Karakana iliyokuwa ikitumika kwa uficho kutengeneza silaha imegundulika na polisi katika kijiji cha Sopa kata ya Matai , katika wilaya ya Sumbawanga , mkoani Rukwa. Pichani ni baadhi ya vifaa vya uhunzi zikiwemo mikasi na nyundo zilizotumika kutengenezea, bunduki mbili aina ya shotgun, bastola mbili, goroli za risasi pamaja na maganda kadhaa matupu ya risasi.
Katika msako huo ndugu wanne wamekamatwa na polisi na kukiri kuhusika na kumiliki na utengenezaji wa silaha hizo ambazo zimeonnywesha wanahabari na Kamanda wa Polisi Mkoani Rukwa Isuto Mantage (hayupo pichani) (Picha na Peti Siyame)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. BADALA YA KUMFUNGA NI BORA WATU KAMA HAO KUWACHUKUWA NA KUWAPA ELIMU NA KUANZISHA VIWANDA KAMA HIVI KWA AJILI YA KUUZA HATA EXPORT MARKET. TUFANYE UTAFITI JUU YA MAMBO AMBAYO YATATULETEA PESA NA MAENDELEO NA UJUZI KWA VIJANA WETU

    ReplyDelete
  2. wawape kazi dili ilo lakuletea pesa za kigeni na kupunguza matumizi ya kununua silaahaa toka nje kipasenti

    ReplyDelete
  3. kweli sumbawanga wachawi!!!! sasa na silaha pia si watatumaliza jamani.Upigwe kombora upepo na risasi pia,huponi jamani!!

    ReplyDelete
  4. kweli lugha ni kitu cha ajabu! mtu ukuisikia shot gan waweza fikiri ni bunduki fupi? kumbe!

    ReplyDelete
  5. Duuuh hii inatia rajha kuona kama watanzania wanavipaji kama hivi.Wanatakiwa wapewe muundo mbinu na kuendeleza vipaji vyao.wanatakiwa wapewe rasilimali na kufungua kiwanda chao.

    ReplyDelete
  6. MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NI MABAYA NA YAMEZAA MTU KAMA Mon Feb 08, 03:23:00 AM AMBAYE HAJUI TOFAUTI YA SHOT NA SHORT, HII NDIYO ELIMU TUNAYOISIFU.

    ReplyDelete
  7. KWELI HUKO KUNA WACHAWI MWANDISHI ANAONA BUNDUKI MBILI TU WAKATI ZIKO TATU!

    ReplyDelete
  8. huo ni ujuzi mkubwa sana! hao watu ni muhimu katika taifa letu! ingawa si vizuri kwa usalama wa nchi, naishauli mamlaka husika itazame vyote viwili faida na hasara ya vipaji kama hivyo!

    ReplyDelete
  9. Sumbawanga mimi nikijua ni uchawi tu kumbe na ujambazi pia?

    ReplyDelete
  10. KWELI WAKIWA NA UJUZI WACHUKULIWE ILA KWA NCHI YETU BORA KUONDOWA UJAMBAZI, SABABU NDIO HAWAHAWA UKIWAWEKA POLISI AU JESHINI INAKUWA TABU KAMA KINA JAMAA WETU KUVAAAAAAAAAA LOL! AU KOVAAAAAAA.

    ReplyDelete
  11. yaani watu wa jadi wanafanya mambo makubwa ya kisayansi wakati mainginia wetu na maprofesa hata kutengeneza kitako cha bunduki hawajui

    tena hilo gobole hata mzungu hana cheap technology kama hiyo na ni silaha inayoaminika sana duniani,tembo anenda chini kama mlevi vile eeeeeh kumbe na siku hizi kuna na bastola.!? hongera sana wazee nyinyi ndio mlifaa muongoze wizara sa sayansi na teknologia, pia hata mvua za asili mnashusha kaaaaa.. na radi pia inatumwa online

    JK naomba uwajaribu hawa wazee waendeshe sayansi na tekhnologia hiyo wizara kwa miaka mitano tu,watafanikisha kauli mbiu ya kilimo kwanza

    ReplyDelete
  12. nafurahi sana kusikia tanzania kuna vijana wanabuni vitu vya maana namna hiyo kwani sisi tuliopo huku nchi za watu tunaulizwa nyinyi mnatengeneza nini?la kujibu hatuna tunaambiwa waafrika hatuna ubunifu haya huo sasa uendelezwe safi sana

    ReplyDelete
  13. nafurahi sana kusikia tanzania kuna vijana wanabuni vitu vya maana namna hiyo kwani sisi tuliopo huku nchi za watu tunaulizwa nyinyi mnatengeneza nini?la kujibu hatuna tunaambiwa waafrika hatuna ubunifu haya huo sasa uendelezwe safi sana

    ReplyDelete
  14. Vizuri sana wapewe mafunzo zaidi mana najua bunduki zilianza kutengenezwa africa na wazungu walivounda viwanda wakaboresh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...