Picha za Utiaji saini wa kitabu cha maombolezo kufuatia msiba wa Simba wa Vita Mzee Rashidi Mfaume Kawawa katika Ubalozi wa Tanzania Umoja wa Mataifa.

Mhe Daniel Antonio, Balozi wa Msumbiji akitoa salamu zake za pole na kueleza kwamba Mzee Rashidi Mfaume Kawawa atakumbukwa kama kiongozi aliyekuwa na msukumo wa aina yake na kielelezo sahihi kwa vijana wazalendo wa Afrika na mpigania uhuru

Balozi wa Finland katika Umoja wa Mataifa, katika salamu zake za rambirambi amemwelezea Mzee Rashid Mfaume Kawawa kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Tanzania Mpya na yenye maendeleo na kwamba urithi na kazi kubwa na nzuri aliyoiasisi haitasahaulika.

Balozi wa Japan katika Umoja wa Mataifa, Mhe. Yukio Takasu, akitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha Mzee Rashid Mfaume Kawawa

Balozi wa Uganda katika Umoja wa Mataifa> Mhe Rukahana Rugunda ambaye katika salamu zake alimwelezea Mzee Rashid Mfaume Kawawa kuwa alikuwa kielelezo kikubwa cha utaifa na Umoja wa Afrika na ambaye hata siku moja hakuwahi kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, TANU, CCM, Tanzania na Afria. " Rashid Kawawa jina lako litaendelea kudumu".

BALOZI WA LIBERIA BI MARJON KAMARA AKISHIRIKI KATIKA UTOAJI WA SALAMU ZA POLE NA KUOMBA KWAMBA ROHO YA MWANAMAPINDUZI NA MPIGANIA UHURU, MZEE RASHID MFAUME KAWAWA IPUMZIKE PEMA PEPONI
Wow kumbe Marjon Kamara ni Balozi wa Liberia UN? How nice. I know Her Excellency. She used to be the UNHCR Representative in Dar miaka ya 1997 hadi 2000 kama sikosei. That time I was working in the Ministry of Home Affairs, Refugee Department under the able leadership of Mama Judy Mtawali. Interestingly how time flies. Michuzi humkumbuki huyu mama? Wakati ule tulipoenda kwenye ziara ya Mandela kule kambi ya wakimbizi wa Kirundi Lukole Ngara? Na wewe ulikuja kutoka Daily News to cover the event. Then tukapanda kale kadege ka UN tukiwa na huyo mama kwa masaa 4 angani kuja Dar. Unakumbuka? Maana kale kadege ukitaka kwenda msalani ilikuwa haiwezekani. Unakumbuka ile trip? Masaa manne non stop from Ngara to Dar. Tukafika tumechoka kweli. Hahaha. Au ninachanganya aisee. Wewe ulikuja ya Mzee Nyerere au ya Mandela? Na Juma Dihule alikuja ya Mandela? Aha whatever the case in bothe events huyu mama ndiye alikuwa UNHCR Representative.
ReplyDeleteBila shaka mdau uliyekumbusha hiyo safari ni Mh. Patrick Tsere maana kwenye kadege kale tulikuwa watano mie, wewe ,Mama Mtawali, Mh Kamara na pilot. Halafu huhjakumbusha jinsi Mwalimu Nyerere ilipombidi adandie kandege kake kwa kukanyaga mbawa. Ilisisimua sana kumuona Mwalimu akiwa mkakamavu. Pia unakumbuka wakati wa kurudi rubani toka Ethiopia alitupoteza angani baada ya luacha njia kwa kukwepa mawingu mazito. Nakumbuka mkuu
ReplyDelete