Ankal.....
Nakupongeza sana kwa kuendeleza libeneke
Nakupongeza sana kwa kuendeleza libeneke
ukiwa kama mkuu wa wilaya ya nanihiii......
Kuna hili jambo moja la hii kitu inaitwa UTABIRI wa hali ya hewa huwa linanichanganya sana. Utamsikia mtangazaji wa utabiri huo akisema mfano "Maeneo ya kati mikoa ya Dodoma na Singida yatakuwa na mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua"!!!
Au "hali ya bahari itakuwa na mawimbi madogo madogo hadi makubwa" Sasa swali ni je? katika utabiri huo ni kipi kilichoachwa hapo?? Maana possible outcomes zote zimesemwa!! yaani mawingu, mvua, jua, mawimbi madogo hadi makubwa!!
Ni hilo tu Ankal...naomba wadau wanielimishe kuhusu hilo.
Mdau wa kweli.
Mdau wa kweli.
IMEACHWA SNOW NA UPEPO MKALI AU DHORUBA
ReplyDeleteHuu sasa ni UCHAWI. wewe unataka sisi na watoto wetu tukale wapi?? kama hutaki kudanganywa acha kusikiliza. macho makubwaa lione vile!!
ReplyDelete-Mfanyakazi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa!!
Hao jamaa tulishazoea huwa wanatabiri tsunami na masika ambayo hayatokea na hata bila aibu.
ReplyDeleteSasa sijui wanachanganywa na hiyo outdated radar ambayo waingereza wameamua kuturudishia pesa tulizotapeliwa?
Na Nambari wani wanapokwambia 'maisha bora kwa kila mtanzania' unafikiri wanamaanisha nini. ukipata jibu la maisha bora kwa kila mtanzania utakuwa umepata jibu la swali lako.
ReplyDeleteUTABIRI WA MAMLAKA YA HALI YA HEWA HUU HAUNA TOFAUTI NA NGUVU ZA GIZA!!
ReplyDeleteumenichekesha sana unajua mimi naonaga kama wazushi sijawahi kuwasikiliza kwa makini kumbe wanatajaga kila kitu ha ha ha sasa hapo umetabiri nini si kila kitu kinaweza kutokea asante kwa kunifumbua macho mdau hawa ni wasanii
ReplyDeletewewe ni jinias
Yaani wewe mdau una akili sana. Ni kweli hata mimi sijawahi kuona hii sentensi inabadilika hata siku moja. Kila siku ni kama ulivyosema. Ndurumo huwa ni ngurumo. Tangu huyu mtangazaji akariri hii sentensi hajawahi kubadilisha.
ReplyDeleteNgoja tuone mawazo ya wengi tuone mawazo ya wengi utapata jibu na mimi nikiwepo.
Mdau wa kweli: Ungekuwa jirani mimi ningekununulia hata soda au bia. Yaani imenichekesha ile mbaya. Uliyosema ni kweli, ila tu sema watu wengi huwa hatufuatilii sana kusikiliza kipindi cha hali ya hewa na kusikiliza nini wanatamka. Unajua si hapa bongo tu watu hawasikilizi vizuri utabiri wa hali ya hewa. Hata ulaya vile vile huwa hawasikilizi sana. Mpaka waandaji wa vipindi huwa wanaweka mamodo ili watangaze.
ReplyDeleteni hayo asante
NakipendaKiswahili
BWAHUHUHUUU nimecheka in capitoli letazi maana kweli kichekesho herihata huwa siwasikilizi loh kwa maana hiyo mtu unabeba jacket mwamvuli na hendikachifu ya jua nacheka nafa hapa mwe mwe mwe
ReplyDeleteHili wala halihitaji darubini kulishtukia, wewe uanitabirije eti kutakuwa na jua, mvua na ngurumo za hapa na pale! Kwani kuna mtu hajui kama Dar jua lipo kila siku? Kusema ukweli hawa waungwana wanatuongopea hivyo nashauri wapunguze wingi wa maneno na waiondoe ile ramani yao ya tangu niko St. Government primary school kwa kusema tu jua litakuwepo na usiku utawadia kama kawaida ila hali ya hewa tutajua kesho hiyo hiyo!
ReplyDeleteHahahah that's funny Baada ya kuangalia super ball nimeamua kuingia kwenye ankal kabla sijalala.
ReplyDeleteNani kwakwambia ulaya watu hawasikilizi hali yahewa....Uzuri wa bongo ni kuwa hali yetu ya hewa inakaa week mbili the same. Huku usiposikiliza unaweza lala njia ukirudi nyumbani usiku. Asubuhi mvua mchana jua usiku snow.....Mtu halali bila kuangalia hali ya hewa ya kesho itakuaje na pia hundoki nyumbani asubuhi bila kuangalia tena weather na traffic.....
Na huku meteorologists ni vichwa kikweli kweli. Hawadanganyi
Hilaliaz
ReplyDeleteNimecheka mbaya
HAPA KITU MUHIMU NI AJIRA TU IDARA HII INATOA AJIRA KWA JAMII LAKINI HAINA FAIDA YA ZIADA KWA JAMII KWANI UTABIRI WAKE NI FINYU SANA INGAWA TULIAMBIWA RADA INGESAIDIA KULETA USAHIHI, MATOKEO WANALIPUA KWA KUTUPA UTABIRI WA JUMLAJUMLA NCHI NZIMA; CHA KUSIKITISHA ZAIDI HAWAJUI HATA TOFAUTI ZA MAJIRA YA MVUA KATI YA MIKOA NDIO KINACHO SABABISHA KUWASHAURI WAKULIMA NCHI NZIMA KUANZA KUANDAA MASHAMBA INAPOTOKEA DAR IMENYESHA MVUA KUBWA!
ReplyDeleteJamani tunashangaa hayo? Mbona hata hao wafadhili wa libeneke hili nao wanatangazo lao linasema
ReplyDeletePATA DAKIKA SITINI BUREEE KWA SHILINGI MIA TANO!!!
Teh teh teh Bure kwa shilingi mia tano. Hiyo BURE nayo inauzwa shilingi mia tano. Hapa ndio Bongo bwana!!!
K.O.R.
nimepaliwa na maziwa hapa
ReplyDeletehahahahaaaaaa uwiii kwi kwi kwi!!
mweee,ntaaza kusikiliza sasa!
mdao ulosema ulaya hawasikilizi hali ya hewa sio kweli labda bongo,Kitu cha kwanza Ukiamka tu ulaya kabla ya hiyo news basi unasubiri hali ya hewa kujua kujipigilia au la,kwa sababu usafiri unaathirika vibaya mfano kipindi cha snow as well,kwa hilo umekosea ila narudia tena HAWAJATABIRI SNOW NA UPEPE MKALI HAPO
ReplyDeleteMi nadhani tatizo linatokana na kichwa cha habari"UTABIRI WA HALI YA HEWA" ila kama ingekuwa ni hali ya hewa kwa kipindi cha saa fulani zijazo basi ingeweza ku-cover hizo outcomes zote.
ReplyDeleteMdau kichali