Home
Unlabelled
tangazo maridhawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hicho ni kiinglishi bora kabisa. Mimi nafikiri hata viongozi wetu wamebeing FISADIS. The so called masuperstars wetu nao wamebeing chokambaya. Yaani la msingi nikubadilika nakuachana na kuBEING. Kwa watanzania wengi, English ni lugha ya 3 kwetu nikimaanisha kila mtu analugha ya kijijini kwao, Kiswahili ndipo KIInglishi kwa hiyo huyu mtu asamehewe bure. Ukienda marekani, utakuta zaidi ya 99% ya wazungu (ukitoa spanish, na wahamiaji) hawajui kuongea lugha nyingine zaidi ya KiiNglishi kwanini hatuwasemi wao? Ndio maana nikiona baraza zima la mawaziri la Kikwete pamoja na yeye mwenyewe wanajitafuna kwenye KIInglishi nawasamehe bure tu. Ni umbumbumbu uliochangamyika na kuendekeza kiswahili wakati dunia imekuwa kijiji.
ReplyDeletewataalamu wetu, mashaka na kanumba nendeni mtengeneze hilo bango.
ReplyDeleteJohn Mashaka Vs. Steven Kanumba nani zaidi?
skills for life!! nafikiri kuna wataalamu wa matangazo, lugha, nk. wakati umefika sio kukurupuka tu na kujiandikia!! tunanyimana ulaji tu hapa, sasa matokeo yake Hoteli nzima inaonekana ipo kimtindo mtindo...... anyway hii ni Bongo au siyo..... kila mbuzi anakula kutokana na urefu wa kamba yake na wateja wataendelea kumiminika pale keep in mind that 'message is delivered' the pool is being chemical' japo kwa mbali jamaa wanaogelea kwa kwenda mbele!!
ReplyDeletemimi nitaongelea logic ya hila bago (tangazo) hapo wenye hoteli walichokifanya ni ku-escape liability (kukimbia hatia) kama mtu ataogelea na kupata madhara yoyote yale yatokanayo na chemical ambazo huwekwa kwenye mabwawa wao (hoteli) hawatokuwa na hatia (liable) kulipa fidia kwa huyo mtu aliedhurika kwa kuogelea. hii inakubalika katika makosa ya madai (tort), na walichofanya ni sahihi kisheria kutoa notice (ilani)mapema juu ya madhara yanayoweza kujitokeza.
ReplyDeleteHUO NI ULIMBUKENI NA UMASIKINI WA FIKRA. KILA NCHI INA LUGHA YAKE YA TAIFA NA UTAMADUNI NA KILA TAIFA LINAJIVUNIA KWA HILO, WATU WASIOTHAMINI LUGHA YAO NI UTUMWA NA AIBU KUBWA.
ReplyDeleteKUTOJUA KIINGEREZA SI KOSA KWANI SIO LUGHA YETU HIYO NI YA WAINGEREZA.
HATA HAPA UINGEREZA TULIPO KUNA LUGHA ZAIDI YA 200 ZINAZOZUNGUMZWA NA BAADHI HAWAWEZI KUIZUNGUMZA VYEMA, NA HATA WIZARA YA MAMBO YA NDANI HAPA INAJUA HILO NA INATOA HUDUMA ZA UKALIMANI KATIKA KUTOA HUDUMA ZAKE.
UKIJA ULAYA KILA NCHI INAZUNGUMZA LUGHA YAKE MFANO UFARANSA,UJERUMANI, POLAND, BELGIUM,DENMARK NK. UKIENDA UJERUMANI UKIONGEA KIINGEREZA HAKUNA MTU ATAKAYEKUDHAMINI WANATAKA UONGEE LUGHA YAO.
TUACHE USHAMBA NA UMASIKINI WA FIKRA.
TUNAJIVUNIA LUGHA YETU YA KISWAHILI, ASIYEJUA HILO BASI AMEPITWA NA WAKATI.
Aah, huna haja ya kushangaa kihivyo!!!! Hiyo lugha hata wakuu wa nchi inawashinda!!!
ReplyDeleteKuna DC alikuwa anatupiga chenga kuonana nae b'se English haipandi maana tulikuwa na wa wafadhili wa Kimarekani!!!! kila ukimpigia simu ya mkononi anampa mtu mwingine apokee na kudai yuko busy!!!!!!!!!!
hapa ujumbe umefika kila nchi wana jinsi ya uongeji wao ni sawa na kiswahili cha kenya na Bongo kinachohitajika tu ni ujumbe ufike kwa mlengwa basi
ReplyDeleteHapa naona kuna tatizo.
ReplyDeletewaajiriwa tunaowapa kazi wanashindwa kuwa na PR. Huku kwa wenzetu, mtu akiandika kitu ambacho anataka kukiweka kwa public huwa anaomba second opinion kabla ya kukitoa.
