choo cha haja kubwa na ndogo hoteli ya beachcomber jijini dar
Ankal habari za sikukuu ya mapinduzi,
Wikiendi iliyopita nilitembelea hoteli hii ya beachcomber iliyo katika ncha ya ufukwe wa kaskazini wa jiji la Dar na kujikutia maajabu ya mwaka. Choo cha hoteli hiyo hakina 'privacy'hata kidogo kati ya wanaoenda SMALL NEED na BIG NEED.
Yaani vyoo vyote viko pamoja, hivyo ukiingia kupiga nanihii kubwa halafu akaja anayepiga nanihiiliu ndogo wote mnatazamana. Ama kwa kutaka staha inabidi ufunge mlango wa kuingilia sehemu hiyo kabisa. na hapo sijatamka jinsi vyoo vya kinababa na kinamama vilivyo ana kwa ana. yaani staha hamna kabisa. Kuuliza nikaambiwa hayo ndiyo mapigo ya hapo. Hapa siju ni jukumu la mabwana afya ama watoa leseni. Wadau nisaidieni ila hii ni kali!
Jengine nililoliona ni huduma mbovu katika hoteli hiyo ambapo mabosi wa kidosi wananyanyasa sio wafanyakazi tu bali hata wateja. Nimejionea bosi mmoja wa kidosi akibishana kwa ujeuri na sauti ya juu na mteja ambaye aliomba muziki kuburudisha wageni toka nchi mbalmbali za afrika waliofkia hapo ambao waliomba wawekewe muziki unaoendana na nchi zao, na sauti iwe ya chini, wakati wanajipatia mlo wa jioni.
Bosi huyo wa kidosi akaja juu na kudai hana muziki anaohitaji na kama vipi alete yeye (mteja) kama anao. Tatizo halikuwa kuwapo ama kutokuwapo kwa muziki huo bali ujeuri wa huyo bosi wa kidosi ambaye alionesha wazi kudharau wateja wake hata akadiriki kusema muziki wenyewe nimewapa bure mnataka kusema nini sasa?
Mmoja wa wageni, ambaye alikereka na muziki huo, akainuka na kwenda kuuzima kabisa. Hebu fikiria, mgeni mwenyewe alikuwa balozi mzima toka nchi jirani!
Mdosi hakuonesha kujali na wala hakuwataka radhi wateja wake. Hii nimeileta baada ya kuona lawama nyingi kwenye mahoteli zinaelekezwa kwa wamatumbi kuwa hawana weledi. huyo mdosi tumwiteje?? Ni kipi hasa kinachompa kiburi huyo bosi wa kidosi???
Hapa sio bure, iko namna na wenye kuhusika mnaombwa mchunguze maana hata wafanyakazi wamatumbi, ambao wanachapa mzigo kwa weledi wa hali ya juu, walipohojiwa waliogopa hata kunong'ona kwa woga kuhusu huo ujeuri wa mabosi na mambo ya chooni (sijui wa nini). Mie nahisi kuna njama za kuipakazia Tanzania katika mambo ya kuhudumia wageni, na si ajabu huyo bosi wa kidosi ni mmoja wa maajenti wa hilo.
Iko haja Watanzania tukaamka sasa na kumaizi hilo na katu tusiruhusu vioja vya aina hii vya kuharibu sifa za nchi yetu viendelee, wakati wenyewe wanajificha nyuma ya pazia la ooohh 'Watanzania hawana weledi kwenye huduma' ambazo pamoja na udhaifu sehemu na sehemu lakini si kweli kwamba wote tumeoza. Mfano hai ni huo

Mdau wa Beachcomber, Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Vyoo vichafuuuuuuuu!!!

    ReplyDelete
  2. Beachcomber mbona ilishajifia siku nyingu tuuu.

    Huyo mdosi anaringa kwa sababu wana tender za dezo dezo kwa kutumia 10% kutoka kwa makampuni mbali mbali yanayofika hapo kutumia ukumbi wao.

    Ukizoea vya kunyonga vya kuchinja huwezi..!!

    ReplyDelete
  3. mleta maoni ni mbaguzi. kulikuwa na haja gani ya kutumia neno wadosi? ingekuwa mnyakyusa ungesema bosi wa kinyakyusa?

    ReplyDelete
  4. Kwani si kila mtu anajisaidia! kwani kuna aibu gani ukienda haja kubwa na mwenzako yuko pembeni anaenda haja ndogo?

    Kama ni kujamba kila mtu anajamba, kama ni harufu kila mtu anatoa harufu, hakuna anayeenda haja kubwa akatoa marashi.

    Tusitake kuoneana aibu kwa vitu ambavyo kila mtu anafanya

    ReplyDelete
  5. Tatizo kubwa la kila kitu ni "RUSHWA". Naam! nasema kwa kujiamini kabisa, niliwahi kufanya kazi kwa mdosi mmoja ana magari ya kusafirisha mizigo pale nyuma ya Legho, huyu bwana alikuwa na orodha ya maafisa wa polisi, halmashauri ya manispaa ya kinondoni ambao wapo kwenye payroll bila kuwa waajiriwa. Jamaa alikuwa anakiburi we acha anakwambia atakufukuza kazi bila kukulipa chochote na popote utakapoenda wewe ndiyo utakuwa loser.

