Ramsey akilia kwa uchungu
baada ya kuvunjwa mguu
Ankal pole sana na kazi na tunakupa heshima zote kwa kutuwezesha kutupa habari mbali mbali za ndani na zile zinazowahusu watanzania ambao wapo nje ya nchi.
Mie leo ningependa kuwawakilisha wadau wanaoishi Uturuki na ambao ni wapenzi wa ARSENAL kutoa pole kwa wapenzi wote wa ARSENAL na wale ambao wapenzi wa soka kwa ujumla kutokana na striker chipukizi na machachali wa ARSENAL (RAMSEY) kuvunjika mguu.
Mungu amsaidie apone ndani ya kipindi kifupi na amjaalie arudi ktk kiwango chake kile kile. Jeraha alilopata isiwe sababu ya kushuka kiwango chake cha mpira atakaporudi dimbani. mungu mjaalie Ramsey afya njema na matibabu mema... Aaamin
From: Bab Tid, Turkey

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka michuzi samahani kuna mtu mmoja anaitwa Irene uwoya alikuwa pale airport anaect movie kwa kweli ule uvaaji wake sio kwanza mke mtu pili ni m-tanzania anavaa chupi nje alafu kwenye public kama ile sio kabisa wenzake walivaa vimini vya heshima tena wao wasichana sembuse mke wa mtu jamani dunia hii tunapita kesho kuna kifo na kila mmoja wetu ni mchungaji ataulizwa kachunga vipi

    ReplyDelete
  2. Inasikitisha sana kijana mdogo alivyovunjika!... arsenal imekua ikikumbwa na majeruhi sana, na ndo kitu kinachotukosesha makombe miaka yote! inasikitisha kwa kweli...

    ReplyDelete
  3. tupo pamoja RAMSEY--Wana terno

    ReplyDelete
  4. Tatizo ni hela watu premier league wanacheza utafikiri ni end of the world bwana mtakuja kuuana uwanjani aisee.kuvunja mguu wa mtu mzima sio mchezo you really have to apply nguvu nyingi za kutosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...