Ndiyo maana makala nyingi ya vijana wetu John Mashaka na Dr Shayo unaziona zimetulia na zinamwelekeo fulani, pamoja na ukweli makosa ya hapa na pale hayakosekani, na ndiyo maana kuna wakosoaji.
Ila hii, tena katika moja ya hotel za kitalii, ni aibu hata kwa wizara.
Hiyo ndiyo nchi yetu, halafu twalalamika eti mambo hayaendi au wanaajiriwa wageni!
Anoy Jan 27/ 1018hrs
ReplyDeleteKama nia ya kuweka tangao ni kuwa mtu akidhurika hotel isiwe liable, then tangao lingekuwa "The pool is being treated by chemicals, swim at ur own risk", otherwise, tangazo hili linamaanisha kuwa at that point of time, (mara nyingi after saa 12 jioni mpaka asubuhi), wameweka chemicals za kusafishia maji, so, mtu asiingie ku-swim, na tangazo lingekuwa hivi "The pool is being treated
by chemicals, please do not swim"...ila si unatujua wabongo, tutaswim tu labda meneja aje kutukataa, ukimkuta na meneja sio makini, atakuacha tu uswim ilimradi kibao kakuwekea
kwa nini wasiandike kiswahili?? unaandika kingereza wakati waswahili wengi hatujui kiingereza.... hayo ndiyo matokeo ya kutumia lugha ya watu. tujenge utaratibu wa kutumia lugha yetu hasa tunapokuwa ndani ya nchi yetu.. ni sisi wenyewe ndiyo n=tutakuza na kudumisha kiswahili chetu.. huyo jamaa aliyeandika bango hilo simshangai kuweka kingereza duni kwani wapo hata wazungu wengi hawajui kiingereza, and by the way english is just a language just like any other languages, knowing english does not mean that you know alot.... China, Japan, German, France etc dont speaks english and still they are making it...
ReplyDeleteTudumishe kiswahili ndugu zangu.
kwa nini wasiandike kiswahili?? unaandika kingereza wakati waswahili wengi hatujui kiingereza.... hayo ndiyo matokeo ya kutumia lugha ya watu. tujenge utaratibu wa kutumia lugha yetu hasa tunapokuwa ndani ya nchi yetu.. ni sisi wenyewe ndiyo n=tutakuza na kudumisha kiswahili chetu.. huyo jamaa aliyeandika bango hilo simshangai kuweka kingereza duni kwani wapo hata wazungu wengi hawajui kiingereza, and by the way english is just a language just like any other languages, knowing english does not mean that you know alot.... China, Japan, German, France etc dont speaks english and still they are making it...
ReplyDeleteTudumishe kiswahili ndugu zangu.
WEE 11:53:00AM NI MTOTO A KIJIWENI NINI? SI WATANZANIA WOTE WANAOJUA KISWAHILI LABDA TU KAMA UMEZOEA VIJIWE VYA DAR NA HAUJAWAHI KUSAFIRI MIKOANI. PIA UJUE KUWA KENYA NDIO WALIOWEZA KUTUNGA VITABU BORA VYA KISWAHILI KULIKO SISI, NA SIJUI KENYA IPI UISEMAYO NAJUA UMECHAGUA KENYA KWA SABABU UKO NYUMA YAKE KWA KILA KITU HIVYO UMEJENGA CHUKI BINAFSI. HATA HIVYO KWA TAARIFA YAKO KISWAHILI KILIANZA KWENYE PWANI YA AFRIKA MASHARIKI TOKA LAMU NCHINI KENYA MPAKA KILWA TANGANYIKA. PIA UJUE KISWAHILI CHA UJIJI SI SAWA NA CHA DAR. ACHANA NA VIJIWE KIJANA.
ReplyDeleteMBONA DAR WENGI WENGI WANAZUNGUMZA KISWAHILI KIBOVUKIBOVU ILI MRADI TU TUNAELEWANA LICHA YA KUWA NDIYO LUGHA TUANAYOITUMIA KILA SIKU KUKIJUI HILI UJUE DARASA BOVU.
ReplyDeleteMIMI LUGHA HAIJANISHANGAZA. NI KITU CHA KAWAIDA KWETU. WENGI SISI HIYO NI LUGHA YA PILI AU YA TATU.
ReplyDeleteKILICHONISHTUA NI HIYO PICHA YA DADA ALIYEKAA PEMBEZONI MWA BWAWA HILO LA KUOGELEA. MIGUU IPO NDANI YA MAJI INAONYESHA AMEOGELEA SASA ANAPUMZIKA KIDOGO AU ANAJIANDAA KUOGELEA. MBALI NA KUOGELEA JE NAMNA HIYO ALIVYOWEKA MIGUU NDANI YA MAJI, INA MAANA HIZO KEMIKALI HAZIWEZI KUMDHURU? AU WAHUSIKA WAMESHAMWELEZA KWAMBA HAKUNA KITU KAMA HICHO. TANGAZO LA ZAMANI?
