Mkurugenzi wa Masoko-TBL Bw. David Minja (wa 3 toka kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Yanga Bw. Lawrence Mwalusako jezi mpya ya timu ya Yanga kwa ajili ya kuzitumia katika mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom ikayotimua vumbi tena terehe 16 Jan 2010. Huu ni udhamini wa TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager tangu mwaka 2008. Katikati (shati la mistari bluu) anaonekana Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.
Mkurugenzi wa Masoko-TBL Bw. David Minja (wa 3 shoto) akimkabidhi Katibu Mkuu Msaidizi wa Simba Bw. Mohamed Mjenga jezi mpya ya timu Simba kwa ajili ya kuzitumia katika Mzunguko wa pili wa ligi ya Vodacom. Udhamini wa TBL kupitia bia yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa timu hizi kongwe, ulianza rasmi tangu mwaka 2008. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkurugenzi wa Utawala na Uanachama wa TFF, Mtemi Ramadhani, na a kulia kabisa ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. washatupa fyekeo la kumfyekelea mbali HAYAWANI wa mikumi, manyara na kwingineko. nani hapendi kuwa yanga bwana!!!!

    ReplyDelete
  2. kwani huko tanzania timu ni mbili tu?harafu ooooooh maximo hafai mnazipa promo timu mbili?wachezaji watapatikanaje kama mambo ndio hivi.kumbukeni wachezaji walikua wanatoka mikoani

    ReplyDelete
  3. i wonder why our country since independence we never been in any international tournaments(football) ????????????? this question i am sure no nobody can answer it although since i was born nasikia simba na yanga wanaupiga But whats results from that nothing except majungu and imani za ushirikina... i remember match between Simba and Al-ahaly in mwanza people shouted ohoooo wachezi wa simba waliona kundi la nyoka uwanjani ndiyo maana tulifungwa!!!!!its really utopia which most of the people in our country still believe on that... .. i wonder why our fellow African countries they believe in uchawi but they are doing better in soccer"""""i just admire our neighbors countries like Malawi,Zambia,Msumbiji even Burundi and Rwanda , countries suffering in civil wars like Angora manage to create presentable national time within short period of time ,we peace country in Africa with population of 35 million people rich in minerals ,wonderful climate and geographical position with stable political system since independence and other many factors... the question in that why we are always behind.....??????????????????????????????????the country with such population we don"t have any STAR to be proud with i saw some pictures here how people keeping msululu to get autograph from the guys of Ivory cost it is so impressive to our young generation but is to pain to see that no any Tanzania in international list.
    Ohooo dear brother and sisters since independence we failed to create at least one Stars(Tukaeni chini tujiulize kwanini maisha yote sisi tuko nyuma ya watu wote lini nasi tutaweza kujigamba mbele ya wenzetu """angalia huyu huyu ni Mtanznia anacheza ligi champion...watu wanazaliwa mpaka unazeeke mambo ni yale yale simba /yangu .....
    Mdau wa Kanyigo(Dr.)

    ReplyDelete
  4. Naungana na anony wa Tarehe Thu Jan 14, 04:34:00 PM, HIVI ligi kuu ya Bara ina timu mbili tu? Hii si sawa na nikuendeleza kudumaza mpira wa tanzania. Naelewa TBL mko kibiashara zaidi na biashara ni matangazo na ni kweli simba na yanga ndio zina mashabiki wengi kwa hiyo ni rahisi kwenu kutangaza bidhaa zenu kwa timu hizo. Lakini ifahamike kuwa ligi kuu ina timu nyingi na zipo nyingine pia zawezatumika kwa staili hiyo, kwa mfano Mtibwa Sukari, Polisi etc...

    Ni mtazamo tu

    ReplyDelete
  5. Wachagaa kwa pombe.. yaani hata kwenye madaraka ya kampuni za bia wapo wao.. Kavishe, Minja, Kileo, Masawe (Finance manager TBL arusha).. hii fani yenu kweli kweli

    ReplyDelete
  6. at least namuona jamaa yangu mtemi ramadhani wa dodoma, shule ya msingi uhuru, dodoma sekondari, alifuatia nyayo za hassan gobos,mohamed o. nyange, ali mwanoga,mohamed saleh,athmani matata. central sekondari alitoka lila shomari

    ReplyDelete
  7. mimi naona soka la tanzania halikui kwa sababu kuna timu mbili tu ambazo mnazijua ukienda timu ya taifa wachezaji wengi ni yanga na simba jamani tuacheni huu usengelema ili tukuze soka letu la tanzania ongeleni sana Azam FC kwa mfumo wenu waundeshaji wa timu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...