Mwenyezi Mungu Umlaze mahali pema peponi Julieth!! Yaani ninapoandika message hii machozi yananilenga..Jamani khaa, Kwa yeyote mwenye contact details za ndugu zake au wanapokaa siku maana zamani walikuwa wanakaa upanga, please let me know, i would like to give them my personal condolence..
    Thanks

    ReplyDelete
  17. Shangwe alikuwa bado anaishi palepale Upanga - mtaa wa Undali.

    RIP my cousin Shangwe.

    ReplyDelete
  18. Damn RIP JULIETH...mimi nilimfahamu pale JKT jitegemee tulisoma nae HGL A level 1997-1999,she was so beautyful,tall,kind, humble,smart,intelligent girl!May her soul rest in peace...u will be remembered forever!

    ReplyDelete
  19. Juliet,i loved you and i will always do,even though you're gone but my love stays the same on how i feel about you.You was so fun to be around,always kept me loughing and happy.I know this world is not my our home,we're all in the same path but i know one day we'll meet again in God's grace and will will lough again reminise the life we lived on earth.May Lord God rest your beautiful soul in Peace.
    Man i just can't take this!!
    Fredy B.

    ReplyDelete
  20. Mungu akulaze maali pema Dada mpendwa Shoto
    Alhakim Maftah (Kim)

    ReplyDelete
  21. R.I.P My friend.May God rest your Soul in eternal peace. Nilisoma nae JKT jitegemee, A level 1997-1999 na tulikuwa wote hostel. I am blessed to have met you and known you, such a wonderful person to be arould.
    Daima Tutakukumbuka.
    FG

    ReplyDelete
  22. Sijui nianzie wapi. I guess, poleni sana wafiwa. Juliet was my closest friend at Jitegemee. We were unseparable. She was not only a friend but a sister. Jamani! so many memories are running through my mind, looking at her picture. Such a shame to lose such a wonderfull person. Always full smiles, kind, loving, caring and a genuine person. We love you but God loves you more sweetheart.
    R.I.P mpenzi.xxxxx

    ReplyDelete
  23. R.I.P Juliet..... She was very beautiful and the coolest girl in GHL class of 1997-1999 Jitegeme High
    Wow!!! Can't believe she is gone!!!

    ReplyDelete
  24. rest in peace sis,, i miss u deadly mpnz. hata cwez kuelezea

    ReplyDelete
  25. Just thought of you today,Rest in Peace Love. miss you a lot!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...