Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Marehemu Balozi Daudi Mwakawago wakati wa mazishi ya Mwanasiasa huyo mkongwe yaliyofanyika katika makaburi ya kisutu jijini Dar leo
akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Seif Shariff Hamad wakati wa mazishi ya mwanasiasa mkongwe na mwanadiplomasia Marehemu Balozi Daudi Mwakawago yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar leo jioni.Katikati ni Rais Mstaafu awamu ya Tatu Mh. Benjamin William Mkapa.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. NAMUONA MKAPA, WARIOBA, SALIM. KIKOMO CHA UTAWALA CHA MIAKA KUMI KWA RAIS, YAANI VIPINDI VIWILI KWA MAONI YANGU NI KIZURI KWA NCHI ZILIZOENDELA, KWA NCHI MASIKI SINA UHAKIKA SANA KAMA INAFAA, NAPIGA PICHA MKAPA ANGETAWALA FOR 20 YEARS TUNGEFIKA MBALA PAMOJA NA WIZI ULIOTOKEWA KATI MAANGALIZI YAKE LAKINI NCHI ILIKUWA INAENDA MBIO KIMAENDELEO KATIKA AFRIKA MASHARKI SINA UHAKIKA SASA TUNAENDAJE!!!!!!!!! IT REMAINS TO DEBATE

    ReplyDelete
  2. WEWE MCHANGIAJI HAPO JUU UNA MAANA GANI UNAVYOSEMA VIONGOZI WATAWALE MIAKA 20.AU WEWE NI MJUKUU WA MKAPA.

    ReplyDelete
  3. Lahaula hivi kiswahili bado kigumu kwa wengine kiasi hichi ?huyo mtowa wa hapo juu kwa mtazamo wangu anamanisha Maraisi wawepo madarakani miaka 20 nafikiri hata uchaguzi usikuwepo mpaka fike 20

    jo

    ReplyDelete
  4. MIMI NINGEPENDA KIONGOZI AMBAYE ANAONYESHA KAZI NZURI KATIKA MIAKA MITANO APEWE MIAKA MITANO MINGINE.NA ANYEFUATA APEWE FIMBO KUWA HII KAZI NZURI ALIYOIFANYA KIONGOZI ALIYEPITA HISIARIBIWE,ILA WEWE UNAKUJA NA KIPI KIPYA ILI NCHI ISONGE MBELE.SIO HUYU KIKWETE KAJA NA MPYA ,SIJAWAHI KUONA KATIKA SERIKALI ZA AFRIKA.SERIKALI YA TANZANIA HAINA PESA NA INAONGEZA UKUBWA WA MATUMIZI YA PESA [WABUNGE WENGI,NA MAKATIBU WABUNGE WENGI,MANAIBU WABUNGE WENGI].HAPO INAONYESHA HUYU RAIS NI MTU WA MATUMIZI TU.WATANZANIA,TUNATAKIWA ATUAMBIA AMEWEZA KUINGIZA KIASI GANI CHA PESA.NANUKUU MARA ULIPOPATA URAIS WAKO NDUGU MRISHO ,ULIFIKA HAPA WASHINGTON DC,NA UKAJIGAMBA KUWA UNAMSIFU MKAPA KWA KUKUACHIA PESA NYINGI KWENYE HAZINA .NA UKASEMA KUWA SASA MIMI NATEMBEA KIFUA MBELE.WATANZANIA TULIOKUWEPO PALE WOTE WATAKUBALIANA NA MIMI.TUNAYO VIDEO YAKE KAMA ATAKATAA.HATUNA MCHEZO SASA HIVI.NDUGU RAIS WEWE NI RAIS WA MATUMIZI ,SIO RAIS WA KUIJENGA NCHI.NAOMBA HUTUPE TAKWIMU YAKO YA PESA HUKO HAZINA ULIKUTA SHILINGI NGAPI,AU DOLLAR NGAPI NA SASA WEWE UMEONGEZA KIASI GANI?WATANZANIA TUNATAKIWA KUMJAJI MTU KWA MAKINI SANA SASA.MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WENYE BUSARA YA KUISONGEZA NCHI MBELE.NAKUSIFU RAIS SHUPAVU KAGAME TUNAONA HUKU ANAESHIMIKA SANA,NA VILE VILE NAKUSIFU MKAPA SANA,INGAWA KUNA MATATIZO MADOGO ULIYAFANYA,LAKINI YOU ARE THE BEST.MUNGU AKUBARIKI PIA.TANZANIA IMESIFIKA HUKU NJE SASA NI KWA AJILI YAKO.SASA HIVI HUYU KIKWETE NI SIJUI AME AKAMPLISHI NINI?KUTEMBEA NJE KULIKO MARAIS WENGINE,KUINVITE MANY LEADERS TO COME TANZANIA.UNAJUA NDUGU KIKWETE UNATUMIA PESA ZA WANANCHI KUWAINVTE VIONGOZI KUJA HAPO.NCHI YETU NI MASIKINI TAZAMA MBELE.TUTAONDOA KINGA YA RAIS KUSHITAKIWA HAPO BAADAE ILI KUWASHITAKI VIONGOZI WOTE WALIOTUMIA MADARAKA YAO VIBAYA.KAMA INVYOTOKEA KWA AKINA YONA NA MRAMBA.MDAU WASHINGTON DC,MAPAMBANO YATAENDELEA TU MPAKA TUTAPATA KIONGOZI WA WATU.

