Rais Jakaya Kikwete akipokelewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita wakati alipowasili makao Makuu ya chama hicho Lumumba, Dar es Salaam, Leo Mchana. kuanza rasmi ziara yake ya siku tatu.

JK akisalimiana na wananchi. Chini akisalimiana na makada wa CCM
Tunaweza Jazz band ilikuwepo kutumbuiza




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. hii michuzi tunaomba habari zaidi juu ya Tunaweza Jazz band

    ReplyDelete
  2. Bwana Michu tafadhali uwe unaweza kutofautisha kazi maana kama nyie wana habari mnatuchanganyia sijui wa kawaida wataelewa vipi.
    Hapa inaonekana kabisa kuwa ni Mwenyekiti wa CCM anatembelea Mkoa wa Dar Es Salaam na sio Raisi wa Jamhuri ya Muungano.

    Haya ni mambo muhimu ambayo waandishi kama mdomo wa raia muweze kuwa makini na kuyafafanua.
    Kwa mfano hapa inatakiwa gharama zote za hii safari hii ukiondoa ulinzi na usalama wa JK kama RAis ziwe ni za CCM na sio serikali.
    Ni wajibu wenu kuhoji haya mambo muhimu na sio kushangilia tu kama raia. Kuna wakati JK alifanya kikao cha chama ndani ya ikulu na wote mkashangilia pia badala ya kuhoji.
    Mnatutia wasiwasi kabisa katika kazi yenu.
    Mdau

    ReplyDelete
  3. Michuzi bwana Muoga? Monica Luwinski na Clinton basi umeogopa Comment umebana. Joke tu, Kova haji humu sijui kama anajuwa kusoma Blog. Pazi.

    ReplyDelete
  4. Inabidi tuige wenzetu kwamba rais hawi mwenyekiti wa chama. Hapa JK karudia kuwa 'rais' wa CCM. Siku tatu hizo atakuwa anaimarisha chama wakati kuna mambo mazito ya Watz wote yanatukabili. Jamaa wa Kilosa wamerudia maisha ya kawaida?

    ReplyDelete
  5. Tangu kujengwa misingi ya Taifa letu wenyeji wa Dar es salaam waliipokea kikamilifu siasa ya Umoja wa Mwafrika(TANU) na baade siasa za Mapinduzi ya Maisha ya Mtanzania na Mwafrika.

    Ndugu Mwenyekiti Kikwete Hongera kuendeleza hamasa na moyo huo.

    Dar es Salaam leo inanufaika kwa makazi na huduma ya karibu kila mzaliwa wa mkoa/wilaya za Tanzania nzima. Mapokezi haya mazuri ni ISHARA ya kukubalika na kuungwa mkono na wananchi wengi Tanzania nzima.

    CCM tawi la UK linawapongeza wana Dar es salaam wote na tunaamini mtamshirikisha Mwenyekiti Kikwete kikamilifu.
    MAPINDUZI DAIMA

    MAINA ANG'IELA OWINO
    CCM UK

    ReplyDelete
  6. Hongera sana TUNAWEZA JAZZ BAND. Mnatupa matumaini kuwa kweli penye nia pana njia na WOTE tukidhamiria tunaweza kulijenga TAIFA letu ilhali yeyote mbele yetu.

    Hongera sana.

    MAINA A OWINO.

    ReplyDelete
  7. hakuna chama kingine kama CCM hiki ni chama imara kitaendelea kudumu kwa mda mrefu sana na ziara ya jana haijapata kutokea

    ReplyDelete
  8. CCJ isipime mziki wa CCM kwani CCM iko JUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  9. Prof. OtienoFebruary 05, 2010

    Sepna, Maina that is too low!

    Michuzi huwezi kubana hii maana tuna uchungu sana na suala la Jerry.

    ReplyDelete
  10. Kudura nakuona, kaza buti kweli mnawezaa!

    ReplyDelete
  11. A0wino usisahau msema wa Yesu Kristo kuwa "wana wakinyamaza basi MAWE haya yatatoa sauti"

    Wananchi wa rorya wanakuita sana usimame ubunge maana wanaojitokeza ni mabangusiro na mtemi wako sarungi ambaye wenzake wanang'atuka yeye anatangaza ufalme...siku wanarorya wasipokuitaji tena usijipeleke.....wakati ni huu.

    usiogope rushwa, wajumbe safari hii kalagabaho.....kinaeleweka kwa wanachama tu..mjomba kikwete kashasema mwendo vijana...maji yakizidi unga walishakwambia fanya kama raila vuka mto nenda CHADEMA.
    Mnibi Jacton.(muhuri wa moto)
    Arts $ Signs design specialist.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...