Mkurugenzi wa Bendi ya African Express yenye makazi yake nchini Japan Fresh Jumbe akiongea na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo leo kuzungumzia onesho lake atakalofanya kwa pamoja na bendi ya African Stars ya jijini litakalofanyika februari 5, mwaka huu kwenye ukumbi wa Land Mark hoteli iliyopo Ubungo jijini Dar. Wengine pichani ni Mratibu wa maonesho hayo Papaa Juma Mbizo, Mkurugenzi wa African Stars Da'Asha Baraka na Kiongozi wa Twanga Pepeta, Lwiza Mbutu


Fresh Jumbe amesema onesho lingine kubwa litafanyika kwenye tamasha kubwa la Sauti za Busara visiwani Zanzibar ambapo wanamuziki wenzie kutoka Japan wanatarajia kuwepo katika onyesho hilo kubwa atakalolifanya nchini kabla ya kufanya lingine mkoani Tanga kwenye ukumbi wa Habours Februari 26, kabla ya kurejea Japan.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. ahhhh!!!ankal hiiii poa sana!!
    fresh jumbe oyeeee!Twanga pepeta !!!! oyeeee!!!!
    watu wakuja ziiiii!kimyaaaa!!!!
    kamua kamua kamua Fresh,wakongo hawana pa kupumua

    ReplyDelete
  2. watanzania lazima tujivunie masupa staa wetu wanaitangaza miziki ya tanzania nje ya nchi

    ReplyDelete
  3. MRATIBU WA MAONYESHO HAYOOOOO PAPAAAAAAAAA JMA MBIZO THEEEEETHEEEE HONGERA JUMBE TUNAKUFUATILIA NA TUANAKUOMBEA UPATE NA MAPROMATA WA KWELI WATAKAO KUTOA.

    ReplyDelete
  4. Fresh Jumbe wewe wa ukweli!wakimbizeee!Aisha madinda yupo jamani? sikuwepo town.

    ReplyDelete
  5. Fresh Jumbe mbona sasa umevaa kofia ya winter wakati hapa joto kali?au unaona baridi kichwani

    ReplyDelete
  6. Jumbe wewe ndiyo tegemeo letu wabongo kwa wanamuziki wa bongo.
    Onyesha mfano wa kweli na uwape somo wote hao waliolala.
    BIG UP Jmbe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...