    ReplyDelete
  5. Roho inakuuma sio kwa JK kuwa Rais? Wewe piga kelele kwa herufi kubwa huku kwenye bllogu weee mpaka mate yakutoke, eti Mkapa angekaa miaka 20 nchi ingefika mbali, hivi hata huku kuanguka kwa uchumi wa dunia angekufanyaje? Kauza migodi yote kwa wazungu, mnapiga kelele, watu wamekula pesa za EPA mnapiga kelele, au nyie ndio wale kina "shemeji" mliokuwa mnanufaika wakati wa Mkapa kwa kutuibia maana wizi ni jadi yenu. Alileta sijui nini Solutions badala ya kusaidia Tanesco ndio ikaiua kabisa.

    Kama ni kuhusu barabara nyingi alizikuta tayari zina pesa mfano mdogo barabara ya kusini na daraja la Rufiji pesa zake zilikuwa zimekwishatafutwa na Mzee Mwinyi na alikuta misingi ya daraja imeishawekwa. Kulikuwa hakuna mtu anayeweza kufungua mdomo wake, leo mmepewa uhuru wa kusema mnachonga.

    Haya niambie huko unakojidau uko huko Marekani uchumi wake haujatetereka? Ni nchi ngapi duniani kwa kipindi hiki cha miaka mitano uchumi wake umekuwa kama ilivyokuwa planned.

    Tunajua kuwa huyu JK mtamsakama kama mlivyosakama Mzee Mwinyi enzi zile, ooh nchi inakwenda hovyo, ooh sijui anaipeleka nchi kubaya, ooh anafanya biashara Ikulu. Kumbe masikini mzee wa watu wala hakuwa anayafanya hayo, ila udini wenu ndio uliozalisha propaganda za ajabu kwa Mzee Mwinyi. Na alivyoingia Mkapa mpaka Migodi kanunua, kajilimbikizia mali, kafungua Benki, hakuna mtu aliyefungua mdomo wake kwa kuwa yeye ni haki yake kufanya hayo.

    Sasa historia inajirudia tena kama wakati ule, hakuna lolote la maana mnalosema sasa kuhusu JK zaidi ya chuki, chuki kwa kuwa tu yu Muislam, hata afanye nini kwenu hamtaliona kuwa ni jema.

    NIMEISHAPASUA JIPU PWAAA! maana tumeshawachoka sasa, kaombeni mkalale!

