Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Nector P. Foya (kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya shs milioni 13 kwa mshindi wa promosheni ya Samsung Mariam Andwele jijini Dar leo. Katikati ni Mwakilishi wa Masoko wa Samsung, Amina Iddy.
Mshindi wa promosheni ya Samsung, Mariam Andwele akionyesha mfano wa hundi ya shs milioni 13 muda mfupi baada ya kukabidhiwa na Meneja Mawasiliano wa Vodacom, Nector P. Foya (katikati) jijini Dar leo. Kulia ni Mwakilishi wa Masoko wa Samsung, Amina Iddy.
Vodacom yamzawadia 13m/-
mshindi wa promosheni ya Samsung
Vodacom yamzawadia 13m/- mshindi wa promosheni ya Samsung
Vodacom Tanzania jana ilimkabidhi Shilingi milioni 13 mshindi wa promosheni ya Samsung Bi. Mariam Andwele (20) mkazi wa Uwanja wa Ndege, Jijini Dar
Mariam aliibuka mshindi mwishoni mwa mwaka jana na aliwataka Watanzania kushiriki kwenye promosheni mbalimbali ili waweze kujishindia zawadi mbalimbali.

“Mwishoni mwa mwaka jana, nilipigiwa simu na kuelezwa kwamba nimeshinda shilingi milioni 13, kwa kweli nilifurahi sana,” alisema.

Alifafanua kwamba lengo lake ni kuzitumia fedha hizo vizuri kwa kujiendeleza kielimu na kwamba amepania kufika hadi Chuo Kikuu.

Mariam ambaye alimaliza kidato cha nne mwaka 2008, Jijini Mbeya na kisha kuhamia jijini Dar Salaam, alisema hakuna kiu kubwa ya maisha yake zaidi ya kujiendeleza kielimu . Aliishukuru Vodacom Tanzania kwa kubadili maisha yake na pia ya Watanzania wengine.

Meneja Uhusiano wa Vodacom, Nector Foya, alisema kampuni yake imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali kwa lengo la kuboresha maisha ya Watanzania.

“Promosheni hii na nyingine tunazoziendesha zinalenga kuboresha maisha ya wateja wetu na Watanzania kwa ujumla, hivyo tunawaomba wateja wetu wajitokeze kwa wingi kushiriki,” alisema.

Naye mwakilishi wa Kampuni ya Samsung Tanzania, kitengo cha Simu za Mkononi, Amina Iddy, aliwaomba wateja wa Samsung waendelee kutumia simu za kampuni yake kwani ni imara na bora.

“Tutaendelea kushirikiana na Vodacom kuendesha promosheni kama hii kwa lengo la kuyaboresha maisha ya wateja wetu,” alisema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Dada Mariam hongera sana kwa ushindi huu ushauri wa bure,k.m unatembelea blog,jua kwamba sasa utapata marafiki wa kila aina,kuwa macho,mshirikishe Mungu katika kupanga matumizi ya pesa yako na utapata mafanikio makubwa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...