Ofisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando na Meneja Masoko wa Bilicanas Club, Samsonite Amosy (kushoto) wakioyesha kipeperushi kinachohusu wasanii watakaotoa burudani katika monyesho ya Sikukuu ya Valentine yatakayodhaminiwa na Tigo sehemu mbalimbali nchini katika hafla ya kutangaza vionjo vipya vya miito ya akupigiaye kwa kupiga 15050 na kuchagua kionjo maalumu kwa msimu wa Sikukuu ya Wapendanao ukiwa na Tigo iliyofanyika jijini Dar leo

Tigo imeamua kuonyesha mapenzi yake kwa wateja wote nchini kwa kuongeza huduma pekee kwenye huduma za miito kwa akupigiae itayowezesha wateja kujipatia nyimbo bomba kwenye simu zao ili kufurahisha wale wote wanaowapigia kuanzia msimu huu wa Valentine

Akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari Ofisa Uhusiano wa Tigo Jackson Mmbando alisema “Mwaka huu tumeamua kuonyesha mapenzi yetu kwa wateja kwa kuhakikisha kuwa wateja wote wanawezakuonyesha hisia zao kupitia huduma zetu za midundo bomba kwa akupigiae.

ili kupata midundo kabambe mteja wa Tigo anaweza kupiga namba 15050 kisha anachagua mwenyewe kwenye orodha maalum ya nyimbo za valentine ambapo orodha ya valentine itakuwa ya kwanza

ili wateja kufahamu nyimbo hizo vizuri zaidi tumeandaa mitoko mizuri kabisa (outing) ambazo itakuwa ni clab bomba sehemu mbali mbali ili mteja aweze kuomba kwa Dj kuburudishwa na nyimbo hizo live

Seheme zilizochaguliwa kutoa burudani ya Tigo Romantic Red Valentine msimu huu wa Dare s salaam ni Traveltine ambapo kutakuwa na Aramba! Aramba Valentine, kisha Club ya kimaifa Bilicanas wasanii Majoisy toka Uganda, na Kasimu Mganga watatumbuiza. Pia kutakuwepo na zawadi kabambe kwa wale watakaopendeza zaidi.

Moshi tunakutana Club Laliga na burudani ya muziki kabambe kutoka mwa maDJ maarufu pia Mwana FA wa Tanzania, Jua Kali na kikosi chake atakuwepo kutoka Kenya watatumbuiza, pia Sound of Sebene pamoja na Boda to Boda Dancers

Tanga kuanzia tarehe 12-14 Club la Vida Loca mambo yatakuwa ni shwari kabisa nyimbo maalum za valentine zitaporomoshwa na ma dj wakali kwa kupokea maombi maalum ya wateja na wapenzi wa burudani kwa kuzingatia chati yetu kali.

Mwanza The Stone Club iliyoko City Center kutakuwa na zawadi za kutosha pamoja na msanii maarufu wa kizazi kipya Diamond anatarajiwa kutumbuiza

Morogoro tunangia katia ukumbi wa makuti ulioko msamvu kwa burudani ya Disco kali baada ya Bendi maarufu ya mjini morogoro Moro Jazz kisha tutachagua aliyependeza sana na tutamzawadia zawadi kali itakayombatana na Valentine wine na kutakuwa na Red Rose kwa wapendanao zakutosha
Watanzania tunawaondoa wasiwasi kuhusu viingilio katika maeneo ambayo sisi tumeyadhamini itakuwa nafuu ili kila mmoja aweze kujitokeza na kuonyesha mapenzi kwa awapendao msimu huu wa Valentine 2010

Kutakuwa na zawadi maalum zitakazotolewa kwa watu 100 watakaongia wa kwanza kwenye sehemu zote za burudani zinazodhaminiwa na Tigo.

Kila wimbo utakaochaguliwa na mteja ataulipia shilingi 27 kila siku na shilingi 300 mara moja tu pale anapouchagua

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. hey hii club lavida roca tanga ipo wapi tena manake mie mtu wa kitanga najua Lacasa tu na last dec nilishuka Ta tika kiwanja lakini sijaisikia hii club ipo sehemu gani wanoijua next time nikishuka nikawakilishe mdau mgosi ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Ankal
    Leta news bwana na sio commercial hapa unless kama umeweka mkwanja ndani,shtuka

    ReplyDelete
  3. alamba,alamba hamm,ham nasema alamba alamba ham ham nasema alamba alamba tena ham ham! michu huko migomigo siku hiyo lazima aliye mtu sababu jahazi ni noma nawakubali viwanjo vyote nimeenda lakini nikifika jahazi hapo full roho inatulia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...