    ReplyDelete
  6. wewe unasema mkapa kaondoka kaacha hela so,kawacha madeni mengi sana pia,mfano mzuri ni barabara ya dodoma morogoro,ile imelipwa na serikali ya JK, japo mkapa ndo aloizindua kwa mbwembwe,wastaafu east africa wamelipwa na JK,MADENI YA WALIMU BILIONI 350 ZA SERIKALI YA MKAPA ZIMELIPWA NA JK.JK ameunyanyuwa uchumi wa tz kwa muda mfupi sana,ameingia madarakani tz inakusanya bilioni 190 kwa mwezi,leo katika maka minne,inakusanya bilioni 398 kwa mwezi,ukiangalia amefanya mabo ya maana sana,sema hamutaki kuona,chuo kikuu dodoma(UDOM) ni cha kisasa chenye kumuwezesha mtoto wa kitanzania kusoma vizuri,kitapoisha kitakuwa one of the bigest university kwa tz,machinga complex zimeisha,ule ndo uwekezaji unaotakiwa kwa wa tz,ingekuwa mkapa pesa ya kujenga uwanja wa taifa angejenga machinga complex zaidi ya nne,angalia leo shule za kata,tz ya leo ni shule chache mno kukuta ziko hoi kimajengo,zamani 76% ya shule zilikuwa hoi kimajengo,benki ya wanawake pia ni score nyengine ya JK,mambo yako mengi tu,sema magazeti siku hizi udaku mwingi,wakati JK ndo amewapa uhuru wa vyombo vya habari.mkapa alileta maendeleo,lakini na uhakika JK akimaliza miaka 10 atakuwa na score kubwa sana kufananisha na mkapa.

    ReplyDelete
  7. nimefurahi sana jamaa mlivyomjipu,kuna watu wanashikilia mkapa aliipeleka nchi kwa speed,ukiwauliza maendeleo watakwambia barabara,kamoon guys,sasa mtu ameingia na kuuza benki zote kwa makaburu,mashirika ya umma yote pia,ziwanda vyote,madini,ukiangalia mzee mwinyi alikuwa ameshapitisha sheria ya vyombo binafsi,so utekelezaji ulianza 1995,zikaanza tv binafsi,magazeti na redio,kauza nyumba za serikali,hivi hayo ndo maendeleo au kuzidi kumuumiza mtanzania wa chini,now madokta hawana hata nyumba za kukaa,kila dokta atafute nyumba mwenyewe,mererani watz walikuwa wanatajirika kule,mkapa kawapa makaburu ili serikali ipate kodi,haangaƦii upande pili,mererani leo watu wameloose hope,alafu lawama anapewa JK hajawafukuza mkaburu,hivi watz hawajui mkapa alisign nini humo ndani.

    ReplyDelete
  8. mama wa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Zitto Kabwe ametangaza kuwa hakuna mtu yeyote mwenye kufaa nafasi hiyo hivi sasa.

    Mama huyo, Shida Salum, ambaye ni mwenyekiti wa walemavu, alitangaza kumuunga mkono Kikwete juzi kwenye viwanja vya Temeke, jijini Dar es salaam, alipokuwa kwenye mkutano wa Aman Forum.

    Alisema Rais amefanya kazi nzuri ya kuimarisha amani na kuwatetea walemavu hivyo ni vema Watanzania wakampa fursa ya kuongoza kwa kuwa wanasiasa waliopo hivi sasa iwe wa CCM au wa vyama vya upinzani hawajafikia viwango vya kuwania urais.

    “Ninasema hivi; hakuna mtu anayeweza kuwatetea walemavu kama Rais Kikwete, amewakamata wauaji wa maalbino, na sasa anatutetea zaidi, kura zote za urais ni kwa Rais Kikwete, wapinzani watapata za ubunge tu!” alisema.

    Aliongeza kuwa wapinzani wanapaswa kujiandaa kumsimamisha mgombea urais mwaka 2015 ili kuepuka matokeo mabaya wanayoweza kuyapata iwapo watamsimamisha mgombea wa urais ili kukabiliana na Kikwete.

    Mkutano huo ambao uliongozwa na Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Walid Aman Kaborou, na pia kuhudhuriwa na wajumbe kutoka vyama vya Tanzania Labour (TLP) na NCCR- Mageuzi, limewashambulia viongozi wa Taasisi ya Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF) kuwa ni wachochezi.

