Ramadhani Nasibu akionekana mtu mwenye furaha usiku huu katika hoteli ya Travertine alikokwenda kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF waliofikia hapo, baada ya ngwe nzito ya kinyang'anyiro cha Umakamu wa Urais wa TFF jana ambapo alimshinda John Nchimbi.
Ramadhani Nasibu akipongezwa usiku huu
Makamu wa Pili wa Rais wa TFF akipiga stori na mashabiki wake usiku huu
Ramadhani Nasibu (kulia) akiwa na Jamal Malinzi wakati wa uchaguzi mkuu wa TFF uliopita ambapo Malinzi alikuwa anagombea urais na Sir Leodegar Chilla Tenga na Nasibu Umakamu wa Pili wa Urais. Malinzi alishindwa na Nasibu alipeta. Tenga alifanikiwa kunyakua kiti cha Urais nwa TFF na anapeta hadi leo.

Mgombea Ramadhani Nasibu leo amekibeba tena kiti cha Makamu wa Pili wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa nafasi hiyo iliyokuwa inagombewa pia John Nchimbi. Kapata kura 54 dhidi ya 47 alizopata mpinzani wake.

Nafasi ya mjumbe wa Kamati ya Utendaji Nyanda za Juu Kusini imenyakuliwa na Bras Kiondo aliyepata kura 63, ambapo wagombea wengine Samson Mkisi aliambulia kura 29 na Gwamaka Mwaihojo 9. nafasi hii imejazwa baada ya aliyekuwa akiishikilia Theophil Sikazwe kufariki dunia.

Nasibu kaijaza nafasi ya Makamu wa Pili wa Rais aliyoipoteza baada ya klabu ya Villa Squad ambayo ndiyo iliyomdhamini kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliopita wa TFF kushuka daraja msimu uliopita .

Kwa mujibu wa Katiba ya Shirikisho hilo, ikitokea timu iliyomdhamini kiongozi inashuka daraja basi nafasi hiyo itajazwa kwenye mkutano unaofuata wa TFF. Safari hii Nasibu alikuja kwa udhamini wa Mtibwa Sugar FC.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Je katika maelezo yako, tenga amechukua urais wa TFF? Michuzi naomba jibu

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Ramadhan Nassib. pamoja na jamaa kununua magazeti na waandishi habari lakini umeshinda.

    ReplyDelete
  3. KANUNI YA OVYO NA YA KIJINGA ETI KUGOMBEA UMAKAMU WA RAIS LAZIMA UDHAMINIWE NA TIMU YA PREMIER LIGI NI UTOTO, HAKUNA KITU KAMA HICHO DUNIANI KOTE EBU FUTENI UPUUZI HUO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...