Huyo dada na wengine wanoonekana kwa mbali miili yao ni chemical proof?
ReplyDelete"swimming pool notice: pool is being chemical please do not swim management"
ReplyDeleteanoy jan 27,12:50:00pm (aka teacher): "The pool is being treated by chemicals, swim at ur own risk", otherwise,"
"The pool is being treated
by chemicals, please do not swim"
mimi: the pool has been chemicaled
please do not swim...
haha! haha! haha! haha! haha! haha! hadi mimi nimekosea
haha! haha! haha! haha! haha! haha!
Waswahili kwa mawazo ya kimasikini hamjambo. eti US na Uingereza pia hawajui lugha zingine! Mwe!!! Ni kweli hawajui lugha zingine lakini huwezi kukuta wanang'ang'ania kutumia lugha wasisizojua. Watakachofanya ni kutumia lugha wanayoijua na kama wewe huijufahamu ni juu yako kuuliza. acheni kushabikia upuuzi.
ReplyDeleteMdau anonymous wed Jan 27, 10:09 AM na Mdau Wed Jan 27, 12:50PM msijifanye kujua.
ReplyDeleteMabwawa yote ya kuogelea lazima yawekwe kemikali fulani, ili waogeleaji wapunguziwe 'risk' ya magonjwa.
Hivyo hilo tangazo halieleweki kabisa maana yake, jambo la msingi ni kuwauliza menejimenti ya White Sands ambayo mameneja na wamiliki ni wageni, labda wametoka India, Italy au hata Kenya.
Hivyo huyo dada hapo hajaelewa kitu, Hoteli inaweza kushitakiwa kwa kuweka tangazo lenye utata kama kweli 'swimming pool is being treated with dangerous/hazardous chemical, please don't swim'
Mdau
Unguja.
"The pool is being chlorinated, please do not swim."
ReplyDeletekwanza kabisa nafikiri ili tangazo linausu watu ambao hawajui kiswahili kwanza ni kosa kuandika lugha ya nje pasipo andika lugha ya taifa angalia nchi za wenzetu kama Ujerumani,china ufaransa,urusi nakadhalika lazima waandike lugha ya taifa baadae ndio kingeleza si ajabu huyo demu hajui kingereza,msimlaum makosa ni hao wahindi
ReplyDeleteThe only chemical that should be going in there is chlorine! If they are pouring other chemicals in there, they should be investigated. Who deals with Pool standards in Tanzania? For a tourist class hotel, that sign is a disgrace.
ReplyDeleteMimi naona tangazo hilo pamoja na kuwa kiingereza kibopvu limewekwa masuksudi kuwazuia wapenda vya bure,jamani tusihahau tulikotoka ni wachache wanaofaidim namaanisha Mafisadi na waliowengi ndo wanasota na kupata taabu.
ReplyDeleteKuhusu lugha iliyotumika hapo juu labda jamaa aliandika akiwa na hasira mara baada ya kuona walala hoi wanaogelea bure.
Ukweli kuhusu lugha ilikuwa inataikiwa mambo yote yawe ktk kiswahili ambayo ndiyo lugha yetu na huwa namshangaa sana John Mashaka anapoandinda article zake kwa kiingereza na kuzimbandika ktk globu ya jamii,hivia anajuwa ni wangapi huwa wanaelewa kindani anachomaanisha.
Mwisho lazima tuelewe kuwa nchi zote zilizoendelea ki kweli kweli ni zile zinazotumia lugha zao na siyo kama sisi tunaotumia lugha ya mkoloni ktk mambo mengi muhimu. Tutaamuka lini sisi Watanzania?
Ha ha ha ha! Kaazi kweli kweli wote mmejaribu kiasi chake.
ReplyDeleteKabla sija comment lolote naomba nijenge hoja ambayo ni kama ifuatavyo: Hivi tunaiita Taulo pale tu inapofungwa kiunoni?au sehemu ingine yoyote ya mwili? je ikifungwa kichwani tutaiita kilemba au tutaendelea kuita taulo? Teh teh teh!
Je, pool tunaiita pool pale tu inapokuwa na maji au pale ambapo hakuna maji ndani yake? Au management walimaanisha pool, lile game ambalo wengi tunalicheza kila siku? Lakini nadhani hawakumaanisha hivyo kwa sababu katika pool table hakuna kuogelea hapo!
So,ni dhahiri kabisa ili mtu awaze kuogelea (ku-swim) ni lazima kuwe na maji. Kwa maana hiyo kinachowekewa chemical ni maji na sio pool. Mpo hapo!
Basi ingesomeka hivi: The water in the pool is being treated by Chemicals, swim at ur own risk!