    Akizungumza kwenye mkutano huo uliohudhuriwa na watu wachache, Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, alisema amejiunga na taasisi ya Aman Forum, kwa sababu amegundua kuwa nchi ina tatizo hasa unapofikia wakati wa uchaguzi wa urais.

    “Kuna kundi la watu lina njama za kumdhuru au kumsambaratisha Rais Kikwete na serikali yake, wajue kuwa wakifanya hivyo hawatakuwa wamekidhuru chama tawala bali ni Watanzania wote, mimi nimeamua kujiunga na Amani Forum, ili sasa nitangaze vita na kundi hilo,” alisema Mrema.

    Mrema alibainisha kuwa ameamua kuitetea nchi na hajahongwa wala kununuliwa na mtu yeyote kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakimtuhumu.

    Aidha, aliwashambulia makada wa CCM na viongozi wastaafu walioshiriki kuchangia hoja katika tamasha la kumuenzi hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, lililofanyika katika ukumbi wa Karimejee mwishoni mwa mwaka jana kuwa ni wachochezi na wanatakiwa kukamatwa kwa sababu hawana heshima kwa rais wa nchi.

    “Kuna tamasha la Mwalimu Nyerere, makada wa CCM wamelitumia kama kichaka cha kuendesha uhaini hawa walinunuliwa; wamesema Kikwete amezungukwa na wezi, wanamtukana rais? Nyie CCM mnamtusi kiongozi wenu anayewapeperushia bendera?”

    Mrema ambaye aliwahi kuibua kashfa ya ufisadi wa kuibiwa kwa sh bilioni 900, ambayo ilimhusisha pia Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alisema katika miaka minne, Rais Kikwete amefanya mambo makubwa ikiwepo kuruhusu wasaidizi wake wajiuzulu, kwa kuhusishwa.

    “Hivi mnamtaka afanye maamuzi gani mazito, wakati amekubali rafiki yake aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa ajiuzulu? Serikali si imewajibika? Mnasema mtamtosa kwa kosa gani alilofanya Rais Kikwete?

    Mrema aliendelea kusema kuwa suala la ufisadi hata Baba wa Taifa alilishindwa kwa sababu baadhi ya viongozi waliokuwa wakifanya naye kazi walipohusishwa na ufisadi aliwahamisha au kuwaongezea majukumu badala ya kuwawajibisha.

    “Mwingira aliuza ndege ya serikali, mbona Nyerere alimhamisha na kumpa ukuu wa mkoa wa Arusha? Balozi Mustafa Nyang’anyi alinunua kivuko kibovu Mwalimu akampa ubalozi wa Marekani; Rais Kikwete amewapeleka watu mahakamani ninyi mnasema mtamtosa!” alishangaa Mrema.

    Mrema aliyekuwa amefuatana na baadhi ya viongozi wa chama chake makao makuu, akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Hamad Tao, aliendelea kusema kuwa hajanunuliwa, na Rais Kikwete, lakini atahakikisha anampigia debe ili ashinde urais Oktoba mwaka huu.

    “Watanzania tuache uongo, unafiki na uzandiki, sijanunuliwa na Rais Kikwete, mbona Seif anayempigia debe Rais Karume kuwa aongezewe muda hamsemi amenunuliwa? Ninasema kura zote za urais ziende kwa Rais Kikwete!” aliongeza.

    Naye Walid Kaborou, ambaye ni mwenyekiti wa taasisi hiyo, alisema wanaosimama na kusema kuwa Rais Kikwete atoswe wanazungumzia kazi ambayo hawajawahi kuifanya.

    ReplyDelete
  9. Katika matukio muhimu ya kitaifa marais wastaafu wanaonekana. Lakini kwa muda mrefu simwoni SALMIN AMOUR kujumuika hata katika vikao adimu kule Zanzibar vya kukubali mwafaka, huyu yuko wapi? Ni mtawa mkaa peke wa jangwani?

    ReplyDelete
  10. wewe mdau hapo juu mbona unatoa takwimu za uwongo.watanzania kwa takwimu sasa hivi wazungu wamewashitukia sana.nyie matonya wakubwa mnaovaa suti.tunataka kuona maendeleo yanaonekana sio takwimu ,kamati,utafiti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...