



Mgombea Ramadhani Nasibu leo amekibeba tena kiti cha Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa nafasi hiyo iliyokuwa inagombewa pia John Nchimbi. Kapata kura 54 dhidi ya 47 alizopata mpinzani wake.
Nafasi ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji Nyanda za Juu Kusini imenyakuliwa na Bras Kiondo aliyepata kura 63, ambapo wagombea wengine Samson Mkisi aliambulia kura 29 na Gwamaka Mwaihojo 9. nafasi hii imejazwa baada ya aliyekuwa akiishikilia Theophil Sikazwe kufariki dunia.
Nasibu kaijaza nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais aliyoipoteza baada ya klabu ya Villa Squad ambayo ndiyo iliyomdhamini kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa TFF kushuka daraja msimu uliopita .
Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo, ikitokea timu iliyomdhamini kiongozi inashuka daraja basi nafasi hiyo itajazwa kwenye mkutano unaofuata wa TFF. Safari hii Nasibu alikuja kwa udhamini wa Mtibwa Sugar FC.
Je katika maelezo yako, tenga amechukua urais wa TFF? Michuzi naomba jibu
ReplyDeleteHongera sana Ramadhan Nassib. pamoja na jamaa kununua magazeti na waandishi habari lakini umeshinda.
ReplyDeleteKANUNI YA OVYO NA YA KIJINGA ETI KUGOMBEA UMAKAMU WA RAIS LAZIMA UDHAMINIWE NA TIMU YA PREMIER LIGI NI UTOTO, HAKUNA KITU KAMA HICHO DUNIANI KOTE EBU FUTENI UPUUZI HUO
ReplyDelete