Mpo hapo?
Ankal usinibanie comments zangu!
Mdau, Kichali
Kama sikosei swimming pool zote lazima ziwe na chlorine ili kuua vijidudu ambavyo watu wengi wanasambaza aidha kwa kutochamba vizuri ama kutochamba kabisa.Hivyo basi hiyo chlorine inazunguka ndani ya system ya pool ambayo ni mzunguko kutoka kwenye mashine za kusafisha maji na kurudi tena na siyo hatari kuogeleakwani hakuna point ya kuweka tangazo mchecheto.
ReplyDeleteMimi naungana na wachangiaji wengi, kuwa sasa umefika wakati sheria itumike kwamba lugha ya matangazo iwe ni kiswahili kwasababu ndiyo lugha yetu.Kama wengi waliowahi kwenda nchi mbalimbali duniani; watakubaliana nami hutakuta wenzetu wanatangaza kwa lugha isiyo lasimi kwa nchi hiyo.Matangazo yao yako kwa lugha yao inayotumika nchini humo;wewe mgeni kama hukuelewa uliza.Wataalamu wetu wengi wamesomeshwa kwa kutumia lugha za nchi walizokwenda kusoma:-Kirusi, Kichina, Kiingereza,Kifaransa,Kiaarabu,Kijerumani na kadha wa kadha lakini wanaporudi Tanzania wanautafasri utaalamu walioupata kwa lugha ya kiswahili ambayo ndiyo lugha yetu ya taifa.Hivyo basi isiwe taabu kwa kuwaambia hata hawa wawekezaji kwamba lugha lasimi Tanzania ni kiswahili na matangazo yao yawe kwa lugha ya kiswahili.Tangazo lisiloeleweka halina maana kwani ujumbe utakuwa haukueleweka, ndiyo maana tunamwona huyo dada yetu kaning'iniza miguu yake ndani ya hayo maji yenye kemikali.
ReplyDelete"NO SWIMMING PLEASE, THE POOL IS UNDER THE INFLUENCE OF ALCOHOL"...HA HA...HA HA...Jamani ngoja tuongee ukweli...kama hamuwezi lugha za watu acheni tu ili msionekane malimbukeni. Ningekuwa HR manager huyo jamaa kingeota ndago...bahati yake...!! Kwanini usiulize watu kama ina-sound right? Utakuta huyo ni msomi aliyemaliza Mlimani..jamani...!! Labda nikusaidie kidogo ili next time usiaibike mimi ningeandika hivi...!!
ReplyDelete"No swimming please, the pool is under chemical treatment" Management.
Simple and clear...!!
Mdau-USA
Hii ni style nyingine ya uongeaji wa Kiingereza..Mngekuwa mnaelewa Eight Form of be wala msingeanza ubishi wa kujiweka chini Ki-Lugha...Hapa mwandishi hajakosea chochote ila muonaji na mapungufu yake ya Kiingereza ndio anaona hivyo.
ReplyDeleteTatizo tuna fanya Direct Translation toka maandshi ya Kiingereza kuja Kiswahili ndio maana mnaona huyu mtu kakosea, Katu Hajakosea..Hapo ana maana The pool is being treated chemically or he can say the Pool is being chemical(ila inaweza kuwa makosa kusema the pool is being chemicalled as no such wording ass chemicalled)
Mwalimu wa zamani wakati wa Ukoloni
Mzee wa Songo Mbingo
Ughaibuni
Uingereza
There is Eight form of be, yaani Be, Being, been, was ,is, am ,are na were...Mkijua hizi hamtakosoa huyo Muandishi tena yuangea Kiingereza maridhawa kuliko nyinyi mnomkosoa hapa
ReplyDeleteAcheni kutetea mambo yasiyostahili, hili ni bango la Tangazo muhimu ktk eneo la kitalii.
ReplyDeleteLirekebishwe haraka.
Our official Gov`t and Buss language are Swahili na English. Official .
http://www.tanzania.go.tz/
PLEASE DONT SWIM IN THE POOL, THERE IS CHEMICAL.
ReplyDeleteTHE POOL IS CHEMICALLY TREATED, SO PLEASE DONT SWIM IN IT.
CHEMICAL IN THE POOL, PLEASE DONT SWIM.
THE POOL WAS RECENTLY TREATED BY CHEMICAL, PLEASE DONT SWIM.
that's just poor management. we need more business schools in tanzania. hicho kiingereza hata mtoto wa kidato cha tatu anaweza kuona kosa. hakuna cha kutetea lugha wala nini.
ReplyDeleteWWAAAW, LENGO NI UJUMBE UFIKE NA UELEWEKE HAPA INAONYESHA HATA WATOTO KUMBE WAMEELEWA NINI MAANA YA HILO TANGAZO, BIGUP WATZ
ReplyDelete