    Sasa si ajabu kiburi cha huyu MUHINDI WA BEACHCOMBER kinatokana na kuwepo na watu wazito kazika maamuzi ya kufuatilia sheria na usafi nyuma yake wanaompatia kiburi hicho. Au huenda kuna kigogo wa serikali ana hisa kubwa tu hotelini hapo ila anamlinda.

    Tunatikiwa na transparency katika biashara hizi ili kukomesha uozo kama huu. Nina hakika kuwa mabwana afya wanajua fika kuwa vyoo hivyo havistahili kwa matumizi ya binadamu kwenye hoteli ila watakuwa wapo kwenye payrol ya MUHINDI HUYU

    ReplyDelete
  6. watanzania kwa maoni ya kibaguzi hawajambo, oh bora tulete watu toka Kenya, India au Ulaya ndio mambo yataenda vizuri!

    Bora tukazanie matumbis,wamanga na wadosi wetu watanzania kuifanya Tanzania Kwanza, sio kupendelea vya wageni , oh wachina wakitengeneza maziwa ya watoto yenye sumu- 'bahati mbaya', ila tunayofanya watanzania(wamatumbi, wamanga na wadosi) kelele nyingii, kwanini lakini hatujipendi ?
    Mdau
    Tanzania Kwanza

    ReplyDelete
  7. Wewe unayesema kuita mdosi ubaguzi unachemka, kwani unajua maana ya mdosi wewe? niambie mdosi lina maana gani mbaya? unajistukia tu ndugu yangu,inaonekana wewe ndo mbaguzi!unataka aitwe Mhindi sio, jina la bara lake, na mtu kutoka Yuropa akiitwa mzungu naye alalamike sababu halijatumika jina la bara lake? Mtanzania akiitwa mmatumbi naye alalamike? Acha hizo!!

    ReplyDelete
  8. Mdau ni vizuri umetoa hoja na ushahidi maana ukiwaambia wabongo wanasema hizo 'chuki' na mnataka kuleta 'machafuko'! na huo ni utangulizi tu, subiri sasa kimbembe cha kilimo kwanza ambapo wakulima huko vijijini watakapogeuzwa kuwa vibarua katika mashamba waliyowahi kuwa wamiliki!!! maisha bora kwa kila mbongo.
    mlalahoi
    kwa mfugamafisadi

    ReplyDelete
  9. ankal mi naona jamaa hayuko fair katika maelezo yake kwa sababu moja kwa moja kama alivosema mwenyewe ametaka kuonyesha uovu wa watu wengine ambao sio wamatumbi.
    Kwa jinsi alivoeleza kesi yake haiingii akili kwa mdosi huyo kujaa juu eti kwa sababu ya muziki tu.
    cha muhimu katika kesi kama hizi na wewe ankal uvamie na upande wapili ufanye nao mahojiano kisha ulete kwenye blog yetu comments kutoka pande zote mbili sio pande moja.
    Haya yalijitokeza karibuni kwa muheshimiwa waziri fulani ambaye imedaiwa kumjibu maneno machafu mlinzi moja kama alivosema huyo mlinzi katika chomba fulani cha habari.
    ili kuwa fair inabidi tupate comments za pande zote mbili.

    ReplyDelete
  10. "ILI TUENDELEE,
    TUNAHITAJI VITU VINNE,
    WATU,
    ARDHI,
    SIASA SAFI,
    NA UONGOZI BORA."

    sikamoooo.....!!! mwaaaaalim....!!!

    ReplyDelete
  11. Jamani wadau wenzangu hivi mnajua nani ni muhimu katika hoteli na anapaswa kuheshimiwa bila kujali ni mkorofi, hana cheo chochote wala pesa. Ni mteja sasa kama huyo mdosi anajiona muhimu kushinda wateja ndio amewakimbiza na sifa mbaya huvuma fasta kushinda nzuri

    ReplyDelete
  12. Nakubaliana na comment ya kwamba " vyoo ni vichafu mno". Nilikuwa mmoja wa wanawake viongozi wa maziwa makuu na nilijionea hali hii lakini nilitoa taarifa hapo reception. Msichana aliyekuwa anasafisha alielezwa na alikuwa na kiburi surani ! Nilimkuta mchana kwenye vyoo vya ukumbini na hali ilikuwa hiyo hiyo pia. Alikuwa anacheea maji kwenye sink la kunawia bila kujali hali ya unyevunyevu, alama za viatu vichafu na mikojo iliyotapakaa kwenye makalio ya vyoo.
    Hata kiwango cha chakula hakiridhishi pia.
    Kwa kweli hoteli imeshuka standards ! Sio siri.

    ReplyDelete
  13. NYIE ENDELEENI KUFURAHIA MTAZARAULIWA MWISHO KWENYE HOTEL MTALETEWA VYOO VYA SHIMO.

    ReplyDelete
  14. hiyo haijawahi tokea wala sijawahi kuona...kama huyo mdosi ndio maana basi amekuwa hana adabu ..uwezi kuweka haja kubwa na ndogo sehem moja...ata angekuwa mwarab..mzungu..mzaram mnyakyusa hiyo ujue sio wala hakuna ata mtoni huku ...haijawahi tokea...ya nn kueka vyoo ...inabidi wateja ingie mitini katika hotel za kukosa heshima kwajamii...wasilete aib kwa taifa letu zima...michuzi usiitoe hiyo picha mpaka arekebishe vyoo..na utuwekee akiwa amefanya jinsi ubinaadam ulivo..one love

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...